Maajabu ya dunia hayaishi: Vichaa wamewabana kwa hoja wasomi wenye Masters na PhDs!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya wasomi(waliobobea katika elimu ya juu) wanaposhindwa kujibu hoja mitandaoni, wanakimbilia kutoa matusi ya kisaikolojia. Hoja hujibiwa kwa hoja.

Mtu akiandika uzi unaowa-challenge wenye shahada za juu, mara nyingi anaambiwa kuwa ana matatizo ya afya ya akili. Duh, yaani, kwa kuwa huwezi kumshinda kwa hoja, basi unamtangaza kuwa ni 'kichaa.'?

Najiuliza: kama mtu ni kichaa kweli, kwa nini unasoma alichoandika? Kwa nini unajibu? Kwanini una-comment? Na kwa nini hoja zake zinakutikisa kiasi hicho hadi ukose cha kumjibu? Kama una akili timamu, je, si ungetambua mapema kwamba huwezi kushindana na mtu asiye na akili?

Mtume Paulo alinena vema:
“Wanajidai kuwa wenye hekima, kumbe ni wapumbavu.”
(Warumi 1:22, BHN)

Elimu ni muhimu sana, lakini haitoshi kumfanya mtu awe na hekima ya kweli. Hekima ya kweli huanzia kwenye unyenyekevu na uwezo wa kusikiliza hata kile kinachotoka kwa mtu usiyemtarajia.

Dunia hii imejaa maajabu. Wakati mwingine, hoja zenye nguvu huja kutoka kwa watu waliodharauliwa!

Sema: "Amen"
 
Maajabu ya dunia hayaishi: Wanaoitwa vichaa wanawaamsha wasomi waliolala kifikra!

Katika nyakati hizi ambazo wenye PhDs "wanajimwambafy" tunashuhudia jambo la ajabu: Hoja "zilizoenda shule" zinatoka kwa watu waliodharauliwa, watu wasio na elimu na kuwasisimua wasomi wa Masters na PhDs. Hili ni jambo la kufikirisha.

Kama mtu anaonekana hana akili timamu, mbona hoja zake zinakugusa moyo na akili? Kama ni wa kudharauliwa, kwa nini unapata upofu wa macho baada ya kusoma maandiko yake?

Kama mtu ameandika pumba, si unampita tu kimya kimya? Kwa nini unajishushia hadhi kujibizana na mtu unayemuita kichaa?

Hii ni ishara kuwa kuna points umeona nzuri lakini hutaki tu kukubali ili watu wasidharau shahada zako!

Paulo anaendelea kusema:
“Mungu amefanya hekima ya dunia hii kuwa upumbavu.”
(1 Wakorintho 1:20)

Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu huu ili awaaibishe wanaojiona wana hekima na nguvu(1 Wakorintho 1:27)

Mara nyingi Mungu amekuwa akiwatumia watu ambao jamii haiwathamini - kuwafunika wenye majigambo ya vyeti. Kumbuka jinsi Mungu alivyomtumia Mchungaji mdogo (Daudi) kulipiga na kuliua jitu la kivita (Goliathi)!

Na tusisahau kauli hii ya Yesu, inayozidi kuchoma mioyo ya wenye majivuno:

“Ninakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na wenye akili mambo haya, ukawafunulia watoto wachanga.”
(Mathayo 11:25)

Haleluyaaa!!
 
Ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya wasomi(waliobobea katika elimu ya juu) wanaposhindwa kujibu hoja mitandaoni, wanakimbilia kutoa matusi ya kisaikolojia. Hoja hujibiwa kwa hoja.

Mtu akiandika uzi unaowa-challenge wenye shahada za juu, mara nyingi anaambiwa kuwa ana matatizo ya afya ya akili. Duh, yaani, kwa kuwa huwezi kumshinda kwa hoja, basi unamtangaza kuwa ni 'kichaa.'?

Najiuliza: kama mtu ni kichaa kweli, kwa nini unasoma alichoandika? Kwa nini unajibu? Kwanini una-comment? Na kwa nini hoja zake zinakutikisa kiasi hicho hadi ukose cha kumjibu? Kama una akili timamu, je, si ungetambua mapema kwamba huwezi kushindana na mtu asiye na akili?

Mtume Paulo alinena vema:
“Wanajidai kuwa wenye hekima, kumbe ni wapumbavu.”
(Warumi 1:22, BHN)

Elimu ni muhimu sana, lakini haitoshi kumfanya mtu awe na hekima ya kweli. Hekima ya kweli huanzia kwenye unyenyekevu na uwezo wa kusikiliza hata kile kinachotoka kwa mtu usiyemtarajia.

Dunia hii imejaa maajabu. Wakati mwingine, hoja zenye nguvu huja kutoka kwa watu waliodharauliwa!

Sema: "Amen"
Ni sawa na pale watwawala vichaa nanapoendesha taifa.
 
Mungu akuhurumie tu haki
Kambaku unataka Mungu anihurumie mara ngapi, mkuu?
Mungu aliishanihurumia, akaniokoa!
Tito 3:5
Alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya.
 
Ni sawa na pale watwawala vichaa nanapoendesha taifa.
Chonde chonde, Bengal usimwite Mtawala kichaa.
Tafadhali sana, jifunze kuwaheshimu Watawala na wenye Mamlaka.
1 Petro 2:17
“Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mheshimuni mfalme.”
Katika Andiko hilo, “mfalme” anawakilisha mtu aliye juu katika mamlaka, hivyo tunatakiwa kumheshimu.

Warumi 13:7
“Wapeni wote haki yao; mtu wa ushuru ushuru, mtu wa kodi kodi, mtu wa kuogopwa na aogopwe, mtu wa kuheshimiwa na aheshimiwe.”
 
Sioni hata point moja ya kujibu Hapo...naona mleta hoja kaamua kudharau wenye PhD Na Masters ....
 
Watwawala,au Watawala?
 
Sioni hata point moja ya kujibu Hapo...naona mleta hoja kaamua kudharau wenye PhD Na Masters ....
Mr What please soma uzi tena kwa makini. Halafu soma comments, soma na reply zake kabla ya kumhukumu mleta hoja
 
Kambaku unataka Mungu anihurumie mara ngapi, mkuu?
Mungu aliishanihurumia, akaniokoa!
Tito 3:5
Alituokoa si kwa sababu ya jambo lolote jema tulilotenda sisi, bali kwa sababu ya huruma yake, kwa njia ya Roho Mtakatifu anayetujalia tuzaliwe upya na kuwa na maisha mapya.
Wape neno hao mama mtumishi.
 
Mtumishi, wewe tambua tu fika humu jukwaani utapoteza tu muda wako. Watu wa humu ni wagumu sana kutoa sadaka za kujimaliza ukilinganisha na wale wa kwa Mwamposa.
 
Shida Ya hoja nyingi kutoka kwa Wenye elimu ndogo kwenda kwa wenye elimu kubwa zimefungwa katikati ya Inferiority Complex walio nao, sio kutaka kujua au kueleweshwa au kutaka kupewa maelezo ta kina juu ya hoja yao.

Mara nyingi wanaishia kubishana, na sio kusikikiza mrejesho wa hoja kutoka upande wa pili, Hii inafanya watu wengi kuwadharau na kuto toa ushirikiano katika kujibu hoja zao.

I stand to be corrected.
 
Ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya wasomi(waliobobea katika elimu ya juu) wanaposhindwa kujibu hoja mitandaoni, wanakimbilia kutoa matusi ya kisaikolojia. Hoja hujibiwa kwa hoja.

Mtu akiandika uzi unaowa-challenge wenye shahada za juu, mara nyingi anaambiwa kuwa ana matatizo ya afya ya akili. Duh, yaani, kwa kuwa huwezi kumshinda kwa hoja, basi unamtangaza kuwa ni 'kichaa.'?

Najiuliza: kama mtu ni kichaa kweli, kwa nini unasoma alichoandika? Kwa nini unajibu? Kwanini una-comment? Na kwa nini hoja zake zinakutikisa kiasi hicho hadi ukose cha kumjibu? Kama una akili timamu, je, si ungetambua mapema kwamba huwezi kushindana na mtu asiye na akili?

Mtume Paulo alinena vema:
“Wanajidai kuwa wenye hekima, kumbe ni wapumbavu.”
(Warumi 1:22, BHN)

Elimu ni muhimu sana, lakini haitoshi kumfanya mtu awe na hekima ya kweli. Hekima ya kweli huanzia kwenye unyenyekevu na uwezo wa kusikiliza hata kile kinachotoka kwa mtu usiyemtarajia.

Dunia hii imejaa maajabu. Wakati mwingine, hoja zenye nguvu huja kutoka kwa watu waliodharauliwa!

Sema: "Amen"
Kuna vyanzo viwili vya elimu:
1: Formal/mfumo rasmi
Huu ni mfumo wa madarasa na walimu walioanishwa. Unapofaulu mitihani ya mfumo huu, haikuhakikishii kuyaaksi yayofundishwa kwako. Pamoja na kuyaaksi uanapofanikiwa si sababu ya msingi kuona elimu isiyo ya mfumo rasmi haifai.

3: Informal/mfumo usio rasmi wa elimu.
Huu ni mfumo unaotokana na mazingira yanayokuzunguka pamoja na watu wake.
Mitihani unayokutana nayo huweza kujifunza zaidi ili kuweza kuutawala ulimwengu. Ukiwa mwanafunzi mzuri utakujenga vyema pia. Si sababu ya kudharau mfumo rasmi kama umefanikiwa kwa mfumo huu.

Mifumo yote miwili ni muhimu ili kuwa na balansi kwenye kutawala maisha yetu kwa kutanabaisha kipi kitumike wapi na kwa namna gani. Ubora wa kipi kitumike wapi hutegemea ni nini unahitaji kukifanya na pia kinahitaji nini.

Hivyo, twahitaji elimu za aina zote mbili ili kuitawala dunia kwa ulinganifu. Ingawa wenye elimu rasmi wanaonekana kuwa wenye ubora kwa kadri ya taratibu zetu za maisha. ILA, kwangu mimi inategemea uko wapi na unatekeleza nini. Mchanganyiko wa vyote na kutanabaisha kioi kinatumika wapi ndo tiba halisi. Wito wangu, tuzingatie na kuheshimu vyote.
 
Back
Top Bottom