Maajabu ya Mbowe, Fatma Karume na Zitto: Wako kimya licha ya gharama za maisha kupanda. Kipindi Magufuli kaziba maslahi yao kelele kila siku!

Status
Not open for further replies.
Inakuaje mtu mzima na gari unamiliki mafuta unanunua wewe lakini bei zikipanda umtegemee mwingine kukupigania? Wengine tunawasoma humu ndani kila wakati wanabeza zinazoitwa harakati, jana nimewasoma wanamlilia mwingine awapiganie. Kwenye nyongeza ya mishahara hivyo hivyo. Vijana wa kitanzania mmekuwa vilema au bubu? Kimsingi sio malamiko genuine ni siasa za kupambania legacy ya mtu na kukumbatia ujinga mliojazwa kwamba mna mkombozi halali anawapenda. Siku itapofika tipping point ndio mwisho wa utegemezi kwa wengine kupambania ya msingi.
 
Zitto anaroho mbaya sana pia udini unamsumbua!
 
Yaleyale ya kupigania masilahi ya wanasiasa tu, ukiona mwanasiasa anapiga sana kelele au anataka muandamane basi hilo ana masilahi nalo kisiasa.
 
Kuna usemi unasema kwamba when things go right go left, wanachokifanya akina Tundurisu na Fatima karume ni kutuonyesha watanzania nikwanamna gani wanapigania Matumbo Yao nasio wananchi, but all in all JPM was the best leader #rest_in_power_my_leader
He was the worst president ever.
 
hehhe na wao wana familia na maisha mengineyo nje ya siasa..wamewekwa mahabusu mara ngap ndani ya kipindi cha miaka 10 iliopita huku wewe ukila ugali wako na dagaa.? wacha maisha yaende hivi.pengine tutaelewana after the next ten years
 
Binafsi ule msemo wa wapinzani wametuchelewesha huwa nauelewa kwa maana ya watu kukaa na kutegemea kuna viongozi wa upinzani huko wapo kwa ajiri ya kutetea masilahi yetu na huwa tunapigania hadi masilahi yao bila kujua. Hali hii imetupotea muda bora toka mwanzo tungekuwa na umoja na kuamua kupigania masilahi yetu sisi wenyewe na sio kutegemea wanasiasa ambao nao wana masilahi yao.

Sasa mwanasiasa mambo yake yamenyooka ana haja gani ya kuingia kwenye kugombana na serikali? Ila sisi ndio tunaangaika.
 
Ni kweli wanasiasa wengi wanapigania maslahi binafsi lakini mapigano yao pia yanatija kwa uma.

Kingine unatakiwa kujuwa kuwa Wabongo ni watu WANAFIKI sana.
 
hehhe na wao wana familia na maisha mengineyo nje ya
siasa..wamewekwa mahabusu
mara ngap ndani ya kipindi
cha miaka 10 iliopita huku
wewe ukila ugali wako na
dagaa.? wacha maisha yaende
hivi.pengine tutaelewana after
the next ten years
Wao ni wachache sana ukilinganisha na wananchi wengi waliyofungwa huko jela kwa uonevu kwa miaka mingi, ila tizama wao wakiingia jela wapo watu wa kuwapigia kelele hadi wanaachiwa hali ya kuwa ndugu zetu bado wapo kule jela .
 
Ina maana baada ya kufa Magufuli na kuingia Samia ndio wao wakapata uchovu na kuchoka kuendelea kukuosoa au kupigania wananchi?
 
Wapinzani walipodhulumiwa
Ubunge na Dikteta Mwendazake MLIKAA KIMYA
Waliposhtakiwa na
Kubambikiziwa Kesi za Uongo
za Ugaidi mliwaachia
Chadema wapambane
hamkupaza Sauti
Chadema wanapigania KATIBA
MPYA mpo KIMYA
Kwahiyo unaona ubunge na udiwani waliyodhurumiwa ni wapinzani tu ila wananchi waliyopiga kura na kuwachagua hao wapinzani wao hawajadhurumiwa?
 
Nenda kamlalamikie bwana wako jiwe huko kuzimu aliko

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Ulitaka wafanyeje? Wewe huna mdomo wa kupaza sauti? Wakiwaambia mtoke Barabarani mtatoka?
 
Haswa tena Zitto na Mbowe hatari sana hawa licha ya kuwa na chawa wengi humu!
We mjinga ulitaka wawasemee kwa niaba? Unataka Mbowe atoke na Familia yake waandamane kwa niaba ya nyie na familia zenu? Wacha ujinga
 
Mmoja anatumia Uzenji kuwaza mambo, wawili wana tonge mdomoni hawawezi kuongea.
Utamaduni wetu mzuri wa Kiafrika unatufundisha usizungumze huku una kula
Ulitaka wafanyeje? Waandamane wao kwa niaba zenu?
 
Kuna usemi unasema kwamba when things go right go left, wanachokifanya akina Tundurisu na Fatima karume ni kutuonyesha watanzania nikwanamna gani wanapigania Matumbo Yao nasio wananchi, but all in all JPM was the best leader #rest_in_power_my_leader
Ulitaka wafanyeje? Watoke waandamane kwa niaba zenu? Wewe ukiwa ndani umelala sio? Yaanu mna uoga kuliko hata Panya then mnataka wao ndo wawapiganie. Never
 
Wakati wanashughurikiwa uliwahi toka Barabarani kuandamana hata?
 
Unataka wafanyeje hasa? Yaani watoke Barabarani waandamane kwa niaba yenu sio? Huo ni upimbi
 
Ulitaka wafanyeje?
Waandamane wao kwa niaba
zenu?
Wakosoe tu kama walivyokuwa wanamkosoa rais aliyepita, kama wanaona sasa hivi wanakula asali na hawana sababu ya kukosoa serikali basi akija kiongozi akikata asali yao wasije kupiga kelele zao na kujidai wamebeba ajenda za wananchi kumbe wana hasira zao binafsi. Wale asali ikikatwa walalamike kukatiwa asali na sio kujifanya kuanza kuongea ufisadi sijui udikteta hatutaki unafki.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…