Sehemu ya pili..
Maajabu ya tairi mbovu na utajiri uliojificha ndani yake
Kiwanda kitanunua tani moja ya tairi kwa shilingi laki mbili bei ya sasa.. Ataichoma mchomo mmoja unaochukua tani nane kwenye boiler kupitia mchakato uitwao pyrolisis (kama kupika gongo tu)
Tani 8 sawa na shilingi milion 1.6
Zitakuletea wastani wao
.Mafuta ya I.D.O (industrial diesel oil) lita 3000 sawa na tani 3..
. Vumbi (black carbon) wastani wa tani 4
.Waya wastani wao tani 2
Gesi wastani wa nusu tani
Lita moja ya I.D.O kwa sasa ni Tsh 2000 zidisha mara 3000 ni Tsh 6,000,000
Vumbi (carbon black) kwasasa tani moja ni kama elfu 70 zidisha mada 4 ni Tsh 280,000
Waya kwasasa tani ni kama shilingi laki 8 zidisha mara 2 ni Tsh. 1,600,000
Gesi sijapiga hesabu
Kwahiyo mzigo wao shilingi 1.6M unakuletea wastani wa shilingi 7, 880,000/=
Ukitoa gharama zote za uendeshaji bado hukosi faida ya Tsh. 5,000,000/= tasilimu
Kwa wasiojua matumizi ya hizi bidhaa
1. Mafuta ya IDO ni kama nishati mbadala viwandani badala ya diesel, kuni, gas au umeme
2. Vumbi ni malighafi kwenye viwanda vya saruji
3. Waya zipo ngumu na Iaini.. Ngumu zinatumika kama binding wire kwenye ujenzi unaohusisha nondo, laini kama carbon catalyst kwenye viwanda vya nondo.. Si mnajua nondo bila carbon ukiipinda inakatika?
4. Gesi kwa matumizi ya kupikia nk
Hayo ndio maajabu na utajiri uliojificha kwenye tairi mbovu
Good morning Tanganyika