Maajabu ya tairi mbovu na utajiri uliojificha ndani yake

Maajabu ya tairi mbovu na utajiri uliojificha ndani yake

Okay nikileta mzigo wangu tani 1 toka huku mkoani unaweza kuchakatwa kwa siku ngapi?
 
Mtoa mada juu ya jambo hili wanaonekana ana uelewa nalo vizuri sana ndiyo maana hata baadhi ya maswali amejibu kwa kunyooka. Labda tungetowa maelekezo kadhaa ikiwemo soko la bidhaa zitokanazo na tajiri, viwanda vinapatikana wapi katika kuchakatia hizo tair. Na idadi ya kuanzia kwa tairi
 
Usafirishaji wamzigo kwa tani inaweza gharimu kiasi gani na gharama huwa juu ya nani kaka🙏 na ubarikiwe Sana.
Magaril yapo mengi kama ni mzigo mkubwa kuna namna ya kuyakata ili mzigo uingie mwingi
Gharama za usafiri ni makubaliano
 
Okay nikileta mzigo wangu tani 1 toka huku mkoani unaweza kuchakatwa kwa siku ngapi?
Wewe Kazi yako ni kuuza tu mzigo na kuchukua chako.. Michakato mengine na faida zake ni vya mwenye kiwanda
 
Okay nikileta mzigo wangu tani 1 toka huku mkoani unaweza kuchakatwa kwa siku ngapi?
Wewe Kazi yako ni kuuza tu mzigo na kuchukua chako.. Michakato mengine na faida zake ni vya mwenye
Mtoa mada juu ya jambo hili wanaonekana ana uelewa nalo vizuri sana ndiyo maana hata baadhi ya maswali amejibu kwa kunyooka. Labda tungetowa maelekezo kadhaa ikiwemo soko la bidhaa zitokanazo na tajiri, viwanda vinapatikana wapi katika kuchakatia hizo tair. Na idadi ya kuanzia kwa tairi
Masoko ya I.D.O
.Viwanda vyote vinavyotumia boilers kama nishati mbadala
.Wajenzi wa barabara kwa ajili ya mitambo na kuchemshia lami
. majokofu makubwa ya huhifadhia vitu vingi kama maua nk
Masoko ya vumbi (Carbon black) au black carbon
Viwanda vya saruji

Masoko y waya
Viwanda vya nondo
Hardware zile binding wire

Masoko ya gesi.. Bado hili halijafanyiwa Kazi.. Lakini tunaweza kuiweka kwenye mitungi na kuuza
 
Sehemu ya pili..
Maajabu ya tairi mbovu na utajiri uliojificha ndani yake

Kiwanda kitanunua tani moja ya tairi kwa shilingi laki mbili bei ya sasa.. Ataichoma mchomo mmoja unaochukua tani nane kwenye boiler kupitia mchakato uitwao pyrolisis (kama kupika gongo tu)
Tani 8 sawa na shilingi milion 1.6
Zitakuletea wastani wao
.Mafuta ya I.D.O (industrial diesel oil) lita 3000 sawa na tani 3..
. Vumbi (black carbon) wastani wa tani 4
.Waya wastani wao tani 2
Gesi wastani wa nusu tani
Lita moja ya I.D.O kwa sasa ni Tsh 2000 zidisha mara 3000 ni Tsh 6,000,000
Vumbi (carbon black) kwasasa tani moja ni kama elfu 70 zidisha mada 4 ni Tsh 280,000
Waya kwasasa tani ni kama shilingi laki 8 zidisha mara 2 ni Tsh. 1,600,000
Gesi sijapiga hesabu
Kwahiyo mzigo wao shilingi 1.6M unakuletea wastani wa shilingi 7, 880,000/=
Ukitoa gharama zote za uendeshaji bado hukosi faida ya Tsh. 5,000,000/= tasilimu
Kwa wasiojua matumizi ya hizi bidhaa
1. Mafuta ya IDO ni kama nishati mbadala viwandani badala ya diesel, kuni, gas au umeme
2. Vumbi ni malighafi kwenye viwanda vya saruji
3. Waya zipo ngumu na Iaini.. Ngumu zinatumika kama binding wire kwenye ujenzi unaohusisha nondo, laini kama carbon catalyst kwenye viwanda vya nondo.. Si mnajua nondo bila carbon ukiipinda inakatika?
4. Gesi kwa matumizi ya kupikia nk

Hayo ndio maajabu na utajiri uliojificha kwenye tairi mbovu


Good morning Tanganyika
Goodafternoon Sir!
 
Kuna hesabu haijakaa sawa au maelezo hayajitoshelezi.

Umepigia hesabu ya msingi ambayo ni tani moja ya matairi chakavu, sasa inakuwaje kila kipengele cha production inayozalishwa kwenye separation iwe na uzito wa tani?

Yaani tani moja ya malighafi ya matairi chakavu izalishe takribani tani tano za reproduction?
Motivation Speaker huwa hawakupi profit loss ni faida mara dufu mkuu.

Tani mona inazalisha kila tone moja ya kila kitu kutoka kwenye first materials 🙂
 
Mikoani wanaleta sana Dar, in fact sio tairi chakavu ni tairi mbovu hata zilizochanika na kusamabaratika, mabaki ya tairi kwa watengeneza ndala yale yanaitwa maini, na kuna unga wa tairi toka viwanda vinavyofanya retrading
Bei ni kuanzia milion 100View attachment 3153493View attachment 3153494View attachment 3153495
Nanukuu "mabaki ya tairi kwa watengeneza ndala yale yanaitwa maini, na kuna unga wa tairi toka viwanda vinavyofanya retrading. Bei ni kuanzia milion 100"

Kwa hali hii hayo maini na huo unga vitakuwa adimu sana kwa sasa.
 
Back
Top Bottom