Uchaguzi 2020 Maalim Seif anapodai "Mamlaka Kamili" anamaanisha kuvunja Muungano?

Uchaguzi 2020 Maalim Seif anapodai "Mamlaka Kamili" anamaanisha kuvunja Muungano?

Muungano ndani ya Katiba ya Warioba ambayo itfanyiwa kazi na serikali mpya ya Lissu katika siku 100 za kwanza unapendekeza serikali 3
Kawadanganye wanasaccos wenzako. Unafikiri rahisi hivyo kuuvunja muungano huu. Mnadanganywa kirahisi sana na beberu Lissu kwa kuwa akili zenu zimechanganyika na kamasi.
 
Tunataka Zanzibar huru yenye mamlaka kamili. Zanzibar ni nchi yenye watu wake, mipaka yake na sheria zake kabla hata huu muungano haujatengenezwa.

Muungano ni koti tu, tukilichoka tunaweza kulivua. Tusilazimishwe kile ambacho hatukitaki.
Jitahidi kuwahandaa wapemba wakubali kutoka bara warudi pemba kama watakubali basi umeshinda.
 
Kawadanganye wanasaccos wenzako. Unafikiri rahisi hivyo kuuvunja muungano huu. Mnadanganywa kirahisi sana na beberu Lissu kwa kuwa akili zenu zimechanganyika na kamasi.

Na unafikiri ni vigumu hivyo kuuvunja uvamizi huu uliopewa jina la muungano?? , Mnadanganywa na sahani ya pilau na paketi za sigara kali hapo Lumumba ?
 
..Majimbo hayawezi kujitangazia uhuru / kujitangaza kuwa dola kwasababu yameundwa kutoka ktk Tanzania Bara / Tanganyika.

..Zanzibar inaweza kujitoa ktk muungano kwasababu kabla ya 1964 walikuwa nchi / dola kamili.

..Msimamo wa Chadema ni muungano wa serikali 3 kama zilivyopendekezwa ktk rasimu ya Jaji Joseph Sinde Warioba.
Endeleeni kuweweseka.....
 
Seif anawahadaa wapambe wake kwani ili kuvunja muungano inabidi ipatikane theruthi mbili ya bara na mbili ya Zanzibar wakati Zanzibar wagombea wake 15 wameshaenguliwa ni wazi hatazipata.
Wapemba wengi wamewekeza bara ikiwamo na yeye mwenyewe ana nyumba bara hivi unafikiri ni wajinga wamruhusu avunje muungano maana kitakachofuata kila mtu arudi kwao
Seif mzee wa kuharibu.
Yule alishawahi kuwa Ccm alilelewa na Ccm
Alifukuzwa kama membe
 
Jitahidi kuwahandaa wapemba wakubali kutoka bara warudi pemba kama watakubali basi umeshinda.

Wapemba wako na walikuwepo na watakuwepo Tanganyika , Msumbiji , Kenya , Ulaya , Marekani kabla ya uvamizi ulioitwa muungano na hata baada ya jeshi la uvamizi kuondoka Zanzibar
 
Seif mzee wa kuharibu.
Yule alishawahi kuwa Ccm alilelewa na Ccm
Alifukuzwa kama membe

Kaharibu au watu waachiwe waamue ?? Hapa hakuna kufuata amri ya Magufuli mvuta bangi na genge lake.
 
Na unafikiri ni vigumu hivyo kuuvunja uvamizi huu uliopewa jina la muungano?? , Mnadanganywa na sahani ya pilau na paketi za sigara kali hapo Lumumba ?
Wenzako wamewekeza Bara hawatakubali kuuvunja Muungano hata huyo Maalim ananyumba Bara na kila mara yupo Bara. By the way sisi wabara hasara ya kuvunja muungano ni ndogo sana labda ni kiulinzi tu lakini as long as makao makuu tumeshaanza kuhamishia Dodoma it is good move.
 
Kuwekeza sio muungano?? Wenzangu wameekeza mpaka Dubai, wamenunua majumba Kenya, Uganda , wengine wana majumba Msumbiji , Hapo Tanganyika watu wamewekeza kabla huo uvamizi haujapewa jina muungano
 
Chadema na maalim seif wote wanasema
Muungano ni jambo la hiari wananchi Ndio waamue muungano gani wanaoutaka
Sioni tatizo na wananchi wakiamua kuuvunja muungano kwa kutumia utaratibu utakaowezesha hilo litokee kwa kutumia njia zitakazowawezesha wananchi kufanya hivyo kwa hiari yao wenyewe; kwa mfano kwa kutumia kura ya maoni juu ya jambo hilo pekee.
 
Akilazimisha anafunguliwa kesi ya uhaini hata yeye anajua.
Muungano ukivunjika na faida zake zinavunjika bakhresa atabaki kama mwekezaji, wapemba aliowaajili watapunguzwa na wanaobaki itabidi walipiwe work permit na resident permit atakosa faida nyingi sana ndio utambue nani anafaidika na muungano

Chuki yako inakufanya uwe kipofu

Una chuki na wapemba...

Muungano ukifa watu watachagua uraia wa nchi wanayotaka..

Hao wapemba wakiamua kuwa watanganyika hutaweza wazuia..wengi wao wamezaliwa ndani ya Muungano ... hutaweza walazimisha kurudi Zanzibar....

Chuki yako kwao haitakusaiidia lolote
 
Maana yake nini?

Kama nchi iko kwenye muungano na nchi nyingine, inaweza kudai kuwa na "mamlaka kamili" bila kuathiri muunganio huo?

Maalim, mgombea urais wa Zanzibar anapodai kuwa na mamlaka kamili, ana maana lengo lake ni kuuvunja muungano?

Akichaguliwa atachukua hatua zipi kuuvunja muungano.

Je, CHADEMA wana maoni gani kuhusu jambo hili? Na huko mbeleni, kama sera yao ya "Majimbo" itakuwa imetekelezwa endapo watapata ushindi, itakuwa halali kwa jimbo fulani kujichukulia "Mamlaka Kamili", kuachana na majimbo mengine?

Ni nini ushiriki wa wananchi katika uamzi wa kuuvunja au kutouvunja muungano, au inatosha tu kwa Maalim kuchaguliwa kwa sera hiyo kuchukua uamzi wa kuuondoa Muungano?

Maalim Seif anaifanya kazi ya Tundu Lissu kuwa ngumu zaidi wakati huu wa kampeni.
Muungano uvunjwe unatusaidia nini?
 
Wananchi wa Zanzibar wangepewa nafasi ya kupiga kura za maoni kama wanataka huu muungano ikiwa hawautaki basi na uvunjwe tu.

Hakuna sababu ya kuwa na ndoa ambayo mwenzako haoni sababu.
Mkuu 'Jocefhurs', kwa nini iwe "wananchi wa Zanzibar" pekee ndio wanaostahiri kuamua hatma ya muungano?

Mimi ningefurahi kama kila mTanzania atapewa fursa hiyo ya kuamua, kwa sababu muungano ni wetu sote.
Mimi sidhani kwamba maoni ya waTanzania wa Tanganyika ni tofauti sana na yele ya waTanzania wa Zanzibar. Kinachoharibu ni hawa wanasiasa wa pande zote mbili wanapoamua kulazimisha mambo bila ya kuwekea maanani maoni ya wananchi wa pande zote.
 
Maana yake nini?

Kama nchi iko kwenye muungano na nchi nyingine, inaweza kudai kuwa na "mamlaka kamili" bila kuathiri muunganio huo?

Maalim, mgombea urais wa Zanzibar anapodai kuwa na mamlaka kamili, ana maana lengo lake ni kuuvunja muungano?

Akichaguliwa atachukua hatua zipi kuuvunja muungano.

Je, CHADEMA wana maoni gani kuhusu jambo hili? Na huko mbeleni, kama sera yao ya "Majimbo" itakuwa imetekelezwa endapo watapata ushindi, itakuwa halali kwa jimbo fulani kujichukulia "Mamlaka Kamili", kuachana na majimbo mengine?

Ni nini ushiriki wa wananchi katika uamzi wa kuuvunja au kutouvunja muungano, au inatosha tu kwa Maalim kuchaguliwa kwa sera hiyo kuchukua uamzi wa kuuondoa Muungano?

Maalim Seif anaifanya kazi ya Tundu Lissu kuwa ngumu zaidi wakati huu wa kampeni.
Zanzibar ni nchi kamili ndani ya muungano, lakini uongozi wa pande zote mbili kwa kutofuata sheria na katiba Zanzibar imekuwa kama wilaya, yeye wanataka kuirudisha hadhi yake kwa mujibu wa katiba; tatizo la CCM kung'ania madaraka pande zote mbili kumeifanya iione Zanzibar kama ofisi ndogo ya chama!
 
Muungano uvunjwe unatusaidia nini?
Nami nitakuuliza, kwani umetunyima nini?
Matatizo yaliyopo hayawezi kurekebishwa, na muungano imara ukaendelea kuwepo?

Mimi nadhani unapouliza maswali kama hilo lako hapo juu, inafaa pia uwe na majibu na maelezo ya kutetea upande unaousimamia.
 
Zanzibar ni nchi kamili ndani ya muungano, lakini uongozi wa pande zote mbili kwa kutofuata sheria na katiba Zanzibar imekuwa kama wilaya, yeye wanataka kuirudisha hadhi yake kwa mujibu wa katiba; tatizo la CCM kung'ania madaraka pande zote mbili kumeifanya iione Zanzibar kama ofisi ndogo ya chama!
Jibu hili lingesaidia zaidi kama ungefafanua ile sehemu ya swali langu kuhusu "nchi kuwa na mamlaka kamili, ilhali imo kwenye muungano." Je, hilo linawezekana?
 
Anamaanisha Zanzibar iwe natambulika kimataifa kama nchi na siyo mkoa
Zanzibar ina nafasi nzuri ya kuwa taifa lenye maendeleo makubwa ikijitenga kuliko sasa.
Lakini inaweza ikaendeleza undugu na Bara ikiwa nje ya Muungano.
Bara itafaidika zaidi Kibiashara ikiwa Zanzibar itajitenga,itauza bidhaa nyingi mno katika visiwa hivyo.
 
Akilazimisha anafunguliwa kesi ya uhaini hata yeye anajua.
Muungano ukivunjika na faida zake zinavunjika bakhresa atabaki kama mwekezaji, wapemba aliowaajili watapunguzwa na wanaobaki itabidi walipiwe work permit na resident permit atakosa faida nyingi sana ndio utambue nani anafaidika na muungano
Sijakuelewa hapa,yaani faida ya kibiashara ni kwa Bakhresa kuwa na Wapemba wengi kwenye Biashara zake?
 
Back
Top Bottom