Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Pande zote 2 hazitaki Muungano. ZNZ wanasema tunawakalia kimabavu na tunawachelewesha kupata maendeleo yao wakati Tanganyika wanadai wanabeba gharama za kuiendesha Serikali ya ZNZ.Maana yake nini?
Kama nchi iko kwenye muungano na nchi nyingine, inaweza kudai kuwa na "mamlaka kamili" bila kuathiri muunganio huo?
Maalim, mgombea urais wa Zanzibar anapodai kuwa na mamlaka kamili, ana maana lengo lake ni kuuvunja muungano?
Akichaguliwa atachukua hatua zipi kuuvunja muungano.
Je, CHADEMA wana maoni gani kuhusu jambo hili? Na huko mbeleni, kama sera yao ya "Majimbo" itakuwa imetekelezwa endapo watapata ushindi, itakuwa halali kwa jimbo fulani kujichukulia "Mamlaka Kamili", kuachana na majimbo mengine?
Ni nini ushiriki wa wananchi katika uamzi wa kuuvunja au kutouvunja muungano, au inatosha tu kwa Maalim kuchaguliwa kwa sera hiyo kuchukua uamzi wa kuuondoa Muungano?
Maalim Seif anaifanya kazi ya Tundu Lissu kuwa ngumu zaidi wakati huu wa kampeni.
Muungano umefeli upigwe chini tu kama miungano mingine tu duniani mfano USSR, Yugoslavia etc. Kuna watu wanasingizia eti ACT inataka kumrudisha Sultani Jamshid Zanzibar. Jamshid anaanzia wapi kurudi? Kwanza unajuwa umri wake ni miaka mingapi na yuko wapi sasa? Ni kibabu cha miaka 91 na kilikuwa kinaishi Portsmouth Uingereza kama mnufaika wa utawala wa Malkia wa Uingereza (Subject of British Empire), last month ndiyo kimeruhuswa kurudi Oman kusubiri maka yake ya mwisho.
Tupige referendum, wananchi waamue