The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,282
- 117,244
Kwanini upewe?Nunua nyumbaNenda Zanzibar kama utapewa ardhi ya kujenga
Mbona zipo zinauzwa kwa yeyote?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwanini upewe?Nunua nyumbaNenda Zanzibar kama utapewa ardhi ya kujenga
Seif anawahadaa wapambe wake kwani ili kuvunja muungano inabidi ipatikane theruthi mbili ya bara na mbili ya Zanzibar wakati Zanzibar wagombea wake 15 wameshaenguliwa ni wazi hatazipata.
Wapemba wengi wamewekeza bara ikiwamo na yeye mwenyewe ana nyumba bara hivi unafikiri ni wajinga wamruhusu avunje muungano maana kitakachofuata kila mtu arudi kwao
Akilazimisha anafunguliwa kesi ya uhaini hata yeye anajua.
Muungano ukivunjika na faida zake zinavunjika bakhresa atabaki kama mwekezaji, wapemba aliowaajili watapunguzwa na wanaobaki itabidi walipiwe work permit na resident permit atakosa faida nyingi sana ndio utambue nani anafaidika na muungano
Zanzibar ina nafasi nzuri ya kuwa taifa lenye maendeleo makubwa ikijitenga kuliko sasa.
Lakini inaweza ikaendeleza undugu na Bara ikiwa nje ya Muungano.
Bara itafaidika zaidi Kibiashara ikiwa Zanzibar itajitenga,itauza bidhaa nyingi mno katika visiwa hivyo.
Kwa hiyo mnataka muvunje muungano halafu mbaki bara kufanya nini, hapa mpo kwa ajili ya muungano ukivunjika mnakuja kwa visa na kibali maalumu maana mnaweza kutuletea ugaidiHivi huyo aliyekwambia kuwa muungano ukivunjika kila mtu atarudi kwao ni nani?
Acha mawazo ya KiCCM hayo ndugu
Hujajibu swaliKwanini upewe?Nunua nyumba
Mbona zipo zinauzwa kwa yeyote?
Ha ha Mimi naupenda Sana Muungano. Sio wa Zanzibar na Tanganyika tu. Natamani hata Afrika ya Mashariki yoote iwe nchi Moja .Kwa hiyo mnataka muvunje muungano halafu mbaki bara kufanya nini, hapa mpo kwa ajili ya muungano ukivunjika mnakuja kwa visa na kibali maalumu maana mnaweza kutuletea ugaidi
Nikikujibu juu ya hati ya muungano nitaongea uongo kwani sijawahi kuiona lakini mkiungana lazima kuna vitu utapoteza sasa kuna wengine hawataki kupoteza ila wanataka kupata tuHa ha Mimi naupenda Sana Muungano. Sio wa Zanzibar na Tanganyika tu. Natamani hata Afrika ya Mashariki yoote iwe nchi Moja .
Lakini naomba nikuulize, Hati/ mkataba wa Muungano Ni Jambo la umma au Siri? Msingi wa Muungano ngano huu ulikua au ni nini?
Je unakua Lina Mambo gani au msingi wake Ni nini?
And For the record Mimi sio mzazibar. Ila Wazanzibar nawapenda Sana.
Soma au fuatilia visa vya hili swala la Muungano utajua huu Muungano una walakini.
Na kuendelea nao kwa namna hii utakuja kuvunjika. Jambo ambalo sipendi litokee kabisa.
Naupenda Bado niendelee kujitambulisha kwa Kujivunia Mimi ni mtanzania. Ila Wazanzibar pia wawe na Ari na Hamu hiyo hiyo wajitambulishe Kama watanzania kwa Kujivunia.
Unalosema ninkweli. Mnapoungana Lazima kila Mmoja apoteze na kutapa kitu.Nikikujibu juu ya hati ya muungano nitaongea uongo kwani sijawahi kuiona lakini mkiungana lazima kuna vitu utapoteza sasa kuna wengine hawataki kupoteza ila wanataka kupata tu
Tatizo kubwa lipo kwa wanasiasa wanatafuta vidosari vidogodogo ili wapare kura kwa wananchi lakini muungano ukivunjika waathirika wakubwa watakuwa ni wananchi wa kawaida wala sio hao viongozi.Unalosema ninkweli. Mnapoungana Lazima kila Mmoja apoteze na kutapa kitu.
Sasa nakushauri hebu Karibu kufuatilia huu Muungano historia yake na Visa vyake. Utagundua tuliungana( prematurely).
Kiukweli sijui kwa nini nchi hizi mbili ziliamua kuungana. Nnalofahamu Ni moja tu inaonekana ilikua Ni matakwa ya Viongozi wawili. Na kwa nini wao wakiungana pia Sina jubu la uhakika.
Lakini ukifuatila historia na Visa vya tangu Muungano huu uwepo Mara nyingi Wazanzibar wamekua na Lawama. Mbaya zaidi kila siku zinavyoenda, nilipo Karibu fuatila Inaonekana Zanzibar inazidi kupokwa Baadhi ya Maswala .
Sasa kwanini serikali hizi mbili zisikae chini Kisha zikubaliane halafu wawaeleweshe wanachi juu ya makubaliano yao, kila upande upigie kura Muafaka. Kama Pande zote mbili zikiridhiwa na wananchi wake tusaini Sasa mkataba wa Muungano wenye mfumo ambao wananchi wa kila.upande wameridhika.
Ila bado nakushauri Fuatilia Visa vya Muungano huu ndipo uweze changanua.
Hilo nalo.Tatizo kubwa lipo kwa wanasiasa wanatafuta vidosari vidogodogo ili wapare kura kwa wananchi lakini muungano ukivunjika waathirika wakubwa watakuwa ni wananchi wa kawaida wala sio hao viongozi.
Seif Sharif Hamad ndiye aliyeiba nyaraka toka kwa Jumbe ambaye alitaka kuanzisha serikali tatu na Zanzibar kuwa na mamlaka yake lakini sijasikia wanaounga kauli za Seif hawajamwuliza mbona kipindi kile alimsaliti Jumbe hivyo ukimfatilia utaona ni tamaa ya madaraka inayomsumbua wala sio uchungu kuwa Zanzibar wananyonywa
Tanzania ya Magufuli bora mgeni kuliko huyo raia , kwani hakuna mgeni aliyebambikiziwa kesi za kijinga
Tanganyika ipo tokea hapo zamani na Zanzibar pia ipo tokea hapo zamani. Watu waliishi na kufanya biashara na hatukusikia hizi fujo mpaka alipokuja Laanatullahi Nyerere akaivamia Zanzibar na kumkamata Waziri Mkuu wake Muhammed Shamte na kumfunga katika jela za Tanganyika kabla huo uvamizi kupewa jina la muungano hapo April 26 1964.
Zawadi yako hii
Unamaanisha kawekeza Starlight Hotel? Labda ataihamishia Pemba!Seif anawahadaa wapambe wake kwani ili kuvunja muungano inabidi ipatikane theruthi mbili ya bara na mbili ya Zanzibar wakati Zanzibar wagombea wake 15 wameshaenguliwa ni wazi hatazipata.
Wapemba wengi wamewekeza bara ikiwamo na yeye mwenyewe ana nyumba bara hivi unafikiri ni wajinga wamruhusu avunje muungano maana kitakachofuata kila mtu arudi kwao
Akilazimisha anafunguliwa kesi ya uhaini hata yeye anajua.
Muungano ukivunjika na faida zake zinavunjika bakhresa atabaki kama mwekezaji, wapemba aliowaajili watapunguzwa na wanaobaki itabidi walipiwe work permit na resident permit atakosa faida nyingi sana ndio utambue nani anafaidika na muungano
Bila muungano mzanzibari ataishi Tanganyika kwa vibali sawa na wageni wengine toka mataifa ya nje. Natamani sana hilo litokee.
Akipunguza wengine watachukua nafasi wapo azania, mo na wengineo wengi..Na Bakhresa kidogo-kidogo ataanza kupunguza uwekezaji Tanganyika.
..Ni lazima uelewe kwamba kila upande unamhitaji mwenzake.
Akipunguza wengine watachukua nafasi wapo azania, mo na wengineo wengi
Tatizo kubwa lipo kwa wanasiasa wanatafuta vidosari vidogodogo ili wapare kura kwa wananchi lakini muungano ukivunjika waathirika wakubwa watakuwa ni wananchi wa kawaida wala sio hao viongozi.
Seif Sharif Hamad ndiye aliyeiba nyaraka toka kwa Jumbe ambaye alitaka kuanzisha serikali tatu na Zanzibar kuwa na mamlaka yake lakini sijasikia wanaounga kauli za Seif hawajamwuliza mbona kipindi kile alimsaliti Jumbe hivyo ukimfatilia utaona ni tamaa ya madaraka inayomsumbua wala sio uchungu kuwa Zanzibar wananyonywa
..serikali makini huwa zinavutia wawekezaji, hazifukuzi wawekezaji.