Uchaguzi 2020 Maalim Seif anapodai "Mamlaka Kamili" anamaanisha kuvunja Muungano?

Uchaguzi 2020 Maalim Seif anapodai "Mamlaka Kamili" anamaanisha kuvunja Muungano?

..na bila muungano Watanganyika hatutalazimika kwenda kuwasaidia CCM-Znz kuiba uchaguzi. Natamani sana hilo litokee.
Likitokea watachinjana watuletee huku mzigo wa wakimbizi, Mungu aepushie mbali.
 
Anamaanisha Zanzibar iwe natambulika kimataifa kama nchi na siyo mkoa
Hivyo ndivyo Zanzibar.Wala bendera ya Zanzibar,Wana wimbo wa Taifa,Wana serikali ya Zanzibar,wana mikoa,wana bunge,wana mawaziri.
Hawana jeshi
Hawana Bank kuu
Hawana Police
Hawana wizara ya mambo ya nje
 
Kwa hiyo mnataka muvunje muungano halafu mbaki bara kufanya nini, hapa mpo kwa ajili ya muungano ukivunjika mnakuja kwa visa na kibali maalumu maana mnaweza kutuletea ugaidi

Hujajibu swali, Unafahamu kuna idadi gani ya ndugu zetu waTanganyika Zanzibar? au wewe ndio unawaona wapemba wa Dar tu?
 
Maana yake nini?

Kama nchi iko kwenye muungano na nchi nyingine, inaweza kudai kuwa na "mamlaka kamili" bila kuathiri muunganio huo?

Maalim, mgombea urais wa Zanzibar anapodai kuwa na mamlaka kamili, ana maana lengo lake ni kuuvunja muungano?

Akichaguliwa atachukua hatua zipi kuuvunja muungano.

Je, CHADEMA wana maoni gani kuhusu jambo hili? Na huko mbeleni, kama sera yao ya "Majimbo" itakuwa imetekelezwa endapo watapata ushindi, itakuwa halali kwa jimbo fulani kujichukulia "Mamlaka Kamili", kuachana na majimbo mengine?

Ni nini ushiriki wa wananchi katika uamzi wa kuuvunja au kutouvunja muungano, au inatosha tu kwa Maalim kuchaguliwa kwa sera hiyo kuchukua uamzi wa kuuondoa Muungano?

Maalim Seif anaifanya kazi ya Tundu Lissu kuwa ngumu zaidi wakati huu wa kampeni.
Huu mada iko juu ya upeo wa mavuvuzela
 
Nani anayemhitaji mwenzake zaidi? Unajua umeme unaotoka Tanganyika wanalipa bei gani!

..Nilikuwa namjibu mchangiaji aliyesema Tanganyika hatuna haja na uwezekezaji wa Bakhresa.

..hayo ni mawazo ya kizamani ya mwaka 1967 tulipotaifisha mali za matajiri wakubwa kama familia ya kina Chande.

..baada ya kutaifisha mali za kina Chande tukaanzisha National Milling Corporation. Sasa tulihangaika na kampuni hiyo mpaka tulipobwaga manyanga wakati wa zoezi la ubinafsishaji.

..Wakati mwingine kuchukua brain power ya majirani zetu siyo jambo baya. Kama kuna entrepreneur mzuri toka Pemba tumchukue. Kama kuna brilliant mathematician, physician, architect, banker, economist, etc toka jirani siyo vibaya kumchukua. Wamarekani walichukua mpaka scientists wa Hitler kuwatengenezea space program yao.
 
Hujajibu swali, Unafahamu kuna idadi gani ya ndugu zetu waTanganyika Zanzibar? au wewe ndio unawaona wapemba wa Dar tu?
Sina idadi wazanzibar wengi asili yao ni huku ndio kina mwinyi wa mkuranga, Nasoro Moyo wa Ruvuma, kuna wanyakyusa na wanyamwezi ila wapemba wao wanajiona asili yao ni Oman na wametapakaa Tanzania nzima
 
Waliokua hawautaki Muungano ni Wananchi wa Zanzibar usilete kisingizio kwa Seif Sharif

Seif ni muwakilishi tu wa matakwa ya wananchi
Kwani unafikiri hata bara wanautaka muungano watu wanataka hadi umeme wanaotumia tuwalipie au umesahau yule.mmbunge Kessy anavyowachamba bungeni
 
huyo anasumbuliwa na chuki moyoni mwake hana jengine
Maneno mengi ya nininsi mvunje muungano halafu kila mtu aweke sheria zake , kenya juzijuzi alijaribu anajua alichopata sidhani kama atajaribu tena na nyinyi fanyeni kama hamjaja kutulamba miguu nantukikubali mtaingia kwa masharti tutakayoyaweka
 
Ha ha ha ... Magu alishasema huwa hajaribiwi. Wakijaribu siku hiyohiyo wanakatiwa umeme hadi walipe matrilioni wanayodaiwa na TANESCO.

Halafu Seif hana washauri wazuri. Wakijitoa kwenye muungano, hata vile visiwa vyao vitatengana. Seif atabaki Rais wa Pemba. Imagine Rais wa taifa lenye wakazi laki tatu!
 
Ya kulipana ndio hakusemeki kwani hamna pesa ya kulipa faini ya uvamizi tokea 1964
 
Maneno mengi ya nininsi mvunje muungano halafu kila mtu aweke sheria zake , kenya juzijuzi alijaribu anajua alichopata sidhani kama atajaribu tena na nyinyi fanyeni kama hamjaja kutulamba miguu nantukikubali mtaingia kwa masharti tutakayoyaweka

Umerudi tena ? Unaweweseka na uvamizi wenu? Au Lisu anawakaranga vizuri
 
Back
Top Bottom