Uchaguzi 2020 Maalim Seif anapodai "Mamlaka Kamili" anamaanisha kuvunja Muungano?

Uchaguzi 2020 Maalim Seif anapodai "Mamlaka Kamili" anamaanisha kuvunja Muungano?

Maana yake nini?

Kama nchi iko kwenye muungano na nchi nyingine, inaweza kudai kuwa na "mamlaka kamili" bila kuathiri muunganio huo?

Maalim, mgombea urais wa Zanzibar anapodai kuwa na mamlaka kamili, ana maana lengo lake ni kuuvunja muungano?

Akichaguliwa atachukua hatua zipi kuuvunja muungano.

Je, CHADEMA wana maoni gani kuhusu jambo hili? Na huko mbeleni, kama sera yao ya "Majimbo" itakuwa imetekelezwa endapo watapata ushindi, itakuwa halali kwa jimbo fulani kujichukulia "Mamlaka Kamili", kuachana na majimbo mengine?

Ni nini ushiriki wa wananchi katika uamzi wa kuuvunja au kutouvunja muungano, au inatosha tu kwa Maalim kuchaguliwa kwa sera hiyo kuchukua uamzi wa kuuondoa Muungano?

Maalim Seif anaifanya kazi ya Tundu Lissu kuwa ngumu zaidi wakati huu wa kampeni.
Mungano hauna faida kwako
 
Ha ha ha ... Magu alishasema huwa hajaribiwi. Wakijaribu siku hiyohiyo wanakatiwa umeme hadi walipe matrilioni wanayodaiwa na TANESCO.

Halafu Seif hana washauri wazuri. Wakijitoa kwenye muungano, hata vile visiwa vyao vitatengana. Seif atabaki Rais wa Pemba. Imagine Rais wa taifa lenye wakazi laki tatu!

..nchi ya watu laki tatu halafu wana MAFUTA kibao!! 😂 😂
 
Tuweke muungano wa mkataba, nahitaji kuiona Tanganyika iliyoachwa na mkoloni , nchi ya maziwa makuu original
 
..nchi ya watu laki tatu halafu wana MAFUTA kibao!! 😂 😂
Usidanganyike ndugu yangu, hayo mafuta wanayodai mengi yapo kwenye mpaka wa Pwani na Tanga na mengine huko wanakopakana na Mombasa.
 
Maana yake nini?

Kama nchi iko kwenye muungano na nchi nyingine, inaweza kudai kuwa na "mamlaka kamili" bila kuathiri muunganio huo?

Maalim, mgombea urais wa Zanzibar anapodai kuwa na mamlaka kamili, ana maana lengo lake ni kuuvunja muungano?

Akichaguliwa atachukua hatua zipi kuuvunja muungano.

Je, CHADEMA wana maoni gani kuhusu jambo hili? Na huko mbeleni, kama sera yao ya "Majimbo" itakuwa imetekelezwa endapo watapata ushindi, itakuwa halali kwa jimbo fulani kujichukulia "Mamlaka Kamili", kuachana na majimbo mengine?

Ni nini ushiriki wa wananchi katika uamzi wa kuuvunja au kutouvunja muungano, au inatosha tu kwa Maalim kuchaguliwa kwa sera hiyo kuchukua uamzi wa kuuondoa Muungano?

Maalim Seif anaifanya kazi ya Tundu Lissu kuwa ngumu zaidi wakati huu wa kampeni.
Nchi kuwa na mamlaka kamili kuvunja muungano.

Ireland ina mamlaka kamili, wales ina mamlaka kamili hii haijaiunja united kingdoms.

muwe mnajisomea kwanza historia ndipo mseme .

Muungano wa Tanganyika Na zanzibar unaifanya Tanganyika kuwa mkoloni wa zanzibar, haikubaliki
 
Ulinzi wa kutuulia ndugu zetu na kuupiga vita uislamu?
Mkuu wa Brigedi ya Nyuki miaka yote Muislam, marais wawili kati ya watano waliowahi kuitawala Tanzania ni waislam. Wote hawa waliupiga vita uislam?!
 
Usidanganyike ndugu yangu, hayo mafuta wanayodai mengi yapo kwenye mpaka wa Pwani na Tanga na mengine huko wanakopakana na Mombasa.

..kwanini uwaombee na kuwatabiria mabaya?

..siyo kweli kwamba wakijitenga na Tanganyika basi ni lazima wataharibikiwa.

..upo uwezekano wa hawa ndugu zetu kufanikiwa na kupaa kiuchumi.

..mafuta yoyote yaliyoko baharini lazima tugawane nao kwasababu tumekaribiana nao sana.

..sasa advantage yao ni kwamba wenzetu wako laki 3, sisi tuko zaidi ya milioni 50.

NB:

..ila ukiniuliza mimi, tatizo la Zanzibar na muungano ni UCHAGUZI.

..Znz imekuwa na tatizo hilo kwa muda mrefu sana, tangu hata kabla ya Uhuru wa 1963 na Mapinduzi ya 1964.

..Watanganyika tuwasaidie Wazanzibari wawe na uchaguzi ulio huru, wa haki, na unaoheshimika.

..Natamani Watanganyika tusaidie haki itendeke, na siyo kusaidia upande mmoja wa Wa-Znz kutesa na kubinya haki za wenzao.
 
Seif anawahadaa wapambe wake kwani ili kuvunja muungano inabidi ipatikane theruthi mbili ya bara na mbili ya Zanzibar wakati Zanzibar wagombea wake 15 wameshaenguliwa ni wazi hatazipata.

Wapemba wengi wamewekeza bara ikiwamo na yeye mwenyewe ana nyumba bara hivi unafikiri ni wajinga wamruhusu avunje muungano maana kitakachofuata kila mtu arudi kwao
akili za wapi hizi mkuu?
 
Labda nisaidie, hali ya wananchi wa Equatorial Guinea kiuchumi ikoje?

..Na mimi nisaidie, hali ya wananchi wa Qatar kiuchumi ikoje?

..binafsi nawaombea heri majirani zetu wote wawe na amani na wapate maendeleo.
 
Seif anawahadaa wapambe wake kwani ili kuvunja muungano inabidi ipatikane theruthi mbili ya bara na mbili ya Zanzibar wakati Zanzibar wagombea wake 15 wameshaenguliwa ni wazi hatazipata.

Wapemba wengi wamewekeza bara ikiwamo na yeye mwenyewe ana nyumba bara hivi unafikiri ni wajinga wamruhusu avunje muungano maana kitakachofuata kila mtu arudi kwao
[emoji38]kwamba muungano ukivunjika kila mtu atarudi kwao!!! Mbona kuna watanzania wanaishi kenya,marekani nk ambazo ni nchi nyingine
 
..Na mimi nisaidie, hali ya wananchi wa Qatar kiuchumi ikoje?

..binafsi nawaombea heri majirani zetu wote wawe na amani na wapate maendeleo.
😆 😆 😆 😆 Qatar si Afrika mkuu, waafrika tuna matatizo makubwa sana ya ubinafsi. Maalim huyu kila uchaguzi anashinda, lakini mara zote amekuwa akilainishwa na watawala kwa fedha (Mzee Moyo alieleza walivyomfata baada ya uchaguzi na kitita kilichotukuka). Can he be trusted?!

Lisu ni miongoni mwa walionufaika na pesa ya Lowasa 2015, na hii imefanya kutofautiana na Mdee baada ya Lisu kugoma kumshambulia Gwajima akihofia kitu ambacho kingefuatia. Unaweza kuwaamini wahuni hawa?!

Mimi nawaombea mabaya yote hawa majirani wakijitoa, labda itawasaidia kujua kuwa muungano ulikuwa kwa faida yao.
 
[emoji38]kwamba muungano ukivunjika kila mtu atarudi kwao!!! Mbona kuna watanzania wanaishi kenya,marekani nk ambazo ni nchi nyingine
Hao watanzania wanaoishi Kenya wanaishi kama wakenya? Wanazo haki zote alizonazo mkenya?
 
Hao watanzania wanaoishi Kenya wanaishi kama wakenya? Wanazo haki zote alizonazo mkenya?
Mkuu,comment yako hapo juu umeonesha kwamba muungano ukivunjika wazanzibari wote watarudi kwao hicho ndicho ninapinga na ni upotoshaji mkubwa,hayo ya haki hayahusiani na tunachozungumzia mimi na wewe
 
Mkuu,comment yako hapo juu umeonesha kwamba muungano ukivunjika wazanzibari wote watarudi kwao hicho ndicho ninapinga na ni upotoshaji mkubwa,hayo ya haki hayahusiani na tunachozungumzia mimi na wewe
Nilichoandika ni kwamba muungano ukivunjika watalazimika kuishi Tanganyika kwa vibali sawa na wageni toka mataifa mengine. Ni post namba ngapi nilipoandika kuwa wote watarudi kwao ili nirekebishe?!
 
Back
Top Bottom