Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Ukisoma vizuri hiyo stori utagundua kabisa huyo dada ni malaya wa kawaida, amekuwa akidanga kwa wanaume watatu kwa mpigo. Na huenda wote watatu mmekuwa mkila mzigo kavu kavu.
Ushauri wangu nenda kwanza mkapime ngoma.

Hilo la kulea mimba ya kahaba utajua wewe mwenyewe, ila tambua kuwa kusema (kuahidi) ni rahisi sana, lakini kutekeleza ndio mtihani. Ngoja siku umchoke huyo mwanamke au vyuma vikaze kwa upande wako, ndio utaelewa hili ninalolisema.

Binafsi sikushauri kulea hiyo mimba. Pambana na hali yako, na yeye apambane na hali yake. Lea mkeo, watoto wako na ndugu zako tu, wapitaji wengine kaa nao mbali.
 
Verse
 

Tujitahidi sana Kuwa fanya watu wewe na Furaha Baraka ya machozi, Sasa wewe utafanywa wa machozi, utanambia huko mbeleni!
 
Hongera mno kaka Mungu akuongoze utimize uliyoahidi. Angalia usije mfanya huyo binti ajute zaidi. Kwa kuwa ulishaonja kuwa makini kama hutachanganya hisani na mapenzi.
 
Mkuu hongera sana kwa uamuzi huo.
USHAURI WANGU!

Kama umeamua kulea mimba hadi mtoto kumtunza hadi kumpa kiwanja n.k ,hilo sawa ila hakikisha unafanya yote hayo pasipo kutarajia shukrani kutoka.kwa mtu yoyote hapa duniani.

Iwe kwa huyo Dada,wazazi wake,au kwa ndugu Jamaa na marafiki toka pande zote.iwe kwako au kwake.Fanya kwa moyo wa kujitoa kama kulea yatima.na usitegemee kusikia hata neno hata asante kwa mtoto.

Pia,achana na swala la mtoto kuitwa ubini wa jina lako,...baba yake yupo ataitwa kwa jina la babaye,au kama ikishindikana watoto waliokataliwa na baba wakati wa mimba huwa wanapewa majina ya wajomba zao.au babu zao upande wa mama.achana na habari za kumpa jina lako.

Kingine naomba huyo Dada ,umwambia ukweli kwamba utamuhudumia tu kadiri ya uwezo wako ...pale utakapokuwa umeshindwa kuhudumia gharama na vitu kama hivyo...ukimwambia awe muelewa...asianze kusema kwa kulaumu kuwa "mbona ulisema utanisaidia...ona sasa hivi nateseka kwa ahadi zako feki...si bora ungesema tu kuwa hutaweza kunisaidia." Mwisho wa kunukuu.

Mwambie utamsaidia kwa kadiri ya uwezo wako...na kadiri ya kipato chako...sio kwamba 100% akutegemee...,mwambie angalau kwenye shida mfano inahitaji 10,000/= utaweza kutoa hata 3000/= ,nyingine naye awe tayari kutafuta,ila ikitokea unayo yote hiyo 10,000/= unampa..ila isiwe ndo uhakika kuwa unamsaidia shida zake zote 100%,hapana mpe tahadhari hiyo....hapo ni kuepuka lawama pale utakaposhindwa kuhudumia 100% huko mbele.

Maana maisha haya,.. Dah! Mungu ndo anajua,Leo unaweza ukawa uko freshi kiuchumi ila ikatokea lakutokea...kila.kitu kikagoma,kwa hiyo mwandae kwa hiyo hali ingawa huwa hatuombei matatizo ya kiuchumi yatokee...ila bora kuwa na utayari huo.

Mwisho hakikisha kweli Mkuu...umeamua kusaidia tu..usije ukaingia mkenge wa kuanza kula tunda taratibu tena...maana ukiendelea kula hapo tayari utakuwa umejipa majukumu halali ya kuhudumia pasipo udhuru wowote.,acha kabisa kula tunda,dhamiria kweli kutoa msaada tu.mambo mengine achana nayo.

Zaidi ya yote ni jambo njema,ulilofanya,sio mbaya kabisa,sema jamii yetu haijawahi kuona wala kuzoea mambo adimu kabisa na la kipekee kama hilo likifanyika ndo maana unaona mawazo hasi ni mengi...ila jamii yetu kiukweli inahitaji watu wengi wa aina kama yako,ili kupunguza vifo au utoaji mimba unaopelekea kuua kiumbe kisicho na hatia.

Fikiria huyo Dada angefanya maamuzi yapi kama usingempa msaada kama huo?je angejiua? Angetoa mimba? Je angebaki na kinyongo na wanaume wote...kutuita wote ni mbwa? Kama msemo wao walio wengi? Hatujui angefanyaje? umesaidia kwa kiasi kizuri sana kwa huyo Dada. HONGERA SANA MKUU.
 
Na kupitia hili la huyo mtoto mkataliwa utabarikiwa uingiapo na utokapo. Kifupi soma Kumb 28:1-13 kama wewe ni a believing Christian. Namba mumpatie jina zuri la kuashiria mafanikio/bahati/FURAHA.
Amen
 
Tunaisha mikoa tofauti mkuu, pia huyo mwenye mtoto anafamilia.
Wakirudiana ni maamuzi yao wala siwazuii mkuu
 
Ushauri mzuri
 
Hongera mno kaka Mungu akuongoze utimize uliyoahidi. Angalia usije mfanya huyo binti ajute zaidi. Kwa kuwa ulishaonja kuwa makini kama hutachanganya hisani na mapenzi.
Nitazingatia hilo asante
 
Tujitahidi sana Kuwa fanya watu wewe na Furaha Baraka ya machozi, Sasa wewe utafanywa wa machozi, utanambia huko mbeleni!
Usiwe mwoga watu kukutenda mkuu, Mungu yupo
 
Ingekuwa vigumu mno asiwepo mchangiaji mwenye mawazo kama yako.
Huyu dada hajawahi kuwa tegemezi kwangu wala mpiga vibomu, alikuwa akitumia hata nauli yake kunifuata.
 
Naona umeandika kwa hisia na hisia ndio zimekutawala mpaka sasa hv, kumsaidia ni jambo jema ila naona hata huyo dada hakuwa na upendo wa kweli kadri ulivyobeba tatizo lake, bora huyo jamaa yake wa nje ndio angekua muhusika ningekushauri ila ni jamaa mwngine baada ya kugombana na mchumba wake, ina maana alivyorudi ikiwa alikua anakupenda angekutafuta akueleze yaliyotokea sio kuanza kugawa kwingne kirahs hvyo au mlikua mnamega wote toka kitambo, naona huyo manzi ana usanii usiacha alama, pole sana babu..tuliza kwanza munkari, sasa kiwanja cha nini bora ungesema umpe elimu bora huyo dogo, naona umeona kiwanja deal umerudia mara kadhaa.
 
Hisia zimemtawala, nimeona hilo pia
 
Hisia zimemtawala, nimeona hilo pia
 
Ma single. Maza wengi diniani wanasumbuliwa na nyumbani za kupanga. Mi staki umpe upendo kiviiiile, maana una wengi wa kuwapenda ikiwemo familiya yako na mama yako,na wengine wajao, Hata ukikutana ma Mimi leo huyo mbona utamsahau!😁 kabla hilo halijatokea wewe MPE nyumbani tu Mungu atakubariki.

Maisha ya usingle mother ni kama kamali, naona umejitoa hadi raha, lakini nature ya usingle mother unaweza ifunye hiyo furaha ulopanga kutoweka, mtoto akizaliwa huwa ni mtamu, baba yake lazima aanze uchokozi, weekend ukiwa kwa mkeo, huyo Dada akakupigia hupokei,unaogopa kuharibu kwa mkeo, Dada mchepuko anapata upweke na hasira, Mara SMS ya mzazi mwenzie inaingia " najua unanichukia ila mm nakupenda, Mke wangu ndo kikwazo, plz njoo umchukulie mtoto matumizi, plz Niko chini ya figo zako"πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜ƒ
 
Sioni kama kutakuwa na tatizo maana mtoa mada hajasema kuwa atakuwa mke wa pili, amesema atampa uhuru kwenye upande wa kimahusiano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…