Mkuu hongera sana kwa uamuzi huo.
USHAURI WANGU!
Kama umeamua kulea mimba hadi mtoto kumtunza hadi kumpa kiwanja n.k ,hilo sawa ila hakikisha unafanya yote hayo pasipo kutarajia shukrani kutoka.kwa mtu yoyote hapa duniani.
Iwe kwa huyo Dada,wazazi wake,au kwa ndugu Jamaa na marafiki toka pande zote.iwe kwako au kwake.Fanya kwa moyo wa kujitoa kama kulea yatima.na usitegemee kusikia hata neno hata asante kwa mtoto.
Pia,achana na swala la mtoto kuitwa ubini wa jina lako,...baba yake yupo ataitwa kwa jina la babaye,au kama ikishindikana watoto waliokataliwa na baba wakati wa mimba huwa wanapewa majina ya wajomba zao.au babu zao upande wa mama.achana na habari za kumpa jina lako.
Kingine naomba huyo Dada ,umwambia ukweli kwamba utamuhudumia tu kadiri ya uwezo wako ...pale utakapokuwa umeshindwa kuhudumia gharama na vitu kama hivyo...ukimwambia awe muelewa...asianze kusema kwa kulaumu kuwa "mbona ulisema utanisaidia...ona sasa hivi nateseka kwa ahadi zako feki...si bora ungesema tu kuwa hutaweza kunisaidia." Mwisho wa kunukuu.
Mwambie utamsaidia kwa kadiri ya uwezo wako...na kadiri ya kipato chako...sio kwamba 100% akutegemee...,mwambie angalau kwenye shida mfano inahitaji 10,000/= utaweza kutoa hata 3000/= ,nyingine naye awe tayari kutafuta,ila ikitokea unayo yote hiyo 10,000/= unampa..ila isiwe ndo uhakika kuwa unamsaidia shida zake zote 100%,hapana mpe tahadhari hiyo....hapo ni kuepuka lawama pale utakaposhindwa kuhudumia 100% huko mbele.
Maana maisha haya,.. Dah! Mungu ndo anajua,Leo unaweza ukawa uko freshi kiuchumi ila ikatokea lakutokea...kila.kitu kikagoma,kwa hiyo mwandae kwa hiyo hali ingawa huwa hatuombei matatizo ya kiuchumi yatokee...ila bora kuwa na utayari huo.
Mwisho hakikisha kweli Mkuu...umeamua kusaidia tu..usije ukaingia mkenge wa kuanza kula tunda taratibu tena...maana ukiendelea kula hapo tayari utakuwa umejipa majukumu halali ya kuhudumia pasipo udhuru wowote.,acha kabisa kula tunda,dhamiria kweli kutoa msaada tu.mambo mengine achana nayo.
Zaidi ya yote ni jambo njema,ulilofanya,sio mbaya kabisa,sema jamii yetu haijawahi kuona wala kuzoea mambo adimu kabisa na la kipekee kama hilo likifanyika ndo maana unaona mawazo hasi ni mengi...ila jamii yetu kiukweli inahitaji watu wengi wa aina kama yako,ili kupunguza vifo au utoaji mimba unaopelekea kuua kiumbe kisicho na hatia.
Fikiria huyo Dada angefanya maamuzi yapi kama usingempa msaada kama huo?je angejiua? Angetoa mimba? Je angebaki na kinyongo na wanaume wote...kutuita wote ni mbwa? Kama msemo wao walio wengi? Hatujui angefanyaje? umesaidia kwa kiasi kizuri sana kwa huyo Dada. HONGERA SANA MKUU.