Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Kwanini usiangalie uwezekano wa kumuoa? Unataka apate njemba mwingine amnyanyase kisha nawe uanze tena kukosa raha mama wa mwanao ananyanyasika?
Tayari ana mtu wake. [emoji16][emoji16] BAK bwana
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Nimemaanisha mkeo/mpenzi wako. Siku akisikia mtoto anaitwa kwa jina lako ... unadhani ataelewa hii stori?
Hili nitaliweka sawa na baadhi ya mambo yataenda kisheria , kutakuwa na ufafanuzi wa kina wa badhi ya vipengele vinavyoweza kuleta utata baadae.
Pili anaishi mbali sana na ninakoishi hivyo kuna ka ugumu kujulikana
 
Kwanini usiangalie uwezekano wa kumuoa? Unataka apate njemba mwingine amnyanyase kisha nawe uanze tena kukosa raha mama wa mwanao ananyanyasika?
Mkuu hili halitawezekana, huruma yangu zaidi ni kwa mtoto zaidi
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
_Mathayo 6:2-4_
“Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo katika masunagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao. Lakini wewe unapomsaidia maskini, fanya hivyo kwamba hata mwandani wako asijue ufanyalo. Toa msaada wako kwa siri, na Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
 
NI MAAMUZI MAGUMU LAKINI YAMETOKA MOYONI

Wapendwa wana jukwa hili la mahusiano, mapenzi na urafiki ninawasalimu nyote.

Kama habari ya awali inavyosemaka kuwa nimechukua uamuzi mgumu wa kuwa baba mtarajiwa wa mtoto mtarajiwa wa rafiki yangu kwa hiyari na kwa kupenda mwenyewe kwa sababu nitakazo zieleza hapa chini, lakini kabla ya hizo sababu naomba nitoe ufafanuzi wa urafiki wetu.

Kuna dada mmoja tulikutana ofisi flani ya serikali, ni dada flani mpole kiasi na mcheshi kiaina.
Kwa muda mfupi sana nilivutiwa naye na ikafikia hatua ya kubadilishana naye namba za simu.

Zoezi la huduma lilienda vyema kwa yeye kufanya koneksheni na mtumishi flani na tukafanikiwa kupata hiyo huduma (pass ya kusafiria kwa haraka)

Baada ya hapo hatukuwasiliana haraka japo nilipanga lazima nimtafute.
Ulifika wakati tukaanza kuwasiliana hapa na pale
Na ukafika wakati nikawa nachomekea viutani kuwa ninamhitaji awe rafiki yangu.

Baada ya muda mrefu tulifanikiwa kuwa marafiki hatimaye tukaanza kushirikiana....hapa wakubwa mmeelewa.
Jambo nililompenda zaidi ni mwelewa na mwenye misimamo yake mizuri.
Tuliwekana wazi kuhusu mahusiano yetu, kwake yeye mpenzi wake alikuwa ni raia wa kigeni na anaishi huko kwao huja mara chache hivyo alikuwa anajiandaa kwenda kumtembelea...na walikuwa wamepanga kuoana.

Nini kilitokea kati yao???

Uliwadia wakati wa kusafiri alinijulisha nami nilimpa nafasi ya kuwa mbali naye kimawasiliano ili ajiweke sawa na akili yake iwaze juu ya mpenzi wake.
Alifanikiwa kwenda na kurudi.
Baada ya kurudi mawasiliano yetu yalikuwa hafifu kwani nilikuwa tight sana na kazi.


Baada ya miezi kama mitatu na nusu, tuliwasiliana na kupiga stori nyingi na mwishowe akanijulisha ni mjamzito.
Nikampa hongera zake..
Lakini mawasiliano yakazidi kuwa hafifu zaidi.
Ukafika wakati nikamuuliza maendeleo na mipango ya ndoa na kama wamepanga lini wataanza kuishi pamoja?

JIBU LAKE NDILO HASA LILINIGUSA NA KUAMUA HAYA
Rafiki yangu huyu alinishtua aliponieleza kuwa walitengana na yule mchumba kwani walipokutana ughaibuni alimfanyia visa vingi vibaya mno..sitavitaja
Na alipotua nchini alimtumia ujumbe kuwa asimtafute tena.
Akiwa katika hali ya kutafakari yaliyompata na jinsi gani atasonga mbele...ndipo alianza mahusiano na jamaa flani aliyeanza kumnyemelea kitambo na muda mfupi akapata ujauzito.

Baada ya kupata ujauzito alimjulisha mhusika lakini hakuwa tayari kuukubali bali alimwambia autoe kwani yeye anafamilia lakini aligoma kuutoa na akajiapiza ataulea na kwa vile jamaa ameukataa hata jina litakuwa la upande wa familia yake yaani ubini wa baba.

Habari hii iliniumiza sana na niliwaza haya yafuatayo;
1. Kuwa huyu dada ataishi kwa sonono kubwa
wakati wa ujauzito na atamwathiri mtoto
akiwa tumboni...wazazi wanajua hili
2. Huyu atakayezaliwa hatakuwa na upendo
katika jamii na anaweza kuja kuwa na tabia
ya ajabu

MAAMUZI YANGU
1. Nikamwomba kama naweza kuwa baba wa
wa hiyari na apewe ubini wa jina langu
kama baba alikubali hili kwa mshangao
mkubwa sana
(Haya[emoji116]sijamshirikisha)
2. Nitamhudumia kipindi chote cha ujauzito
3. Nitamfanya mwenye furaha ili kulinda afya
mama na ya mtoto atakaye zaliwa
4. Baada ya mtoto kukua yeye yuko huru kuwa
na maisha yake bila mimi kumwingilia uhuru
wake
5. Nitampa mtoto kiwanja na kumjengea kadri Mungu atakaponiweka hai na kunibariki, ili apate malazi na malezi bora.

Uamuzi huu nimeufanya mwenyewe japo sipangi kuishi na mtoto isipokuwa kumsapoti kimalezi tu.

Baada ya kukubaliana naye hasa kuhusu mtoto kuitwa kwa jina langu kama baba, alifurahi sana kiasi cha kulia machozi na nikamwahidi kuwa siku chache zijazo atakuja mkoa nilipo apate mapumziko ya muda mfupi...sio nyumbani kwangu lakini.
Amemweleza mama yake mzazi na hajaamini kuwa kuna mtu anaweza kufanya maamuzi magumu kiasi hiki.

Pamoja na hayo sijamweleza kwa undani namna nilivyojipanga kumsapoti mtoto hasa kumpa eneo na kumjengea, hili nimebaki nalo nikiomba Mungu aniwezeshe kulitimiza.

Wapendwa wana jf, inaweza kuonekana kuwa uamuzi wangu ni wa kijinga sana lakini kwangu mimi nitaona fahari kubwa kama hili litafaniniwa kwani;
Sisi wanaume tunapaswa kuwa chemichemi ya furaha ya wake zetu, mama, watoto na dada zetu lakini kinyume chake tumekuwa ni chanzo cha machozi.

Tujitahidi sana kuwafanya watu kuwa na furaha badala ya machozi.
Muwe na wakati mwema wote.
Mchaichai
 
_Mathayo 6:2-4_
“Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo katika masunagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao. Lakini wewe unapomsaidia maskini, fanya hivyo kwamba hata mwandani wako asijue ufanyalo. Toa msaada wako kwa siri, na Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.
Huyu sio masikini na sijataja jina
 
Hili nitaliweka sawa na baadhi ya mambo yataenda kisheria , kutakuwa na ufafanuzi wa kina wa badhi ya vipengele vinavyoweza kuleta utata baadae.
Pili anaishi mbali sana na ninakoishi hivyo kuna ka ugumu kujulikana
Kila la heri mkuu, barikiwa sana
 
Yeye ndio anajua hivyo, akija kujua hutomuoa huzuni itarudi tena kwake
Anafahamu kila kitu kuhusu mimi, hajaniomba bali mimi nimetaka.
Pili baba halisi ana uwexo mkubwa tu lakini hakuona haja ya kulazimisha mambo wala kutaka kwenda eti kwa mke wake.
Pili hata kwao wako vizuri kiasi sio hahehohe.
 
Mkuu wewe ni time Traveller uliishi zama za Yesu sasa umerudi katika ulimwengu huu[emoji23][emoji23][emoji23] Sema anyway itakuwa unampenda sana huyo mdada lakini Angalia usiwe unategemea kulipwa wema 100% huyo dada anaweza kuendeleza mechi za ugenini na Jamaa aliekataa mimbaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Maana wanawake achana nao mkuu.


Ataendelea kuliwa kimasihara
 
Anafahamu kila kitu kuhusu mimi, hajaniomba bali mimi nimetaka.
Pili baba halisi ana uwexo mkubwa tu lakini hakuona haja ya kulazimisha mambo wala kutaka kwenda eti kwa mke wake.
Pili hata kwao wako vizuri kiasi sio hahehohe.
Kitu kitakachokuwa kinamtesa kisaikolojia,kwa nini yeye hana mume?
 
Mi nimenukuu tu.

Alaf masikini sio mpaka hawe hana pesa, ata kutokuwa na furaha pia ni umaskini
Mkuu, maisha tunayoishi yamesababishwa na mambo na tabia zinazotuxunguka.
Hili nimeshea ili kuleta changamoto katika jamii.
Yesu alishea mengi mfano wa yule mjane kutoa sadaka tena aliitaja na kuinyanyua juu.
Mnapotosha mengi katika biblia.
Maana ya sadaka kutoonyeshwa ni watu wasitoe kwa nia ya wengine wawaone bora bali tutoe sadaka kama sehemu ya utumishi katika uchaji na ibada.
 
Back
Top Bottom