Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Jichanhanyee ndo utajuaa hujuiii[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Utakulaa mitamaaa
@yna2 ni rafiki yangu hahitaji kujichanganya.
Anajua mapito wapitiayo wanawake
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mi napita kwa tamaa za kiuanaume wenyewe wanaachia na ya mtoto na wanafurahia hilo mi nifanyeje sasa[emoji23][emoji23]
Lea mtoto bro
 
We jamaa huwezi kua serious..na hizo Ni element za. Kishoga....mwanaume unajisifia kuvutia..wakati unakaa na mwanamke unaloweka Hadi wenzio wanakuja kukusaidia kutia mimba...ukiendeleza hizo tabia huyo mwanamke atakutia dildo
Mdomo ni wako tukana tu mkuu
 
Malaika bado wapo hapa duniani[emoji7][emoji7]
We Kaka ubarikiwe mpaka ushangae.
Rafiki yangu yna2 mimi sina hata chembe ya umalaika, bali nilijaribu kuvaa viatu vya mwingine anavyofeel, vikanipwaya...najaribu kufanya kilicho ndani ya uwezo wangu huu mdogo
 
Rafiki yangu yna2 mimi sina hata chembe ya umalaika, bali nilijaribu kuvaa viatu vya mwingine anavyofeel, vikanipwaya...najaribu kufanya kilicho ndani ya uwezo wangu huu mdogo
Hata ivyo unafanya Jambo jema
 
1. Msichana ana boyfriend wake ukawa unamhudumia akiwa hapa dar boyfriend nje ya nchi.umeshindwa mtia mimba ulikuwa unashika mapembe.anakwambia usinitafute naenda kwa bwana angu...unasema haya - huu ni ubwege.

2. Kaenda kagombana na jamaa yake huko katua tu dar wanaume wamekamata na kuanza kumbwenga.wakamtia mimba - wewe hukuweza mtia mimba miezi yote unapiga naye love stories tu - huu ni ukosefu wa nguvu za kiume.

3. Kapigwa chini tena na jamaa wapili.wewe unapewa jukumu la kumchagulia mtoto jina na kulea sababu huzalishi.na unakuja jitapa hapa- huu ni ubwege plus plus na uthibitisho una shida kimwili.

Wanaume tunakusomaaaaaa..... Tunasema hiiiiiiiiiiii. Wewe ni YEYE.
 
1. Msichana ana boyfriend wake ukawa unamhudumia akiwa hapa dar boyfriend nje ya nchi.umeshindwa mtia mimba ulikuwa unashika mapembe.anakwambia usinitafute naenda kwa bwana angu...unasema haya - huu ni ubwege.

2. Kaenda kagombana na jamaa yake huko katua tu dar wanaume wamekamata na kuanza kumbwenga.wakamtia mimba - wewe hukuweza mtia mimba miezi yote unapiga naye love stories tu - huu ni ukosefu wa nguvu za kiume.

3. Kapigwa chini tena na jamaa wapili.wewe unapewa jukumu la kumchagulia mtoto jina na kulea sababu huzalishi.na unakuja jitapa hapa- huu ni ubwege plus plus na uthibitisho una shida kimwili.

Wanaume tunakusomaaaaaa..... Tunasema hiiiiiiiiiiii. Wewe ni YEYE.
Nikujibu sawa uchizi wako?
Hivi kila demu ukilala naye lazima umtie mimba?
Nani amekwambia mimi sina uzao?

Hivi kwasababu chizi unaishi dar, unafikiri wote ni wakazi wa dar?
Bado una nyeg..e za kitoto
 
NI MAAMUZI MAGUMU LAKINI YAMETOKA MOYONI

Wapendwa wana jukwa hili la mahusiano, mapenzi na urafiki ninawasalimu nyote.

Kama habari ya awali inavyosemaka kuwa nimechukua uamuzi mgumu wa kuwa baba mtarajiwa wa mtoto mtarajiwa wa rafiki yangu kwa hiyari na kwa kupenda mwenyewe kwa sababu nitakazo zieleza hapa chini, lakini kabla ya hizo sababu naomba nitoe ufafanuzi wa urafiki wetu.

Kuna dada mmoja tulikutana ofisi flani ya serikali, ni dada flani mpole kiasi na mcheshi kiaina.
Kwa muda mfupi sana nilivutiwa naye na ikafikia hatua ya kubadilishana naye namba za simu.

Zoezi la huduma lilienda vyema kwa yeye kufanya koneksheni na mtumishi flani na tukafanikiwa kupata hiyo huduma (pass ya kusafiria kwa haraka)

Baada ya hapo hatukuwasiliana haraka japo nilipanga lazima nimtafute.
Ulifika wakati tukaanza kuwasiliana hapa na pale
Na ukafika wakati nikawa nachomekea viutani kuwa ninamhitaji awe rafiki yangu.

Baada ya muda mrefu tulifanikiwa kuwa marafiki hatimaye tukaanza kushirikiana....hapa wakubwa mmeelewa.
Jambo nililompenda zaidi ni mwelewa na mwenye misimamo yake mizuri.
Tuliwekana wazi kuhusu mahusiano yetu, kwake yeye mpenzi wake alikuwa ni raia wa kigeni na anaishi huko kwao huja mara chache hivyo alikuwa anajiandaa kwenda kumtembelea...na walikuwa wamepanga kuoana.

Nini kilitokea kati yao???

Uliwadia wakati wa kusafiri alinijulisha nami nilimpa nafasi ya kuwa mbali naye kimawasiliano ili ajiweke sawa na akili yake iwaze juu ya mpenzi wake.
Alifanikiwa kwenda na kurudi.
Baada ya kurudi mawasiliano yetu yalikuwa hafifu kwani nilikuwa tight sana na kazi.


Baada ya miezi kama mitatu na nusu, tuliwasiliana na kupiga stori nyingi na mwishowe akanijulisha ni mjamzito.
Nikampa hongera zake..
Lakini mawasiliano yakazidi kuwa hafifu zaidi.
Ukafika wakati nikamuuliza maendeleo na mipango ya ndoa na kama wamepanga lini wataanza kuishi pamoja?

JIBU LAKE NDILO HASA LILINIGUSA NA KUAMUA HAYA
Rafiki yangu huyu alinishtua aliponieleza kuwa walitengana na yule mchumba kwani walipokutana ughaibuni alimfanyia visa vingi vibaya mno..sitavitaja
Na alipotua nchini alimtumia ujumbe kuwa asimtafute tena.
Akiwa katika hali ya kutafakari yaliyompata na jinsi gani atasonga mbele...ndipo alianza mahusiano na jamaa flani aliyeanza kumnyemelea kitambo na muda mfupi akapata ujauzito.

Baada ya kupata ujauzito alimjulisha mhusika lakini hakuwa tayari kuukubali bali alimwambia autoe kwani yeye anafamilia lakini aligoma kuutoa na akajiapiza ataulea na kwa vile jamaa ameukataa hata jina litakuwa la upande wa familia yake yaani ubini wa baba.

Habari hii iliniumiza sana na niliwaza haya yafuatayo;
1. Kuwa huyu dada ataishi kwa sonono kubwa
wakati wa ujauzito na atamwathiri mtoto
akiwa tumboni...wazazi wanajua hili
2. Huyu atakayezaliwa hatakuwa na upendo
katika jamii na anaweza kuja kuwa na tabia
ya ajabu

MAAMUZI YANGU
1. Nikamwomba kama naweza kuwa baba wa
wa hiyari na apewe ubini wa jina langu
kama baba alikubali hili kwa mshangao
mkubwa sana
(Haya[emoji116]sijamshirikisha)
2. Nitamhudumia kipindi chote cha ujauzito
3. Nitamfanya mwenye furaha ili kulinda afya
mama na ya mtoto atakaye zaliwa
4. Baada ya mtoto kukua yeye yuko huru kuwa
na maisha yake bila mimi kumwingilia uhuru
wake
5. Nitampa mtoto kiwanja na kumjengea kadri Mungu atakaponiweka hai na kunibariki, ili apate malazi na malezi bora.

Uamuzi huu nimeufanya mwenyewe japo sipangi kuishi na mtoto isipokuwa kumsapoti kimalezi tu.

Baada ya kukubaliana naye hasa kuhusu mtoto kuitwa kwa jina langu kama baba, alifurahi sana kiasi cha kulia machozi na nikamwahidi kuwa siku chache zijazo atakuja mkoa nilipo apate mapumziko ya muda mfupi...sio nyumbani kwangu lakini.
Amemweleza mama yake mzazi na hajaamini kuwa kuna mtu anaweza kufanya maamuzi magumu kiasi hiki.

Pamoja na hayo sijamweleza kwa undani namna nilivyojipanga kumsapoti mtoto hasa kumpa eneo na kumjengea, hili nimebaki nalo nikiomba Mungu aniwezeshe kulitimiza.

Wapendwa wana jf, inaweza kuonekana kuwa uamuzi wangu ni wa kijinga sana lakini kwangu mimi nitaona fahari kubwa kama hili litafaniniwa kwani;
Sisi wanaume tunapaswa kuwa chemichemi ya furaha ya wake zetu, mama, watoto na dada zetu lakini kinyume chake tumekuwa ni chanzo cha machozi.

Tujitahidi sana kuwafanya watu kuwa na furaha badala ya machozi.
Muwe na wakati mwema wote.

Alipoenda kwa jamaa yake nani alizingua demu au mwanaume? kama demu alizingua basi pakaa mikosi
 
Uamuzi huu najua sio wa kawaida, niko tayari kwa changamoto zote siogopi, ili nitimize amani ya moyo wangu.
Kuna mambo ni vigumu kueleweka na jamii
Yaani huogopi kuvunja familia yako kwa sababu ya uzinzi? Au sijaelewa
 
Back
Top Bottom