Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

"Uanaume" na "Uvulana" ni utofauti mkubwa sana kimaamuzi , ni kama mbingu na nchi mkuu.
 
Hili nitaliweka sawa na baadhi ya mambo yataenda kisheria , kutakuwa na ufafanuzi wa kina wa badhi ya vipengele vinavyoweza kuleta utata baadae.
Pili anaishi mbali sana na ninakoishi hivyo kuna ka ugumu kujulikana
Ukianza kuficha vitu sababu ya umbali utakuja kuharibu kila kitu na wema wako ukakuletea balaa kwenye familia yako ya sasa na mtu wako wa sasa.

Usidhani binadamu wote wema, wana huruma au wana shukrani kama wewe. Huyo mtoto wa kuasili anaweza kuja kudai mali unazochuma na mtu wako wa sasa ukija kufa.
Wengine hawatajali wewe ulijitolea tu kwa huruma zako, hujui damu anayobeba huyo mtoto toka kwa biological father ina ukatili, tamaa na uovu kiasi gani. Kuna kurithi tabia za ajabu na za kikatili.

Fanya ulivyopanga lakini lazima uweke sawa kisheria na mkeo ajue kila kitu, usifiche jambo.
Uongo ni dhambi ambayo itafuta wema wako.
 
Asante kwa ushauri.
Nimegusia kuwa nitaweka mambo sawa kisheria
 
Mkuu umetoa ushauri mzuri sana na hii jamaa inaonekana Amempenda demu kwa muda tu maana hana mpango wa Kumuoaa...[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Genye zitaishaa tuuu ataamka toka usingizinii
Yani wewe, Extrovert na mimi ni wahenga pekee tuliobakia karne hii kuonesha uanaume kiuhalisia bila ya unafki.
 
Asante kwa ushauri.
Nimegusia kuwa nitaweka mambo sawa kisheria
" Pili anaishi mbali sana na ninakoishi hivyo kuna ka ugumu kujulikana " kauli yako hiindio imenistua nikasema huyu hajui binadamu siyo milima?
Umbali haiwezi kuwa hakikisho la mkeo kutojua, kama ni wema kwanini ufiche?
 
Mkuu! Tofautisha plan na ushuhuda!! Kwa maamuzi yako ulitakiwa uandike kama ushuhuda sio plan. Mie nakuomba utanipa mrejesho baada ya mtoto kuacha ziwa!!!
 
" Pili anaishi mbali sana na ninakoishi hivyo kuna ka ugumu kujulikana " kauli yako hiindio imenistua nikasema huyu hajui binadamu siyo milima?
Umbali haiwezi kuwa hakikisho la mkeo kutojua, kama ni wema kwanini ufiche?
Mkuu hili la kuweka wazi linahitaji timing, liko kwenye process lkn sitalikimbiza ...unajua madhara yake
 
Rikiboy, wewe bado mvulana kwa ufahamu ulio nao.
Age yangu na uzoefu wangu nimemaliza mihemko ya kingono.
Nimevuka utoto huo.
Nina ushawishi kwa mwansmke yeyote nimtakaye na sina haja ya kutumia hila hii
Mkuu unajua humu tuko wanaume wa rika nyingi nyingi na hizi scenario zishatupata ila ktk kudeal nazo ndo tunatofautiana. Mimi najua wewe ni mwerevu na umeleta hii mada upate maoni ya wadau kabla hujatekeleza mipango yako kisheria kama usemavyo. Tuendelee lakini majibu ya 'Wajumbe' yapo wazi.
 
Unajua hakuna ukomo wa maarifa, niliandika hapo juu kuwa ushauri wa kuboresha unahitajika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…