Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Sio kweli kwamba umeamua kumsaidia kuulea ujauzito na mtoto,na kuwa baba wa mtoto kwa hiari kama ulivyosema,ila kuna (mhemko-sijapata neno zuri kwenye hili badala yake) na umeenda nalo speed bila kulifikiria kiundani. Kuna uwezekano wa kujutia uamuzi wako baadae. (Japo sikupingi kwa uamuzi wako). Hasa hasa ninachokiona hapo uko mapenzini kwa huyo dada,mpaka umeenda speed kwenye maamuzi mazito kama hayo. Muda mwingine kwa sasa unaweza ukafikiria ni huruma imekujia lakini ni hulka ya mapenzi yamuingiapo mtu,anaweza akaamua lolote ili kuonyesha kama hali ya kujali. Hasa nafikiri ni kufuatana na umri wako na kipato ulichonacho. Angalizo mwanamke ni kiumbe kigeugeu,lazima uje kujuta baadae. Kwa hadithi yako tu wewe amekuruka katikati yao hao wapenzi,yaani yuko kwenye mahusiano,akaingia tena kwako kwenye mahusiano,akamfuata ughaibuni,amerudi mawasiriano yapo na wewe,lakini akakushit akapigwa mimba na mwingine,tena akarudi kwako. Si bure kuna kitu kinakusumbua. Jitulize. Na ingekuwa vizuri sana ungekuja hapa kupata ushauri kabla hujamwambia chochote ningekushauri achana na huyo demu kabisa. Wewe amekufanya kivuli chake tu wakati wa jua kali.
"Uanaume" na "Uvulana" ni utofauti mkubwa sana kimaamuzi , ni kama mbingu na nchi mkuu.
 
Hili nitaliweka sawa na baadhi ya mambo yataenda kisheria , kutakuwa na ufafanuzi wa kina wa badhi ya vipengele vinavyoweza kuleta utata baadae.
Pili anaishi mbali sana na ninakoishi hivyo kuna ka ugumu kujulikana
Ukianza kuficha vitu sababu ya umbali utakuja kuharibu kila kitu na wema wako ukakuletea balaa kwenye familia yako ya sasa na mtu wako wa sasa.

Usidhani binadamu wote wema, wana huruma au wana shukrani kama wewe. Huyo mtoto wa kuasili anaweza kuja kudai mali unazochuma na mtu wako wa sasa ukija kufa.
Wengine hawatajali wewe ulijitolea tu kwa huruma zako, hujui damu anayobeba huyo mtoto toka kwa biological father ina ukatili, tamaa na uovu kiasi gani. Kuna kurithi tabia za ajabu na za kikatili.

Fanya ulivyopanga lakini lazima uweke sawa kisheria na mkeo ajue kila kitu, usifiche jambo.
Uongo ni dhambi ambayo itafuta wema wako.
 
Ukianza kuficha vitu sababu ya umbali utakuja kuharibu kila kitu na wema wako ukakuletea balaa kwenye familia yako ya sasa na mtu wako wa sasa.

Usidhani binadamu wote wema, wana huruma au wana shukrani kama wewe. Huyo mtoto wa kuasili anaweza kuja kudai mali unazochuma na mtu wako wa sasa ukija kufa.
Wengine hawatajali wewe ulijitolea tu kwa huruma zako, hujui damu anayobeba huyo mtoto toka kwa biological father ina ukatili, tamaa na uovu kiasi gani. Kuna kurithi tabia za ajabu na za kikatili.

Fanya ulivyopanga lakini lazima uweke sawa kisheria na mkeo ajue kila kitu, usifiche jambo.
Uongo ni dhambi ambayo itafuta wema wako.
Asante kwa ushauri.
Nimegusia kuwa nitaweka mambo sawa kisheria
 
Mkuu umetoa ushauri mzuri sana na hii jamaa inaonekana Amempenda demu kwa muda tu maana hana mpango wa Kumuoaa...[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Genye zitaishaa tuuu ataamka toka usingizinii
Yani wewe, Extrovert na mimi ni wahenga pekee tuliobakia karne hii kuonesha uanaume kiuhalisia bila ya unafki.
 
Asante kwa ushauri.
Nimegusia kuwa nitaweka mambo sawa kisheria
" Pili anaishi mbali sana na ninakoishi hivyo kuna ka ugumu kujulikana " kauli yako hiindio imenistua nikasema huyu hajui binadamu siyo milima?
Umbali haiwezi kuwa hakikisho la mkeo kutojua, kama ni wema kwanini ufiche?
 
NI MAAMUZI MAGUMU LAKINI YAMETOKA MOYONI

Wapendwa wana jukwa hili la mahusiano, mapenzi na urafiki ninawasalimu nyote.

Kama habari ya awali inavyosemaka kuwa nimechukua uamuzi mgumu wa kuwa baba mtarajiwa wa mtoto mtarajiwa wa rafiki yangu kwa hiyari na kwa kupenda mwenyewe kwa sababu nitakazo zieleza hapa chini, lakini kabla ya hizo sababu naomba nitoe ufafanuzi wa urafiki wetu.

Kuna dada mmoja tulikutana ofisi flani ya serikali, ni dada flani mpole kiasi na mcheshi kiaina.
Kwa muda mfupi sana nilivutiwa naye na ikafikia hatua ya kubadilishana naye namba za simu.

Zoezi la huduma lilienda vyema kwa yeye kufanya koneksheni na mtumishi flani na tukafanikiwa kupata hiyo huduma (pass ya kusafiria kwa haraka)

Baada ya hapo hatukuwasiliana haraka japo nilipanga lazima nimtafute.
Ulifika wakati tukaanza kuwasiliana hapa na pale
Na ukafika wakati nikawa nachomekea viutani kuwa ninamhitaji awe rafiki yangu.

Baada ya muda mrefu tulifanikiwa kuwa marafiki hatimaye tukaanza kushirikiana....hapa wakubwa mmeelewa.
Jambo nililompenda zaidi ni mwelewa na mwenye misimamo yake mizuri.
Tuliwekana wazi kuhusu mahusiano yetu, kwake yeye mpenzi wake alikuwa ni raia wa kigeni na anaishi huko kwao huja mara chache hivyo alikuwa anajiandaa kwenda kumtembelea...na walikuwa wamepanga kuoana.

Nini kilitokea kati yao???

Uliwadia wakati wa kusafiri alinijulisha nami nilimpa nafasi ya kuwa mbali naye kimawasiliano ili ajiweke sawa na akili yake iwaze juu ya mpenzi wake.
Alifanikiwa kwenda na kurudi.
Baada ya kurudi mawasiliano yetu yalikuwa hafifu kwani nilikuwa tight sana na kazi.


Baada ya miezi kama mitatu na nusu, tuliwasiliana na kupiga stori nyingi na mwishowe akanijulisha ni mjamzito.
Nikampa hongera zake..
Lakini mawasiliano yakazidi kuwa hafifu zaidi.
Ukafika wakati nikamuuliza maendeleo na mipango ya ndoa na kama wamepanga lini wataanza kuishi pamoja?

JIBU LAKE NDILO HASA LILINIGUSA NA KUAMUA HAYA
Rafiki yangu huyu alinishtua aliponieleza kuwa walitengana na yule mchumba kwani walipokutana ughaibuni alimfanyia visa vingi vibaya mno..sitavitaja
Na alipotua nchini alimtumia ujumbe kuwa asimtafute tena.
Akiwa katika hali ya kutafakari yaliyompata na jinsi gani atasonga mbele...ndipo alianza mahusiano na jamaa flani aliyeanza kumnyemelea kitambo na muda mfupi akapata ujauzito.

Baada ya kupata ujauzito alimjulisha mhusika lakini hakuwa tayari kuukubali bali alimwambia autoe kwani yeye anafamilia lakini aligoma kuutoa na akajiapiza ataulea na kwa vile jamaa ameukataa hata jina litakuwa la upande wa familia yake yaani ubini wa baba.

Habari hii iliniumiza sana na niliwaza haya yafuatayo;
1. Kuwa huyu dada ataishi kwa sonono kubwa
wakati wa ujauzito na atamwathiri mtoto
akiwa tumboni...wazazi wanajua hili
2. Huyu atakayezaliwa hatakuwa na upendo
katika jamii na anaweza kuja kuwa na tabia
ya ajabu

MAAMUZI YANGU
1. Nikamwomba kama naweza kuwa baba wa
wa hiyari na apewe ubini wa jina langu
kama baba alikubali hili kwa mshangao
mkubwa sana
(Haya[emoji116]sijamshirikisha)
2. Nitamhudumia kipindi chote cha ujauzito
3. Nitamfanya mwenye furaha ili kulinda afya
mama na ya mtoto atakaye zaliwa
4. Baada ya mtoto kukua yeye yuko huru kuwa
na maisha yake bila mimi kumwingilia uhuru
wake
5. Nitampa mtoto kiwanja na kumjengea kadri Mungu atakaponiweka hai na kunibariki, ili apate malazi na malezi bora.

Uamuzi huu nimeufanya mwenyewe japo sipangi kuishi na mtoto isipokuwa kumsapoti kimalezi tu.

Baada ya kukubaliana naye hasa kuhusu mtoto kuitwa kwa jina langu kama baba, alifurahi sana kiasi cha kulia machozi na nikamwahidi kuwa siku chache zijazo atakuja mkoa nilipo apate mapumziko ya muda mfupi...sio nyumbani kwangu lakini.
Amemweleza mama yake mzazi na hajaamini kuwa kuna mtu anaweza kufanya maamuzi magumu kiasi hiki.

Pamoja na hayo sijamweleza kwa undani namna nilivyojipanga kumsapoti mtoto hasa kumpa eneo na kumjengea, hili nimebaki nalo nikiomba Mungu aniwezeshe kulitimiza.

Wapendwa wana jf, inaweza kuonekana kuwa uamuzi wangu ni wa kijinga sana lakini kwangu mimi nitaona fahari kubwa kama hili litafaniniwa kwani;
Sisi wanaume tunapaswa kuwa chemichemi ya furaha ya wake zetu, mama, watoto na dada zetu lakini kinyume chake tumekuwa ni chanzo cha machozi.

Tujitahidi sana kuwafanya watu kuwa na furaha badala ya machozi.
Muwe na wakati mwema wote.
Mkuu! Tofautisha plan na ushuhuda!! Kwa maamuzi yako ulitakiwa uandike kama ushuhuda sio plan. Mie nakuomba utanipa mrejesho baada ya mtoto kuacha ziwa!!!
 
" Pili anaishi mbali sana na ninakoishi hivyo kuna ka ugumu kujulikana " kauli yako hiindio imenistua nikasema huyu hajui binadamu siyo milima?
Umbali haiwezi kuwa hakikisho la mkeo kutojua, kama ni wema kwanini ufiche?
Mkuu hili la kuweka wazi linahitaji timing, liko kwenye process lkn sitalikimbiza ...unajua madhara yake
 
Rikiboy, wewe bado mvulana kwa ufahamu ulio nao.
Age yangu na uzoefu wangu nimemaliza mihemko ya kingono.
Nimevuka utoto huo.
Nina ushawishi kwa mwansmke yeyote nimtakaye na sina haja ya kutumia hila hii
Mkuu unajua humu tuko wanaume wa rika nyingi nyingi na hizi scenario zishatupata ila ktk kudeal nazo ndo tunatofautiana. Mimi najua wewe ni mwerevu na umeleta hii mada upate maoni ya wadau kabla hujatekeleza mipango yako kisheria kama usemavyo. Tuendelee lakini majibu ya 'Wajumbe' yapo wazi.
 
Mkuu unajua humu tuko wanaume wa rika nyingi nyingi na hizi scenario zishatupata ila ktk kudeal nazo ndo tunatofautiana. Mimi najua wewe ni mwerevu na umeleta hii mada upate maoni ya wadau kabla hujatekeleza mipango yako kisheria kama usemavyo. Tuendelee lakini majibu ya 'Wajumbe' yapo wazi.
Unajua hakuna ukomo wa maarifa, niliandika hapo juu kuwa ushauri wa kuboresha unahitajika
 
Back
Top Bottom