Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Hongera
NI MAAMUZI MAGUMU LAKINI YAMETOKA MOYONI

Wapendwa wana jukwa hili la mahusiano, mapenzi na urafiki ninawasalimu nyote.

Kama habari ya awali inavyosemaka kuwa nimechukua uamuzi mgumu wa kuwa baba mtarajiwa wa mtoto mtarajiwa wa rafiki yangu kwa hiyari na kwa kupenda mwenyewe kwa sababu nitakazo zieleza hapa chini, lakini kabla ya hizo sababu naomba nitoe ufafanuzi wa urafiki wetu.

Kuna dada mmoja tulikutana ofisi flani ya serikali, ni dada flani mpole kiasi na mcheshi kiaina.
Kwa muda mfupi sana nilivutiwa naye na ikafikia hatua ya kubadilishana naye namba za simu.

Zoezi la huduma lilienda vyema kwa yeye kufanya koneksheni na mtumishi flani na tukafanikiwa kupata hiyo huduma (pass ya kusafiria kwa haraka)

Baada ya hapo hatukuwasiliana haraka japo nilipanga lazima nimtafute.
Ulifika wakati tukaanza kuwasiliana hapa na pale
Na ukafika wakati nikawa nachomekea viutani kuwa ninamhitaji awe rafiki yangu.

Baada ya muda mrefu tulifanikiwa kuwa marafiki hatimaye tukaanza kushirikiana....hapa wakubwa mmeelewa.
Jambo nililompenda zaidi ni mwelewa na mwenye misimamo yake mizuri.
Tuliwekana wazi kuhusu mahusiano yetu, kwake yeye mpenzi wake alikuwa ni raia wa kigeni na anaishi huko kwao huja mara chache hivyo alikuwa anajiandaa kwenda kumtembelea...na walikuwa wamepanga kuoana.

Nini kilitokea kati yao???

Uliwadia wakati wa kusafiri alinijulisha nami nilimpa nafasi ya kuwa mbali naye kimawasiliano ili ajiweke sawa na akili yake iwaze juu ya mpenzi wake.
Alifanikiwa kwenda na kurudi.
Baada ya kurudi mawasiliano yetu yalikuwa hafifu kwani nilikuwa tight sana na kazi.

Baada ya miezi kama mitatu na nusu, tuliwasiliana na kupiga stori nyingi na mwishowe akanijulisha ni mjamzito.
Nikampa hongera zake..
Lakini mawasiliano yakazidi kuwa hafifu zaidi.
Ukafika wakati nikamuuliza maendeleo na mipango ya ndoa na kama wamepanga lini wataanza kuishi pamoja?

JIBU LAKE NDILO HASA LILINIGUSA NA KUAMUA HAYA
Rafiki yangu huyu alinishtua aliponieleza kuwa walitengana na yule mchumba kwani walipokutana ughaibuni alimfanyia visa vingi vibaya mno..sitavitaja
Na alipotua nchini alimtumia ujumbe kuwa asimtafute tena.
Akiwa katika hali ya kutafakari yaliyompata na jinsi gani atasonga mbele...ndipo alianza mahusiano na jamaa flani aliyeanza kumnyemelea kitambo na muda mfupi akapata ujauzito.

Baada ya kupata ujauzito alimjulisha mhusika lakini hakuwa tayari kuukubali bali alimwambia autoe kwani yeye anafamilia lakini aligoma kuutoa na akajiapiza ataulea na kwa vile jamaa ameukataa hata jina litakuwa la upande wa familia yake yaani ubini wa baba.

Habari hii iliniumiza sana na niliwaza haya yafuatayo;
1. Kuwa huyu dada ataishi kwa sonono kubwa
wakati wa ujauzito na atamwathiri mtoto
akiwa tumboni...wazazi wanajua hili
2. Huyu atakayezaliwa hatakuwa na upendo
katika jamii na anaweza kuja kuwa na tabia
ya ajabu

MAAMUZI YANGU
1. Nikamwomba kama naweza kuwa baba wa
wa hiyari na apewe ubini wa jina langu
kama baba alikubali hili kwa mshangao
mkubwa sana
(Haya[emoji116]sijamshirikisha)
2. Nitamhudumia kipindi chote cha ujauzito
3. Nitamfanya mwenye furaha ili kulinda afya
mama na ya mtoto atakaye zaliwa
4. Baada ya mtoto kukua yeye yuko huru kuwa
na maisha yake bila mimi kumwingilia uhuru
wake
5. Nitampa mtoto kiwanja na kumjengea kadri Mungu atakaponiweka hai na kunibariki, ili apate malazi na malezi bora.

Uamuzi huu nimeufanya mwenyewe japo sipangi kuishi na mtoto isipokuwa kumsapoti kimalezi tu.

Baada ya kukubaliana naye hasa kuhusu mtoto kuitwa kwa jina langu kama baba, alifurahi sana kiasi cha kulia machozi na nikamwahidi kuwa siku chache zijazo atakuja mkoa nilipo apate mapumziko ya muda mfupi...sio nyumbani kwangu lakini.
Amemweleza mama yake mzazi na hajaamini kuwa kuna mtu anaweza kufanya maamuzi magumu kiasi hiki.

Pamoja na hayo sijamweleza kwa undani namna nilivyojipanga kumsapoti mtoto hasa kumpa eneo na kumjengea, hili nimebaki nalo nikiomba Mungu aniwezeshe kulitimiza.

Wapendwa wana jf, inaweza kuonekana kuwa uamuzi wangu ni wa kijinga sana lakini kwangu mimi nitaona fahari kubwa kama hili litafaniniwa kwani;
Sisi wanaume tunapaswa kuwa chemichemi ya furaha ya wake zetu, mama, watoto na dada zetu lakini kinyume chake tumekuwa ni chanzo cha machozi.

Tujitahidi sana kuwafanya watu kuwa na furaha badala ya machozi.
Muwe na wakati mwema wote.
Ila naona tu unataka papuchi ya bure sababu mwenye papuchi kwa sasa anajitahidi kutafuta furaha.

Haya uloandika uwezekano wa kutokuyafanya ni mkubwa sana yaan 99.9%.huku wakufanya ni 0.1 %
 
" Pili anaishi mbali sana na ninakoishi hivyo kuna ka ugumu kujulikana " kauli yako hiindio imenistua nikasema huyu hajui binadamu siyo milima?
Umbali haiwezi kuwa hakikisho la mkeo kutojua, kama ni wema kwanini ufiche?
Mkuu,
Wako ktk sexual relationship. Mkewe na jamaa akijua kuhusu mtoto atajua kuhusu sexual relationship...women have basic instincts ktk kutambua hizo mambo. Ndiyo maana ni siri. Hata kukutana ni hotelini hapa jamaa atasex naye kisha kila mtu anarudi kwake.

My take
Demu ni caliber ya tofauti na mjumbe wetu kila yupo unstable emotionally ndiyo maana anakubali kila kitu for now. Huyo Dada akitoka leba tena baada ya miaka mitatu kipindi hiko mtoto kalipiwa ada ya boarding baby class tutarajie ID mpya na Uzi wa kulalamika
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]watabiri bhana hamuwazagi positive hata siku moja.
Nimejaribu kusapoti jamii mara kadhaa.
Nimewahi sapoti mama mmoja wakati wa uzazi mwanzo mwisho hadi alipoweza kujitegemea kibiashara...alikimbiwa na mume na msaada ulikuwa unapitia mtu mwingine na hakujua anayemsapoti hadi baadae sana.
...Nimesapoti mabinti 2 kusoma hadi chuo kikuu bila kutaka hata ukaribu bali kulipa ada zao tu tena nimeanza nikiwa kijana mdogo.
Katika hili sina wasiwasi ninachoomba ni afya njema.
Sifungwi na sijaahidi kufanya makubwa kupita uwezo wangu bali sawa na uwezo atakao nipa Mungu.
 
Basi busara jamaa amsaidie malezi tu huyo mwanamke na hiyo nyumba na mengine lakini asimpe mtoto jina lake na mke wa huyu mjumbe asijue kitu kuhusu hili sakata lote.
 
Basi busara jamaa amsaidie malezi tu huyo mwanamke na hiyo nyumba na mengine lakini asimpe mtoto jina lake na mke wa huyu mjumbe asijue kitu kuhusu hili sakata lote.
Ndiyo tunamwambia hapa kuwa afanye kama msaada isiwe kisheria. Ikiwa kisheria hata ikiwa kuna umbali gani huyo atakuwa mtoto wake mwenye haki sawa na wa kuwazaa ( kama anao) hii italeta shida ktk familia yake hapo mbeleni.

Pia sijafahamu hebu nisaidie kisheria ukiasili mtoto kuna uwezekano wa kubatilisha kisheria?
 
Umekomenti kutokana na tabia yako mkuu, hujaacha tu?
Tabia gan mkuu??.......

Kwamba sasa utalea mimba ??.

Akizaa utalea na kufanya kedekede kwa ajili ya mtoto...???

Alafu kisha [emoji116]
kwamba akishazaa utamwacha huru na maisha yake yaan uchaguzi ???...

Maswali...

1--Wewe umeoa ?? Una mtoto au watoto ??.

2—Wakati huo wote ,utakua unakula papuchi yake au hapana ? Ukila utaila kama nani kwake ???.

3---Saizi unataka akutembelee kupunguza stress ulipo.. Huyu Mama anamimba, Je utamla?? Na kama utamla, huonei huruma kiumbe chake ???.

4--Je usipomla, utaendelea kumhudumia nakumpa kila hitaj sawa nauwezo wako hata km papuchi hakupi???

[emoji117]Ndio maana hayo mengine hujawambia, sababu unajua kabisa Ahadi inamaana gani.

[emoji117]Umemwambia yakumwambia sababh utekelezaji wa ulokwisha mwambia ni wa maneno ambayo yatabakia kuishi moyon mwake kihisia.

Embu fanya hili....

Kabla hajaja kukutembeleaa, embu fanya kitu kimoja wapo ukiweke kwa matendo kwanzaa....

Achana na maneno ya " mie nitakua baba wa hiyari , pakuanzia naomba uje upoze mawazo huku niliko , usijali mtoto nitamleaaa, ataitwa kwa jina languuu "....
 
Jamaa sio tu alizingua bali alimdhalilisha sana
Kwanza ubarikiwe lakini kuwa makini sana na maamuzi yako usije kuja kujutia baadae ameachwa na wanaume wawili hujui walipendana vipi na sababu gani wameshijdwa kupendana mara nyingi wadada ni wanyooshaji wazuri wa vidole hivyo usiamini maneno yake 100%. Fanya vyoooote wachana na jina la mtoto, usije kuja kumlaumu baadae bila sababu
 
Kwa kitendo hicho obviously itakugarimu hapo badaye..ulipaswa kuomba ushauri kabla ya kutekeleza ,,uko na confident sana lakn amini kuna watu wanauelewa mkubwa na experience katika haya maswala
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]watabiri bhana hamuwazagi positive hata siku moja.
Nimejaribu kusapoti jamii mara kadhaa.
Nimewahi sapoti mama mmoja wakati wa uzazi mwanzo mwisho hadi alipoweza kujitegemea kibiashara...alikimbiwa na mume na msaada ulikuwa unapitia mtu mwingine na hakujua anayemsapoti hadi baadae sana.
...Nimesapoti mabinti 2 kusoma hadi chuo kikuu bila kutaka hata ukaribu bali kulipa ada zao tu tena nimeanza nikiwa kijana mdogo.
Katika hili sina wasiwasi ninachoomba ni afya njema.
Sifungwi na sijaahidi kufanya makubwa kupita uwezo wangu bali sawa na uwezo atakao nipa Mungu.
Wanaume lazima tupeane ABCs wewe si wa kwanza wala wa mwisho ktk scenario hiyo
 
Ukianza kuficha vitu sababu ya umbali utakuja kuharibu kila kitu na wema wako ukakuletea balaa kwenye familia yako ya sasa na mtu wako wa sasa.

Usidhani binadamu wote wema, wana huruma au wana shukrani kama wewe. Huyo mtoto wa kuasili anaweza kuja kudai mali unazochuma na mtu wako wa sasa ukija kufa.
Wengine hawatajali wewe ulijitolea tu kwa huruma zako, hujui damu anayobeba huyo mtoto toka kwa biological father ina ukatili, tamaa na uovu kiasi gani. Kuna kurithi tabia za ajabu na za kikatili.

Fanya ulivyopanga lakini lazima uweke sawa kisheria na mkeo ajue kila kitu, usifiche jambo.
Uongo ni dhambi ambayo itafuta wema wako.
Mimi ninavyojua tabia hairithiwi, tabia ya mtu ni matokeo ya malezi aliyopewa na si vinginevyo
 
Mimi ninavyojua tabia hairithiwi, tabia ya mtu ni matokeo ya malezi aliyopewa na si vinginevyo
Upo sahihi, lakini kuna vitu ni kama hardcoded genetically.
Hii nadharia yangu ni layman thinking "Huyu mtoto kachukua tabia za baba yake".
Hili jambo lina ukweli flani maana my son amechukua tabia zangu flani kupita maelezo, tangu alipozaliwa hata mwezi hajafikisha alionesha hizo tabia.
 
Hongera mkuu
Ila wanawake Hawa!!!!!!!!!
Atakuja akuone mavi nakuambia
Mkuu bado huwa unategemea shukrani.
Niliwahi kumfadhili rafiki yangu mwanaume kiasi cha 10m na mkewe 2m, walikuwa wanapitia kipindi kigumu sana hata petrol walikuwa wanashindwa kuweka japo wana gari 3.
Basi nami kilikuja kipindi changu cha shida, mkataba wa kazi uliisha kwa kampuni kufilisika.
Walilijua hilo...kuna siku nilimpigia simu akajua labda naomba pesa...alijifanya hanifahamu kabisa.
Ukitenda wema kimbia au sahau kabisa...ukisubiri shukrani umekwisha
 
Back
Top Bottom