jaap
JF-Expert Member
- Dec 25, 2018
- 4,888
- 6,459
Mkuu atatokea Raisi mwingine ataivunjilia mbali mikata ya nyinya damu.Maamuzi ya Samia yatatugharimu zaidi ya miaka 100 ijayo kwa kuuza bandari yetu kwa waarabu wajomba zake.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu atatokea Raisi mwingine ataivunjilia mbali mikata ya nyinya damu.Maamuzi ya Samia yatatugharimu zaidi ya miaka 100 ijayo kwa kuuza bandari yetu kwa waarabu wajomba zake.
Tukana tu afu mtuingize tena kwenye DPW.Mikataba ya kijinga kabisa.Yule mwehu pungu one eti kuna wehu wanamlilia kila saa.
Jambo kidogo tu utawasikia angekuwa pungu one Jiwe, tunammiss mwehu Jiwe.
Daah
Kwani unasema tulipishwe mimi nilikuepo wakati mnachukua 10% nakuanguka sahihi?Kwanza huo mkataba wa ovyo hakuingia Magufuli, pili bora tulipishwe hiyo amount kuliko madini kuchotwa milele. Kulipishwa fidia sio mara zote ni hasara mfano hatujui investment iliyokwishafanyika.
Hizo tunazolipa ni gharama za uzembe wa mikataba ya ovyo. Acha tule hasara kwa ujinga wetu. Mbaya zaidi usikute kuna Watanzania "wazito" walikuwa na shares mlango wa nyuma.
Imagine Nachingwea iko incorporated huko UK! Michongo tu ndio maana mzilankende akaona aifyatue miradi irudi kwa umma kwanza.
Kasome ujumbe vizuri uelewe.Kwani unasema tulipishwe mimi nilikuepo wakati mnachukua 10% nakuanguka sahihi?
Kila mmoja anaona akiushtaki serikali wanashinda ,lazima wajitokeze wengineMaamuzi ya kijasiri ya Magufuli wacha yaigharimu nchi hayo mapesa, hatuwezi kukaa na mikataba ya hovyo yenye unyonyaji kwa taifa, huku walafi wachache walioingia wakifaidi 10% halafu nije kumlaumu Magufuli aliyeivunja, Never. Wacha tudaiwe lakini heshima yetu iwepo.
Kwangu Magufuli kwenye hili ni genius, naamini iko siku, hata huu wa Samia na DPW yake nao utavunjwa, wakati huo Samia akiwa amelala kaburini na laana.
Sawa mgodi ukirudishwa kwa umma nani alipe hizo hii amount? Je unaakika gani kama huu godi hatapewa mtu mwingine kwa mkataba mbovu zaidi ya huu uliovunjwa?Kwanza huo mkataba wa ovyo hakuingia Magufuli, pili bora tulipishwe hiyo amount kuliko madini kuchotwa milele. Kulipishwa fidia sio mara zote ni hasara mfano hatujui investment iliyokwishafanyika.
Hizo tunazolipa ni gharama za uzembe wa mikataba ya ovyo. Acha tule hasara kwa ujinga wetu. Mbaya zaidi usikute kuna Watanzania "wazito" walikuwa na shares mlango wa nyuma.
Imagine Nachingwea Nickel ltd iko incorporated huko UK! Michongo tu ndio maana mzilankende akaona aifyatue miradi irudi kwa umma kwanza.
Ni muhimu kutambua kuwa Mkataba wa Tume ya Kimataifa ya Kusuluhisha Migogoro ya Uwekezaji umepitishwa na nchi wanachama 158 wa Benki ya Dunia, ikiwa ni pamoja na Tanzania. Hii inamaanisha kuwa adhabu yoyote iliyotolewa na tume hiyo inaweza kutekelezwa katika nchi hizo kama uamuzi wa mahakama zao wenyewe.
Anazo😀😀Huna akili
Kweli huna akili lisu hakuwa na uwezo wa kupata kura nyingi dhidi ya Magufuli.Magufuli alipora uchaguzi akajaza wabunge wa CCM kwa kisingizio kuwa ni wazalendo. Mbona hatuoni hao wazalendo wakifanya uzalendo wao? Kibaya zaidi ndio hao wanapelekewa bill ya kubadili hizo sheria walizotunga wenyewe.
Ameitia hasara nchi,kubwa sanaMaamuzi ya kijasiri ya Magufuli wacha yaigharimu nchi hayo mapesa, hatuwezi kukaa na mikataba ya hovyo yenye unyonyaji kwa taifa, huku walafi wachache walioingia wakifaidi 10% halafu nije kumlaumu Magufuli aliyeivunja, Never. Wacha tudaiwe lakini heshima yetu iwepo.
Deni la taifa lenyewe kila siku linaongezeka, tumeshazoea kuishi kwa madeni, wacha ibaki hivyo.
Kwangu Magufuli kwenye hili ni genius, naamini iko siku, hata huu wa Samia na DPW yake nao utavunjwa, wakati huo Samia akiwa amelala kaburini na laana.
Wakulaumiwa ni aliyevunja,sio aliyetengeneza.Wakulaumiwa ni Kikwete aliyeingia mikataba ya kipuuzi. Kama ambavyo tutamlaumu Samia kwa mikataba yake ya Dubai.
Magufuli alifanya kilichotakiwa kufanyika ili kuinusuru nchi. Akaleta na sheria mpya ya kulinda rasilimali zetu, tuanze upya, UPUMBAVU wa zamani usijirudie.
Inaumiza SANA SANA leo kuona upumbavu umerudi tena, na sheria inakwenda kubadilishwa ili kuhalalisha UPUMBAVU.
Wanaoitwa usalama wa taifa wapo wanashangaa shangaa tu, kiongozi wa nchi anadanhanywa na kundi la wahuni. Hayo maslahi ya nchi mnayoyalinda ni yapi hayo???
Hapa aliyevunja ndio kaharibu.Mtu mwenye kuipenda nchi yake lazima avunje mikataba yote ya kitumwa kama huu wa DP World akija Rais anayeipenda nchi yake lazima auvunje tu mkataba wa DP World.
Nafikiri sasa tuwetunavunja hii mikataba na tunawashughulikia wote walioingia mikataba hiyo mibovu hapo ndio tutakomesha ujinga wa kusaini mikataba mibovu.
Kwani yeye ndo kaingia mikataba vibovu kweli kuna watu hamna akili.Ameitia hasara nchi,kubwa sana
Aliyeingiza nchi hasara ni aliyeingia huo mkataba mbovu.tumia akiliHivi karibuni, Tume ya Kimataifa ya Kusuluhisha Migogoro ya Uwekezaji, ambayo ni sehemu ya Benki ya Dunia, imefunga usuluhishi dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tume hiyo imetoa adhabu yake, ikiamuru Tanzania kulipa fidia ya zaidi ya Dola za Marekani Milioni 109.5 sawa na takribani bilioni 266 za kitanzania (ikiwa ni pamoja na limbikizo la riba) kwa wadai. Adhabu hii inahusu madai ya uharibifu kutokana na kunyang'anywa kwa mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill kwa njia isiyo halali.
Indiana Resources Limited (ASX: IDA), ambayo ni mmiliki mkuu wa kampuni za Ntaka Nickel Holdings Ltd, Nachingwea UK Ltd, na Nachingwea Nickel Ltd, ambao kwa Pamoja ni "wadai", katika mgogoro huu, imetoa sasisho kuhusu tukio hili. Kwamba Indiana ndiye msimamizi wa miradi tajwa hapo juu ambayo shughuli zake ndio kiini cha mgogoro huu dhidi ya Tanzania.
Adhabu hiyo imetolewa baada ya jopo la usuluhishi kubaini kuwa Tanzania ilinyang'anya mradi huo kinyume cha sheria mnamo tarehe 10 Januari 2018, na hivyo kukiuka Mkataba wa Uwekezaji wa Kimataifa kati ya Uingereza na Tanzania. Hivyo basi, Tanzania imeamriwa kulipa fidia pamoja na hasara zingine, ikiwemo na malimbikizo ya riba kwa kiwango cha 2%. Riba hii ni juu ya kiwango cha msingi cha Dola za Marekani kuanzia tarehe ya kunyang'anywa miradi hadi tarehe ya malipo.
Katika maamuzi yake, Tume hii imeamua kuibebesha Tanzania gharama za usuluhishi, ikiwa ni pamoja na ada na gharama za Tume. Aidha, Tanzania imeamriwa pia kulipa gharama walizoingia wadai katika usuluhishi huo.
Katika taarifa yake kupitia mwenyekiti mtendaji ndugu Bronwyn Barnes, Indiana Resources Limited imeeleza furaha yake juu ya maamuzi haya. Imesisitiza kuwa kiasi cha adhabu kinathibitisha uwekezaji mkubwa ambao umepotea kutokana na kunyang'anywa kwa mradi huo na amewashukuru wanahisa ambao wamemsaidia katika kipindi chote cha usuluhishi.
Indiana sasa inakusudia kuanza mchakato wa kukazia hukumu hiyo. Ni muhimu kutambua kuwa Mkataba wa Tume ya Kimataifa ya Kusuluhisha Migogoro ya Uwekezaji umepitishwa na nchi wanachama 158 wa Benki ya Dunia, ikiwa ni pamoja na Tanzania. Hii inamaanisha kuwa adhabu yoyote iliyotolewa na tume hiyo inaweza kutekelezwa katika nchi hizo kama uamuzi wa mahakama zao wenyewe.
Kwa upande wake, Bronwyn Barnes ameahidi kuendelea kuwajulisha wanahisa kadri mchakato wa utekelezaji unavyoendelea.
Historia ya madai haya inaanzia tarehe 21 Aprili 2015, ambapo Tanzania ilitoa Leseni ya Kuhifadhi kwa Mradi huo. Hata hivyo, mnamo Julai 2017, Serikali ya Tanzania ilibadilisha Sheria ya Madini ya 2010 na kuondoa daraja la Leseni ya Kuhifadhi bila kutoa mbadala wake.
Kufikia tarehe 10 Januari 2018, Tanzania ilichapisha kanuni mpya za madini, zilizoweka bayana kuwa leseni za kuhifadhi hazitakuwepo tena na haki zote zilirejeshwa kwa Serikali. Indiana Resources Limited ilishiriki katika majadiliano na Serikali ya Tanzania kuanzia Januari 2018 hadi Desemba 2019, kujaribu kutatua suala la umiliki wa mradi huo. Hata hivyo, jitihada hizo hazikuzaa matunda na Serikali ya Tanzania ilifanya tangazo la mwaliko wa umma kwa zabuni ya pamoja kwa maendeleo ya maeneo yaliyokuwa chini ya leseni za kuhifadhi.
Maamuzi haya ya Tume ya usuluhishi ni muhimu sana kwa Indiana Resources Limited na wadai wengine, kwani inawakumbusha umuhimu wa kulinda na kuheshimu mikataba ya uwekezaji. Pia inatupa fundisho kuhusu jukumu letu la kuhakikisha kuwa haki za wawekezaji zinalindwa na kwamba serikali zinaheshimu mikataba iliyosainiwa.
Hii pia inatoa fursa kwa nchi yetu, Tanzania, kutathmini upya sera zake za uwekezaji na kuhakikisha kwamba inashirikiana vizuri na wawekezaji ili kuleta maendeleo endelevu ya uchumi wetu na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni.
Pia soma: Tanzania yashindwa kwenye kesi, yaamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 260
Wewe ndo huna akili aliyesababisha hasara ni aliyeingia mkataba mbovu.Huna akili
Usikute hata hilo deni kuna asilimia za Watu. Mdai anasema mia, wengine wa dili wanamwambia sema mia tano. Ikilipwa yangu mia mbili ingine yako.Maamuzi ya kijasiri ya Magufuli wacha yaigharimu nchi hayo mapesa, hatuwezi kukaa na mikataba ya hovyo yenye unyonyaji kwa taifa, huku walafi wachache walioingia wakifaidi 10% halafu nije kumlaumu Magufuli aliyeivunja, Never. Wacha tudaiwe lakini heshima yetu iwepo.
Deni la taifa lenyewe kila siku linaongezeka, tumeshazoea kuishi kwa madeni, wacha ibaki hivyo.
Kwangu Magufuli kwenye hili ni genius, naamini iko siku, hata huu wa Samia na DPW yake nao utavunjwa, wakati huo Samia akiwa amelala kaburini na laana.