Maamuzi ya Hayati Magufuli yaigharimu Tanzania zaidi ya Bilioni 266

Tatizo Lako hufikirii inje ya box. . Magufuli ndiye aliyeingia Mkataba wa kifala Hivyo.?

Bora tulipe hizo pesa kuliko kuendelea kukamuliwa. Hata Bandari mkisaini kuna Mzalendo atatokea ataufyekelea mbali
Uamuzi wa kesi sio kuingia mkataba,uamuzi ni kuvunja mkataba ndio kosa.
 
Usalama wa nchi wanateuliwa kulinda wakubwa na sio maslahi ya nchi. Wanalazimishwa kufanya wasiyoyapenda ila kwa kua sheria ni hamna kukaidi amri ya mkuu wako, wao ni kutekeleza tu.

Muundo wa uongozi ni mbovu sana. Unaruhusu Watu kuchumia na kushuhudia matumbo yao na sio uma.
 
Mkiambiwa mtaje bei aliyouzia mnapiga kimya.
Wazushi tu nyie
Hii kesi imefunguliwa kuvunja mkataba,na uamuzi umetoka wa kuvunja mkataba.Hawa wehu wanamlaumu aliyeweka mkataba,wakati kesi ni kuvunja mkataba,aliyevunja ndio wa kulaumiwa.Maarifa kuwa nayo muhimu.
 
Mh. Tundu Antiphas Lissu aliposhauri namna nzuri ya kuachana na hao watu na hivyo kuepuka mambo kama haya aliitwa msaliti na kuambulia risasi 30 mwilini. Yapo maamuzi ya kijinga na matokeo yake ndio kama haya...mtaikumbuka MIGA na bado!
Shida ni kwamba alishauri katika namna ambayo siyo sahihi. Angefanya kwa usahihi angefungwa mkono na wengi, sio kuiba taarifa na kuzisema public katika namna yake ya kuwatisha na kuwaogofya watu
 
Tulipe tu, kama sisi kizazi hiki tumeshindwa kuvuna madini yetu kwa faida, tuwaachie vizazi vyetu watakuja kupata akili ya kuyavunja kwa faida.
 
Tukutane uchaguzi 2024 na 2025 tujue namna Magufuli atakavyowagharimu kwenye kura
 
Mh. Tundu Antiphas Lissu aliposhauri namna nzuri ya kuachana na hao watu na hivyo kuepuka mambo kama haya aliitwa msaliti na kuambulia risasi 30 mwilini. Yapo maamuzi ya kijinga na matokeo yake ndio kama haya...mtaikumbuka MIGA na bado!
Hivi sasa anajutia Uharakati wake na mazingira aliyotuwekea Watanzania wakati akiwakatia viuno Mabeberu.

Msaliti ni msaliti tu.
 
Kweli huna akili lisu hakuwa na uwezo wa kupata kura nyingi dhidi ya Magufuli.
Hakuna mwenye tatizo na kura nyingi, tulitaka kura halali basi. Hapo ndio ungejua ukweli wa kukubalika kwake against Lisu.
 
Ukiangalia uwezo wa wanasheria wa serikali hata huwezi kushangaa.
 
Naungana na wengi hapa. Maamuzi ya Hayati Raisi siyo yale yaliyoigharimu Serikali. Ni maamuzi ya wale walioingia mikataba Mibovu!
Wakati hiyo mikataba inaingiwa alikuwa kwenye baraza la mawaziri kimya akilinda cheo.
 
@dataz njoo na huku
 
Mikataba mibovu mfano mzuri huu wa dp utamsumbua sana rais ajaye
 
Wakati hiyo mikataba inaingiwa alikuwa kwenye baraza la mawaziri kimya akilinda cheo.
Kuhusu uwepo wake kwenye baraza la Mawaziri, hilo ni suala lingine.

Ila kuna la kujifunza hapa kuhusu mikataba mibovu na hususani mbinu dhalimu zinazotumika; Lugha, Sheria na rushwa zinazotumiwa na wawekezaji uchwara. Hayati alijaribu kurekebisha(kutokomeza) haya, na hakika alijua kulikuwa na gharama za kulipwa ikiwa pamoja na Fedha hizi.... itakuwa ni ulimbukeni kudai kwa namna yeyote ile, alikuwa hajui haya yatatokea! Na ni aibu kwa hawa waliopo, kufikia sehemu na kubadilisha sheria tena na kurudi kwenye hali ya kunyolewa-Kwani alijua fika, tija na manufaa ya kufanya hivyo ni mapana na marefu na makubwa kwa mustakabhali wa Nchi

Kuondoa Wananchi kutoka kwenye minyororo ya utumwa na unyonyaji na kujihakikishia Uhuru wa kujiamlia kisiasa na kiuchumi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…