Wanajf kuna jambo limenifanya niilete hii mada kwenu.
Kuna kaka alihitaji na alipendelea kuwa na watoto watatu, na walikubaliana na mkewe wawe na watoto watatu Mungu akiwajaalia.
Baada ya mkewe kujifungua mtoto wa pili akamwambia mumewe asingeweza kwenda leba tena(alijifungua kwa njia ya kawaida na hakukuwa na complications zozote).
Mume alihisi ni kwavile ametoka kujifungua ndio maana anasema hivyo, lakini baada ya miaka mi4 kupita bado msimamo wa mkewe ni uleule, amemwambia ikiwa ni lazima apate huyo mtoto wa tatu anamruhusu kwa roho safi tu akamtafute.
Naomba kuwauliza haswa wanandoa, maamuzi ya idadi ya watoto mnaohitaji kuwa nao huwa ni ya nani? And how if kila mmoja akawa na idadi yake ya watoto anaohitaji inayotofautiana na mwenzie?
Na wanawake utafanya nini ikiwa mumeo anahitaji idadi kubwa ya watoto tofauti na matakwa yako?