Maamuzi ya idadi ya watoto ni ya nani?

Maamuzi ya idadi ya watoto ni ya nani?

Wanajf kuna jambo limenifanya niilete hii mada kwenu.

Kuna kaka alihitaji na alipendelea kuwa na watoto watatu, na walikubaliana na mkewe wawe na watoto watatu Mungu akiwajaalia.
Baada ya mkewe kujifungua mtoto wa pili akamwambia mumewe asingeweza kwenda leba tena(alijifungua kwa njia ya kawaida na hakukuwa na complications zozote).

Mume alihisi ni kwavile ametoka kujifungua ndio maana anasema hivyo, lakini baada ya miaka mi4 kupita bado msimamo wa mkewe ni uleule, amemwambia ikiwa ni lazima apate huyo mtoto wa tatu anamruhusu kwa roho safi tu akamtafute.

Naomba kuwauliza haswa wanandoa, maamuzi ya idadi ya watoto mnaohitaji kuwa nao huwa ni ya nani? And how if kila mmoja akawa na idadi yake ya watoto anaohitaji inayotofautiana na mwenzie?

Na wanawake utafanya nini ikiwa mumeo anahitaji idadi kubwa ya watoto tofauti na matakwa yako?
Inategemea nani ni anatawala nyumba
 
Nini tena?? Bibi zetu walizaa mpaka 15. Madingi zetu wakaanza kulegeza, sasa na Sisi tukilegeza itafika kipindi mtatuambia tuzae mmoja tu.

8 please
Aisee ..
Utafananisha maisha ya enzi hizo na siku hizi? Mke awe hausiwaifu labda!
 
Hapana si niliona siku amekuambia.
Halafu hapo hapo akakutandika injili hadi ukamkimbia[emoji23][emoji23][emoji23]akabaki Don kagangamala weee na yeye yakamshinda.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni makubaliano ya wawili, huku wakiangalia vigezo kadhaa. Umri wao, uwezo wa kiuchumi, utayari wa kila mmoja na afya hasa ya mke.

Kuna wakati inabidi mmoja akubali kukubaliana na mwenzake katika baadhi ya mambo, kuna kupata na kukosa, so mmoja anaweza kupata katika idadi ya watoto, mwingine akapata katika issues zingine kama mahali pa kuishi/kujenga, nk.

Hivyo kwa maoni yangu sio lazima ukubaliane katika hiyo vita, utakubaliwa katika vita nyingine.
Oooh kumbe!!
 
Bi mdashi, usitake kunlisha maneno hapa. Kama wewe unataka kusema uislam ndio umesema tuwatawale wake zetu through dictatorship wewe sema tu.

cc: cute b
Atoto
Mimi sijasema hivyo infact ninachojua ni kwamba hakuna dini inayofundisha kwamba mwanaume anatakiwa amtawale mwanamke through dictatorship japo kuna watu (ambao ni waislam) waliwahi kuniambia kuwa katika uislam mwanamke hana sauti kabisa japo sikukubaliana nao ila ilibidi niwaamini tu kishingo upande sababu ni dini yao na mimi sheria za kiislam sizijui
 
Mkuu usifananishe wanawake wa kizungu na wanawake wa kibongo wanawake wengi wa kibongo hawana matunzo yaani waume zao wanataka watoto wengi ila hawako tayari au hawana uwezo wa kuwatunza wake zao mwanamke anahitaji matunzo
Kuna dada jirani yetu amefariki asilimia 90 yule mumewe alichangia mwanamke katoka kujifungua anamshindisha na vipiro vya ugali afya ilikuwa mbaya akawa wakijani usoni kwa kukosa rishe alifariki yule dada kaacha watoto 3😪.
 
Back
Top Bottom