liwaya
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 2,384
- 1,648
Duh well captured credit kwakoHii ndio taarifa iliyotufikia , kwamba leo Mke wa Mshitakiwa aliyeteswa kinyama komando Adam kasekwa leo atapanda kizimbani akiwa ni shahidi wa tatu wa upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa inayomkabili Freeman Mbowe na Wenzake watatu
Endelea kufuatilia
========
Saa 3 na Dakika 11 Tupo Chumba Cha Mahakama Tayari, Kwa Mawakili wa Utetezi wapo tayari Mahakamani ila Mshitaka bado wapo Nje
Jaji: ameshaingia Sasa Mahakamani
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021, Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire,Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe
Kesi inatajwa
Jaji: Habarini za Asubuhi, Tuendeleeni ni Siku Nyingine
Jaji: sawa
Wakili wa Serikali: naomba Radhi tumeingia wakati umeshaingia
Jaji: Wakili wa Serikali
Wakili wa Serikali: Kidando anatambulisha wenzake
Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulimanywa Majigo
Jaji: Utetezi
Kibatala: anatambulisha Wenzake
Advocate Peter Kibatala
Advocate Jonathan Mndeme
Advocate Fredrick Kiwhelo
Advocate John Malya
Advocate Sisty Aloyce
Advocate Alex Masaba
Advocate Idd Msawanga
Advocate Gaston Garubindi
Advocate Evaresta Kisanga
Advocate Faraj Mangula
Advocate Maria Mushi
Advocate Bonifasia Mapunda
Wakili Dickson Matata anaombewa Ruhusa Mdogo wake anafanyiwa Operesheni Hospitali ya Lugalo
Jaji: Wakili wa Serikali
Jaji: John Mallya
Wakili wa Serikali: Tumekuja kwa ajili ya kesi Ndogo ambapo Shahidi wa tatu yupo tayari kuendelea Kutoa Ushahidi wake
Mallya: Tunaye Shahidi, Na Shahidi yupo tayari kutoa Ushahidi
Shahidi: Mdada anatokea Nyuma kabisa ya Chumba Cha Mahakama anaenda Kizimbani
Jaji: Shahidi wa tatu upande wa Utetezi ambaye ameandaliwa Tafadhali anaweza Kuja
Jaji: anaandika Kidogo na Ukimya wa Mahakama
Jaji: Shahidi unaitwa nani
Jaji: Shahidi upo Mahakamani ondoa Hofu, nitakuuliza Majina yako na Nitakuapisha, Wakili wa Utetezi atakuongoza na Mawakili wengine watakuuliza Swali na Mawakili wa Serikali watakuuliza Maswali pia huna Haja ya Kuogopa, tupo hapa kutafuta Haki
Shahidi: Lilian Kibona
Dini Mkristo
Jaji: wakili Mallya endelea
Jaji: Liliani utachagua Kukaa au Kusimama,Hata Ukikaaa nitakuona
Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa Ukweli na Ukweli Mtupu , Mungu ni Saidie
Mallya: Shahidi Unaishi wapi
Shahidi: Chalinze Mkoa wa Pwani
Shahidi: Ramboni
Mallya: sehemu gani huko Chalinze,
Jaji: ni Mtaa.?
Mallya: Unaishi na nani..?
Shahidi: Ndiyo
Shahidi: Na mmewangu na Watoto ambaye kwa Sasa Mme wangu ameshikiliwa
Shahidi: Ndiyo
Jaji: ni Miongoni Mwa washitakiwa ??
Mallya: Mme wako anaitwa nani.?
Mallya: hapa kila nikiwa namuita Mshitakiwa wa Pili nitakuwa namaanisha pia ni yeye
]
Shahidi: ndiyo
Shahidi: Adamu Khalfani Kasekwa
Mallya: Ndoa Ya Kiserikali
Mallya: Mmeona lini 05 08 2016
Shahidi: Ndiyo
Shahidi: Palepale Chalinze
Mallya: Mlikuwa mnaishi wapi
Mallya: unaweza Kukumbuka Mmewako alikuwa anafanya kazi gani wakati huo
Mallya: alikuwa anafanya kazi gani Nyingine
Shahidi: Askari jeshi wa JWTZ kikosi cha 92 Ngerengere
Shahidi: alikuwa hana kazi Nyingine zaidi ya hiyo ya Serikali
Mallya: naruka nakuja 2020 Mme wako alikuwa anafanya kazi gani
Shahidi: alikuwa anafanya shughuli zake za Biashara
Mallya: Kabla ya Kwenda Moshi mlikuwana Hali gani kati yako na Mme wako
Mallya: Mwanzoni Mwa Mwezi wa Nane Mwaka 2020 unakumbuka Kilitokea Kitu gani kati yako na Mme wako
Shahidi: Mme wangu alikuwa Moshi, tulikuwa tunawasiliana naye Vizuri
Shahidi: Palikuwa na Mawasiliano
Shahidi: Rafiki yake Ling'wenya waliwasiliana kuwa kuna Kazi imepatikana Moshi
Mallya: kabla ajaenda Moshi kitu gani kilitokea
Shahidi: Hapana sikumbuki
Mallya: Unaweza Kukumbuka Siku na Saa ya hayo mawasiliano
Jaji: unasema palikiwa na Mawasiliano Kati ya Mme wako na Ling'wenya .?
Jaji: Ndiyo
Shahidi: Ndiyo Kwamba Ling'wenya alimpigia Simu kuwa kuna kazi Imepatikana Moshi
Mallya: Simu zilikuwa zinapigwa kati ya Ling'wenya na Mme wako wewe ulijuaje
Mallya: Jambo gani lilifanyika, kabla ya Mme wako kwenda Moshi
Mimi kama Mke nilimruhusu
Shahidi: Mimi Kama Mke wake alinishirikisha
Mallya: Hali ya Mme wako ki Afya Wakati anaenda Moshi hali yake ilikuwaje
Shahidi: Nakumbuka walikutana na Ling'wenya wakaemda Kwanza Morogoro, Wakarudi, Waliporudi wakajiandaa Wakaenda Moshi
Shahidi: aumwi na Kwamba anaweza Kwenda Moshi
Shahidi: Ilikuwa Nzuri inamruhusu kwenda Kufanya kazi
Mallya: Hali Nzuri unamaanisha nini , Mwambie Mheshimiwa Jaji
Mallya: mlikuwa mnatumia Njia gani kufanya mazungumzo
Shahidi: alinitaarifu kuwa amefika Moshi
Mallya: kitu gani kilifuata baada ya Kwenda Moshi
Mallya: Siku ya Tarehe 05 08 2020 kitu gani kilitokea
Shahidi: alinipigia na akaongea na watoto, tulipokuwa tunaongea akasema Hebu subiri nikamsubiri
Shahidi: kwa Njia ya Simu
Mallya: kitu gani Kilifuata
Mallya: ilikuwa Saa ngapi Kama Saa Moja
Mallya: alipokwambia Subiri kidogo nitakupigia Kidogo
Shahidi: Sikumbuki Kichwani lakini ipo kwenye Simu yangu
Shahidi: Nilipoona Muda umeenda ilipofika Saa 10 ilibidi nimpigie,Simu iliita ikawa imepokelewa lakini Kina nikisema Hallo Sisikii Mtu akiongea
Mallya: Unaweza Kukumbuka namba ya Simu uliyopiga ambayo ulipiga Ikapokelewa.?
Mallya: Baadae kilifuata nini baada ya Simu kutokupelewa
Mallya: kitu gani Kilifuata
Shahidi: baadae Ikawa haipatikani
Mallya: baada ya Kumpigia Ling'wenya.?
Shahidi: kwakuwa nilikuwa na namba ya Mwenzake Ling'wenya nikampigia Ling'wenya
Mallya: Sasa wewe ilipata hisia gani baada ya kuona Inaita hadi Kesho yake haipokelewi
Shahidi: niliona labda ni Mambo ya Kazi, sikuwa na wasiwasi wowote
Shahidi: Ikawa ainaita Mpaka jioni ,Mpaka Usiku ,Mpaka Kesho yake inaita haipokelewi
Shahidi: Wewe ulichukua hatua gani..?
Shahidi: Sikuwa na mtu Mwingine yoyote wa akumuuliza Zaidi ya Ling'wenya
Mallya: Baada ya hapo Kitu gani Kilifuata baada ya kuhisi ni Mambo ya kazi
Shahidi: Miaka 3 na Miezi 9
Shahidi: Sikuwa na namna yoyote zaidi ya Kusubiri simu kutoka kwao
Mallya: Una mtoto unesema anaumri gani?
Shahidi: nakumbuka ilikuwa 09 08 Mwaka 2020 niliamka Asubuhi ikiwa siku ya Jumapili, Mtoto alikuwa anasumbuliwa na tumbo
Jaji: Mtoto wa Jinsia gani
Mallya: Nataka kukupeleka Tarehe 09 Mwezi 08 kitu gani Kilitokea
Mallya: kwanini Unakumbuka kuwa ilikuwa Siku ya Jumapili
Shahidi: Wakike
Shahidi: Sababu ilikuwa Siku ya Ibada
Shahidi: Sikwenda Ibadani badala yake nikaenda Hospitali
Mallya: ikawaje huko Hospitali
Mallya: Ikawaje
Shahidi: Nilipokelewa
Mallya: Hospitali gani
Shahidi: Hospitali ya Serikali palepale Chalinze
Mallya: baada ya Kupokelewa Hospitali
Shahidi: nilipatiwa Huduma nikarudi Nyumbani
Mallya: Ule Mlango ulikuwa katika hali gani
Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani niliona Miguu ya watu kama Imekanyaga, Wakati natoka Nyumbani nilifunga Mlango lakini niliporudi nikakuta Milango ipo wazi
Shahidi: Mlango ulikuwa wazi na Kitasa nikakuta kimevunjwa
Shahidi: kwa akili ya harakaharaka nilijua Wezi, Cha ajabu kila kitu nilikuta Vipo, Kitu kama Tv lakini vipo
Mallya: enheeee ikawaje
Mallya: kitu gani kikatokea
Jaji: Za Mme wako
Shahidi: zote zimemwaga,na Mabegi yamefunguliwa
Shahidi: Nikaingia Chumbani nikakuta Nguo za zimemwagwa Chini
Shahidi: Alinunua Congo Begi lenye Mabaka Mabaka ya Jeshi
Shahidi: Kuna begi alinunua Congo nilipokuja kikakuta halipo
Mallya: Jirani yako anaitwa nani.?
Mallya: Kitu gani kilifuata
Shahidi: Nilienda Kuuliza Majirani zangu
Shahidi: niliemda Kuuliza kama Mme wangu amekuja Nyumbani? wamemuona.? kwamba kunakitu huenda alikuja Kukitafuta kwa haraka haraka
Shahidi: Judith Charles
Mallya: lengo la kwenda kwa Jirani lilikuwa nini
Mallya: Jirani alikwambiaje
Jaji: Ndiyo
Shahidi: Kuna Magari yalikuja hapa Ya Kipolisi, Moja walikuwa wamevaa Sare na Wengine walikuwa Wamevaa Kiraia
Mallya: Taarifa Nyingine alikupa Jirani yako ni Ipi
Mallya: baada ya hapo Mapolisi walishuka kwenye gari wakaingia Ndani
Shahidi: kwamba Mapolisi walimuita kwa lengo la Kuniulizia Mimi
Mallya: yeye Jirani alikuwa anafanya nini wakati huo
Mallya: Kitu gani kingine walikufahamisha au Kumpatia
Shahidi: alikuwa anashuhudia wakati wanaingia ndani ya Nyumba yako
Walichukua Hati ya Uwanja
Shahidi: walisema walichukua Begi, Vyeti vyake vya Kijeshi vya Adamu walichukua Kadi ya pikipiki
Shahidi: aliongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze
Mallya: Kitu gani Kingine alikwambia
Mallya: aliyeongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze alikuwa ni ameongozana na akina nani
Shahidi: Jirani yangu aliongozana na Mkuu wa Upelelezi na aliacha namba ya Simu kwa Jirani,
Jaji: kwa ajili ya Nini
Shahidi: alisema Kama Kuna Lolote ambalo hajalielewa ampigie
Mallya: Siku ya Jumapili 08 Mwezi 09 Jumapili, Nyumba imesachiwa na Umekuta namba ya simu ya Mkuu wa Upelelezi Chalinze kitu gani Kilifuata baada ya hapo
Mallya: alikufahamisha kuwa alipigiwa Simu na nani..?
Shahidi: nilimpigia Simu,yeye aliniambia kuwa alipigiwa tuh simu kuwa inabidi waongozane kwenda Kusachi kwenye Nyumba ya Adamu Kasekwa
Jaji: labda nisikilize Mawakili
Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba tubreak Kidogo kwa Sababu Shahidi akitumia Sana Nguvu anaweza akupoteza Energy na huenda akawa na siku Ndefu
Jaji: Mnasikia au Mvua inasababisha Kupoteza Usikivu tuhairishe kidogo.?
Jaji: upande wa Serikali
Jaji: kama Mvua imeacha Kidogo, Hebu tuendelee Kidogo ,Ikirudi na tukashindwa ,Tutaharishi
Wakili wa Serikali: hatuna Pingamizi
Jaji: uliishia Kuhusu kumpigia simu Mkuu wa Upelelezi Chalinze
Mallya: nilimuuliza Mkuu wa Upelelezi alijibu Kitu gani
Shahidi: alisema amepigiwa simu Kutoka Moshi
Jaji: naona Mvua haituoi Muda wa kuendelea,siwezi Kukadiria kwa muda gani, Kwa muda Mchache nahairisha Shauri
Jaji anatoka Nje
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021,Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire,Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe
Kesi inatajwa
Jaji amerejea Mvua Imekatika Sasa
Jaji: wakili John Mallya tuendelee
Mallya: Baada ya Kuwa ameshakwambia kuwa alipigiwa simu Kutoka Moshi kitu gani kilifuata
Jaji: Tunasikilizana, kama Mvua Inanisubiri Mimi, (Imeanza Kunyesha)
Mallya: Kesho yake ikawaje?
Shahidi: Muda ulikuwa umeshaenda, nikasema itabidi Kesho yake niende kwa sababu sikuamini alichoniambia
Mallya: Ulisema Ulienda Kituoni kesho yake wapi
Shahidi: Kituo cha Chalinze
Jaji: sasa ilikuwa Jumatatu
Shahidi: Nikaomba Kuonana na Mpelelezi,Nilipo muina nikajitambulisha Kuwa Mimi ni Yule Dada qmbaye Mmekuja Nyumbani Kusachi
Mallya: akakwambiaje?
Mallya: tarehe 05 Umepigia Umemkosa, Tarehe 09 ukakuta umesachiwa, Kitu gani kilitokea Tarehe 10 Ya Jumatatu pale Kituoni?
Mallya: Wewe ulikuwa unafanya Jitaihada gani zingine
Sina ninachokujua Zaidi
Shahidi: akasema kama nilivyokueleza sina ambacho nakijua zaidi ya Kuchukuliwa na kuwasindikiza Kwenda Nyumbani Kwako
Shahidi: nilianza kutafuta namba za Mke wa Ling'wenya
Mallya: awali ulituambia namba za Ling'wenya ulikuwa nazo na Ukampigia, za Mke wake unazitafuta, Za Ling'wenya ulitoa wapi
Shahidi: ni Mtu wa Karibu wa Mme wangu, Rafiki yake tuseme siku wanaondoka walikuwa naye
Mallya: ulitumia Njia gani za Kupata namba za Mke wa Ling'wenya?
Jaji: Mwenzao Kwamba alikuwa Askari Jeshi
Shahidi: nilimtafuta Mwenzao SHIKUNZI aliyekuwa anaishi nao Kimara
Mallya: alikuwa kimara aanakaa na nani
Shahidi: Ndiyo
Shahidi: alikuwa anakaa karibu na Ling'wenya
Shahidi: Nilitaka kumuuliza Mke wa Ling'wenya ili Kumuuliza huko kwake ni nini kilikuwa kinaendelea.?
Mallya: kikichokufanya Umtafute SHIKUNZI ili umtafute Mke wa Ling'wenya ni nini.?
Jaji: Kwanini ukimtafuta SHIKUNZI?
Mallya: SHIKUNZI akafanyeje..?
Shahidi: walikuwa ni Majirani
Shahidi: alinipatia namba ya Mke wa Ling'wenya
Shahidi: nilimpigia Mke wa Ling'wenya
Mallya: ulifanya hatua gani?
Mallya: nini kilifuata baada ya hapo
Shahidi: akaniambia baada ya hapo walienda Kwa Mwingine anaitwa Bwire, tumtafute Mke wa Bwire
Iliku ya siku ya Jumatatu, na yeye akaniambia Siku ya Jumapili ambayo ni Jana yake walienda Nyumbani Kwake wakafanya Upekuzi
Nikamwambia wewe huko Jirani huko Mtafute Mke wa Bwire
Shahidi: kwamba nilitaka Kujua kama kwake walienda kusachi akaniambia Wameenda kusachi, akaniambia pia tutafute Mke wa Bwire
Mallya: Kitu gani alikueleza Mke wa Ling'wenya
Shahidi: Mke wa Bwire anaitwa mama Itham na Mke wa Ling'wenya anaitwa Mama Somoye
Mallya: ulipata namba ya Mke wa Bwire na Unaweza kukumbuka Majina yao
Mallya: nini Kinafuata
Shahidi: Mke wa Bwire alikuwa Dar es salaam anakasema Inabidi nitoke Chalinze nije Dar es salaam
Jaji: alisema utoke wapi?
Mallya: hii sintofahamu yote ilitokana na nini
Shahidi: Kutokana na kuto kujua Mwenza wangu yupo wapi,namtafuta simpati alafu Nyumbani wamekuja Kusachi
Shahidi: Chalinze ni Dar es salaam
Mallya: ilikuwa lini.?
Shahidi: Nilitafuta Nauli nikaja Dar es salaam
Mallya: baada ya Kushauriwa Ulichukua hatua gani
Shahidi: Sikumbuki
Mallya: Baada ya Kufika Dar es salaam nini Kilifuata
Mallya: unaweza Kujua Nyumbani Kwake Bwire
Shahidi: Maeneo ya Temeke
Shahidi: tulishauriana tuanze Kutafuta Vituo Vyote vya Polisi
Mallya: Ndiyo
Mallya: Unaweza kukumbuka mlianzia Wapi
Shahidi: Kituo cha Polisi CHANG'OMBE
Shahidi: Polisi wa zamu
Mallya: mlikumkuta Polisi gani?
Shahidi: Tukajitambulisha kuwa sisi Wame zetu Wamekamatwa hatujui wamepelekwa Kituo gani
Mallya: Mkajitambulishaje?
Shahidi: Kwa Majina yetu na Waume zetu
Mallya: baada ya hapo yule Askari alifanyeje?
Shahidi? akaanza kupekua Kitabu kwa kuangalia yale Majina ya waume zetu hatukuyaona
Mallya: Baada ya Kutoyaona Majina ya Mnaowatafuta Kitu gani Kilifuata?
Shahidi: tulienda kituo Kingine
Mallya: Kituo gani
Shahidi: cha Central Police Dar es salaam
Mallya: Ikawaje?
Shahidi: vilevile tukajitambukisha na kwamba sisi waume zetu wameletwa polisi na hatujui Kituo gani
Mallya: baada ya Kujitambulisha kwa Askari nini Kilifuata?
Shahidi: aliangalia kile Kitabu hakuona yale Majina yetu
Shahidi: Wakati anaangalia Kitabu,Wote tuliinama kuangalia Majina ya Waume zetu kwa usahihi
Mallya: Mmeangalia pamoja na Askari Majina wenza wenu hamjayaona, nini Kiliendelea baada ya hapo?
Mallya? wakati anaangalia Majina ya wame zenu Nyie Mlishiriki Vipi?
Tukajitambulisha kwa Askari wa zamu akaangalia kwenye kitabu, Majina yao hayakwepo
Shahidi: tulitoka Kituo cha Polisi Central Police tukaenda Oysterbay
Mallya: baada ya Kuwakosa Central nini kilifuata
Shahidi: tulienda Tazara
Mallya: Unaweza Kueleza Kwanini Mlienda Tazara
Mallya: Unaweza Kuiambaia Mahakama mara zote mlipokuwa mnatafuta mlikuwa mnawatafuta kwa Namna gani
Shahidi: mara zote tunataja Majina na Mimi nilitaja Jina la Mme wangu Adamu Khalfani Kasekwa
Shahidi: tulienda kwa Sababu tulikuwa kwenye Kuendelea kuwatafuta Kituo gani cha Polisi wamepelekwa
Mallya: Kitu gani Kilifuata
Mallya: Kitu gani Kilifuata
Shahidi: Hatukuyaona Majina yao
Shahidi: Hatukuyaona Majina yao
Mallya: Mmeshaenda Vituo Vinnne Kutafuta wenza wenu, hatua gani ilifuata baada ya hapo?
Shahidi: Tulirudi Nyumbani kwa sababu Muda ulikuwa umeenda, na tuliacha watoto wadogo
Mallya: Nyumbani kwa Maana Wapi?
Shahidi: Kwa Mke wa Bwire
Mallya: kwa Mazungumzo yako na Mke wa Bwire alikwambia nini kimetokea Kule Moshi
Jaji: twendeni Taratibu, Mmeshazunguka Vituo Vyote ilikuwa siku gani..?
Shahidi: akaniambia Kule Moshi kuna wifi yake ambaye ni Dada wa Mohammed Abdilah Ling'wenya
Jaji: ooohhh tunakosa Mtiririko kwa sababu nilikuwa bado nipo kwenye Vituo Vya Polisi
Shahidi: Tarehe 13
Mallya: Samahani Mheshimiwa Jaji nilirudi Nyuma Kumuuliza kama waliongea na Mke wa Bwire
Mallya: Nini kilifuata
Shahidi Kwamba Wifi yake amempigia Simu Kuwa Adam wakiwa Moshi na Mohammed akiwa anakunywa Chai Adamu alikuwa anazungumza na Simu ,ikawa kama kelele za Mvutano,Niache niache baada ya hapo wakawa wanamvuta Kumleta Sehemu za Vyakula sasa
Mallya: alikwambia nini sasa?
Shahidi: Kwamba alikuwa amepigwa akawa anavuja Damu,
Jaji: hii ni Habari ambayo umesema Umeambiwa na Mke wa nani..?
Shahidi: Mke wa Ling'wenya Tukiwa kwa Mke wa Bwire
Jaji: nafikiri tulirudi kwenye Mstari hapo tunaanza kuzungumzia "Here say" yeye kaambiwa na Mke wa Ling'wenya na Mke w Ling'wenya kaambiwa na Wifi nafikiri Mkiona Kuna Umuhimu mumuite Wifi aje kutoa Ushahidi ila Hatuwezi Kwenda hivyo.
Mallya: huyo wifi yake anaitwa nani?
Shahidi: anaitwa Athima
Mallya: Mliporudi Nyumbani ikawaje?
Mallya: sawa Mheshimiwa Jaji
Mallya: Mlikuwa na Nyenzo gani katika Kuwatafuta
Shahidi: tulikubaliana tupite Hospitalini
Shahidi: Tulikuwa na Picha zao
Shahidi: tulianzia Hospitali ya Muhimbili
Mallya: na Mlianzia Wapi?
Shahidi: Ni baada ya Kuwakosa Kwenye Vituo vya Polisi
Jaji: Kwanini Mlianza Kuwatafuta Kwenye Mahospitali
Jaji: Kwa Off Record tuh,Moshi waliwambiaje
Shahidi: kwamba huku hawapo wameletwa Dar es salaam tukahisi labda wamepata Ajali
Shahidi: Tukajitambulisha na kueleza kuwa tunawatafuta Wame zetu
Mallya: Mlipofika Muhimbili ikawaje
Shahidi: tulizunguka Kwenye wodi na Monchwari hatukuwaona
Mallya: nini Kikafuata
Shahidi: Tukaenda Hospitali ya Amana, Tukajitambulisha na Kuingia Kwenye Mawodi na Monchwari hatukuwaona pia
Shahidi: tulienda Mwananyamala tukajitambulisha na Kuwatafuta wame zetu kwenye Mawodi na Mochwari hatuwaona
Mallya: baada ya Amana?
Mallya: Siku ya tatu Sasa Mmeeanda Muhimbili, Amana na Mwananyamala mkawakosa, Ulichukua hatua gani
Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani, kwa Mara ya kwanza Ulipata Taarifa ya Mumewako yupo wapi
Shahidi: ilibidi nirudi Chalinze kwa Sababu nauli ilikuwa imeshaanza kuisha na Kwa sababu nina mawasiliano ikabidi nirudi Chalinze
Shahidi: Mahakamani Kisutu
Shahidi: Ilikuwa kwenye Taarifa Ya Habari ya Jioni
Mallya: uliwaona wakiwa wapi?
Shahidi: ITV
Mallya: Kituo gani Cha Habari?
Mallya: Uliwaona au Ulisimuliwa
Shahidi: niliona
Mallya: wanatuhumiwa kwa Makosa gani
Shahidi: Anashitakiwa kwa Ugaidi na uhujumu Uchumi
Shahidi: kwamba Kuna kazi Imepatikana anaenda kuifanya
Mallya: mara Ya Mwisho Mmewako wakati anakuaga alikwambia anaenda Moshi Kufanya nini?
Mallya: ikawaje?
Mallya: Uliona hiyo Taarifa ya Habari ITV saa ngapi
Shahidi: Ilikuwa Saa 2 za Usiku
Shahidi: Niliwasiliana na wenzangu
Shahidi: tulikubaliana Twende Mahabusu kwa Sababu hatukujua wamepelekwa Mahabusu gani
Mallya: Baada ya hapo nini kilifuata?
Mallya: mkafanya Mawasiliano, Mawasiliano gani
Shahidi: Mzee Ling'wenya alikuja kutoka Mtwara
Mallya: kitu gani alifanya baada ya Kutoka Mtwara Mzee Ling'wenya?
Shahidi: Mimi sikwepo nilikuwa Chalinze, Tulifanya Mawasiliano
Mallya: mlianza kutafuta Mahabusu gani?
Shahidi: Tulikuwa hatuelewi wapo Mahabusu gani, Tulianza kutafuta Mahabusu waliopo
Jaji: ni akina nani?
Mallya: wakakwambiaje?
Shahidi: Kwamba wameenda Keko wamewakosa ila Segerea Wamewakuta wapo
Jaji: Mke wa Ling'wenya na nani..?
Shahidi: Mke wa Mohammed Abdilah Ling'wenya na Mzee Ling'wenya
Shahidi: Na Baba Mke wake,Mzee Ling'wenya
Mallya: sasa Ushajua Mwenza wako yupo Segerea hatua gani ilifuata
Shahidi: Nilikuja Jumapili kutoka Chalinze, Jumatatu tuliamka wote Mke wa Bwire, Ling'wenya tukaenda Wote Segerea
Mallya: Mlipofika Segerea ikawaje?
Mallya: baada hapo ulifanya Hatua gani?
Shahidi: Tulipokelewa na Askari wa Jinsia ya kike akatueleza leo siyo siku ya kuwaona Mahabusu Mje Jumamosi au Junapili
Shahidi: niliskia Ma ASKARI wakisema ndiyo Yule Jamaa ambaye yupo Kabatini
Mallya: ni nani aliteyaongea hayo?
Shahidi: Nilienda Jumamosi
Mallya: hatua gani ilifuata
Shahidi: Wakachukua funguo wakasema tunaenda kumleta
Shahidi: ni Ma Askari niliowaleza Majina kuwa namtafuta Mme wangu
Mallya: Kitu gani kilifuata
Mallya: unaweza Kutuambia hapo ulipokuwepo pana taswira gani ili Mheshimiwa jaji apate Picha?
Shahidi: Ukiingia Segerea maeneo ambayo kuna Meza ya Kuwekea Chakula na Kuna Chuma kama Grill lililotenganisha
Shahidi: Alikuwa amevaa kama Singlendi
Shahidi: nilimuona Mmewangu akitembea Kwa tabu kama Vile inaonekana ameteswa
Mallya: Unaweza Kukumbuka Mme wako amevaaje?
Mallya: hali yake ilikuwaje?
Shahidi: Amedhoofika, alikuwa amekonda Sana
Mallya: Mwendo wake ulikuwaje, alivyokuwa anatembea?
Mallya: Ulichukua hatua gani?
Shahidi: alikuwa anachechemea
Shahidi: Chakula, shuka na Sabuni
Jaji: ulikuwa umeleta Vitu gani
Shahidi: Kama Utaratibu ulivyo wa pale, Nilibeba kwa ajili yake
Shahidi: Askari akishakagua anachukua ukiwa unamuona:
Jaji? Vitu ulimkabidhi nani.?
Mallya? ulisema ulikuwa unamuona Mme wako sasa anaelekea sehemu, Ni sehemu gani
Shahidi: Eneo la Nyavu ambalo mnaweza Kuzungumza
Mallya: ilikuwaje Mazungumzo kati yenu
Shahidi: Nilimuuliza Hali yake na Kilichotokea
Shahidi: Hali yangu ni hivyo hivyo ila siyo Nzuri
Mallya: alikujibu nini?
Mallya: alikwambia kwanini hali yake siyo Nzuri
Mallya: Baada ya Hapo.?
Shahidi: aliniambia Kuna Mateso alipitia wakati yupo Moshi, alipigwa sana Ndiyo Maana Unaniona nipo Kwenye hali hii
Mallya: nitakurudisha Nyuma Kidogo, Kilichokufanya utafute Vituo vya Polisi na Mahospitali Mme wako ni Kitu gani?
Shahidi: alichukuliwa akapelekwa Mahabusu
Wakili wa Serikali: OBJECTION wakili ameshauliza
Wakili wa Serikali Ameshaliuliza hilo swali
Mallya: Sikuuliza, Kama aliulizwa ni Off Records nataka sasa iingie kwenye Records
Jaji: Sijachoka Kuandika, Muulize tena
Mallya: nitakurudisha Nyuma Kidogo, Kilichokufanya umtatafute Vituo vya Polisi na Mahospitali Mme wako ni Kitu gani?
Shahidi: Kwa sababu tuliambiwa kuwa Walitolewa Moshi Kuja Dar es salaam na tulienda Vituo Vya Polisi Kwa Sababu tuliamini Kama wangetusaidia
Shahidi: alikuja Mama yake, tukaenda naye Moshi
Mallya: Kwanini wewe namba ya Mme wako umesema huikumbuki kwa kichwa mie ya Mke wangu naikumbuka
Mallya: Vipi Kuhusu Ushiriki wa Ndugu zake Mwanamme
Shahidi: Kwa sababu alikuwa na line Mpya aliyotoka Kuisajili
Mallya: Kwanini Unasema Ulipoenda Segerea hali yake ilikuwa tofauti
Shahidi: alikuwa amekonda sana na Macho yameingia Ndani Kama Yameganda, amekonda kwa kweli na Pia Nilimuona akiwa na alama Kwenye Mkono wakati anaenda Moshi alikuwa hana
Mallya: ya kwangu ni hayo
Jaji: ulisema Uliona nini Kwenye Nkono
Shahidi: alama ya Kovu kwenye Mkono, Awali alikuwa hana wakati anaenda Moshi
Jaji: Asante sana Mallya
Lakini tutabreak tena kidogo kama Dakika 17
Jaji: Pamoja Mvua kutuharibia ratiba yetu tutarejea Saa 6 Kamili
Jaji ananyanyuka anatoka
Shahidi anapanda tena Kizimbani
Jaji amerejea
Kesi inatajwa na Washitakiwa wanakaa Kizimbani Kwao
Jaji: Wakili Fredrick Kihwelo kama Unaswali.?
Jaji: Wakili Nashon kama Unaswali lolote
Nashon: Sitokuwa na Swali Kwa Shahidi
Fredrick Kihwelo: sitokuwa na Swali kwa Niaba ya Mshitakiwa wa tatu hatutokuwa na Swali
Jaji: Wakili Kibatala kwa niaba ya Mashtakiwa wa Nne
Kibatala: Shahidi Ulijisikiaje uliporudi Nyumbani Kukuta Nyumba yako Imevunjwa na Mme wako alikuwa hapatikani Muda wote
Shahidi: Niliogopa Kwanza Nilihisi ni wezi
Kibatala: Ulitegemea kuwa Polisi wanaweza kufanya hivyo?
Shahidi: Hapana sikuwahi Kutegemea Polisi wanaweza Kufanya tendo hilo
Kibatala: Umeongelea kwamba Ulikuta Tv na Vingime Kukuta Vipo, ila Kadi ya Pikipiki na Hati ya Kiwanja Vilikuwa Vimechukuliwa
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Mpaka leo hii Ujawahi kuambiwa kuwa nani ana hivyo vitu Kituo cha Polisi Chalinze au afisa yoyote wa Polisi?
Shahidi: Hakuna aliye wahi Kuniambia
Shahidi: Sahihi sijui nani nimdai
Kibatala: Mpaka leo hii Ujui nani wa Kumdai hivyo Vitu?
Kibatala: Kuna Mgogoro wowote wa Kiwanja sehemu unayoishi au Kupelekwa hata Kwa Mjumbe?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Ushawahi Kujua Kwanini Adamoo alisimamishwa kazi au Utumiahi wake wa Kijeshi Ulivyokomea
Kibatala: Sawa tuachane na hilo
Shahidi: Nafikiri huko kwenye Mambo ya Kijeshi tusiende Sana Miye sijui lolote kuhusu Jeshi
Kibatala: nimesikia kuwa ulienda Kumtafuta Mmeo Vituo Vya Polisi, Naomba Nikuonyeshe Kielelezo Namba 1 Kitabu fulani
Kibatala: unasema ulienda Polisi ukaoneshwa Kijitabu kama hiki au Kinachofanana na Hili na bado baada ya Kupekua hukuona Kitabu kama hiki?
Mahakama inampatia Kibatala Kielelezo DETENTION REGISTER
Kibatala: na Bado Jina la Mme hakuliwepo?
Kibatala: unasababu yoyote ya Kutunga Story ya Uongo kuwa Hukwenda Polisi Central alafu leo Uje useme ulienda Polisi Central, Je unasababu yoyote ya Kutunga?
Shahidi: Ndiyo
Shahidi: Hapana sina Sababu yoyote
Kibatala: Nimesikia Kuwa kilichowafanya Muanze Kutafuta Dar es salaam baada ya Mke wa Ling'wenya, kuwasiliana na Dada yake Ling'wenya Kule Moshi, akasema kuwa Adamoo na Ling'wenya Wameletwa Dar es salaam
Shahidi; Ndiyo
Kibatala: Je nilikusikia Sahihi
Kibatala: Nimekusikia Sahihi Kuwa Mlipita Kote ikiwemo Chang'ombe, Central Station, na Tazara pamoja na Vyumba Vya Kuhifadhia Maiti kwa sababu ya Kukosa Taarifa?
Kibatala: Mlilazimika Kufunguliwa Mwili Mmoja baada ya Mwingine Kwenye vyumba vya Kuhifadhia Maiti
Shahidi: Ndiyo
Shahidi: Ndiyo Nililazimika Kufungukiwa Maiti Moja baada ya Nyingine ilikuweza kuthibitisha kama Mmewangu yupo huko
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ni sahihi Kwamba wakati unapitia hali hii ulikuwa na Miaka 25 tuh.?
Kibatala: na Wakati huo ulikuwa na Mtoto Mdogo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: wakati huo Ulikuwa kwenye Ndoa kwa muda gani Mpaka unapitia Matukio haya Mazito Matatu?
Jaji: Hesabu zenu zipo Vizuri?
Jaji: naona hakuna tatizo Mtu kukosea hesabu Mahakamani,Hilo swali tunaweza Kuliacha
Kibatala: Minne
Kutoka 2016 August Mpaka 2020 ni Miaka Mingapi?
Kibatala: Asante Mheshimiwa Jaji ni hayo tuh
Shahidi: ni baada ya Tarehe 09
Kibatala ni Sahihi wakati nakuja kupekuliwa Ilikuwa ni Kabla ya Tarehe 09 au ni baada ya tarehe 09
Shahidi: Ndiyo tuendeleee
Jaji: Shahidi unanguvu za Kuendelea Kujibu??
Jaji: wakili gani Serikali ataanza Kuuliza Maswali
Wakili Kidando: ataanza Jenitreza Kitali
Wakili wa Serikali: Jenitreza Kitali Ni sahihi Shahidi Umesema Adamu ni Mme wako
Wakili wa Serikali Jenitreza: Ni sahihi ujatoa Cheti Cha Ndoa
Wakili wa Serikali: Ni sahihi umesema Kuwa Adamu walikuaga wanaenda Moshi Mwanzoni Mwa Mwezi wa nane
Shahidi: ni sahihi
Wakili wa Serikali: ni kweli umeeleza Kuwa walikuaga wanaenda Kwa Mheshimiwa Mbowe
Shahidi: Sahihi
Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app