Maamuzi ya kesi ndogo katika Kesi ya Mbowe na Wenzake kutolewa Oktoba 19, 2021

Maamuzi ya kesi ndogo katika Kesi ya Mbowe na Wenzake kutolewa Oktoba 19, 2021

Kesi hii imefunua machache kati ya mengi wanayofanya polisi kwa raia mpaka hapa naamini ushahidi uliotolewa na adamoo na mwenzie ni ukweli, polisi yetu ina uhuni mwingi na wanakurupuka kukamata watu bila kupata ushahidi, ni wavivu wa kufuatilia ukweli wajiridhishe, katika kamatakamata zao hizi za ugaidi wamekamatwa wengi na kupewa mateso mazito na mwisho wakaachiwa baada ya kubaini hawana makosa, yanahitajika mabadiliko makubwa ya sheria na katiba yetu ili uonevu ukomeshwe
 
Shahidi: Mlango ulikuwa wazi na Kitasa nikakuta kimevunjwa,kwenye hii sentensi mimi sioni sehemu aliyosema polisi walivunja mlango bali amesema alikuta kitasa kimevunjwa bila kuelewa nini kimetokea.

..shahidi anasema alipouliza majirani aliambiwa kuna watu waliovalia kiraia na kipolisi walionekana nyumbani kwake.

..sidhani kama utetezi wanaweza kuuangusha ushahidi wote kwa mara moja. Wanachotakiwa kufanya ni kujenga kidogo-kidogo, hatua kwa hatua, hoja kwamba kuna mapungufu ktk ushahidi na maelezo ya polisi.
 
Kesi Hii Ni Kimeo Kwa Jamhuri Mbona Wanashupuza tu Shingo!!!! Hawajagundua Wako Uchi...time will tell ebu tuwe wapole.
Umekariri tu kuwa wapo uchi. Hebu fafanua basi. Maana unakuta tu mtu anasema Mbowe hatoki....haweki sababu za kitaalamu. Mwingine kama wewe unasema Jamhuri sijui nini....huweki sababu. Haya mambo kama hamyafaham muwe mnanyamaza tu
 
Inasikitisha Sana Mkuu. Sasa hivi Tz haiongozwi na Rais Bali na Jopo la Marais. Hapo ndiyo tatizo linakoanzia.
Unajaribu kumlaumu nani? Raisi samia eti?

Kwa taarifa yako hawa watu walifanyiwa huu unyama wakati wa mwendazake. Na ujue,serikalini watu wa mwendazake wamejaa,hususani kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Na hii kesi ni initiative yao,siyo ya raisi samia.
 
Hivi polisi wanapomtia mtu nguvuni wana haki ya kumficha asijulikane alipo kweli...!!!

Sirro ana maana gani kuwambia watu eti wafuate sheria bila shuruti wakati polisi wanafanya kinyume cha sheria kwa kuwateka watu na kuwaficha ili wawatese.

Bila katiba mpya itakayoweka utaratibu wa polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria akina Hamza watazidi kuongezeka tu.
 
Hii ndio taarifa iliyotufikia , kwamba leo Mke wa Mshitakiwa aliyeteswa kinyama komando Adam kasekwa leo atapanda kizimbani akiwa ni shahidi wa tatu wa upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa inayomkabili Freeman Mbowe na Wenzake watatu

Endelea kufuatilia

========

Saa 3 na Dakika 11 Tupo Chumba Cha Mahakama Tayari, Kwa Mawakili wa Utetezi wapo tayari Mahakamani ila Mshitaka bado wapo Nje

Jaji: ameshaingia Sasa Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021, Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire,Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe

Kesi inatajwa

Jaji: Habarini za Asubuhi, Tuendeleeni ni Siku Nyingine

Jaji: sawa

Wakili wa Serikali: naomba Radhi tumeingia wakati umeshaingia

Jaji: Wakili wa Serikali

Wakili wa Serikali: Kidando anatambulisha wenzake
Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulimanywa Majigo


Jaji: Utetezi

Kibatala: anatambulisha Wenzake

Advocate Peter Kibatala
Advocate Jonathan Mndeme
Advocate Fredrick Kiwhelo
Advocate John Malya
Advocate Sisty Aloyce
Advocate Alex Masaba
Advocate Idd Msawanga
Advocate Gaston Garubindi
Advocate Evaresta Kisanga
Advocate Faraj Mangula
Advocate Maria Mushi
Advocate Bonifasia Mapunda

Wakili Dickson Matata anaombewa Ruhusa Mdogo wake anafanyiwa Operesheni Hospitali ya Lugalo

Jaji: Wakili wa Serikali

Jaji: John Mallya

Wakili wa Serikali: Tumekuja kwa ajili ya kesi Ndogo ambapo Shahidi wa tatu yupo tayari kuendelea Kutoa Ushahidi wake

Mallya: Tunaye Shahidi, Na Shahidi yupo tayari kutoa Ushahidi

Shahidi: Mdada anatokea Nyuma kabisa ya Chumba Cha Mahakama anaenda Kizimbani

Jaji: Shahidi wa tatu upande wa Utetezi ambaye ameandaliwa Tafadhali anaweza Kuja

Jaji: anaandika Kidogo na Ukimya wa Mahakama

Jaji: Shahidi unaitwa nani

Jaji: Shahidi upo Mahakamani ondoa Hofu, nitakuuliza Majina yako na Nitakuapisha, Wakili wa Utetezi atakuongoza na Mawakili wengine watakuuliza Swali na Mawakili wa Serikali watakuuliza Maswali pia huna Haja ya Kuogopa, tupo hapa kutafuta Haki

Shahidi: Lilian Kibona
Dini Mkristo

Jaji: wakili Mallya endelea

Jaji: Liliani utachagua Kukaa au Kusimama,Hata Ukikaaa nitakuona

Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa Ukweli na Ukweli Mtupu , Mungu ni Saidie

Mallya: Shahidi Unaishi wapi

Shahidi: Chalinze Mkoa wa Pwani

Shahidi: Ramboni

Mallya: sehemu gani huko Chalinze,

Jaji: ni Mtaa.?

Mallya: Unaishi na nani..?

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Na mmewangu na Watoto ambaye kwa Sasa Mme wangu ameshikiliwa

Shahidi: Ndiyo

Jaji: ni Miongoni Mwa washitakiwa ??

Mallya: Mme wako anaitwa nani.?

Mallya: hapa kila nikiwa namuita Mshitakiwa wa Pili nitakuwa namaanisha pia ni yeye
]
Shahidi: ndiyo

Shahidi: Adamu Khalfani Kasekwa

Mallya: Ndoa Ya Kiserikali

Mallya: Mmeona lini 05 08 2016

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Palepale Chalinze

Mallya: Mlikuwa mnaishi wapi

Mallya: unaweza Kukumbuka Mmewako alikuwa anafanya kazi gani wakati huo

Mallya: alikuwa anafanya kazi gani Nyingine

Shahidi: Askari jeshi wa JWTZ kikosi cha 92 Ngerengere

Shahidi: alikuwa hana kazi Nyingine zaidi ya hiyo ya Serikali

Mallya: naruka nakuja 2020 Mme wako alikuwa anafanya kazi gani

Shahidi: alikuwa anafanya shughuli zake za Biashara

Mallya: Kabla ya Kwenda Moshi mlikuwana Hali gani kati yako na Mme wako

Mallya: Mwanzoni Mwa Mwezi wa Nane Mwaka 2020 unakumbuka Kilitokea Kitu gani kati yako na Mme wako

Shahidi: Mme wangu alikuwa Moshi, tulikuwa tunawasiliana naye Vizuri

Shahidi: Palikuwa na Mawasiliano

Shahidi: Rafiki yake Ling'wenya waliwasiliana kuwa kuna Kazi imepatikana Moshi

Mallya: kabla ajaenda Moshi kitu gani kilitokea

Shahidi: Hapana sikumbuki

Mallya: Unaweza Kukumbuka Siku na Saa ya hayo mawasiliano

Jaji: unasema palikiwa na Mawasiliano Kati ya Mme wako na Ling'wenya .?

Jaji: Ndiyo

Shahidi: Ndiyo Kwamba Ling'wenya alimpigia Simu kuwa kuna kazi Imepatikana Moshi

Mallya: Simu zilikuwa zinapigwa kati ya Ling'wenya na Mme wako wewe ulijuaje

Mallya: Jambo gani lilifanyika, kabla ya Mme wako kwenda Moshi

Mimi kama Mke nilimruhusu

Shahidi: Mimi Kama Mke wake alinishirikisha

Mallya: Hali ya Mme wako ki Afya Wakati anaenda Moshi hali yake ilikuwaje

Shahidi: Nakumbuka walikutana na Ling'wenya wakaemda Kwanza Morogoro, Wakarudi, Waliporudi wakajiandaa Wakaenda Moshi

Shahidi: aumwi na Kwamba anaweza Kwenda Moshi

Shahidi: Ilikuwa Nzuri inamruhusu kwenda Kufanya kazi

Mallya: Hali Nzuri unamaanisha nini , Mwambie Mheshimiwa Jaji

Mallya: mlikuwa mnatumia Njia gani kufanya mazungumzo

Shahidi: alinitaarifu kuwa amefika Moshi

Mallya: kitu gani kilifuata baada ya Kwenda Moshi

Mallya: Siku ya Tarehe 05 08 2020 kitu gani kilitokea

Shahidi: alinipigia na akaongea na watoto, tulipokuwa tunaongea akasema Hebu subiri nikamsubiri

Shahidi: kwa Njia ya Simu

Mallya: kitu gani Kilifuata

Mallya: ilikuwa Saa ngapi Kama Saa Moja

Mallya: alipokwambia Subiri kidogo nitakupigia Kidogo

Shahidi: Sikumbuki Kichwani lakini ipo kwenye Simu yangu

Shahidi: Nilipoona Muda umeenda ilipofika Saa 10 ilibidi nimpigie,Simu iliita ikawa imepokelewa lakini Kina nikisema Hallo Sisikii Mtu akiongea

Mallya: Unaweza Kukumbuka namba ya Simu uliyopiga ambayo ulipiga Ikapokelewa.?

Mallya: Baadae kilifuata nini baada ya Simu kutokupelewa

Mallya: kitu gani Kilifuata

Shahidi: baadae Ikawa haipatikani

Mallya: baada ya Kumpigia Ling'wenya.?

Shahidi: kwakuwa nilikuwa na namba ya Mwenzake Ling'wenya nikampigia Ling'wenya

Mallya: Sasa wewe ilipata hisia gani baada ya kuona Inaita hadi Kesho yake haipokelewi

Shahidi: niliona labda ni Mambo ya Kazi, sikuwa na wasiwasi wowote

Shahidi: Ikawa ainaita Mpaka jioni ,Mpaka Usiku ,Mpaka Kesho yake inaita haipokelewi

Shahidi: Wewe ulichukua hatua gani..?

Shahidi: Sikuwa na mtu Mwingine yoyote wa akumuuliza Zaidi ya Ling'wenya

Mallya: Baada ya hapo Kitu gani Kilifuata baada ya kuhisi ni Mambo ya kazi

Shahidi: Miaka 3 na Miezi 9

Shahidi: Sikuwa na namna yoyote zaidi ya Kusubiri simu kutoka kwao

Mallya: Una mtoto unesema anaumri gani?

Shahidi: nakumbuka ilikuwa 09 08 Mwaka 2020 niliamka Asubuhi ikiwa siku ya Jumapili, Mtoto alikuwa anasumbuliwa na tumbo

Jaji: Mtoto wa Jinsia gani

Mallya: Nataka kukupeleka Tarehe 09 Mwezi 08 kitu gani Kilitokea

Mallya: kwanini Unakumbuka kuwa ilikuwa Siku ya Jumapili

Shahidi: Wakike

Shahidi: Sababu ilikuwa Siku ya Ibada

Shahidi: Sikwenda Ibadani badala yake nikaenda Hospitali

Mallya: ikawaje huko Hospitali

Mallya: Ikawaje

Shahidi: Nilipokelewa

Mallya: Hospitali gani

Shahidi: Hospitali ya Serikali palepale Chalinze

Mallya: baada ya Kupokelewa Hospitali

Shahidi: nilipatiwa Huduma nikarudi Nyumbani

Mallya: Ule Mlango ulikuwa katika hali gani

Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani niliona Miguu ya watu kama Imekanyaga, Wakati natoka Nyumbani nilifunga Mlango lakini niliporudi nikakuta Milango ipo wazi

Shahidi: Mlango ulikuwa wazi na Kitasa nikakuta kimevunjwa

Shahidi: kwa akili ya harakaharaka nilijua Wezi, Cha ajabu kila kitu nilikuta Vipo, Kitu kama Tv lakini vipo

Mallya: enheeee ikawaje

Mallya: kitu gani kikatokea

Jaji: Za Mme wako

Shahidi: zote zimemwaga,na Mabegi yamefunguliwa

Shahidi: Nikaingia Chumbani nikakuta Nguo za zimemwagwa Chini

Shahidi: Alinunua Congo Begi lenye Mabaka Mabaka ya Jeshi

Shahidi: Kuna begi alinunua Congo nilipokuja kikakuta halipo

Mallya: Jirani yako anaitwa nani.?

Mallya: Kitu gani kilifuata

Shahidi: Nilienda Kuuliza Majirani zangu

Shahidi: niliemda Kuuliza kama Mme wangu amekuja Nyumbani? wamemuona.? kwamba kunakitu huenda alikuja Kukitafuta kwa haraka haraka

Shahidi: Judith Charles

Mallya: lengo la kwenda kwa Jirani lilikuwa nini

Mallya: Jirani alikwambiaje

Jaji: Ndiyo

Shahidi: Kuna Magari yalikuja hapa Ya Kipolisi, Moja walikuwa wamevaa Sare na Wengine walikuwa Wamevaa Kiraia

Mallya: Taarifa Nyingine alikupa Jirani yako ni Ipi

Mallya: baada ya hapo Mapolisi walishuka kwenye gari wakaingia Ndani

Shahidi: kwamba Mapolisi walimuita kwa lengo la Kuniulizia Mimi

Mallya: yeye Jirani alikuwa anafanya nini wakati huo

Mallya: Kitu gani kingine walikufahamisha au Kumpatia

Shahidi: alikuwa anashuhudia wakati wanaingia ndani ya Nyumba yako

Walichukua Hati ya Uwanja

Shahidi: walisema walichukua Begi, Vyeti vyake vya Kijeshi vya Adamu walichukua Kadi ya pikipiki

Shahidi: aliongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze

Mallya: Kitu gani Kingine alikwambia

Mallya: aliyeongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze alikuwa ni ameongozana na akina nani

Shahidi: Jirani yangu aliongozana na Mkuu wa Upelelezi na aliacha namba ya Simu kwa Jirani,

Jaji: kwa ajili ya Nini

Shahidi: alisema Kama Kuna Lolote ambalo hajalielewa ampigie

Mallya: Siku ya Jumapili 08 Mwezi 09 Jumapili, Nyumba imesachiwa na Umekuta namba ya simu ya Mkuu wa Upelelezi Chalinze kitu gani Kilifuata baada ya hapo

Mallya: alikufahamisha kuwa alipigiwa Simu na nani..?

Shahidi: nilimpigia Simu,yeye aliniambia kuwa alipigiwa tuh simu kuwa inabidi waongozane kwenda Kusachi kwenye Nyumba ya Adamu Kasekwa

Jaji: labda nisikilize Mawakili

Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba tubreak Kidogo kwa Sababu Shahidi akitumia Sana Nguvu anaweza akupoteza Energy na huenda akawa na siku Ndefu

Jaji: Mnasikia au Mvua inasababisha Kupoteza Usikivu tuhairishe kidogo.?

Jaji: upande wa Serikali

Jaji: kama Mvua imeacha Kidogo, Hebu tuendelee Kidogo ,Ikirudi na tukashindwa ,Tutaharishi

Wakili wa Serikali: hatuna Pingamizi

Jaji: uliishia Kuhusu kumpigia simu Mkuu wa Upelelezi Chalinze

Mallya: nilimuuliza Mkuu wa Upelelezi alijibu Kitu gani

Shahidi: alisema amepigiwa simu Kutoka Moshi

Jaji: naona Mvua haituoi Muda wa kuendelea,siwezi Kukadiria kwa muda gani, Kwa muda Mchache nahairisha Shauri


Jaji anatoka Nje


Kesi namba 16 ya Mwaka 2021,Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire,Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe

Kesi inatajwa

Jaji amerejea Mvua Imekatika Sasa


Jaji: wakili John Mallya tuendelee

Mallya: Baada ya Kuwa ameshakwambia kuwa alipigiwa simu Kutoka Moshi kitu gani kilifuata

Jaji: Tunasikilizana, kama Mvua Inanisubiri Mimi, (Imeanza Kunyesha)

Mallya: Kesho yake ikawaje?

Shahidi: Muda ulikuwa umeshaenda, nikasema itabidi Kesho yake niende kwa sababu sikuamini alichoniambia

Mallya: Ulisema Ulienda Kituoni kesho yake wapi

Shahidi: Kituo cha Chalinze

Jaji: sasa ilikuwa Jumatatu

Shahidi: Nikaomba Kuonana na Mpelelezi,Nilipo muina nikajitambulisha Kuwa Mimi ni Yule Dada qmbaye Mmekuja Nyumbani Kusachi

Mallya: akakwambiaje?

Mallya: tarehe 05 Umepigia Umemkosa, Tarehe 09 ukakuta umesachiwa, Kitu gani kilitokea Tarehe 10 Ya Jumatatu pale Kituoni?

Mallya: Wewe ulikuwa unafanya Jitaihada gani zingine

Sina ninachokujua Zaidi

Shahidi: akasema kama nilivyokueleza sina ambacho nakijua zaidi ya Kuchukuliwa na kuwasindikiza Kwenda Nyumbani Kwako

Shahidi: nilianza kutafuta namba za Mke wa Ling'wenya

Mallya: awali ulituambia namba za Ling'wenya ulikuwa nazo na Ukampigia, za Mke wake unazitafuta, Za Ling'wenya ulitoa wapi

Shahidi: ni Mtu wa Karibu wa Mme wangu, Rafiki yake tuseme siku wanaondoka walikuwa naye

Mallya: ulitumia Njia gani za Kupata namba za Mke wa Ling'wenya?

Jaji: Mwenzao Kwamba alikuwa Askari Jeshi

Shahidi: nilimtafuta Mwenzao SHIKUNZI aliyekuwa anaishi nao Kimara

Mallya: alikuwa kimara aanakaa na nani

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: alikuwa anakaa karibu na Ling'wenya

Shahidi: Nilitaka kumuuliza Mke wa Ling'wenya ili Kumuuliza huko kwake ni nini kilikuwa kinaendelea.?

Mallya: kikichokufanya Umtafute SHIKUNZI ili umtafute Mke wa Ling'wenya ni nini.?

Jaji: Kwanini ukimtafuta SHIKUNZI?

Mallya: SHIKUNZI akafanyeje..?

Shahidi: walikuwa ni Majirani

Shahidi: alinipatia namba ya Mke wa Ling'wenya

Shahidi: nilimpigia Mke wa Ling'wenya

Mallya: ulifanya hatua gani?

Mallya: nini kilifuata baada ya hapo

Shahidi: akaniambia baada ya hapo walienda Kwa Mwingine anaitwa Bwire, tumtafute Mke wa Bwire

Iliku ya siku ya Jumatatu, na yeye akaniambia Siku ya Jumapili ambayo ni Jana yake walienda Nyumbani Kwake wakafanya Upekuzi

Nikamwambia wewe huko Jirani huko Mtafute Mke wa Bwire

Shahidi: kwamba nilitaka Kujua kama kwake walienda kusachi akaniambia Wameenda kusachi, akaniambia pia tutafute Mke wa Bwire

Mallya: Kitu gani alikueleza Mke wa Ling'wenya

Shahidi: Mke wa Bwire anaitwa mama Itham na Mke wa Ling'wenya anaitwa Mama Somoye

Mallya: ulipata namba ya Mke wa Bwire na Unaweza kukumbuka Majina yao

Mallya: nini Kinafuata

Shahidi: Mke wa Bwire alikuwa Dar es salaam anakasema Inabidi nitoke Chalinze nije Dar es salaam

Jaji: alisema utoke wapi?

Mallya: hii sintofahamu yote ilitokana na nini

Shahidi: Kutokana na kuto kujua Mwenza wangu yupo wapi,namtafuta simpati alafu Nyumbani wamekuja Kusachi

Shahidi: Chalinze ni Dar es salaam

Mallya: ilikuwa lini.?

Shahidi: Nilitafuta Nauli nikaja Dar es salaam

Mallya: baada ya Kushauriwa Ulichukua hatua gani

Shahidi: Sikumbuki

Mallya: Baada ya Kufika Dar es salaam nini Kilifuata

Mallya: unaweza Kujua Nyumbani Kwake Bwire

Shahidi: Maeneo ya Temeke

Shahidi: tulishauriana tuanze Kutafuta Vituo Vyote vya Polisi

Mallya: Ndiyo

Mallya: Unaweza kukumbuka mlianzia Wapi

Shahidi: Kituo cha Polisi CHANG'OMBE

Shahidi: Polisi wa zamu

Mallya: mlikumkuta Polisi gani?

Shahidi: Tukajitambulisha kuwa sisi Wame zetu Wamekamatwa hatujui wamepelekwa Kituo gani

Mallya: Mkajitambulishaje?

Shahidi: Kwa Majina yetu na Waume zetu

Mallya: baada ya hapo yule Askari alifanyeje?

Shahidi? akaanza kupekua Kitabu kwa kuangalia yale Majina ya waume zetu hatukuyaona

Mallya: Baada ya Kutoyaona Majina ya Mnaowatafuta Kitu gani Kilifuata?

Shahidi: tulienda kituo Kingine

Mallya: Kituo gani

Shahidi: cha Central Police Dar es salaam

Mallya: Ikawaje?

Shahidi: vilevile tukajitambukisha na kwamba sisi waume zetu wameletwa polisi na hatujui Kituo gani

Mallya: baada ya Kujitambulisha kwa Askari nini Kilifuata?

Shahidi: aliangalia kile Kitabu hakuona yale Majina yetu

Shahidi: Wakati anaangalia Kitabu,Wote tuliinama kuangalia Majina ya Waume zetu kwa usahihi

Mallya: Mmeangalia pamoja na Askari Majina wenza wenu hamjayaona, nini Kiliendelea baada ya hapo?

Mallya? wakati anaangalia Majina ya wame zenu Nyie Mlishiriki Vipi?

Tukajitambulisha kwa Askari wa zamu akaangalia kwenye kitabu, Majina yao hayakwepo

Shahidi: tulitoka Kituo cha Polisi Central Police tukaenda Oysterbay

Mallya: baada ya Kuwakosa Central nini kilifuata

Shahidi: tulienda Tazara

Mallya: Unaweza Kueleza Kwanini Mlienda Tazara

Mallya: Unaweza Kuiambaia Mahakama mara zote mlipokuwa mnatafuta mlikuwa mnawatafuta kwa Namna gani

Shahidi: mara zote tunataja Majina na Mimi nilitaja Jina la Mme wangu Adamu Khalfani Kasekwa

Shahidi: tulienda kwa Sababu tulikuwa kwenye Kuendelea kuwatafuta Kituo gani cha Polisi wamepelekwa

Mallya: Kitu gani Kilifuata

Mallya: Kitu gani Kilifuata

Shahidi: Hatukuyaona Majina yao

Shahidi: Hatukuyaona Majina yao

Mallya: Mmeshaenda Vituo Vinnne Kutafuta wenza wenu, hatua gani ilifuata baada ya hapo?

Shahidi: Tulirudi Nyumbani kwa sababu Muda ulikuwa umeenda, na tuliacha watoto wadogo

Mallya: Nyumbani kwa Maana Wapi?

Shahidi: Kwa Mke wa Bwire

Mallya: kwa Mazungumzo yako na Mke wa Bwire alikwambia nini kimetokea Kule Moshi

Jaji: twendeni Taratibu, Mmeshazunguka Vituo Vyote ilikuwa siku gani..?

Shahidi: akaniambia Kule Moshi kuna wifi yake ambaye ni Dada wa Mohammed Abdilah Ling'wenya

Jaji: ooohhh tunakosa Mtiririko kwa sababu nilikuwa bado nipo kwenye Vituo Vya Polisi

Shahidi: Tarehe 13

Mallya: Samahani Mheshimiwa Jaji nilirudi Nyuma Kumuuliza kama waliongea na Mke wa Bwire

Mallya: Nini kilifuata

Shahidi Kwamba Wifi yake amempigia Simu Kuwa Adam wakiwa Moshi na Mohammed akiwa anakunywa Chai Adamu alikuwa anazungumza na Simu ,ikawa kama kelele za Mvutano,Niache niache baada ya hapo wakawa wanamvuta Kumleta Sehemu za Vyakula sasa

Mallya: alikwambia nini sasa?

Shahidi: Kwamba alikuwa amepigwa akawa anavuja Damu,

Jaji: hii ni Habari ambayo umesema Umeambiwa na Mke wa nani..?

Shahidi: Mke wa Ling'wenya Tukiwa kwa Mke wa Bwire

Jaji: nafikiri tulirudi kwenye Mstari hapo tunaanza kuzungumzia "Here say" yeye kaambiwa na Mke wa Ling'wenya na Mke w Ling'wenya kaambiwa na Wifi nafikiri Mkiona Kuna Umuhimu mumuite Wifi aje kutoa Ushahidi ila Hatuwezi Kwenda hivyo.

Mallya: huyo wifi yake anaitwa nani?

Shahidi: anaitwa Athima

Mallya: Mliporudi Nyumbani ikawaje?

Mallya: sawa Mheshimiwa Jaji

Mallya: Mlikuwa na Nyenzo gani katika Kuwatafuta

Shahidi: tulikubaliana tupite Hospitalini

Shahidi: Tulikuwa na Picha zao

Shahidi: tulianzia Hospitali ya Muhimbili

Mallya: na Mlianzia Wapi?

Shahidi: Ni baada ya Kuwakosa Kwenye Vituo vya Polisi

Jaji: Kwanini Mlianza Kuwatafuta Kwenye Mahospitali

Jaji: Kwa Off Record tuh,Moshi waliwambiaje

Shahidi: kwamba huku hawapo wameletwa Dar es salaam tukahisi labda wamepata Ajali

Shahidi: Tukajitambulisha na kueleza kuwa tunawatafuta Wame zetu

Mallya: Mlipofika Muhimbili ikawaje

Shahidi: tulizunguka Kwenye wodi na Monchwari hatukuwaona

Mallya: nini Kikafuata

Shahidi: Tukaenda Hospitali ya Amana, Tukajitambulisha na Kuingia Kwenye Mawodi na Monchwari hatukuwaona pia

Shahidi: tulienda Mwananyamala tukajitambulisha na Kuwatafuta wame zetu kwenye Mawodi na Mochwari hatuwaona

Mallya: baada ya Amana?

Mallya: Siku ya tatu Sasa Mmeeanda Muhimbili, Amana na Mwananyamala mkawakosa, Ulichukua hatua gani

Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani, kwa Mara ya kwanza Ulipata Taarifa ya Mumewako yupo wapi

Shahidi: ilibidi nirudi Chalinze kwa Sababu nauli ilikuwa imeshaanza kuisha na Kwa sababu nina mawasiliano ikabidi nirudi Chalinze

Shahidi: Mahakamani Kisutu

Shahidi: Ilikuwa kwenye Taarifa Ya Habari ya Jioni

Mallya: uliwaona wakiwa wapi?

Shahidi: ITV

Mallya: Kituo gani Cha Habari?

Mallya: Uliwaona au Ulisimuliwa

Shahidi: niliona

Mallya: wanatuhumiwa kwa Makosa gani

Shahidi: Anashitakiwa kwa Ugaidi na uhujumu Uchumi

Shahidi: kwamba Kuna kazi Imepatikana anaenda kuifanya

Mallya: mara Ya Mwisho Mmewako wakati anakuaga alikwambia anaenda Moshi Kufanya nini?

Mallya: ikawaje?

Mallya: Uliona hiyo Taarifa ya Habari ITV saa ngapi

Shahidi: Ilikuwa Saa 2 za Usiku

Shahidi: Niliwasiliana na wenzangu

Shahidi: tulikubaliana Twende Mahabusu kwa Sababu hatukujua wamepelekwa Mahabusu gani

Mallya: Baada ya hapo nini kilifuata?

Mallya: mkafanya Mawasiliano, Mawasiliano gani

Shahidi: Mzee Ling'wenya alikuja kutoka Mtwara

Mallya: kitu gani alifanya baada ya Kutoka Mtwara Mzee Ling'wenya?

Shahidi: Mimi sikwepo nilikuwa Chalinze, Tulifanya Mawasiliano

Mallya: mlianza kutafuta Mahabusu gani?

Shahidi: Tulikuwa hatuelewi wapo Mahabusu gani, Tulianza kutafuta Mahabusu waliopo

Jaji: ni akina nani?

Mallya: wakakwambiaje?

Shahidi: Kwamba wameenda Keko wamewakosa ila Segerea Wamewakuta wapo

Jaji: Mke wa Ling'wenya na nani..?

Shahidi: Mke wa Mohammed Abdilah Ling'wenya na Mzee Ling'wenya

Shahidi: Na Baba Mke wake,Mzee Ling'wenya

Mallya: sasa Ushajua Mwenza wako yupo Segerea hatua gani ilifuata

Shahidi: Nilikuja Jumapili kutoka Chalinze, Jumatatu tuliamka wote Mke wa Bwire, Ling'wenya tukaenda Wote Segerea

Mallya: Mlipofika Segerea ikawaje?

Mallya: baada hapo ulifanya Hatua gani?

Shahidi: Tulipokelewa na Askari wa Jinsia ya kike akatueleza leo siyo siku ya kuwaona Mahabusu Mje Jumamosi au Junapili

Shahidi: niliskia Ma ASKARI wakisema ndiyo Yule Jamaa ambaye yupo Kabatini

Mallya: ni nani aliteyaongea hayo?

Shahidi: Nilienda Jumamosi

Mallya: hatua gani ilifuata

Shahidi: Wakachukua funguo wakasema tunaenda kumleta

Shahidi: ni Ma Askari niliowaleza Majina kuwa namtafuta Mme wangu

Mallya: Kitu gani kilifuata

Mallya: unaweza Kutuambia hapo ulipokuwepo pana taswira gani ili Mheshimiwa jaji apate Picha?

Shahidi: Ukiingia Segerea maeneo ambayo kuna Meza ya Kuwekea Chakula na Kuna Chuma kama Grill lililotenganisha

Shahidi: Alikuwa amevaa kama Singlendi

Shahidi: nilimuona Mmewangu akitembea Kwa tabu kama Vile inaonekana ameteswa

Mallya: Unaweza Kukumbuka Mme wako amevaaje?

Mallya: hali yake ilikuwaje?

Shahidi: Amedhoofika, alikuwa amekonda Sana

Mallya: Mwendo wake ulikuwaje, alivyokuwa anatembea?

Mallya: Ulichukua hatua gani?

Shahidi: alikuwa anachechemea

Shahidi: Chakula, shuka na Sabuni

Jaji: ulikuwa umeleta Vitu gani

Shahidi: Kama Utaratibu ulivyo wa pale, Nilibeba kwa ajili yake

Shahidi: Askari akishakagua anachukua ukiwa unamuona:

Jaji? Vitu ulimkabidhi nani.?

Mallya? ulisema ulikuwa unamuona Mme wako sasa anaelekea sehemu, Ni sehemu gani

Shahidi: Eneo la Nyavu ambalo mnaweza Kuzungumza

Mallya: ilikuwaje Mazungumzo kati yenu

Shahidi: Nilimuuliza Hali yake na Kilichotokea

Shahidi: Hali yangu ni hivyo hivyo ila siyo Nzuri

Mallya: alikujibu nini?

Mallya: alikwambia kwanini hali yake siyo Nzuri

Mallya: Baada ya Hapo.?

Shahidi: aliniambia Kuna Mateso alipitia wakati yupo Moshi, alipigwa sana Ndiyo Maana Unaniona nipo Kwenye hali hii

Mallya: nitakurudisha Nyuma Kidogo, Kilichokufanya utafute Vituo vya Polisi na Mahospitali Mme wako ni Kitu gani?

Shahidi: alichukuliwa akapelekwa Mahabusu

Wakili wa Serikali: OBJECTION wakili ameshauliza

Wakili wa Serikali Ameshaliuliza hilo swali

Mallya: Sikuuliza, Kama aliulizwa ni Off Records nataka sasa iingie kwenye Records

Jaji: Sijachoka Kuandika, Muulize tena

Mallya: nitakurudisha Nyuma Kidogo, Kilichokufanya umtatafute Vituo vya Polisi na Mahospitali Mme wako ni Kitu gani?

Shahidi: Kwa sababu tuliambiwa kuwa Walitolewa Moshi Kuja Dar es salaam na tulienda Vituo Vya Polisi Kwa Sababu tuliamini Kama wangetusaidia

Shahidi: alikuja Mama yake, tukaenda naye Moshi

Mallya: Kwanini wewe namba ya Mme wako umesema huikumbuki kwa kichwa mie ya Mke wangu naikumbuka

Mallya: Vipi Kuhusu Ushiriki wa Ndugu zake Mwanamme

Shahidi: Kwa sababu alikuwa na line Mpya aliyotoka Kuisajili

Mallya: Kwanini Unasema Ulipoenda Segerea hali yake ilikuwa tofauti

Shahidi: alikuwa amekonda sana na Macho yameingia Ndani Kama Yameganda, amekonda kwa kweli na Pia Nilimuona akiwa na alama Kwenye Mkono wakati anaenda Moshi alikuwa hana

Mallya: ya kwangu ni hayo

Jaji: ulisema Uliona nini Kwenye Nkono

Shahidi: alama ya Kovu kwenye Mkono, Awali alikuwa hana wakati anaenda Moshi

Jaji: Asante sana Mallya

Lakini tutabreak tena kidogo kama Dakika 17

Jaji: Pamoja Mvua kutuharibia ratiba yetu tutarejea Saa 6 Kamili

Jaji ananyanyuka anatoka


Shahidi anapanda tena Kizimbani

Jaji amerejea


Kesi inatajwa na Washitakiwa wanakaa Kizimbani Kwao

Jaji: Wakili Fredrick Kihwelo kama Unaswali.?

Jaji: Wakili Nashon kama Unaswali lolote

Nashon: Sitokuwa na Swali Kwa Shahidi

Fredrick Kihwelo: sitokuwa na Swali kwa Niaba ya Mshitakiwa wa tatu hatutokuwa na Swali

Jaji: Wakili Kibatala kwa niaba ya Mashtakiwa wa Nne

Kibatala: Shahidi Ulijisikiaje uliporudi Nyumbani Kukuta Nyumba yako Imevunjwa na Mme wako alikuwa hapatikani Muda wote

Shahidi: Niliogopa Kwanza Nilihisi ni wezi

Kibatala: Ulitegemea kuwa Polisi wanaweza kufanya hivyo?

Shahidi: Hapana sikuwahi Kutegemea Polisi wanaweza Kufanya tendo hilo

Kibatala: Umeongelea kwamba Ulikuta Tv na Vingime Kukuta Vipo, ila Kadi ya Pikipiki na Hati ya Kiwanja Vilikuwa Vimechukuliwa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mpaka leo hii Ujawahi kuambiwa kuwa nani ana hivyo vitu Kituo cha Polisi Chalinze au afisa yoyote wa Polisi?

Shahidi: Hakuna aliye wahi Kuniambia

Shahidi: Sahihi sijui nani nimdai

Kibatala: Mpaka leo hii Ujui nani wa Kumdai hivyo Vitu?

Kibatala: Kuna Mgogoro wowote wa Kiwanja sehemu unayoishi au Kupelekwa hata Kwa Mjumbe?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ushawahi Kujua Kwanini Adamoo alisimamishwa kazi au Utumiahi wake wa Kijeshi Ulivyokomea

Kibatala: Sawa tuachane na hilo

Shahidi: Nafikiri huko kwenye Mambo ya Kijeshi tusiende Sana Miye sijui lolote kuhusu Jeshi

Kibatala: nimesikia kuwa ulienda Kumtafuta Mmeo Vituo Vya Polisi, Naomba Nikuonyeshe Kielelezo Namba 1 Kitabu fulani

Kibatala: unasema ulienda Polisi ukaoneshwa Kijitabu kama hiki au Kinachofanana na Hili na bado baada ya Kupekua hukuona Kitabu kama hiki?

Mahakama inampatia Kibatala Kielelezo DETENTION REGISTER

Kibatala:
na Bado Jina la Mme hakuliwepo?

Kibatala: unasababu yoyote ya Kutunga Story ya Uongo kuwa Hukwenda Polisi Central alafu leo Uje useme ulienda Polisi Central, Je unasababu yoyote ya Kutunga?

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Hapana sina Sababu yoyote

Kibatala: Nimesikia Kuwa kilichowafanya Muanze Kutafuta Dar es salaam baada ya Mke wa Ling'wenya, kuwasiliana na Dada yake Ling'wenya Kule Moshi, akasema kuwa Adamoo na Ling'wenya Wameletwa Dar es salaam

Shahidi; Ndiyo

Kibatala: Je nilikusikia Sahihi

Kibatala: Nimekusikia Sahihi Kuwa Mlipita Kote ikiwemo Chang'ombe, Central Station, na Tazara pamoja na Vyumba Vya Kuhifadhia Maiti kwa sababu ya Kukosa Taarifa?

Kibatala: Mlilazimika Kufunguliwa Mwili Mmoja baada ya Mwingine Kwenye vyumba vya Kuhifadhia Maiti

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Ndiyo Nililazimika Kufungukiwa Maiti Moja baada ya Nyingine ilikuweza kuthibitisha kama Mmewangu yupo huko

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ni sahihi Kwamba wakati unapitia hali hii ulikuwa na Miaka 25 tuh.?

Kibatala: na Wakati huo ulikuwa na Mtoto Mdogo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: wakati huo Ulikuwa kwenye Ndoa kwa muda gani Mpaka unapitia Matukio haya Mazito Matatu?

Jaji: Hesabu zenu zipo Vizuri?

Jaji: naona hakuna tatizo Mtu kukosea hesabu Mahakamani,Hilo swali tunaweza Kuliacha

Kibatala: Minne

Kutoka 2016 August Mpaka 2020 ni Miaka Mingapi?

Kibatala: Asante Mheshimiwa Jaji ni hayo tuh

Shahidi: ni baada ya Tarehe 09

Kibatala ni Sahihi wakati nakuja kupekuliwa Ilikuwa ni Kabla ya Tarehe 09 au ni baada ya tarehe 09

Shahidi: Ndiyo tuendeleee

Jaji: Shahidi unanguvu za Kuendelea Kujibu??

Jaji: wakili gani Serikali ataanza Kuuliza Maswali

Wakili Kidando: ataanza Jenitreza Kitali

Wakili wa Serikali: Jenitreza Kitali Ni sahihi Shahidi Umesema Adamu ni Mme wako

Wakili wa Serikali Jenitreza: Ni sahihi ujatoa Cheti Cha Ndoa

Wakili wa Serikali: Ni sahihi umesema Kuwa Adamu walikuaga wanaenda Moshi Mwanzoni Mwa Mwezi wa nane

Shahidi: ni sahihi

Wakili wa Serikali: ni kweli umeeleza Kuwa walikuaga wanaenda Kwa Mheshimiwa Mbowe

Shahidi: Sahihi

Wakili wa Serikali Jenitreza: ni kweli au Si Kweli Mme wako na Ling'wenya walikuwa marafiki sana

Wakili wa Serikali: Mme wako pamoja na Ling'wenya waliondoka Pamoja Chalinze, Sahihi.?

Shahidi: Sahihi

Shahidi: Nikweli

Wakili wa Serikali Jenitreza: wakati Mmewako anajianda Kwa ajili ya Safari, Mazingira ya Nyumba yenu yakoje?

Shahidi: Nyumba ya Vyumba Vinne, Kuna Seble Dinning na Choo

Wakili wa Serikali: Wakati Mmeo anajiandaa na Safari nitakuwa sahihi nikisema Kuwa Adamu alikuwa ndani ya Chumba wakati Mgeni akiwa Sebleni

Shahidi: Sikusema, Sikumbuki ilikuwa tarehe ngapi

Shahidi: Sahihi Mgeni alikuwa sebleni

Wakili wa Serikali: Katika Ushahidi wako Mwanzo Mpaka Mwisho ujasema ni lini walianza Safari?

Wakili wa Serikali: nitakuwa sahihi kama nitasema kama ukumbuki tarehe na unachokisema siyo sahihi?

Shahidi: sikumbuki tarehe lakini walianza Kusafiri panoja Mwishoni mwa Mwezi wa Saba

Wakili wa Serikali: baada ya Adamu na Ling'wenya Kufika Moshi ulipewa taarifa kwamba Wamekatwa.?

Shahidi: Niliambiwa

Wakili wa Serikali: aliyeniambia ni Mke wa Ling'wenya, nitakuwa sahihi kuwa Mtu aliyekwambia wamekamatwa Moshi siyo Mtu aliyekwepo wakati wanakamatwa Moshi?

Shahidi: ni sahihi

Wakili wa Serikali: Naomba Nikurejeshe Nyuma, Wakati Mmeo anajianda na Safari, Ling'wenya aliakuwa sebleni, Ni kweli Ling'wenya hakujua Vitu gani Vimewekwa Katika begi

Shahidi: ni sahihi awezi Kujua

kweli au si Kweli

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba Ujaiambia Mahakama kwamba wakati Mmeao anapakia Vitu vyake alibeba Vitu hivi na hivi

Shahidi: Si kweli

Wakili wa Serikali: Ni kweli umesema Kwamba Adamu alipigwa Moshi Mpaka akatoa damu

Mallya: OBJECTION hicho anachouliza Tayari Mahakama ishatoa Malekezo kuhusu Here say

Jaji: ngoja niseme kuwa wakati tunaanza zoezi nilisema Vitu amabavyo Shahidi anaweza asiulizwe ni Vile Vinavyotezwa Utu wake

Jaji: Wakili wa Serikali

Wakili wa Serikali: labda Mahakama ituonyeshe kama Ilitia Muongozo huo

Wakili wa Serikali: ulisema ulisikia kuwa Adamuu amepigwa Mpaka Kutoa Damu

Jaji: sasa Vingime Vyote unaweza Kuuliza na anaweza Kujibu

Shahidi: Sahihi

Wakili wa Serikali: Umesema Ulisema kuwa baada ya Kuwa hapatikani kwenye simu mlianza kumtafuta Vituo vya Polisi

Shahidi: kweli

Wakili wa Serikali: Mlianza kituo gani cha Polisi

Shahidi: Kituo cha Polisi Chang'ombe

Wakili wa Serikali: Mlipofika Kituo cha Polisi wewe na wenzako mlianza Kuomba Huyo Mtu aangaliwe kama yupo Kituoni hapo

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: ilikuwa tarehe ngapi

Jaji: Mwenzi wa Ngapi?

Shahidi tarehe 13 Mwezi wa 09

Shahidi: Mwezi wa 08

Shahidi: Mwezi wa 08

Jaji: sasa niandike lipi Mwezi wa 08 au 09

Wakili wa Serikali: Utakubaliana na Mimi kuwa wakati Nyumba inasachiwa hukuwepo

Shahidi: ndiyo nimeeleza

Wakili wa Serikali: Utakubaliana na Mimi kuwa wakati Nyumba inasachiwa hukuwepo

Wakili wa Serikali: Kwahiyo Maneno ya kwamba Kuna Vitu vimechukuliwa ni Maneno ya Kuambiwa

Shahidi: Ndiyo sikumtafuta

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukosekana Adamu Mpaka wakati unamtafuta hukuwahi Kumtafuta Mheshimiwa Mbowe mbali na Kwamba walikwambia wanaenda Moshi kufanya kazi kwake

Shahidi: Nilifuata Utaratibu

Wakili wa Serikali: ujaieleza mahakama kwamba Wakati Mnaenda Monchwari mlifuata Utaratibu wa kukagua

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Lakini wakati unatoa Ushahidi Hukusema ni Taratibu zipi ulizifuata?

Wakili wa Serikali: Lakini wakati unatoa Ushahidi Hukusema ni Taratibu zipi ulizifuata.?

Wakili wa Serikali: Wakati wote wa Shauri hili linaendelea Mahakamani ulipata kulifuatilia.?

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Kwa Njia gani.?

Hadhana inalia

Mahakama bado ipo kimya

Wakili wa Serikali: Kwa Njia gani

Jaji: anamuomba Wakili wa serikali akae Kidogo

Mahakama Kimyaaaaaaa

Jaji: tuendeleeee

Shahidi: Nilisikia kupitia Vyombo vya Habari na Yeye pia aliniambia

Wakili wa Serikali: Ni sahihi kwamba Wakati Mmeo anaelekea Moshia alikuwa ni Mzima wa Afya na hakuwa na Majeraha?

Wakili wa Serikali: Kwakuwa ulikuwa unafuatilia Kesi hii kwenye vyombo Vya Habari, na Kwakuwa Ushahidi uliokuwa Unaendelea Kuwa Adam Kasekwa kateswa, Ni sahihi Ulisikia?

Shahidi: Niliona Kwenye Mikono

Shahidi: Ni sahihi

Wakili wa Serikali: na wakati unamtembelea Segerea Uliona Makovu ,Je uliyaona wapi?

Wakili wa Serikali: Kwenye Mikono yote Miwili?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Wewe kama Mke wa Adamu Kasekwa utakubaliana na Mimi kuwa Unaieleza Mahakama kama Adama Kasekwa aliwahi Kuwa na Makovu Mengine kabla ya wewe Kumkuta na hayo Segerea?

Shahidi: Ni sahihi

Shahidi: Ndiyo baada ya kuona anachechemea

Wakili wa Serikali: Adamu Kasekwa alipokuwa Segerea, Mshitakiwa alimweleza kuwa amepigwa

Shahidi: Sikueleza lini

Wakili wa Serikali: lakini hukueleza Mahakama kama alipigwa Wapi na lini

Wakili wa Serikali: Unaifahamu sana Dar es salaam

Shahidi: Kiasi Kidogo

Wakili wa Serikali: Ulisema Ulitembelea Vituo vya Tazara, Chang'ombe, Central na Oysterbay

Shahidi: Nisahihi sikusema Sababu

Wakili wa Serikali: Hukuiambia Mahakama Sababu ya kwanini hukutembelea Vituo Vingie vidogo

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Ni sahihi ulimuona Adamu amakekonda sana

Wakili wa sarikali: huku ieleza Mahakama kwanini alikonda?

Shahidi: ni Sahihi

Wakili Jenitreza Kitali: naomba Niwachie wenzangu


Anasimama Wakili Robert Kidando


Shahidi:
Ni sahihi sikueleza Sababu za Kukonda

Wakili wa Serikali: Uwezi Kujua kama alikuwa ameridhia?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali Kidando: Mpaka siku Nyumba yako inafanyiwa Upekuzi, Ni kweli ulikuwa hujui Adam yupo wapi.?

Shahidi: Sijui

Wakili wa Serikali: Mpaka sasa Askari waliovaa Uniforms Ujui walikuwa ni akina nani.?

Shahidi: Ndiyo sijui kwa sababu Sikwepo

Wakili wa Serikali: na Mpaka sasa wale waliovalia Kiraia ujui walikuwa wakina nani

Wakili wa Serikali: na pale Chalinze Mtaa wako Unaoishi unasema unaitwaje

Shahidi: Ramboni

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Na Nyumba yako bila shaka itakuwa na Grill/Geti

Wakili wa Serikali: na ulikuwa umelifungwa

Shahidi: Hapana,alikwepo Mjumbe wa Nyumba 10

Shahidi: hapana huwa naurudishia, Mlango ndiyo huwa nafunga

Wakili wa Serikali: Baada ya kwenda kwa Jirani yako Kuuliza alikwambia Mwenyekiti wa Mtaa alikwepo.?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Mpaka sasa yupo pale Chalinze?

Wakili wa Serikali: Unasema uliambiwa Kuwa Wamechukua begi la Adamu alilotoka nalo Congo, Je lipo tofauti na Sare za Jeshi la JWTZ

Shahidi: Lipo tofauti na Mabaka Mabaka ya Tanzania

Shahidi: Mabaka Mabaka ambayo ni Maua ya Sare za JWTZ yapo tofauli na Mabakamabaka ya lile begi

Mahakama Kichekooooooo

Jaji
: Iweke Vizuri mabaka mabaka ya Nini,Isije kuwa unasema Watanzania Wanamabaka Maabaka

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Ukumbuki tarehe ambazo waliondoka Kwenda Moshi?

Jaji: hapo Umeweka Sawa

Shahidi: Ndiyo Sikumbuki

Shahidi: Ndiyo inawezekana

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Inaweza ikawa hata Mwishoni mwa Mwezi wa 07

Wakili wa Serikali: Ujaieleza mahakama kama Mmeo aliondoka na kiasi gani cha fedha

Wakili wa Serikali: Ujaeleza Kwamba wakati wanaenda Moshi Walitumia usafiri gani.?

Shahidi: Sijaeleza

Shahidi: Sijaeleza Ila walitumia Usafiri wa Basi

Wakili wa Serikali: umeeleza Polisi walichukua Kadi ya Pikipiki na Hati, ila Ujasema Ni Pikipiki ya aina gani wala namba gani, Ujasema

Shahidi: Ndiyo Sijasema

Shahid: Sijasema

Wakili wa Serikali: Pia Mahakamani ujasema Namba ya Kiwanja wala Brock au namba ya hati ya kiwanja

Wakili wa Serikali: Ujasema Pia Kuwa hiyo Pikipiki ama kiwanja Vimesajiliwa kwa Jina la nani

Wakili wa Serikali: turudi kabla hawajaondoka Kwenda Moshi, Ulisema walienda Kwanza Morogoro wakarudi

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Sijasema

Shahidi: Sijasema

Wakili wa Serikali: Ila Ujasema kwamba Morogoro walienda kufanya Nini.?

Wakili wa Serikali: kwa Sababu ulisema kadi ya Pikipiki ilichukuliwa, Ujasema pikipiki hiyo ipo wapi?

Wakili wa Serikali: Tuje 05 Mwezi 08 2020 Kwamba Uliwasiliana na Adam Kasekwa kuwajulia hali wewe na Watoto, akasema subiri nitakupigia, Lakini Hakukupigia tena

Shahidi: Sijasema

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: na hakukupigia

Shahidi: Hakunipigia

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: na Ilipofika Jioni wewe Mwenyewe uliamua kumtafuta

Wakili wa Serikali: na Ujasema mahakamani kwamba Kazi hiyo ya Ulinzi alikuwa ameianza

Tutaendelea Saa 8 Na Dakika 15

Jaji: Wakili trubreak Kidogo Kwa Saa 1

Kwa hiyo naahirisha Shauri hili Mpaka Saa 8 na Dakika 15

Mawakili wa Serikali Wanasema wao wapo tayari

Kesi Imetajwa tena

Jaji: nakukumbusha kuwa upo chini ya kiapo ,Wakili wa Serikali atakuuliza Maswali au Bado

Mawakili wa Utetezi wapo tayari na wao

Jaji: Wakili Ungependa Nikukumbushe

Wakili wa Serikali: Kabla ya Tarehe 05 palikuwa hakuna tatizo, Ni sahihi Kwamba hamkuwasiliana na Mohammed Ling'wenya kabisa

Wakili wa Serikali Liliani: Kipindi chote Mmeo Adam Kasekwa kipindi yupo Moshi, Ni kweli Kuwa Ujaiambia Mahakama Mmeao alikuwa anaishi wapi huko Moshi

Shahidi: Sijasema

Wakili wa Serikali: Nikweli kwamba wakati Mmepoteza Mawasiliano na Mmeo Adam Kasekwa Mpaka Mnaenda Mahospitali ulikuwa ujaongea na Athima Dada yake Ling'wenya?

Shahidi: Hatukukuwasiliana naye

Shahidi: Ni sahihi Nilikuwa sijaongea naye

Wakili wa Serikali: Na Taarifa za Kwamba Wamekatwa Kule Moshi, Ulizipata Kwa Mke wa Mohammed Ling'wenya

Shahidi: Sahihi

Shahidi: Ndivyo alivyoniambia

Wakili wa Serikali: Wakati Mnamtafuta Vituoni, Ujasema katika Ushahidi wako Kwamba hujamuona Kamanda wa Kanda Maalum ya polisi Dar es salaam wala Kiongozi wa Polisi yoyote?

Wakili wa Serikali: Na Kwamba wamesafirishwa Kuja Dar es salaam na Polisi.

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Sijasema

Wakili wa Serikali: Hapa Mahakamani Umeonyeshwa Kitabu kuwa kilikuwa na Kitu gani kinacho fanya Kufanana na Vitabu Vingine kule kituoni

Wakili wa Serikali: Na hufahamu Kwenye Kitabu kuna Mahitaji gani yanayomuongoza Askari Kukitunza au Kukiandika, Hizo taratibu huzifahamu?

Wakili wa Serikali: Ni kweli Kwamba Wakati Mkipita Vituo Vya Polisi Tarehe 13 08 2020 nipo sahihi

Shahidi: Sizifahamu

Wakili wa Serikali: Na Kule Mlipoenda Mochwari ilikuwa tarehe 14 Mwezi 08 2020

Shahidi: Upo sahihi

Shahidi: Kweli

Wakili wa Serikali: Tuje Ukaguzi wa Mochwari Ujasema Kama ulionyeshwa Miili ya waliokufa wote au Ile isiyotambuliwa na Ndugu zao

Shahidi: Sijasema

Shahidi: Sijasema hayo

Wakili wa Serikali: Ulitaja Hospitali 3 tofauti, Muhimbili, Amana na Mwananyamala Ujasema Hospitali hizi Hapa. Dar es salaam zipo wilaya gani

Shahidi: Sijasema

Wakili wa Serikali: Ujatumabia Kuwa katika Kila Monchwari Jina la Afisa wa Monchwari aliye waruhusu kukagua Miili

Wakili wa Serikali: Ujasema Katika Kila Moja ya Monchwari hizo Hospitalini ni Miili Mingapi Mliikagua

Shahidi: Sijasema

Wakili wa Serikali: Wala Ujasema Cheo Chake

Wakili wa Serikali: Mlipokuwa pale Hospitali na hata sasa, Kama Kweli Mlikagua Miili, Mlikuwa mnakiuka taratibu za Afya

Shahidi: Nilikuwa sifahamu kama nakiuka taratibu

Shahidi: Hapana Sijasema

Wakili wa Serikali: Tueleze Kama Unafahamu na kama Umeeleza Katika Ushahidi Wako, Kama Taratibu za Kujilinda Ki Afya ulizingatia kama Ulivyojikinga na Barakoa hapa Mahakamani

Shahidi: Nilijikinga, Nilivaa Barakoa

Wakili wa Serikali: Lakini Ujasema Katika Ushahidi Wako

Wakili wa Serikali: Kwanini Umevaa Barakoa Leo..?

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Ndiyo najikinga na Virusi vya Corona

Wakili wa Serikali: Na tatizo hilo Mwaka jana lilikwepo

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Hapana Sijaidanganya Mahakama

Wakili wa Serikali: Wewe Umesema Ujawahi Kuwasiliana Moja Kwa Moja tangu tukio la Kukamatwa Kwa Adamu Kasekwa

Wakili wa Serikali: Je unakubali unaidanganya Mahakama Kwa Sababu wasingekuruhusu uingie tuh Kukagua Miili

Shahidi: Ndiyo sijawahi

Wakili wa Serikali: Katika Ushahidi Uliopo Mahakamani, Adamu ajawahi Kusema Mahakamani Kwamba alipokuwa Moshi aliwahi Kupigwa na Kutoa Damu Je unaweza kutuambia hizi taarifa ulipozitoa .?

Shahidi: Ndiyo sikuwahi Kuwa Moshi

Shahidi: Kama nilivyosema Mwanzo, Kwamba Hizi taarifa Nilizipokea Kwa Mke wa Ling'wenya na Yeye alizitoa kwa Wifi yake huko Moshi

Wakili wa Serikali: Mambo yaliyokuwa yanaendelea Moshi Hakuna hata Moja Ulilowahi kushuhudia

Wakili wa Serikali: Utakubaliana na Mimi Kwamba Ujawahi Kutoa taarifa iwe Serikali ya Mtaa au Polisi

Wakili wa Serikali: Kwa Sababu Hukutoa Taarifa Polisi na Hukuwa na Taarifa kwamba amekufa,Wewe Ukaenda kukagua Monchwari

Shahidi: Nilienda Ndiyo

Wakili wa Serikali: tuje katika Tukio unalodai Kwamba Nyumbani Kwenu pale Chalinze, Umekubali Kuwa Palikuwa Mjumbe wa Serikali ya Mtaa na Unice Charles, Wakati wa Upekuzi wewe hukuwepo na wao walikwepo, Sema Kama Umeongea nao waje Kutoa ushahidi

Shahidi: Siyo kazi yangu kuleta Mashahidi

Shahidi: Sina taarifa


Wakili wa Serikali: Unataarifa kuwa siku ya Upekuzi Walikuwa na Adam kasekwa

Shahidi: Mimi Kama Mwenyenyumba Ndiyo nasema nina Mlango Wa Grill na Mlango wa kawaida, ambao Ulivunjwa

Wakili wa Serikali: Ulisema Ulipoenda Segerea Unasema Ulimuona Adam Kasekwa alikuwa na Makovu, je yalikuwa Maeneo gani ka unaweza Kuonyesha?

Wakili wa Serikali: kwa sababu wewe Hukuwepo ,na Sababu wanasema kuwa Nyumba yenu ina Grill tuh haina Mlango

Shahidi: Maeneo Hayaaa ( Naonyesha Kwenye Joint za Mikono kabla ya Kiganja kwa kuzungusha Mikono)

Shahidi: Ilikuwa Jumamosi, Nikaja Jumapili na siku iliyofuata Jumatatu tukaenda lakini hatukuruhusiwa

Wakili wa Serikali Unasema Uliona Taaarifa zake Kwenye Taarifa za Habari ilichukua muda Muda gani kwenda kumuona

Wakili wa Serikali: Sasa Wewe huna Uhakika?

Wakili wa Serikali: Ikatokea Kuna tofauti ya Sehemu anayosema Adam na unayo onyesha wewe nani atakuwa anaongea Ukweli

Shahidi: Ni yeye Adam ndiye aliyeumia

Shahidi: Naongea Nilichokiona

Wakili wa Serikali Ndiyo Sasa ailitokeaaaaa.......

Jaji: Ndiyo amejibu hilo swali

Wakili wa Serikali: Naomba Mahakama iseme kama Imerekodi kuwa amejibu

Mallya: OBJECTION nafikiri Shahidi ameshajibu swali

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Umesema Kuna namba uliyokuwa unatumia kumpigia Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: Sawa Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali: Unayo hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali: lakini Hukuimba Mahakama ruhusa ya Kuionyesha

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Ndiyo sikuomba

Wakili wa Serikali: Ulisema Ile hati ya kiwanja hujui wapi pa Kuanzia

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Hukusema kwenye Ushahidi wako kama ulimuuliza Mkuu wa Upelelezi alikuwa navyo au hakuwa navyo

Shahidi: Sikusema

Mawakili wa Serikali Wanashauriana Kidogo

Mahakama bado ipo Kimya

Jaji:
Ndiyoo

Wanapitishaiana Vikaratasi

Wananong'ona


Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji mimi nimemaliza naomba Mwenzangu aendelee

Bado wapo wapo Kimyaaaa

Jaji:
Shahidi bado una nguvu ya Kuendelea?

Jaji: Sawa lakini Msirudierudie maswali kama yameshaulizwa

Shahidi: Hapana

Wakili wa Serikali: Kwanini Wakili alikuwa anawasiwasi kuwa unatunga Story

Wakili wa Serikali Liliani wewe ushawahi Kutunga Story.?

Shahidi: nilivyomuelewa nilimwamba Mimi siwezi Kutunga story, kwa sababu mimi ni mke Wake nilihusika Sehemu zote

Shahidi: nimemuelewa Vizuri labda wewe Hukumuelewa

Wakili wa Serikali kwanini Sasa wakili akuulize?

Jaji: wakili endelea Sasa

Shahidi: Nimeelewa Mimi ni Muhusika kama Mke wake siyo wa Kuadithiwa

Jaji: wewe Shahidi Umeelewaje

Wakili wa Serikali: Lakini Kibatala alikuuliza hilo Swali

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: wewe na Polisi nani anaweza Kukizungumzia kile kitabu?

Wakili wa Serikali: ulionyeshwa Kitabu fulani hapa Kuwa vinafanana na Vile mlivyokuwa mnapekua

Shahidi: Polisi

Wakili wa Serikali: Ni kweli ulishindwa Kutaja namba ya Mme wako

Shahidi: Ni kweli ilikua namba Ngeni Imetoka Kusajiliwa

Jaji: Sasa Namba Mpya anaishikaje Kichwani?

Wakili wa Serikali: Ni kweli Leo Ujamuonyesha kuwa Yule pale ndiyo Adamu kasekwa

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Ndiyo nimeeleza Kinafanana kwa Nje

Jaji: Unamaanisha kuwa anaweza asiwe anamfahamu Mme wake?

Wakili wa Serikali: Ni kweli kwamba kwenye Kile Kitabu ujaangalia Ndani Kuna nini?

Shahidi: Nilishirikiana nao kwa Njia ya simu, wengi wapo Mbeya

Wakili wa Serikali: Unasema uliambiwa ameshatolewa Moshi Kuja Dar es salaam? Ni kweli Kwamba Ujawasiliana na Ndugu zake Adamu wakati wote?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: ukiwa unajua yupp Polisi lakini ukaenda Mochwari

Shahidi: Nilienda Polisi kwanza sababu sikuwa na fahamu
HIVI VYOMBO VYA DOLA HAVIJAGUNDUA TU KWAMBA HII KESI INAIVUA NGUO SERIKALI MBELE YA DUNIA NA KUFUNUA WAZI SIRI ZA SERIKALI NA NCHI? NAWAAMBIA HAO WATU WA KILA AINA WANAOIFUATILIA HIYO KESI WANAPATA TAARIFA MUHIMU MNO AMBAZO NI HATARI KWA NCHI KIUSALAMA. UTENDAJI WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA UNAANIKWA WAZI. IPO SIKU TUTASHANGAA KITABU KINAANDIKWA MAMBO YA AJABU KUHUSU TANZANIA. JE, MNAWAFAHAMU VIZURI HAO WANAOHUDHURIA HAPO MAHAKAMANI? WENGINE NI KUTOKA NJE YA NCHI. HAO MAKOMANDOO WA JESHI WANAFUNUA SIRI AMBAZO HAZISTAHILI KUTOKA NJE YA JESHI LENYEWE. KWANINI SERIKALI INAKUBALI MAMBO YA SIRI ZA NCHI YAANIKWE HADHARANI?
 
HIVI VYOMBO VYA DOLA HAVIJAGUNDUA TU KWAMBA HII KESI INAIVUA NGUO SERIKALI MBELE YA DUNIA NA KUFUNUA WAZI SIRI ZA SERIKALI NA NCHI? NAWAAMBIA HAO WATU WA KILA AINA WANAOIFUATILIA HIYO KESI WANAPATA TAARIFA MUHIMU MNO AMBAZO NI HATARI KWA NCHI KIUSALAMA. UTENDAJI WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA UNAANIKWA WAZI. IPO SIKU TUTASHANGAA KITABU KINAANDIKWA MAMBO YA AJABU KUHUSU TANZANIA. JE, MNAWAFAHAMU VIZURI HAO WANAOHUDHURIA HAPO MAHAKAMANI? WENGINE NI KUTOKA NJE YA NCHI. HAO MAKOMANDOO WA JESHI WANAFUNUA SIRI AMBAZO HAZISTAHILI KUTOKA NJE YA JESHI LENYEWE. KWANINI SERIKALI INAKUBALI MAMBO YA SIRI ZA NCHI YAANIKWE HADHARANI?
Fafanua kivipi. Kesi ngumu hii.
 
Unajaribu kumlaumu nani? Raisi samia eti?

Kwa taarifa yako hawa watu walifanyiwa huu unyama wakati wa mwendazake. Na ujue,serikalini watu wa mwendazake wamejaa,hususani kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Na hii kesi ni initiative yao,siyo ya raisi samia.
Sio yeye aliyeiambia dunia ktk BBC kwamba wana ushahidi wa kutosha?
 
Back
Top Bottom