Karibuni hapa kwa updates kutoka mahakama ya uhujumu uchumi kwenye kesi namba 16 ya mwaka 2021 inayomuhusu mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu...
Watuhumiwa tayari wamefikishwa mahakamani, leo shahidi wa tatu upande wa utetezi ataanza kutoa ushahidi wake.
View attachment 1956923
Mawakili upande wa Utetezi tayari wapo katika ukumbi wa Mahakama. Mawakili upande wa Mashtaka bado wapo Nje.
-------------------------------------------------------------------------
Jaji ameshaingia Sasa Mahakamani, kesi inatajwa.
Wakili wa Serikali: naomba radhi tumeingia wakati umeshaingia
Jaji: sawa
Wakili wa Serikali: Kidando Wakili wa Serikali anatambulisha wenzake
1. Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulimanywa Majigo
Kibatala: anatambulisha Wenzake
Adv. Peter Kibatala
Adv. Jonathan Mndeme
Adv. Fredrick Kiwhelo
Adv. John Malya
Adv. Sisty Aloyce
Adv. Alex Masaba
Adv. Idd Msawanga
Adv. Gaston Garubindi
Adv. Evaresta Kisanga
Adv. Faraj Mangula
Adv. Maria Mushi
Adv. Bonifasia Mapunda
Wakili Dickson Matata: anaombewa Ruhusa Mdogo wake anafanyiwa Operesheni Hospitali ya Lugalo
Jaji: Wakili wa Serikali
Wakili wa serikali: Tumekuja kwa ajili ya kesi ndogo ambapo Shahidi wa tatu yupo tayari kuendelea Kutoa Ushahidi wake
Jaji: John Mallya
Mallya: Tunaye, na Shahidi yupo tayari kutoa Ushahidi
Jaji: anaandika Kidogo na Ukimya wa Mahakama
Jaji: Shahidi wa 3 upande wa Utetezi ambaye ameandaliwa Tafadhali anaweza Kuja
Shahidi Mdada anatokea Nyuma kabisa ya Chumba Cha Mahakama anaenda Kizimbani
Jaji: Shahidi upo Mahakamani ondoa Hofu, nitakuuliza Majina yako na Nitakuapisha, Wakili wa Utetezi atakuongoza na Mawakili wengine watakuuliza Swali na Mawakili wa Serikali watakuuliza Maswali, pia huna Haja ya Kuogopa, tupo hapa kutafuta Haki.
Jaji: Shahidi unaitwa nani
Shahidi: Lilian Kibona, Dini Mkristo Shahidi Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa Ukweli na Ukweli Mtupu, Mungu ni Saidie.
Jaji: Liliani utachagua Kukaa au Kusimama, Hata Ukikaaa nitakuona.
Jaji: wakili Mallya endelea
Mallya: Shahidi Unaishi wapi
Shahidi: Chalinze Mkoa wa Pwani
Mallya: sehemu gani huko Chalinze
Shahidi: Ramboni
Jaji: ni Mtaa.?
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Unaishi na nani..?
Shahidi: Na mme wangu na Watoto ambaye kwa Sasa Mme wangu ameshikiliwa.
Jaji: ni Miongoni Mwa washitakiwa?
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Mme wako anaitwa nani?
Shahidi: Adamu Khalfani Kasekwa
Mallya: hapa nitakuwa namuita Mshitakiwa wa Pili nitakuwa namaanisha pia ni yeye
Shahidi: ndiyo
Mallya: Mmeoana lini, 05/08/2016, Ndoa Ya Kiserikali
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Mlikuwa mnaishi wapi
Shahidi: Pale pale Chalinze
Mallya: unaweza Kukumbuka Mme wako alikuwa anafanya kazi gani wakati huo
Shahidi: Askari Jeshi la JWTZ, kikosi cha 92 Ngerengere
Mallya: alikuwa anafanya kazi gani Nyingine
Shahidi: alikuwa hana kazi Nyingine zaidi ya hiyo ya Serikali
Mallya: naruka nakuja 2020 Mme wako alikuwa anafanya kazi gani
Shahidi: alikuwa anafanya shughuli zake za Biashara
Mallya: Mwanzoni Mwa Mwezi wa Nane Mwaka 2020 unakumbuka Kilitokea Kitu gani kati yako na Mme wako
Shahidi: Mme wangu alikuwa Moshi, tulikuwa tunawasiliana naye Vizuri
Mallya: Kabla ya Kwenda Moshi mlikuwa na Hali gani kati yako na Mme wako
Shahidi: Palikuwa na Mawasiliano
Mallya: kabla hajaenda Moshi kitu gani kilitokea
Shahidi: Rafiki yake Ling'wenya waliwasiliana kuwa kuna Kazi imepatikana Moshi
Mallya: Unaweza Kukumbuka Siku na Saa ya hayo mawasiliano
Shahidi: Hapana sikumbuki
Jaji: unasema palikiwa na Mawasiliano Kati ya Mme wako na Ling'wenya .?
Shahidi: Ndiyo Kwamba Ling'wenya alimpigia Simu kuwa kuna kazi Imepatikana Moshi
Jaji: Ndiyo
Mallya: Simu zilikuwa zinapigwa kati ya Ling'wenya na Mme wako, wewe ulijuaje
Shahidi: Mimi Kama Mke wake alinishirikisha, Mimi kama Mke nilimruhusu
Mallya: Jambo gani lilifanyika, kabla ya Mme wako kwenda Moshi
Shahidi: Nakumbuka walikutana na Ling'wenya wakaenda Kwanza Morogoro, Wakarudi, Waliporudi wakajiandaa Wakaenda Moshi
Mallya: Hali ya Mme wako kiAfya Wakati anaenda Moshi hali yake ilikuwaje
Shahidi: Ilikuwa Nzuri inamruhusu kwenda Kufanya kazi
Mallya: Hali Nzuri unamaanisha nini ,Mwambie Mheshimiwa Jaji
Shahidi: haumwi na Kwamba anaweza Kwenda Moshi
Mallya: kitu gani kilifuata baada ya Kwenda Moshi
Shahidi: alinitaarifu kuwa amefika Moshi
Mallya: mlikuwa mnatumia Njia gani kufanya mazungumzo
Shahidi: kwa Njia ya Simu
Mallya: Siku ya Tarehe 05/08/2020 kitu gani kilitokea
Shahidi: alinipigia na akaongea na watoto, tulipokuwa tunaongea akasema Hebu subiri nikamsubiri
Mallya: ilikuwa Saa ngapi
Shahidi: Kama Saa Moja
Mallya: alipokwambia Subiri kidogo nitakupigia Kidogo kitu gani Kilifuata
Shahidi: Nilipoona Muda umeenda ilipofika Saa 10 ilibidi nimpigie, Simu iliita ikawa imepokelewa lakini Kila nikisema Hallo Sisikii Mtu akiongea
Mallya: Unaweza Kukumbuka namba ya Simu uliyopiga, ambayo ulipiga Ikapokelewa.?
Shahidi: Sikumbuki Kichwani lakini ipo kwenye Simu yangu
Mallya: Baadae kilifuata nini baada ya Simu kutokupokelewa
Shahidi: baadae Ikawa haipatikani
Mallya: kitu gani Kilifuata
Shahidi: kwa kuwa nilikuwa na namba ya Mwenzake Ling'wenya nikampigia Ling'wenya
Mallya: baada ya Kumpigia Ling'wenya.?
Shahidi: Ikawa inaita Mpaka jioni, Mpaka Usiku, Mpaka Kesho yake inaita haipokelewi
Mallya: Sasa wewe ulipata hisia gani baada ya kuona Inaita hadi Kesho yake haipokelewi
Shahidi: niliona labda ni Mambo ya Kazi, sikuwa na wasiwasi wowote
Mallya: Wewe ulichukua hatua gani..?
Shahidi: Sikuwa na namna yoyote zaidi ya Kusubiri simu kutoka kwao
Mallya: umesema una mtoto, anaumri gani
Shahidi: Miaka 3 na Miezi 9
Mallya: Nataka kukupeleka Tarehe 09 Mwezi 08 kitu gani Kilitokea
Shahidi: nakumbuka ilikuwa tarehe 09 mwezi 08 Mwaka 2020 niliamka Asubuhi ikiwa siku ya Jumapili, Mtoto alikuwa anasumbuliwa na tumbo
Jaji: Mtoto wa Jinsia gani
Shahidi: Wa kike
Mallya: kwanini Unakumbuka kuwa ilikuwa Siku ya Jumapili
Shahidi: Sababu ilikuwa Siku ya Ibada
Mallya: Ikawaje
Shahidi: Sikwenda Ibadani badala yake nikaenda Hospitali
Mallya: ikawaje huko Hospitali
Shahidi: Nilipokelewa
Mallya: Hospitali gani
Shahidi: Hospitali ya Serikali pale pale Chalinze
Mallya: baada ya Kupokelewa Hospitali
Shahidi: nilipatiwa Huduma nikarudi Nyumbani
Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani
Shahidi: niliona Miguu ya watu kama Imekanyaga, Wakati natoka Nyumbani nilifunga Mlango lakini niliporudi nikakuta Milango ipo wazi
Mallya: Ule Mlango ulikuwa katika hali gani
Shahidi: Mlango ulikuwa wazi na Kitasa nikakuta kimevunjwa
Mallya: kitu gani kikatokea
Shahidi: kwa akili ya haraka haraka nilijua Wezi, Cha ajabu kila kitu nilikuta Vipo, Kitu kama Tv lakini vipo
Mallya: enheeee ikawaje
Shahidi: Nikaingia Chumbani nikakuta Nguo zimemwagwa Chini
Jaji: Za Mme wako
Shahidi: zote zimemwaga,na Mabegi yamefunguliwa
Shahidi: Kuna begi la jeshi alinunua Congo nilipokuja nikakuta halipo
Jaji: ukisema begi la jeshi alinunua Congo unamaanisha nini
Shahidi: Alinunua Congo Begi lenye Mabaka Mabaka ya Jeshi
Mallya: Kitu gani kilifuata
Shahidi: Nilienda Kuuliza Majirani zangu
Mallya: Jirani yako anaitwa nani.?
Shahidi: Judith Charles
Mallya: lengo la kwenda kwa Jirani lilikuwa nini
Shahidi: nilienda Kuuliza kama Mme wangu amekuja Nyumbani.? wamemuona.? kwamba kuna kitu huenda alikuja Kukitafuta kwa haraka haraka
Mallya: Jirani alikwambiaje
Shahidi: Kuna Magari yalikuja hapa Ya Kipolisi, Moja walikuwa wamevaa Sare na Wengine walikuwa Wamevaa Kiraia
Mallya: Taarifa Nyingine alikupa Jirani yako ni Ipi
Shahidi: kwamba Mapolisi walimuita kwa lengo la Kuniulizia Mimi. baada ya hapo Mapolisi walishuka kwenye gari wakaingia Ndani
Mallya: yeye Jirani alikuwa anafanya nini wakati huo
Shahidi: alikuwa anashuhudia wakati wanaingia ndani ya Nyumba yako
Mallya: Kitu gani kingine walikufahamisha au Kumpatia
Shahidi: walisema walichukua Begi, Vyeti vyake vya Kijeshi vya Adamu, Walichukua Hati ya Uwanja, Kadi ya pikipiki
Mallya: Kitu gani Kingine alikwambia
Shahidi: aliongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze
Mallya: aliyeongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze alikuwa ameongozana na akina nani
Shahidi: Jirani yangu aliongozana na Mkuu wa Upelelezi na aliacha namba ya Simu kwa Jirani.
Jaji: kwa ajili ya Nini
Shahidi: alisema Kama Kuna Lolote ambalo hajalielewa ampigie
Mallya: Siku ya Jumapili 08 Mwezi 09 Nyumba imesachiwa na Umekuta namba ya simu ya Mkuu wa Upelelezi Chalinze, kitu gani Kilifuata baada ya hapo
Shahidi: nilimpigia Simu,yeye aliniambia kuwa alipigiwa tu simu kuwa inabidi waongozane kwenda Kusachi kwenye Nyumba ya Adamu Kasekwa
Mallya: alikufahamisha kuwa alipigiwa Simu na nani..?
Jaji: Mnasikia au Mvua inasababisha Kupoteza Usikivu tuhairishe kidogo.?
Jaji: labda nisikilize Mawakili
Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba tubreak Kidogo kwa Sababu Shahidi akitumia Sana Nguvu anaweza kupoteza Energy na huenda akawa na siku Ndefu
Jaji: upande wa Serikali
Wakili wa Serikali: hatuna Pingamizi
Jaji: kama Mvua imeacha Kidogo, Hebu tuendelee Kidogo, Ikirudi na tukashindwa ,Tutaahirisha
Jaji: uliishia Kuhusu kumpigia simu Mkuu wa Upelelezi Chalinze
Mallya: nilimuuliza Mkuu wa Upelelezi alijibu Kitu gani
Shahidi: alisema amepigiwa simu Kutoka Moshi
Jaji: naona Mvua haitupi Muda wa kuendelea, siwezi Kukadiria kwa muda gani. Kwa muda Mchache nahairisha Shauri, Jaji anatoka Nje.
--------------------------------------------------------
Jaji amerejea Mvua Imekatika Sasa Kesi inatajwa Kesi namba 16 ya Mwaka 2021,Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire, Adam Hassan Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe
Jaji: wakili John Mallya tuendelee
Mallya: Baada ya Kuwa ameshakwambia kuwa alipigiwa simu Kutoka Moshi kitu gani kilifuata
Shahidi: Muda ulikuwa umeshaenda , nikasema itabidi Kesho yake niende kwa sababu sikuamini alichoniambia
Mallya: Kesho yake ikawaje
Jaji: Tunasikilizana, kama Mvua Inanisubiri Mimi, (Imeanza Kunyesha)
Mallya: Ulisema Ulienda Kituoni kesho yake wapi
Shahidi: Kituo cha Chalinze
Jaji: sasa ilikuwa Jumatatu
Mallya: tarehe 05 Umepigia Umemkosa, Tarehe 09 ukakuta kumesachiwa, Kitu gani kilitokea Tarehe 10 Ya Jumatatu pale Kituoni
Shahidi: Nikaomba Kuonana na Mpelelezi, Nilipo muona nikajitambulisha Kuwa Mimi ni Yule Dada ambaye Mmekuja Nyumbani Kusachi
Mallya: akakwambiaje
Shahidi: akasema kama nilivyokueleza sina ambacho nakijua zaidi ya Kuchukuliwa na kuwasindikiza Kwenda Nyumbani Kwako Kusachi,Sina ninachokijua Zaidi
Mallya: Wewe ulikuwa unafanya Jitihada gani zingine
Shahidi: nilianza kutafuta namba za Mke wa Ling'wenya
Mallya: awali ulituambia namba za Ling'wenya ulikuwa nazo na Ukampigia, za Mke wake unazitafuta, Za Ling'wenya ulitoa wapi
Shahidi: ni Mtu wa Karibu wa Mme wangu, Rafiki yake, tuseme siku wanaondoka walikuwa naye
Mallya: ulitumia Njia gani za Kupata namba za Mke wa Ling'wenya
Shahidi: nilimtafuta Mwenzao SHIKUNZI aliyekuwa anaishi nao Kimara
Jaji: Mwenzao, Kwamba alikuwa Askari Jeshi
Shahidi: Ndiyo
Mallya: alikuwa kimara anakaa na nani
Shahidi: alikuwa anakaa karibu na Ling'wenya
Mallya: kikichokufanya Umtafute SHIKUNZI ili umtafute Mke wa Ling'wenya ni nini.?
Shahidi: Nilitaka kumuuliza Mke wa Ling'wenya ili Kumuuliza huko kwake ni nini kilikuwa kinaendelea.?
Jaji: Kwanini hukumtafuta SHIKUNZI.?
Shahidi: walikuwa ni Majirani
Mallya: SHIKUNZI akafanyeje..?
Shahidi: alinipatia namba ya Mke wa Ling'wenya
Mallya: ulifanya hatua gani..?
Shahidi: nilimpigia Mke wa Ling'wenya Ilikuqa siku ya Jumatatu, na yeye akaniambia Siku ya Jumapili ambayo ni Jana yake walienda Nyumbani Kwake wakafanya Upekuzi
Mallya: nini kilifuata baada ya hapo
Shahidi: akaniambia baada ya hapo walienda Kwa Mwingine anaitwa Bwire, tumtafute Mke wa Bwire. nikamwambia wewe huko ni Jirani Mtafute Mke wa Bwire
Mallya: Kitu gani alikueleza Mke wa Ling'wenya
Shahidi: kwamba nilitaka Kujua kama kwake walienda kusachi akaniambia Wameenda kusachi, akaniambia pia tutafute Mke wa Bwire
Mallya: ulipata namba ya Mke wa Bwire na Unaweza kukumbuka Majina yao
Shahidi: Mke wa Bwire anaitwa mama Itham na Mke wa Ling'wenya anaitwa Mama Somoye
Mallya: nini Kinafuata
Shahidi: Mke wa Bwire alikuwa Dar es salaam anakasema Inabidi nitoke Chalinze nije Dar es salaam
Jaji: alisema utoke wapi.?
Shahidi: Chalinze nije Dar es salaam
Mallya: hii sintofahamu yote ilitokana na nini
Shahidi: Kutokana na kutokujua Mwenza wangu yupo wapi, namtafuta simpati alafu Nyumbani wamekuja Kusachi
Mallya: baada ya Kushauriwa Ulichukua hatua gani
Shahidi: Nilitafuta Nauli nikaja Dar es salaam
Mallya: ilikuwa lini.?
Shahidi: Sikumbuki
Mallya: Baada ya Kufika Dar es salaam nini Kilifuata
Shahidi: tulishauriana tuanze Kutafuta Vituo Vyote vya Polisi
Mallya: unaweza Kujua Nyumbani Kwake Bwire
Shahidi: Maeneo ya Temeke
Mallya: Unaweza kukumbuka mlianzia Wapi
Shahidi: Kituo cha Polisi CHANG'OMBE
Mallya: halafu
Shahidi: Tukajitambulisha kuwa sisi Waume zetu Wamekamatwa hatujui wamepelekwa Kituo gani
Mallya: mlimkuta Polisi gani
Shahidi: Polisi wa zamu
Mallya: Mkajitambulishaje..
Shahidi: Kwa Majina yetu na Waume zetu
Mallya: baada ya hapo yule Askari alifanyeje
Shahidi: akaanza kupekua Kitabu kwa kuangalia yale Majina ya waume zetu hatukuyaona
Mallya: Baada ya Kutoyaona Majina ya Mnaowatafuta Kitu gani Kilifuata
Shahidi: tulienda kituo Kingine
Mallya: Kituo gani
Shahidi: Central Police Dar es salaam
Mallya: Ikawaje
Shahidi: vile vile tukajitambukisha ya kwamba, sisi waume zetu wameletwa polisi na hatujui Kituo gani
Mallya: baada ya Kujitambulisha kwa Askari nini Kilifuata
Shahidi: aliangalia kile Kitabu hakuona yale Majina yetu
Mallya: wakati anaangalia Majina ya waume zenu Nyie Mlishiriki Vipi
Shahidi: Wakati anaangalia Kitabu, Wote tuliinama kuangalia Majina ya Waume zetu kwa usahihi
Mallya: Mmeangalia pamoja na Askari Majina ya wenza wenu hamjayaona, nini Kiliendelea baada ya hapi
Shahidi: tulitoka Kituo vha Polisi Central Police tukaenda Oysterbay, Tukajitambulisha kwa Askari wa zamu akaangalia kwenye kitabu, Majina yao, hayakwepo
Mallya: baada ya Kuwakosa Central nini kilifuata
Shahidi: tulienda Tazara
Mallya: unaweza Kueleza Kwanini Mlienda Tazara
Shahidi: tulienda kwa Sababu tulikuwa kwenye Kuendelea kuwatafuta Kituo gani cha Polisi wamepelekwa
Mallya: Unaweza Kuiambaia Mahakama mara zote mlipokuwa mnatafuta mlikuwa mnawatafuta kwa Namna gani
Shahidi: mara zote tunataja Majina na Mimi nilitaja Jina la Mme wangu Adamu Khalfani Kasekwa
Mallya: Kitu gani Kilifuata
Shahidi: Hatukuyaona Majina yao
Mallya: Mmeshaenda Vituo Vinne Kutafuta wenza wenu, hatua gani ilifuata baada ya hapo
Shahidi: Tulirudi Nyumbani kwa sababu Muda ulikuwa umeenda na tuliacha watoto wadogo
Mallya: Nyumbani kwa Maana Wapi
Shahidi: Kwa Mke wa Bwire
Mallya: kwa Mazungumzo yako na Mke wa Bwire alikwambia nini kimetokea Kule Moshi
Shahidi: akaniambia Kule Moshi kuna wifi yake ambaye ni Dada wa Mohammed Abdilah Ling'wenya
Jaji: twendeni Taratibu, Mmeshazunguka Vituo Vyote ilikuwa siku gani..?
Shahidi: Tarehe 13
Jaji: ooohhh tunakosa Mtiririko kwa sababu nilikuwa bado nipo kwenye Vituo Vya Polisi
Mallya: Samahani Mheshimiwa Jaji nilirudi Nyuma Kumuuliza kama waliongea na Mke wa Bwire
Mallya: alikwambia nini sasa
Shahidi: Kwamba Wifi yake amempigia Simu Kuwa Adam wakiwa Moshi na Mohamed, akiwa anakunywa Chai Adamu alikuwa anazungumza na Simu, ikawa kama kelele za Mvutano, Niache niache baada ya hapo wakawa wanamvuta Kumleta Sehemu za Vyakula sasa.
Mallya: Nini kilifuata
Shahidi: Kwamba alikuwa amepigwa akawa anavuja Damu
Jaji: hii ni Habari ambayo umesema Umeambiwa na Mke wa nani..?
Shahidi: Mke wa Ling'wenya Tukiwa kwa Mke wa Bwire
Mallya: huyo wifi yake anaitwa nani.?
Shahidi: anaitwa Athima
Jaji: nafikiri tulirudi kwenye Mstari hapo tunaanza kuzungumzia "Here say" yeye kaambiwa na Mke wa Ling'wenya na Mke wa Ling'wenya kaambiwa na Wifi nafikiri Mkiona Kuna Umuhimu mumwite Wifi yake aje kutoa Ushahidi ila Hatuwezi Kwenda hivyo.
Mallya: sawa Mheshimiwa Jaji
Mallya: Mliporudi Nyumbani ikawaje
Shahidi: tulikubaliana tupite Hospitalini
Mallya: Mlikuwa na Nyenzo gani katika Kuwatafuta
Shahidi: Tulikuwa na Picha zao
Mallya: Mlianzia Wapi
Shahidi: tulianzia Hospitali ya Muhimbili
Jaji: Kwanini Mlianza Kuwatafuta Kwenye Mahospitali
Shahidi: Ni baada ya Kuwakosa Kwenye Vituo vya Polisi
Jaji: Kwa Off Record tu, Moshi waliwambiaje
Shahidi: kwamba huku hawapo wameletwa Dar es salaam tukahisi labda wamepata Ajali
Mallya: Mlipofika Muhimbili ikawaje
Shahidi: Tukajitambulisha na Kueleza kuwa tunawatafuta Waume zetu, tulizunguka Kwenye wodi na Monchwari hatukuwaona
Mallya: nini Kikafuata
Shahidi: Tukaenda Hospitali ya Amana, Tukajitambulisha na Kuingia Kwenye Mawodi na Monchwari hatukuwaona pia
Mallya: baada ya Amana .?
Shahidi: tulienda Mwananyamala tukajitambulisha na Kuwatafuta waume zetu kwenye Mawodi na Mochwari hatukuwaona
Mallya: Siku ya tatu Sasa Mmeanda Muhimbili, Amana na Mwananyamala mkawakosa, Ulichukua hatua gani
Shahidi: ilibidi nirudi Chalinze kwa Sababu nauli ilikuwa imeshaaanza kuisha na Kwa sababu nina wawasiliano ikabidi nirudi Chalinze
Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani, kwa Mara ya kwanza Ulipata Taarifa ya Mume wako yupo wapi
Shahidi: Ilikuwa kwenye Taarifa Ya Habari ya Jioni
Mallya: uliwaona wakiwa wapi
Shahidi: Mahakamani Kisutu Mallya Kituo gani Cha Habari
Shahidi: ITV
Mallya: Uliwaona au Ulisimuliwa
Shahidi: niliona
Mallya: wanatuhumiwa kwa Makosa gani
Shahidi: Anashitakiwa kwa Ugaidi na uhujumu Uchumi
Mallya: mara Ya Mwisho Mme wako wakati anakuaga alikwambia anaenda Moshi Kufanya nini
Shahidi: kwamba Kuna kaz Imepatikana anaenda kuifanya
Mallya: ikawaje
Shahidi: Niliwasiliana na wenzangu
Mallya: Uliona hiyo Taarifa ya Habari ITV saa ngapi
Shahidi: Ilikuwa Saa 2 za Usiku
Mallya: mkafanya Mawasiliano, Mawasiliano gani
Shahidi: tulikubaliana Twende Mahabusu kwa Sababu hatukujua wamepelekwa Mahabusu gani
Mallya: Baada ya hapo nini kilifuata
Shahidi: Mzee Ling'wenya alikuja kutoka Mtwara
Mallya: kitu gani alifanya baada ya Kutoka Mtwara Mzee Ling'wenya
Shahidi: Tulikuwa hatuelewi wapo Mahabusu gani, Tulianza kutafuta Mahabusu waliopo
Mallya: mlianza kutafuta Mahabusu gani
Shahidi: Mimi sikwepo nilikuwa Chalinze, Tulifanya Mawasiliano
Mallya: wakakwambiaje
Shahidi: Kwamba wameenda Keko wamewakosa ila Segerea Wamewakuta wapo
Jaji: ni akina nani
Shahidi: Mke wa Mohammed Abdilah Ling'wenya na Mzee Ling'wenya
Jaji: Mke wa Ling'wenya na nani..?
Shahidi: Na Baba Mkwe wake, Mzee Ling'wenya
Mallya: sasa Ushajua Mwenza wako yupo Segerea hatua gani ilifuata
Shahidi: Nilikuja Jumapili kutoka Chalinze, Jumatatu tuliamka wote Mke wa Bwire, Ling'wenya tukaenda Wote Segerea
Mallya: Mlipofika Segerea ikawaje
Shahidi: Tulipokelewa na Askari wa Jinsia ya kike akatueleza leo siyo siku ya kuwaona Mahabusu Mje Jumamosi au Junapili
Mallya: baada hapo ulifanya Hatua gani
Shahidi: Nilienda Jumamosi
shahidi: nilisikia Ma ASKARI wakisema ndiyo Yule Jamaa ambaye yupo Kabatini
Mallya: ni nani aliteyaongea hayo
Shahidi: ni Ma Askari niliowaleza Majina kuwa namtafuta Mme wangu
Mallya: hatua gani ilifuata
Shahidi: Wakachukua funguo wakasema tunaenda kumleta
Mallya: unaweza Kutuambia hapo ulipokuwepo pana taswira gani ili Mheshimiwa jaji apate Picha
Shahidi: Ukiingia Segerea maeneo ambayo kuna Meza ya Kuwekea Chakula na Kuna Chuma kama Grill lililotenganisha
Mallya: Kitu gani kilifuata
Shahidi: nilimuona Mume wangu akitembea Kwa tabu kama Vile inaonekana ameteswa
Mallya: Unaeeza Kukumbuka Mume wako alikuwa amevaaje
Shahidi: Alikuwa amevaa kama Singlendi
Mallya: hali yake ilikuwaje
Shahidi: Amedhoofika, alikuwa amekonda Sana
Mallya: Mwendo wake ulikuwaje, alivyokuwa anatembea.?
Shahidi: alikuwa anachechemea
Mallya: Ulichukua hatua gani
Shahidi: Kama Utaratibu ulivyo wa pale, Nilibeba vitu kwa ajili yake
Jaji: ukikuwa umeleta Vitu gani
Shahidi: Chakula, shuka na Sababuni
Jaji: Vitu ulimkabidhi nani.?
Shahidi: Askari akishakagua anachukua ukiwa unamuona
Mallya: ulisema ulikuwa unamuona Mume wako anaelekea sehemu, Ni sehemu gani
Shahidi: Eneo la Nyavu ambalo mnaweza Kuzungumza
Mallya: ilikuwaje Mazungumzo kati yenu
Shahidi: Nilimuuliza Hali yake na Kilichotokea
Mallya: alikujibu nini
Shahidi: HaLi yangu ni hivyo hivyo ila siyo Nzuri
Mallya: alikwambia kwanini hali yake siyo Nzuri
Shahidi: aliniambia Kuna Mateso alipitia wakati yupo Moshi, alipigwa sana Ndiyo Maana Unaniona nipo Kwenye hali hii
Mallya: Baada ya Hapo.?
Shahidi: alichukuliwa akapelekwa Mahabusu
Mallya: nitakurudisha Nyuma Kidogo, Kilichokufanya utamtafute Vituo vya Polisi na Mahospitali Mume wako ni Kitu gani
Wakili wa Serikali: OBJECTION wakili ameshauliza
Mallya: Sikuuliza, Kama aliulizwa ni Off Records nataka sasa iingie kwenye Records
Wakili wa Serikali: Ameshaliuliza hilo swali
Jaji: Sijachoka Kuandika, Muuulize tena
Mallya: nitakurudisha Nyuma Kidogo, Kilichokufanya umtafute Vituo vya Polisi na Mahospitali Mume wako ni Kitu gani.
Shahidi: Kwa sababu tuliambiwa kuwa Walitolewa Moshi Kuja Dar es salaam na tulienda Vituo Vya Polisi Kwa Sababu tuliamini Kama wangetusaidia
Mallya: Vipi Kuhusu Ushiriki wa Ndugu zake Mwanamme
Shahidi: alikuja Mama yake, tukaenda naye Moshi
Mallya: Kwanini wewe namba ya Mume wako umesema huikumbuki kwa kichwa miye ya Mke wangu naikumbuka
Shahidi: Kwa sababu alikuwa na line Mpya aliyotoka Kuisajili
Mallya: Kwanini Unasema Ulipoenda Segerea hali yake ilikuwa tofauti
Shahidi: alikuwa amekonda sana na Macho yameingia Ndani Kama Yameganda, amekonda kwa kweli na Pia Nilimuona akiwa na alama Kwenye Mkono wakati anaenda Moshi alikuwa hana
Jaji: ulisema Uliona nini Kwenye mkono
Shahidi: alama ya Kovu kwenye Mkono, Awali alikuwa hana wakati anaenda Moshi
Mallya: ya kwangu ni hayo
Jaji: Asante sana Mallya
Jaji: pamoja na Mvua kutuharibia ratiba yetu, lakini tutabreak tena kidogo tutarejea Saa 6 Kamili, Jaji ananyanyuka anatoka.