Maamuzi ya kesi ndogo katika Kesi ya Mbowe na Wenzake kutolewa Oktoba 19, 2021

Kesi hii imefunua machache kati ya mengi wanayofanya polisi kwa raia mpaka hapa naamini ushahidi uliotolewa na adamoo na mwenzie ni ukweli, polisi yetu ina uhuni mwingi na wanakurupuka kukamata watu bila kupata ushahidi, ni wavivu wa kufuatilia ukweli wajiridhishe, katika kamatakamata zao hizi za ugaidi wamekamatwa wengi na kupewa mateso mazito na mwisho wakaachiwa baada ya kubaini hawana makosa, yanahitajika mabadiliko makubwa ya sheria na katiba yetu ili uonevu ukomeshwe
 
Shahidi: Mlango ulikuwa wazi na Kitasa nikakuta kimevunjwa,kwenye hii sentensi mimi sioni sehemu aliyosema polisi walivunja mlango bali amesema alikuta kitasa kimevunjwa bila kuelewa nini kimetokea.

..shahidi anasema alipouliza majirani aliambiwa kuna watu waliovalia kiraia na kipolisi walionekana nyumbani kwake.

..sidhani kama utetezi wanaweza kuuangusha ushahidi wote kwa mara moja. Wanachotakiwa kufanya ni kujenga kidogo-kidogo, hatua kwa hatua, hoja kwamba kuna mapungufu ktk ushahidi na maelezo ya polisi.
 
Kesi Hii Ni Kimeo Kwa Jamhuri Mbona Wanashupuza tu Shingo!!!! Hawajagundua Wako Uchi...time will tell ebu tuwe wapole.
Umekariri tu kuwa wapo uchi. Hebu fafanua basi. Maana unakuta tu mtu anasema Mbowe hatoki....haweki sababu za kitaalamu. Mwingine kama wewe unasema Jamhuri sijui nini....huweki sababu. Haya mambo kama hamyafaham muwe mnanyamaza tu
 
Kingai atuambie Lilenje yuko wapi? Au tume iundwe kumtafuta wakati Kingai na Mahita wakiwa mahabusu kwa kesi ya mauaji. Tuna hitaji tume huru kama ile ya Zombe na wenzake
 
Inasikitisha Sana Mkuu. Sasa hivi Tz haiongozwi na Rais Bali na Jopo la Marais. Hapo ndiyo tatizo linakoanzia.
Unajaribu kumlaumu nani? Raisi samia eti?

Kwa taarifa yako hawa watu walifanyiwa huu unyama wakati wa mwendazake. Na ujue,serikalini watu wa mwendazake wamejaa,hususani kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Na hii kesi ni initiative yao,siyo ya raisi samia.
 
Hivi polisi wanapomtia mtu nguvuni wana haki ya kumficha asijulikane alipo kweli...!!!

Sirro ana maana gani kuwambia watu eti wafuate sheria bila shuruti wakati polisi wanafanya kinyume cha sheria kwa kuwateka watu na kuwaficha ili wawatese.

Bila katiba mpya itakayoweka utaratibu wa polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria akina Hamza watazidi kuongezeka tu.
 
HIVI VYOMBO VYA DOLA HAVIJAGUNDUA TU KWAMBA HII KESI INAIVUA NGUO SERIKALI MBELE YA DUNIA NA KUFUNUA WAZI SIRI ZA SERIKALI NA NCHI? NAWAAMBIA HAO WATU WA KILA AINA WANAOIFUATILIA HIYO KESI WANAPATA TAARIFA MUHIMU MNO AMBAZO NI HATARI KWA NCHI KIUSALAMA. UTENDAJI WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA UNAANIKWA WAZI. IPO SIKU TUTASHANGAA KITABU KINAANDIKWA MAMBO YA AJABU KUHUSU TANZANIA. JE, MNAWAFAHAMU VIZURI HAO WANAOHUDHURIA HAPO MAHAKAMANI? WENGINE NI KUTOKA NJE YA NCHI. HAO MAKOMANDOO WA JESHI WANAFUNUA SIRI AMBAZO HAZISTAHILI KUTOKA NJE YA JESHI LENYEWE. KWANINI SERIKALI INAKUBALI MAMBO YA SIRI ZA NCHI YAANIKWE HADHARANI?
 
Fafanua kivipi. Kesi ngumu hii.
 
Sio yeye aliyeiambia dunia ktk BBC kwamba wana ushahidi wa kutosha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…