Maamuzi ya kiume na nafasi ya mwanaume kwa sasa ndani ya familia zetu

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Hello jamiiforum

Ni jumapili ya mwisho wa mwezi wa Kwanza mwaka 2025.
Kumekucha kupambana,siyo mapambano ya kazi za kimwili,pengine ni mapambano ya kuridhisha nafsi na roho zetu.

Huko makanisani kumejaa leo,wapo wanaotafuta wenza,wapo wanaotaka kuonana na mchungaji ili kunusuru ndoa zao,wapo walio tayari kutaka kuvunja ndoa zao ili wawe huru.wapo ambao wapo wote kanisani mke na mume lakini wanalala vyumba tofauti hawataki mambo yao yakae hadharani wapo tu kwaajili ya hatima za watoto na mali walizochuma.

Wengi wa walalamikaji wa ndoa hizi ni wanawake,wanaume tupo tu tunaugua kimyakimya,tunajipoza na ulabu au kuperuzi mitandaoni,tunalazimisha furaha usoni ilhali mioyo yetu ina furushi la majonzi.

Tunajaribu kupoza machungu Kwa kutafuta mwanamke au mchepuko mpya ili tu kupoza machungu ,lakini hakuna nafuu ni kama kuzima moto unaoteketeza nyumba kwa kutemea mate .uchungu wa kudharauliwa na mke unakuwa upper level.

Tunajipoza Kwa kusema hayana muongozo,tunawacheka vijana na timu kataa ndoa,yote hayo ni kujifariji tu ukweli ni kwamba hakuna namna.

Unajitutumua na kutanua kifua na kumkoromea mkeo huku ukimtishia utampiga,halafu anakuangaliaaaa kisha anasema.

Nipige kama kweli wewe ni mwanaume,piga niuwe.
Anaongea Kwa sauti ya kujiamini na kumaanisha,unakaa kimya huku ukiwaza Uhuru wako ,kuna Sheria na hizi Sheria zinampendelea zaidi mwanamke ,unasonya na kumtolea macho huku ukimwambia.

Ipo siku yako nitakufanya kitu kibaya,huku ukiwasha Gari na kuingia mtaani kuepusha zogo.

Anakujibu,huna uwezo huo na hakuna kitu utafanya,kama mwanaume fanya kweli sasa hivi siyo kusubiri siku gani ikifika.

Huna ujanja unaamua kupotezea na kuacha maisha yaende,watoto wenu wote si wa kike wala wakiume,wanamezeshwa sumu kwamba wewe Baba Yao ni mnyanyasaji na ni mtu mbaya sana

Ni vile tu ushakuwa Baba yao,anaenda mbali zaidi na kusema anajuta kuolewa na kuzaa na wewe sema ndo hivyo ,watoto nao hawaoni kosa la mama wanabaki kuona Mzee unazingua.

Unajaribu kutotoa pesa ya matumizi zaidi ya wiki mbili,lakini unagundua hakuna kilichopungua,watu wanakula na wanashiba,friji geji haishuki kila kitu kipo,unapata majibu kuwa mwanamke naye ana miradi na mishe zake hivyo suala la njaa siyo shida zake.

Pamoja na yote hayo unayokumbana nayo ndoa yako mtaani inaonekana ni mfano wa kuigwa ,tena na wachungaji na mapadre hawaishi kuitolea mfano.

Tuishi nao Kwa akili NDOA ni gereza dogo.
 
Unataka mapadre na wachungaji wahalalishe mpigane miti bila ndoa. Kama ulivomalizia ni kuishi kwa akili.
 
Daaaah ndoa tamu , ila ni gereza kwa kweli , Mungu atusaidie tuendelee kuwa na furaha kama mwanzo tulipokuwa hatuna kitu .
Ila tukumbuke wanaume kutimiza wajibu wetu katika familia lasivyo hatutakuwa na furaha wala amani maishani.
 
Back
Top Bottom