Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Baada ya Katiba kubakwa vibaya sana na Mhimili wa Serikali na Vyombo vyake ni TLS waliojitokeza kuikumbusha Mahakama na Vyombo vya Kikatiba kusimama kwenye nafasi zao bila kuogopa.
Hatimaye Umuhimu wa TLS umeonekana Nchini. Hatimaye akili za Wazee wa zamani walioweka kifungu cha 4 cha Sheria ya TLS imeonekana dhahiri. Kifungu hiki kiliwekwa purposely kuifanya TLS kusimama endapo Mihimili ya dola itajisahau au itatekwa na kushindwa kusimamia Katiba.
Kusimama imara kwa TLS ya Mwabukusi kumefanya Mahakama kujua nafasi yake Kikatiba na Kusimamia kweli Haki.
Kusimama Imara kwa TLS kumesababisha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutoka mafichoni jana na kutoa tamko kuhusu mwendendo wa masuala ya haki nchini.
Kongole nyingi kwake pia Mzee wetu wa maana kabisa Jaji Joseph Sinde Warioba na Mawakili wa Tundu Antipass Lissu wakiongozwa na Senior Counsel Mzee wangu Mwaisa Mpale Mpoki.
Maamuzi haya kwangu mimi ni ushahidi tosha wa umuhimu wa kuwepo wa TLS imara inayosimama kwa niaba ya Wananchi.
Lord denning,
Kisutu.