Maamuzi ya Mahakama Kesi ya Lissu: Uthibitisho wa Umuhimu wa TLS kama " Shadow 4th Organ of the State"

Maamuzi ya Mahakama Kesi ya Lissu: Uthibitisho wa Umuhimu wa TLS kama " Shadow 4th Organ of the State"

Sasa yule Mwanasheria Mkuu wa Serikali itakuaje? Maana yeye alisisitiza shauri lisikilizwe kwa njia ya mtandao na akatetea kweli Bungeni zaidi ya dakika 10
Yule hastahili hata kuwa Mkurugenzi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kipindi tunafanya internship kwenye ile Ofisi miaka ya 90 kulikuwa na vichwa hasa. Ni bahati mbaya tu nchi hii Wanasiasa ndo wameshika hatamu ila Wataalam wangekuwa wanaheshimiwa nchi hii ingekuwa mbali sana.
 
Huyu mzee akili kubwa ndiyo angepewa kuisimamia Tume ya uchaguzi
Ili tuwe na Tume bora ya Uchaguzi ni vizuri tutengeneze chombo huru katiba kikatiba ambacho hakina uhusiano wowote na Mamlaka ya Viongozi hasa Wanasiasa.
 
Sio tu kifungu hicho.

Je unakumbuka kwamba Kabla ya Lissu kugombea Uriais TLS ilikuwa haifahamiki? Pamoja na hicho kifungu?

Tundu Lissu ndio mtu wa kwanza kuipa Heshima Taasisi hiyo
Uko sahihi kuwa TLS ilikuwa haifahamiki ila chama cha wanasheria wa Tanzania kilikuwa kinafahamika.
 
TLS wapo vzuri sana..kama societies zote za kitaaluma.(walimu, wahandisi, madaktari, wasanifu, wachumi, wahasibu, wakulima, wafugaji, wachimbaji wa madini.n.k) wangekuwa na umoja huu kama TLS taifa hili lingepiga hatua kubwa sana kwenye sekta zote nyeti..katika taifa.
 
TLS ina nafasi kubwa sana kwenye hili Taifa. Ni vile tu vijana wa sasa hamlifahamu hili.

Ile ni kama Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyoundwa kwa Sheria ya Nchi na ikawekwa nje ya Mifumo rasmi ya Nchi kwa nia moja tu ya kusaidia mifumo rasmi ya nchi kutotoka nje ya mistari yake.
 
Kongole kwao.

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Kikubwa ,dada ake ambae wote walikuwa kwenye kamati ya sheria na katiba kwenye bunge maalum la katiba pendekezwa ya jaji warioba ,hataki kusikia mdogo wake ,kaumizwa...Risasi zilimtosha

uvccm hapo vipi, swala la serikalikali tatu kwenye muungano na kupelekea mwanasheria zanzibar kufukuzwa bungeni ,liliazia usoni kwa lisu na samia
 
Wazee wa zamani walikuwa na akili kuweka ile Section 4 kwenye Sheria ya TLS.

Watu wengi hawajui kuwa kile uwepo wa kile kifungu ulifanywa kwa makusudi ili Taasisi hii iwe inasimama kuirudisha Mihimili Mikuu ya Dola kwenye mstari endapo inakuwa imekosea.
Hicho kifungu unacho kipa 'credit' kubwa hivi kinasemaje. Viongozi hawa hawa wamekanyaga Katiba yenyewe, sasa waje wakiogope "kifungu" cha sheria?

Ni stahiki kuwapa TLS na viongozi wao 'credit' zao; hasa kwa kuendesha mhadhara ule na kumwalika Mzee Warioba; ambaye alifafanua vizuri sana hili swala lililopo sasa.
Ukiunganisha mkutano huo na matokeo sambamba yaliyotokea wakati huo huo, kama mkasa wa Fr, Dr Kitima; yote haya yamechangia kwa kiasi kikubwa kusukuma na kubadili mioyo ya baadhi ya wanaohusika na hali ya sasa ya kisiasa.
 
Hongera Mwabukusi. Imethibitisha kama TLS ni the 4th Shadow Organ of the State.

Samia afanyie kazi ushauri aliopewa na wasomi
 
Back
Top Bottom