Scaramanga
JF-Expert Member
- Aug 19, 2020
- 490
- 704
labda swali kidogo la kujiuliza katika uzi huu , je umeshwahi fatilia faida za kujiunga na AU,SADEC NA EAC. maana nachojua kuna faida na hasara sasa ushwahi fanya tafiti ya kutosha kuona kuna faida ipi au hasara ipi na kwa kiwango gani kati ya faida na hasara. Labda kwa uchache niongelee faida chache tu ambazo unaweza kukubaliana namiUkweli usemwe
Mwalimu Julias Kambarage Nyerere aliwahi kusema kuwa katika uongozi wake yapo mambo mazuri alifanya na pia yapo ya kipuuzi ambayo alifanya. Akaendelea kusema anashangaa wanaomfuatia wanayaacha yenye tija na kuendeleza yale mabaya yake.
Katika mambo ya kipuuzi aliyoyafanya mojawapo ni lile la kuipeleka nchi kwenye Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) ambayo sasa inaitwa Umoja wa Afrika (AU) bila kuzingatia utashi na maamuzi ya wananchi.
Ikumbukwe kipindi hiko, Mwalimu alikuwa anaungwa mkono hata na watoto wadogo hivyo angepeleka jambo la kujiunga na jumuia za kikanda wangepiga kura na kumbukumbu ingebaki. Lakini maamuzi yake aliyoyafanya kwa niaba ya Taifa zima hayakuzingatia utashi wa nchi na kiukweli hata Katiba yetu hairuhusu jambo hilo. Katiba ipo kimya kama ilivyonyamazishwa na waliyoiandika.
Sambamba na hilo, uamuzi wa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ni mufilis endapo utaratibu haukufuatwa. Sidhani kama wananchi enzi hizo waliulizwa na kuridhia kupitia kura kabla ya Nyerere na Karume kuungana. Leo tuna muungano unaolindwa kwa mtutu wa bunduki na wizi wa kura. Muungano ambao viongozi wanaapa kuulinda kwa sababu una maslahi kwao na si kwa wananchi.
NINI KIFANYIKE
Mzee wa Msoga aliwahi kusema kwenye kikao cha wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki kuwa, kabla ya kupata Rais mmoja wa Jumhiya ni sharti wananchi waulizwe kwanza.
Pamoja na mapungufu kadha wa kadha yanayozungumzwa dhidi ya JK, lakini hili la kurudi kwa wananchi kupata ridhaa ni jambo ambalo hakuna rais wa Afrila aliwahi siyo kusema tu, bali hata kuliwaza.
Nashauri, serikali ianze mchakato wa kura za maoni kuhusu sisi kujiunga jumuiya zote za kikanda yaani
AU (African Union)
SADC (Southern African Developing Countries)
EAC (East African Comunity)
ADB
OIC (YKWIM)
Na zingine ambazo wametupeleka huko kama misukule.
Bunge lisitumike kama mhuri wa kufanya maamuzi yanayohitaji utashi wa wananchi ambao ndiyo wenye nchi
Kinyume na hapo, hizo jumuiya zina manufaa makubwa kwa viongozi badala ya kunufaisha nchi.
CC: Gwappo Mwakatobe FaizaFoxy zitto junior Pascal Mayalla Erythrocyte Mzee Kigogo Retired raraa reree Extrovert Mdude_Nyagali Depal Mamndenyi Joannah Mzee Mwanakijiji funzadume Mshana Jr Bujibuji Simba Nyamaume
1: Kuwa mwanachama wa jumuiya hizi moja kunaongeza nguvu ya nchi katika maswala ya kimataifa kuweza toa kauli moja ndiyo maana unaona sasa hivi Russia,India,Afrika ya Kusini na nchi nyingine wanapambana kuungana.
2: Ukiwa mwananchama wa nchi kama sadec ukivamiwa na nchi nyingine basi unapata usaidizi wa kiusalama ikiwa pamoja na nguvu za kijeshi toka wanachama wengine.
3: Kiuchumi kuna mambo ya kuuziana bidhaa au wananchi kupitisha bidhaa zilizotengenezwa ndani ya nchi wananchama bila kulipa baadhi ya kodi mfano afrika mashariki kama bidhaa imetengenezwa ndani ya nchi mojawapo mwananchama kwa kutumia malighafi ya ndani basi ikivuka kwenda nchi nyingine mwananchama kuna baadhi ya kodi hatolipishwa.
4: Ushirikiano katika nyanja za afya na kubadilishana uzoefu mbali mbali .Urahisi wa wananchi wa jumuiya mwananchama kuweza kuvuka kwenda nchi nyingine mwanachama.
Hizi ni baadhi ya faida