Maamuzi ya Nyerere kutuingiza AU, SADC, EAC na hatimaye Muungano yatatutesa hadi kiama. Nini kifanyike?

Kwanza Wana majumui waafrika walikuwa ni waota ndoto za mchana(Day dreamer)

Hawakuangalia hali halisi ya kipindi hicho na wakati ujao ambao kila nchi ingeangalia maslahi yake.

Tatu Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa wa Viongozi na wananchi hawakushirikishwa.

Ndio maana huu muungano hauachwi kupingwa toka kale, Sasa na wakati ujao
 
Wale wazee waliamini wananchi wataendelea kutokuwa na akili daima
 
Umesoma uzi wangu vizuri au unajitia hamnazo?

Nimesoma ndiyo ,wewe umesema kwamba serikali ianze michakato upya ,kwani tatizo ni kwamba nyerere alikuwa hajawashirikisha wananchi ila miungano ipo poa? Kama ipo poa ila tatizo ni kwamba hatujashirikishwa hauoni kurudia upya ni upotevu wa pesa? Kama ina hasara ni zipi?
 
Muungano upi upo poa?

Huu huu uliopigiwa kelele toka na kundi la G55 mpaka Leo?

Mungu huu unaowapa Wazanzibari kuwa raia daraja la kwanza?
 
Sijaelewa bado kosa la nyerere hapo ni nini
alipenda kufanya maamuzi ya nchi ya tanganyika peke yake au na bunge lake la chama kimoja bila kusikiliza sauti au kushauri wananchi wenye nchi yao wanasemaje?

ni nyerere aliyesababisha leo tanganyika (taifa lenye watu milioni 60) linaongozwa na mwanamke kutoka unguja, kama vile tanganyika, imekodi kiongozi kwa mkataba.

iko siku, wajukuu na vitukuu wa wananchi wa tanganyika watakuja kuwasuta na kuona wazee (mababu na mabibi) zao walikosa akili, kwa kufanya mambo ya kijinga kwa nchi yao.

vipi, unaamuaje suala la wananchi peke yako bila kuwashirikisha wenyewe kupata ridhaa yao na uhalali wao.

leo samia kawa dume, anawachezea watanganyika anavyotaka.

kila siku ni kuchagua kuapisha kutengua..
 
Yaani ukitumia mizania kupima uanachama wa Tanzania kwenye hizi jumuiya unaona zina hasara kuliko faida?
 
Basi umeusoma na haujaelewa kitu.

Subiri muda wa elimu ya katiba kwa miaka mitatu labda nitapata wasaa wa kukufundiaha kuhusu haya mazonge Onhe unayoyaita Poa tu
 
Yaani ukitumia mizania kupima uanachama wa Tanzania kwenye hizi jumuiya unaona zina hasara kuliko faida?
Wachumia tumbo humu wanajifaragua kuwa mambo yapo poa.

Manufaa ya haya majumuiya yapo kwa viongozi zaidi ya nchi na watu wake
 
Wachumia tumbo humu wanajifaragua kuwa mambo yapo poa.

Manufaa ya haya majumuiya yapo kwa viongozi zaidi ya nchi na watu wake
Manufaa yapo kwa viongozi kwa misingi gani? tuelemishane. Sababu hizi jumuia zina majukumu ya kiuchumi, kisiasa na kijamii....
 
Daah... Karne ya 21 ambapo Dunia inazidi kuwa Kijiji na nchi haziwezi kuhimili bila mafungamano Bado Kuna watu hawataki mafungamano??
No wonders ni ngumu kwa nchi za Afrika kufanya biashara baina yao!
Akili za kushoto!
 
Lisu yupo sahihi. Kuiboresha hoja yake ningesema mwenye eneo lazima awe mwanahisa kwenye mradi wa uchimbaji kwa mgawanyo ufuatao
Serikali 50%
Mwekezaji 43%
CSR 4%
Mmiliki wa eneo 3%

Kwa kuanzia
Yaani eneo ulilonunua wewe serikali iwe na hisa 50% na wewe mmiliki uwe na 3%??
Are you serious??
 
Yaani eneo ulilonunua wewe serikali iwe na hisa 50% na wewe mmiliki uwe na 3%??
Are you serious??
Nimesema kwa kuanzia.
Sababu za kusema hivyo ni kutokana na sheria mbovu ya ardhi inayomnyima mwananchi kufaidi rasilimali anazozikuta chini ya ardhi anayomiliki

Tukianzia hapo labda tutaanza kuelewa namna tunavyokandamizwa na kuibiwa
 
Sawa... lakini twende full swing!
50% mwenye eneo... hizo 50% nyingine serikali igawane na wadawa wake!
 
Lisu yupo sahihi. Kuiboresha hoja yake ningesema mwenye eneo lazima awe mwanahisa kwenye mradi wa uchimbaji kwa mgawanyo ufuatao
Serikali 50%
Mwekezaji 43%
CSR 4%
Mmiliki wa eneo 3%

Kwa kuanzia

Serikali 45%
Mwekezaji 40%
CSR 5%
Mmiliki wa eneo 10%

Kwa kuanzia.
 
Basi umeusoma na haujaelewa kitu.

Subiri muda wa elimu ya katiba kwa miaka mitatu labda nitapata wasaa wa kukufundiaha kuhusu haya mazonge Onhe unayoyaita Poa tu

Sawa itakuwa vyema ikifika muda wa kutoa elimu uipandishe hii mada tena.
 
Muungano mara nyingi na hasa unapofanyika kwa nia njema, ni jambo jema lenye heri.

Ninalokuunga mkono, hayo yote yasikiuke taratibu za kupata ridhaa za 'wanaounganishwa', yaani wananchi.

Lakini kubwa zaidi, siafiki bunge kuwa wawakilishi wa kila jambo linalohusu ridhaa za wananchi, kwani, hakuna asiyejua sasa kuwa hawa viumbe si wazuri sana katika kuwakilisha aunkulinda maslahi ya wanaowawakilisha (si wote wapo hivyo, ila wengi wao) na hawajali sana maoni ya waliowatuma, bali hujali maslahi yao binafsi na vyama vyao.

Mambo ya msingi sana, wananchi vema wahusike moja kwa moja na sio kupitia wabunge.

Yale mengine, kwa sababu ya ugumu,gharama na shida mbali mbali za kuhusisha wananchi mmoja mmoja, bunge liendelee na blah blah za kiuwakilishi kama kawaida....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…