ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Viti Maalum vya wabunge Wanawake vimewekwa ili kulipa fursa kundi hilo la jamii kwenye ulingo wa siasa.
Mantiki yake ni kuwa, katika vurugumechi za siasa, wanaume huwazidi wanawake kutokana na sababu mbalimbali za kijamii na kitamaduni.
Katika kuheshimu misingi ya malengo hayo ya kuwa na viti maalum, ni muhimu maamuzi juu ya viti maalum yakaachwa mikononi mwa wanawake wenyewe.
Haitakuwa sahihi, kikao cha wanaume kiamue kupinga maamuzi ya wanawake kuhusu nafasi za Ubunge wa wanawake.
Ni matumaini ya wajali usawa wa kijinsia kuwa Spika wa Bunge atazingatia na kulinda haki za wabunge wanawake pale itakapotokea viongozi wanaume ndani ya vyama vyao wakitumia ubabe kupindua maamuzi ya wanawake wenyewe.
Vilevile ni muhimu sasa itungwe sheria mahsusi kwa ajili ya kuyalinda makundi maalumu kama la viti maalum vya wanawake Bungeni dhidi ya ubabe na ukandamizaji wa viongozi wanaume.
=================================
Update 27/11/2020
Hatimaye maamuzi rasmi ya Baraza la Wanawake yametenguliwa na kikao kilichojaa Wanaume.
Historia ya kupigania haki za Mwanamke inafungua ukurasa mpya...