Maamuzi ya Wakinamama yasiingiliwe

Maamuzi ya Wakinamama yasiingiliwe

Mchungaji Erasto anasema haiwezekani wanaume wawateulie wanawake viongozi wa kuwawakilisha, huo ni mfumo dume uliopitiliza.

Mchungaji anasema pamekuwepo malalamiko yaliyofika hadi kwa Spika kwamba wabunge wa viti maalumu huombwa rushwa " maalumu " kabla ya uteuzi na hili ni jambo baya kabisa.

Sasa kama Halima Mdee amewaokoa wenzake kutoka mdomoni mwa mwamba na kuwafikisha bungeni wakiwa " hawajaguswa" hilo mi jambo la kumpongeza amesisitiza mchungaji.

Maendeleo hayana vyama!
Mfano mzuri...
 
Cha kushangaza povu jingi linatoka kwa wanaume Kama sio wivu na mfumo dume kitu gani?
Wanaume acheni ubinafsi wenu heshimuni wanawake
Ivi ww uliumia Matiko alipopgwa dole? Halima alipovunjwa mkono?
 
Viti Maalum vya wabunge Wanawake vimewekwa ili kulipa fursa kundi hilo la jamii kwenye ulingo wa siasa.

Mantiki yake ni kuwa, katika vurugumechi za siasa, wanaume huwazidi wanawake kutokana na sababu mbalimbali za kijamii na kitamaduni.

Katika kuheshimu misingi ya malengo hayo ya kuwa na viti maalum, ni muhimu maamuzi juu ya viti maalum yakaachwa mikononi mwa wanawake wenyewe.

Haitakuwa sahihi, kikao cha wanaume kiamue kupinga maamuzi ya wanawake kuhusu nafasi za Ubunge wa wanawake.

Ni matumaini ya wajali usawa wa kijinsia kuwa Spika wa Bunge atazingatia na kulinda haki za wabunge wanawake pale itakapotokea viongozi wanaume ndani ya vyama vyao wakitumia ubabe kupindua maamuzi ya wanawake wenyewe.

Vilevile ni muhimu sasa itungwe sheria mahsusi kwa ajili ya kuyalinda makundi maalumu kama la viti maalum vya wanawake Bungeni dhidi ya ubabe na ukandamizaji wa viongozi wanaume.
Haya Kamchumbieni Halima hana mme...bazazi nyie...vivuruge
 
Mfumo dume sasa inabidi utungiwe sheria kali kuudhibiti.
Jeuri ya kutunga Sheria CCM hawana wanaogopa itauma kwao pia.badilini iwe mbunge akivuliwa uanachama anaendelea na ubunge,udiwani au urais.spika ataendelea kuwalinda wakifukuzwa na upinzani si kubali sheria.ccm ni waoga mno.
 
Jamani ni kikundi gani kinajaribu kutupotosha hapa? Hivi siyo Viti vya UWT ni vya Chadema kwa ajili ya members wao walio wanawake! Pamoja na mimi kuwahurumia sana wakina Halima na Matiko na Bulaya kwamba walipoteza viti vya majimbo katika mazingira ya ajabu, na wana hamu ya kuwa bungeni tendo lao limenisikitisha sana!
Kwa watu waliopigania chama kiasi kile na leo wakawa wasaliti hasa wakiwa wanawake ni aibu!
Mwanzoni nilidhani waliruhusiwa lakini kama wamekwenda kwa tamaa zao wenyewe hakuna wapenda haki watakaowatetea!
 
Uzuri harakati ya akimama cdm inaongozwa na mwenyekiti wa akina mama. Kitendo chochote cha kumnyanyasa ni sawa na kunyanyasa wanawake wote cdm. Sioni kiongozi mwenye uwezo na busara wa kushughulikia mtafaruku uliopo sasa ndani cdm.

Cha msingi ni kumshauri hata yule Mbunge wa Nkasi ajivue uanachama na kujiunga na CCM kisha arudi tena Bungeni.
Chadema ibaki kama NGO ya Kupigania haki za mashoga! Ambayo pia itafutwa .
 
Jeuri ya kutunga Sheria CCM hawana wanaogopa itauma kwao pia.badilini iwe mbunge akivuliwa uanachama anaendelea na ubunge,udiwani au urais.spika ataendelea kuwalinda wakifukuzwa na upinzani si kubali sheria.ccm ni waoga mno.
Hatimaye maamuzi rasmi ya Baraza la Wanawake yametenguliwa na kikao kilichojaa Wanaume.

Historia ya kupigania haki za Mwanamke inafungua ukurasa mpya...
 
Back
Top Bottom