Maana sahihi ya Mzinifu na Malaya ni ipi?

Maana sahihi ya Mzinifu na Malaya ni ipi?

Mzinifu- Mtu anaefanya tendo bila kufunga ndoa Kanisani/Msikitini.

Malaya-Mtu asiyetulia na mwanamke/Mwanaume mmoja.
Haijalishi Yuko kwenye ndoa au hayuko.

Nimejaribu
Execellent¡
 
Mgoni ni mtu aliyeoa au kuolewa akafanya rendo na mwingine asiye mume au mkewe.

Mzinifu ni yule ambaye anafanya tendo na mwingine bila kuwa ameoa au ameolewa. Mfano wanafunzi kulana wenyewe kichochoroni ule ndiyo uzinifu hakuna hata mmoja mwenye ndoa kati yao. Ikitokea mmoja ana ndoa ni ugoni huo
Na uasherati ni nini?
 
Mzinifu ni mwanaume au mwanake ambaye ana mke au mume lakini anatafunwa au kutafuna nje.

Malaya: ni mwanaume/au mwanamke asiyeweza kutulia na mwanamme au mwanaume mmoja, na hapa kwenye umalaya inaweza kuwa ni mradi wa mtu unaompatia faida fulani
na vipi inakua kwa mashoga na wazinifu, je watakua wanagawanyika katika umalaya na uzinifu au inakuaje?
 
Mzinifu huwa anajificha asijulikane, lakini malaya yeye anajiuza waziwazi kwa sababu it’s a business venture.
 
Mzinifu ni Malaya, ila si kila malaya ni mzinifu. Kwa sababu kuzini ni kuvunja kiapo; sasa kama hujaoa unavunja kiapo cha nani? Mtu huyu anakuwa anafanya uasherati, maana yake anafungamana na kila roho anayokutana nayo kwa sababu hakuna nafsi iliyotawala mwili wake.
cha kwanza unavunja kiapo kwa kufanya zinaa, maana M'mungu ametukataza kuzini. Na kila malaya ni mzinifu, maana huwezi kuwa malaya ispokua unazini tu.
 
Mzinifu ni mtu anayefanya tendo la ndoa au ngono pasipokua na ndoa,anaweza kua hata mke au mume anayetembea na mtu mwingine nje ya ndoa yake,huyu anafanya ngono ili tu kujifurahisha na sio kwa kujiingizia kipato,

Malaya ni Prostitute kwa jina lingine Kahaba,
Huyu huifanya ngono kama biashara yake ya kumuingizia kipato,ni mtu anayeuza mwili wake,mtu aliyeugeuza mwili wake kua biashara ya kustarehesha watu kwa malipo,

Kifupi umalaya ni kitendo cha mtu kutoa huduma ya ngono kwa lengo la kujipatia faida,iwe ni faida ya kipesa,mali,kazi au hata jambo fulani.
Hii definition yako ya umalaya imetuokoa wengi, hizo za juu hapo 🥵
 
Yoyote anaefanya ngono kabla ya ndoa uyn ni mzinifu bila kujali jinsia na yoyote anaefanya ngono na watu tofauti bila kujali jinsia wala ndoa uyo ni malaya kwakuongezea tu kahaba ni mwanamke anaefanya ngono kama kazi au nja yakupata kipato
 
Hizo dhana zote mbili ni za kufikirika tuu!
Hazina uhalisia, ni dhana zimewekwa na binadamu ili kutenga/kubagua watu.
Nature haitambui umalaya wala uzinifu. Inatambua kitendo cha kujamiiana.
 
Mzinifu ni mtu anayefanya tendo la ndoa au ngono pasipokua na ndoa,anaweza kua hata mke au mume anayetembea na mtu mwingine nje ya ndoa yake,huyu anafanya ngono ili tu kujifurahisha na sio kwa kujiingizia kipato,

Malaya ni Prostitute kwa jina lingine Kahaba,
Huyu huifanya ngono kama biashara yake ya kumuingizia kipato,ni mtu anayeuza mwili wake,mtu aliyeugeuza mwili wake kua biashara ya kustarehesha watu kwa malipo,

Kifupi umalaya ni kitendo cha mtu kutoa huduma ya ngono kwa lengo la kujipatia faida,iwe ni faida ya kipesa,mali,kazi au hata jambo fulani.

Tajiri, kwa maana yako hata ndani ya ndoa kuna umalaya basi. Maana kwenye ndoa pia kuna kujipatia faida, upendeleo, mali, kasi n.k. 😊
 
Hizo dhana zote mbili ni za kufikirika tuu!
Hazina uhalisia, ni dhana zimewekwa na binadamu ili kutenga/kubagua watu.
Nature haitambui umalaya wala uzinifu. Inatambua kitendo cha kujamiiana.
ila kuna kufanya kwa uhalali, yani kwa kuoana. Na kufanya kwa haramu ambayo ndio zinaaa yenyewe kwa kuto kuoana.
 
cha kwanza unavunja kiapo kwa kufanya zinaa, maana M'mungu ametukataza kuzini. Na kila malaya ni mzinifu, maana huwezi kuwa malaya ispokua unazini tu.
Hapana, hakuna kiapo cha asili kati ya Mungu na Mwanadamu. Amri ya KUTOZINI inahusisha uvunjivu wa kiapo, kama hukufanya kiapo ndio maana kuna neno mahsusi nalo ni UASHERATI. Mungua liyeagiza ukaijaze dunia hakuwaambia muoe kwanza, ndoa ni ustaarabu wa binadamu, concept ya ndoa ya kwanza ya Eden ni hypothetical tu, hakuna kitu kama hiko. Uasherati unatafuna generation, uzinzi unatafuna nafsi husika.
 
Back
Top Bottom