Kuna dogo mmoja almanusra aache mke kisa hakumkuta na bikra. Lakini tukamshauri ya kuwa maisha hayaishii katika BIKRA, atulie ajenge familia. Alitusikiliza na ametulia sasa.
Nina nukta kadhaa za kuwasilisha mintarafu jambo hili :
1. Watoto wa kike ambao walipoteza bikra zao kwa ujuaji( hapa nawatoa wale wote walio tenzwa nguvu) na kufurahia jambo hilo wakae wajue ya kuwa hawana hoja hata watembelee kichwa ya kudogosha BIKRA, wanachotakiwa wajue tu ya kuwa bikra ni hazina ambayo binti huzaliwa nayo, wajiulize kwanini wanazaliwa na hilo kufuli na mwisho wawasihi watoto zao kama wamejaaliwa juu ya kutunza zawadi hii adhimu.
2. Suala la upya ni kwa wote, yaani muoaji na muolewaji wote wakioana wakiwa wapya huwa nzuri sana. Nawauliza swali waungwana nani asiye penda kuanzisha jambo ? Jibu sote tuna penda kuwa wa kwanza.
Narudi kuendelea hapa nilipoishia...