Maana ya Mwanamke Bikra, Kuwa na Mahusiano/Kuoa Mwanamke Bikra

Kuna wengine wanatolewa ubikra na baiskeli sasa hapo inakuaje sasa.

Hakuna kitu kama hicho,

Bikra ni lazima itolewe na uume au sex machine, yaani lazima kitu kiingie ndani ya uke ndipo bikra itoke
 
kweli kabisa..
Gal. 6. 7............ Kwa maana lolote analopanda mtu, ndilo atakalovuna pia;
 
wakiendesha baiskeli hua zinachomoka waulize watakupa jibu.😄😄😄

Mkuu hakuna kitu kama hicho, hiyo ni janja ya Nyani Mkuu

Wanawake ni wajanja kwa wanaume wenye akili ndogo.

Huwa wanajiliza liza kinafiki ili kupata huruma kwa wanaume wasio thabiti. Pia hujichekesha chekesha kukulaghai.

Ukiona mwanaume yeyote anasema wazi kuwa mwanamke anaakili kuliko mwanaume jua tayari ni mpumbavu
 
ila bora me ndo niwe mchepuko
 
Wakuu Kwema!

SOMO MAALUM LA BIKRA

UTANGULIZI
Nimeona niandike humu Somo hili kwa Lengo la kuelimisha kizazi cha sasa, hasa Vijana. Siku za hivi karibuni kumezuka mjadala mkubwa sana kuhusu umuhimu wa ubikira katika imani na jamii kwa ujumla, wote tunafahamu kuwa Maandiko katika Agano la kale na Agano jipya na hata tamaduni kwa ujumla yalisisitiza sana umuhimu wa kuoa mwanamke bikira!, Mila nyingi na tamaduni nyingi pia zinathamini sana umuhimu wa mume kuoa au kupata mwanamke Bikira, Bikira ni nini na ina umuhimu gani kiimani? Je kuna ulazima wa kuoa mwanamke Bikira?
\
Kwa nini Mungu aliiweka bikira na kwa nini alisisitiza mwanamwali kuolewa bikira kuna jambo gani katika ulimwengu wa kiroho kuhusu ubikira, je kuoa mwanamke ambaye hakuwa na bikira kuna faida gani au hasara gani? Maswala haya yote yote yanatufikisha mahali hapa ambapo tunapaswa kuliangalia swala hili kwa kina na mapana na marefu.


Mabinti Bikira Uko Afrika ya Kusini hupewa uthamani mkubwa sana katika tamaduni zao

Maana ya Neno Bikira kimaandiko!
Kwa mujibu wa tafasiri za Agano la kale neno bikira lilitumika kumaanisha Mwanamwali yaani mwanamke kijana asiyejua Mume au ambaye hajawahi kushiriki tendo la Ndoa, na kuna maneno kadhaa ya kiebrania yaliyotumika kuwataja wanawake hao, yaani BETULAH mwanamwali bikira asiyejua mwanaume au ambaye hajaingiliwa na uume bado kwa kiarabu BATULI, na BAHUR mwanamke au mwanamwali kijana na ALMAH mwanamwali bikira aliyetolewa mahari au ambaye yuko karibu kuolewa, Almah pia ilitumika kumaanisha mwanamke safi ambaye hakuna maswali katika kuthibitisha usafi wake.

Neno hili ALMAH ndilo analolitumia Isaya Nabii katika Unabii unaohusu Mwanamwali atakayemzaa Masihi Isaya 7: 14. “Tazama Bikira (ALMAH) atachukua Mimba!.” Kwa hiyo kibiblia hii ilikuwa ndio maana ya neno Bikira. Hata hivyo Neno la Mungu lilikuwa na maana ya ndani zaidi kama tutakavyoiona baadaye.

Umuhimu wa Ubikira katika Ndoa.
Ni ukweli usiopingika kabisa kuwa kwa mujibu wa mafundisho ya kibiblia yaani Agano la kale na Agano jipya na katika mtazamo wa Mungu, Ndoa ilithibitika kuwa ni halali na takatifu endapo alama za ubikira zingeonekana katika tendo la kwanza la ndoa, Damu ambayo ingemwagika kwa mara ya kwanza ingeweza kuthibitisha kuwa mwanamke huyu ameingiliwa kwa mara ya kwanza, Damu hii ilihusianishwa kama damu ya agano lililo wazi kabisa kuwa ndoa hiyo ni ya halali na ni safi na kwa mume na kwa sababu hiyo huyo ndio angekuwa mkeo halali na mwenye kumuingilia ndio mmiliki halali wa Mume huyo

Walawi 21: 1,7 Biblia inasema hivi “ Kisha Bwana akamwambia Musa Nena na hao makuhani wana wa Haruni kuwaambia, Mtu ASIJINAJISI……. Wasimumwoe mwanamke aliye Kahaba, au huyo aliye mwenye UNAJISI, wala wasimuoe mwanamke aliyeachwa na mumewe: kwa kuwa yeye ni kuhani ni mtakatifu kwa bwana Mungu wake” ni wazi kuwa hapa BIBLIA iliwakatza Makuhani kuoa wanawake wenye UNAJISI yaani ambao sio safi yaani ambao wameshabikiriwa hivyo kwa ufupi walitakiwa kuoa mwanamke Bikira! Yaani ASIYENAJISIWA!

Ubikira katika agano la kale na wakati wa sheria uliinua sana thamani ya mwanamke, licha ya kuweko kwa mahari maalumu (Waebrania waliita Mohar Betulot) kiarabu (Mahar al Batul) sawa na “bride price for virgin” Mahari maalumu ya Ubikira, kwa sababu ya kukutwa Bikira, heshima kwa wazazi kwa matunzo mazuri ya binti yao, heshima kwa binti kwa kujitunza lakini pia ilithibitisha uwezo na kiwango cha juu cha uadilifu.

Katika Torati ya Musa mwanaume alipolala na mwanamwali aliyeposwa “ALMAH” na kuharibu uanawali wake alitakiwa kumuoa yeye, na kama Baba yake angekataa asimuoze binti yake kwa mtu aliyembikiri, mwanaume huyo alipaswa kulipa mahari sawa tu na ile ya muoaji wa mwanamke Bikira “Kutoka 22:16-17

Kama mwanamume angembaka mwanamke Bikira alipaswa kwa mujibu wa torati kulipa shekel 50 sawa na mahari ya mwanamwali bikira na alilazimika kumuoa na hakupaswa kumuacha maisha yake yote Kumbukumbu 22:28-29
Kumbukumbu 22: 13-22
Biblia inasema hivi “13.Mtu akitwaa mke, akamwingilia na kumchukia, 14. kisha akamshitaki mambo ya aibu kumzushia jina baya, akasema, Nimemtwaa mwanamke huyu, nami nilipomkaribia sikuona kwake alama za ubikira; 15. ndipo babaye yule kijana na mamaye watakapotwaa alama za yule kijana za ubikira, wawatolee wazee wa mji langoni; 16. na baba yake yule kijana awaambie wazee, Mwanamume huyu nilimpa binti yangu awe mkewe, naye amchukia; 17. angalieni, amemwekea mambo ya aibu, asema, Sikuona kwa binti yako alama za ubikira, nazo hizi ndizo alama za binti yangu za ubikira.

Na wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa mji. 18. Basi wazee wa mji ule na wamtwae yule mtu mume na kumrudi, 19. wamtoze shekeli mia za fedha, wampe babaye yule kijana, kwa kuwa amemzulia jina baya mwanamwali wa Israeli; naye awe mkewe; hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote. 20. Lakini likiwa ni kweli neno hili, la kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira; 21. na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Kupoteza ubikira kungegharimu adhabu ya kifo kwa kijana wa kike na, kuondoa bikira ya mwanamwali kulilazimu kulipa mahari na kumuao hii ilikuwa sheria nzima ya uanawali au ubikira katika agano la kale au torati ya Musa

Katika agano jipya pia mwanzoni Ubikira ulichukuliwa kuwa ni sehemu ya Maisha ya kujitoa na kumtumikia Mungu, mtu alipaswa kuishi maisha ya uanawali siku zote za maisha yake ni hii ingekuwa ni sadaka Sacrifice kuwa ameyatoa maisha yake kwa Yesu na hataki kuruhusu Unajisi katika maisha yake hivyo wazee wengi nyakati za Kanisa la kwanza waliwatunza binti zao, wasiolewe waishi maisha ya kumtumikia Mungu, jambo hili lilifanywa kwa usimamizi wa mzazi vilevile kama ilivyokuwa katika agano la Kale kwa vile kama binti angenajisiwa au kubikiriwa aibu ingekuwa kwa familia nzima, lakini ingekuwaje sasa kama binti anajisikia kutaka kuolewa Paulo mtume akashauri

1Wakoritho 7: 8-9 Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane Ni heri wakae Kama mimi nilivyo, Lakini kama hawawezi kujizuia na waoe; maana ni afhadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa”
1Wakoritho 7: 25-28 “ Kwa habari za wanawali sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kwa rehema za Bwana kuwa mwaminifu. Basi, naona hili kuwa jema, kwa ajili ya shida iliyopo, kwamba ni vema mtu akae kama alivyo. Je! Umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? Usitafute mke. Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.

Wanawali wanaotajwa hapo ni vijana wa kike walio bikira kwamba kwa mujibu wa Paulo kama wanaamua kujitoa na kuishi maisha hayo ya utawa ni vema na kama wanaamua kuolewa hawana hatia yaani sio dhambi
Kwa hiyo katika falsafa za agano jipya kuishi maisha ya ubikira ilikuwa ni aina ya sadaka Sacrifice ambayo madada wengi wanaishi maisha ya utawa hulazimika kuwa bikira na hawasumbuki katika maisha yao kwa vile hawajui lolote HAWAJANAJISIKA!.

Umuhimu wa Ubikira kwa mujibu wa Tamaduni za kiyahudi.
Kwa mujibu wa tamaduni za Kiyahudi na katika vitabu vya tamaduni zao vijulikanavyo kama Talmud, Halakhah na Hagadah Marabi wakuu kama Gamaliel na Eliezer na Joshua bin Hananiah wanatoa maoni yao kuwa kulikuweko na utata kadhaa katika kuziangalia alama za ubikira kwani wakati mwingine alama za Damu hazikuonekana kabisa katika harusi kadhaa huku kikiwa na uhakika kuwa mabinti hao walikuwa safi na hawakuwa wamenajisiwa ugumu wa uume kuingia katika uke ulionekana na ulisumbua katika hatua za awali za ndoa au tendo la ndoa hii ilipelekea kuondoa umuhimu wa Damu katika kuthibitisha ubikira wa mwanamke hata ingawa damu ya ubikira ina kiherehere na humwagika kwa wingi tu katika mtindo ulio wazi kuwa mwanamke huyu ni bikira lakini sio wote wanakuwa na alama hiyo na hivyo labda kungekuweko uwezekano wa kuhukumiwa kwa mabinti wasio na hatia ambao ubikira wao uliweza kutokuthibitika katika mazingira mengine

Mkazo mkubwa wa ubikira unapochunguzwa vyema Katika maandiko ulimaanisha KUTOKUNAJISIKA, ASIYENAJISIKA, UNAJISI ni lazima kujiuliza unajisi ni nini kunajisika kunakozungumzwa hapo ni nini? Neno unajisi kwa urahisi ni kuchafuka, kuchafuliwa n.k. kuingiliwa kwa mwanamke katika tendo la ndoa kungepeleka taarifa ya uzuri au ubaya wa tendo hilo katika Ubongo na ungerekodiwa mara moja, taarifa ya utamu wa tendo la ndoa ingekuwa imeingizwa kwa mwanamwali ambaye hakuna mtu wa kumuoa bado, uhitaji wa tendo ungeingizwa mapema kwa binti katika ubongo wake, angeanza kuwakwa tamaa ya kutaka mume huku hakuna wa kumuoa na hivyo roho ya ukahaba ingeingia kichwani na hivyo kumbikiri mwanamke kungeitwa kumnajisi au kumfanya kuwa kahaba, na kama binti aneshindwa kujitunza angeitwa mpumbavu kwa hiyo maana kubwa ya kiroho kuhusu UBIKIRA ni KUTOKUNAJISIKA.

Nisiwachoshe sana.

Kauli mbiu Yetu Miaka kumi hii: Usioe mwanamke asiye na bikra, usinajisi kizazi chako mwenyewe.

Jokajeusi
 
Braza, hakika umedhamiria kuwaweka vijana kwenye njia! Ila shida inakuja hata kama ukipata bikira bado na yeye atataka kutest mitambo kujua size na mikato ya dushes tofauti na iliyotumika kumvunja bikra,

Mume ni kichwa yaani kiongozi, yaani namba moja, kitendo cha kukubali kuongozwa, kutanguliwa kinapoteza sifa nzima ya kuwa Mume yaani kichwa cha familia.

Sisi kwetu wengi tumebahatika kuoa bikra, hii ni kutokana na utaratibu wa ukoo wetu. Hii imepunguza kwa asilimia 90% malalamiko ya wanawake kutoka nje ya ndoa.

Niliwahi kusema mwanamke bikra ukimuoa kutoka nje ya ndoa ni 10% hizo 90% ni ngumu kwake kutoka.
Lakini mwanamke asiye na bikra ukimuoa kutoka nje ya ndoa ni 95% hizo 5% ndio ngumu kutoka.

Umalaya wa kizazi cha sasa unatokana na wanawake wengi kutoolewa bikra, na ndio maana Mungu akasisitiza na hata wazee wa zamani wakasisitiza vijana waoe wasichana katika ubikra wao.
 
Vijana tuikimbie zinaa. Kwa zinaa mzigo wa dhambi umetuelemea.tuliyoyapanga mengi hayatimii kwa sababu ya ufuska.tunazitumikia tamaa za miili yetu.
Sema nini mleta thread nimekupata kiukweli kwa hili bandiko.
 
Aiseee, inawezekana ni kweli.. Na vipi kuhusu sisi wanaume? Inatakiwa wanawake waolewe na wanaume ambao hawajawahi kunyandua?
 
Aiseee, inawezekana ni kweli.. Na vipi kuhusu sisi wanaume? Inatakiwa wanawake waolewe na wanaume ambao hawajawahi kunyandua?

Wanawake wakishajitunza automatic mwanaume hawezi kunyandua.

ZIngatia mwanaume hawezi kujitunza kwa sababu ya mwanamke bali mwanamke ndiye anayejitunza kwa sababu ya mumewe. Hii ni kutokana na sababu kuwa mwanaume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke bali mwanamke kwa ajili ya mwanaume.

Yaani mwanamke ndiye anajitunza kwa ajili ya mume wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…