Maana ya Mwanamke Bikra, Kuwa na Mahusiano/Kuoa Mwanamke Bikra

Mkuu hadi nimekuuliza hivyo ni kwamba nimeshasoma hizo threads zako sana tu na nimegundua bado haujui maana ya bikira hivyo bado haujui unachokiongelea... Itoshe tu kusema kwamba huwa unaandika kwa mihemko na siyo facts...

Tukikwambia utuletee takwimu hapa za wanawake wangapi walioolewa mabikira ndoa zao zina amani na wangapi hazina amani... Na wanawake wangapi ambao hawakuolewa mabikira ndoa zina amani na wangapi hazina amani sidhani kama utatuletea...

Pia tukikwambia utupe takwimu ni wanawake wangapi walioolewa mabikira na wamebarikiwa na wangapi hawajabarikiwa... Na wanawake wangapi ambao hawakuolewa mabikira wamebarikiwa na wangapi hawajabarikiwa sidhani kama utatupa...

JF sijajiunga jana wala juzi huwa napita sana humu kusoma namna vijana wa siku hizi mnavyokaa mnadanganyana kuhusu mapenzi na mahusiano kwa ujumla wake... Na wengi huwa mnajadili haya mambo kwa mihemko tu na siyo facts...
 
Akikujibu nishitue.
 
Kimsingi ni kutafuta mwanamke asie na hulka ya umalaya suala la bikra ni ziada tu ukiikuta sawa usipoikuta fresh
Hizi sheria za bikra nadhan zibakie kwa mataifa husika
 
Nilichoelewa mimi ni kwamba, kama wanawake wakiwa na uwezo wa kujitunza unadhani wanaume tungefanya ngono na nani?! Uzinzi utatokea wapi..
Hata mimi nimemwelewa sana na nilitaka aje hapo hapo ila sasa mkuu unamwambiaje mwanamke ajitunze halafu unamwacha mwanaume aendelee kutongoza tu hovyo? Unafikiri wanawake wataweza kukwepa vishawishi vyote vya kutongozwa ikiwa wanaume wataendelea kutongoza hovyo?

Ndiyo maana tunasema haya mambo mnapoyapigia kelele hakikisheni mnayapigia kelele kwa pande zote mbili maana ngono inahusisha jinsia zote mbili! Tusiongelee haya mambo as if wanaume wanafanya ngono na viumbe vingine na wanawake wanafanya ngono na viumbe vingine!
 
[emoji4] mwanamke akijitunza, mwanaume atafanya ngono na nani!?... [emoji16] stick on it dude...



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…