Miaka kadhaa iliyopita kuna demu niliwahi kutembea nae, baadae tulikuja kupotezana kama miaka miwili, kumbe ndani ya hiyo miaka miwili demu aliolewa.
Siku zote hizo namba yangu alikua bado anayo kichwani kwake, siku moja alinipigia simu ndo akanieleza kuwa ameolewa na ana mtoto mmoja. Nilimpa hongera tukapiga story mbili tatu tukaagana, basi ikawa kila mara ananipigia simu ananisalimia na kuna wakati ananipiga vizinga nami bila hiyana namtumia fresh tu.
Sasa kuna siku aliniomba pesa nikagoma kumpa, nikamwambia muombe mumeo, haiwezekani raha umpe yeye halafu pesa nikupe mimi. Dah yale maneno yalimuingia sana, bila ajizi demu akanijibu hata wewe ukitaka nitakupa wewe sema tu lini unataka nikuletee. Nilichoka sana, nikasema kama ndoa zenyewe ndo hizi ni bora vijana tusioe, yule demu mpaka leo namkwepa. Sitaki kabisa mchezo wa kula wake za watu
Sent from my SM-A105F using
JamiiForums mobile app