From what I know kuhusu bk ni kujitunza(hujawahi make love), na ndyo maana nikakwambia kujitunza ni kwa watu wote tu ke & me, Usomi wa mtu huwa unaugunduaje? I'm not msomi btw, na hata ingelikua hivo, watu tunaendelea kujifunza daily and I hope hujamaster kila kitu kama ni msomi pia.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Afadhali umesema from What you Know. Sasa nami nakujuza kuwa Bikra maana yake ya msingi ni Mwanamke ambaye hajawahi kufanya ngono. Na hilo huthibitishwa na alama za ubikra alizonazo sehemu za siri. Hata Biblia inaeleza kuwa Mwanamke kama utamkuta hana alama za ubikra unaruhusa ya kumpa talaka.
Maana ya Ziada au dokezi ya neno Bikra ni kitu chochote kisichowahi kufanyiwa matumizi. Maana hii huwa si ya msingi japo inatokana na Maana ya msingi.
Nakupa Mfano;
Neno :KUPE" maana ya msingi ya neno kupe ni mdudu mdogo anayenyonya damu wanyama wengine.
Lakini maana ya ziada ya neno "Kupe" ni Mtu yeyote mnyonyaji. Kwa mfano Nchi za ulaya Nyerere aliziita kupe kutokana na Unyonyaji waliokuwa wanaoufanya. Lakini kimsingi nchi hizo sio wadudu bali ni kutokana na tabia au sifa walizokuwa nazo.
Mfano mwingine ni neno "SIMBA" ni mnyama wa mwituni jamii ya paka. Hii ni maana ya msingi ya neno Simba.
Lakini maana dokezi au ya ziada mtu anaweza kujiita simba kutokana na kuwa na sifa fulani za mnyama huyo. Aidha ni ujasiri, nguvu au mamlaka.
Mfano Diamond Platinum anajiita simba lakini kimsingi sio simba.
Hivyo unapoambiwa neno lolote lile ni lazima ujue maana yake ya msingi kwanza sio unakuja kukurupuka kama mpumbavu.
Shamba au ardhi kuitwa bikra yaani haijatumika ni maana dokezi ambayo inatokana na kutotumika kwake. Lakini kimsingi bikra ni mwanamke ambaye hajawahi kufanya mapenzi. Na anaalama hizo za ubikra.
Mwanaume ataitwa bikra ikiwa mtu ataamua kutumia maana dokezi ya Ubikra lakini kimsingi mwanaume sio bikra.
Mfano; Mwanaume anaweza kuitwa Mwanamke ikiwa anatabia au sifa za mwanamke lakini kimsingi yeye sio mwanamke. Bali watu wataangalia maana dokezi au ya ziada ambayo huzingatia sifa, tabia au umbo la kitu husika.
Nakupa mfano mwingine.
Neno KIFARU. Ni mnyama mkubwa wa porini anayekula majani. Hiyo ndiyo maana ya msingi.
Lakini ipo dhana ya kivita iitwayo pia "kifaru" hii ni maana dokezi kutokana na dhana hii kuchukua umbo la mnyama kifaru.
Lakini maana ya msingi ya neno Kifaru ni mnyama wa porini.
Haya mambo kama hujui ni bora uombe muongozo.
Nafurahi kuona na kusikia kuwa ulikuwa tayari kujifunza.
Mkienda shule muwe mnajifunza mambo mengi.
Mtu aliyeenda shule sishindwi kutambua jinsi anavyoandika. Kwa hiyo usinibishie wakati muandiko wako unakushtaki.