Maana ya neno hallelujah Diamond Platnumz amekosea kulitumia?

Maana ya neno hallelujah Diamond Platnumz amekosea kulitumia?

Kwenye wimbo wa sauti Sol na alikiba neno hallelujah limetumika pia na watu wameuimba sana hawakukumbuka kama hill neno humtukuza Mungu..
 
Ingekuwa kwa maustadh angechezea mikwaju huyo dogo...maustadh hawataki mchezo ktk dini.
 
Huyo jamaa alichokifanya HAKIELEWEKI....mara ana vaa MISALABA mara ALELUJAH.....mara anajenga misikiti .....hilo neno hakupaswa kulitumia sababu yeye yupo tofauti na upande huo....ni sawa na PADRI sikike anasema ALAH AKBAR....hata kama ni mwanamuziki alipaswa atafute neno lingine kufikisha UJUMBE...alelujah hapana...
Unajua nyie watu mmekaririshwa na wala hamjui mnachoongea!!!

Mosi, Hallelujah is just a word lililotokana na Kigiriki na Kihebrania ambazo lugha zake zimetumika sana kwenye Bible. Tafsiri ya hilo neno ni "Tumsifu Mungu" kwa Kiswahili au Praise to the Lord kwa Kiingereza.

Kama ukisema neno la kumsifu Mungu unapata thawabu 1000, basi ukisema "Tumsifu Mungu" utapata thawabu 1000 na ukisema Hallelujah utapata thawabu zile zile 1000 cuz' Hallelujah is just a word!!!

Neno linalotumika na Waislamu (read Arabs) sio Allah Akbar kama ulivyotoa mfano wako wa Padri kanisani bali Alhamdulillah! Tafsiri ya neno Alhamdulillah in English ni Praise be to God, kwa Kiswahili Ahsante Mungu!!! Unatumia hilo neno kwa kumshukuru Mungu kwa kile alichokupa au kufanya.

And YES, Arab Christians wanasema Alhamdulillah kwa sababu, that's just arabic world linalotumika kumsifu au kumshukuru Mungu kama ambavyo Mgiriki angemshukuru Mungu kwa kusema Halleluyah hata kama yeye sio Mkristo au kama ambavyo Diamond alivyomsifu Mungu kwa kumpa mwanamke mzuri lakini yeye hakutumia Kiswahili bali ametumia neno la Kiingereza lililotoholewa kutoka kwenye Kihebrania.
 
Nakuuliza tu maana ulisema uislamu na ukristo ni utumwa
No! Sijasema Uislamu na Ukristo ni utumwa bali Waislamu na Wakristo wasiosoma ni watumwa!!!

Ni watumwa kwa sababu, kwa mfano hapa watu wanatoka povu kwa sababu Diamond ambae Mwislamu ametumia neno "Hallelujah!" Ni kutokana na kutosoma ndio maana wanadhani hilo neno ndio Ukristo wenyewe kumbe ni neno tu lenye tafsiri ya kumsifu Mungu! Na ni kwavile tu Bible imetumia sana Kihebrania na Kigiriki ndo maana hilo neno lipo lakini kama original text ingekuwa ni Kiarabu kwa mfano, hapa leo hii tungekuwa tunazungumzia "Alhamdulillah" na sio Hallelujah!
 
Nyie wakristu isomeni biblia vizuri. Vitu kama hivyo sio big deal kabisa, wenye uelewa haitawasumbua.
Kuna watumishi wa mungu wanatamka jina la yesu kila siku lakini inaeleweka kabisa kuwa wanatumia nguvu za giza.
Neno lolote linaweza kutumika sehemu yoyote ile. Kama hakuna utukufu wa Mungu ndani yake basi halina maana yoyote kimungu.
So diamond ni kama anajifurahisha tu, sio issue!
 
Kwanza mkuu unatakiwa utambue kwamba kila kitu kina sababu,
kwahiyo unaposema Mungu apewe sifa unatakiwa ujiulize "apewe sifa kwaajili gani?"
anhaa maybe kwa kukuzawadia kitu flani,

okay hata kwa diamond, unatakiwa ujiulize amesema Mungu apewe sifa kwaajili gani? ndipo jibu linakuja
'Apewe kwaajili ya kumpatia zawadi ya Mwanamke mzuri ambaye ndiye anayemsifia ndani ya huo wimbo!...'

Vilevile unatakiwa ukumbuke kwamba Mapenzi sio dhambi, na kumshukuru Mungu na kumtukuza kwa zawadi aliyokupatia pia sio dhambi.
Usipomkumbuka Mungu kwa vitu vidogo basi hata kwa vikubwa hautomshukuru..

HALELLUJAH......
Yaani nilikuwa natafuta jinsi ya kuiweka ila wewe umeeleweka vizuri sana watu wengine hata church hawaendi ila wanajua kilakitu.
 
Free mason followers hujifanya wanatamka maneno ya Mungu muumba mbingu na nchi kumbe siyo hivyo, wanamtukuza LUCIFER, Angebisha kama si mfuasi wa shetani Gwajima angeleta video, lakini akanywea.
 
Free mason followers hujifanya wanatamka maneno ya Mungu muumba mbingu na nchi kumbe siyo hivyo, wanamtukuza LUCIFER, Angebisha kama si mfuasi wa shetani Gwajima angeleta video, lakini akanywea.
nasikia Gwaji boy ataliamsha dude jpili
 
ac79e673900816a880b7419ebedbf26b.jpg

Zawadi Lupelo

Wanajamvi salamu kwanza!

Nimeusikiliza wimbo mpya wa Diamond Platnumz kwa makini sana. Kitu kilichonitatiza na kuja kunishughulisha hapa jamvini ni neno hallelujah na namna lilivyotumika ni maoni yangu kwamba limetumika kimakosa katika wimbo huo ambao ni wa mapenzi hasa ukizingatia maana ya msingi ya neno ambapo huwa linatumika kwenye ibada katika kumsifu Mungu ni neno linalomaanisha "Mungu apewe sifa".

Ni neno ambalo linaenda sambamba na maneno Bwana asifiwe, tumsifu Yesu Kristo na kadhalika huko makanisani kufikia hatua ya kulitumia hili neno kwenye wimbo wa mapenzi katika muktadha wa Diamond Platnumz ni kufeli kwake katika uteuzi wa maneno.

Haiwezekani umezungukwa na mademu wapo nusu uchi unaimba Hallelujah huku ni kuitweza imani na utukufu wa Mungu.

Ni matumaini yangu wakati mwingine atakuwa makini kwenye kuchagua maneno ya kutumia ili kuhakikisha haleti mkanganyiko wowote.

I rest my case.

Zawadi Lupelo.

Ni wengi wana muziki wa Merekani wametumia neno hilo, hawana kosa isipo kuwa nyimbo nyingi za wana muziki waleoo no zamafumbo, hivyo munazisikia hazimanishi kama hivyo zinasikika kwenye masikio ya kawaida, zina Ujumbe wa ndani niwachache na wala wanao jua dunia Yoko he

Unaweza kuwa sahihi kwa manana ya neno ya Hallelujah. But they mean that.
 
Unajua nyie watu mmekaririshwa na wala hamjui mnachoongea!!!

Mosi, Hallelujah is just a word lililotokana na Kigiriki na Kihebrania ambazo lugha zake zimetumika sana kwenye Bible. Tafsiri ya hilo neno ni "Tumsifu Mungu" kwa Kiswahili au Praise to the Lord kwa Kiingereza.

Kama ukisema neno la kumsifu Mungu unapata thawabu 1000, basi ukisema "Tumsifu Mungu" utapata thawabu 1000 na ukisema Hallelujah utapata thawabu zile zile 1000 cuz' Hallelujah is just a word!!!

Neno linalotumika na Waislamu (read Arabs) sio Allah Akbar kama ulivyotoa mfano wako wa Padri kanisani bali Alhamdulillah! Tafsiri ya neno Alhamdulillah in English ni Praise be to God, kwa Kiswahili Ahsante Mungu!!! Unatumia hilo neno kwa kumshukuru Mungu kwa kile alichokupa au kufanya.

And YES, Arab Christians wanasema Alhamdulillah kwa sababu, that's just arabic world linalotumika kumsifu au kumshukuru Mungu kama ambavyo Mgiriki angemshukuru Mungu kwa kusema Halleluyah hata kama yeye sio Mkristo au kama ambavyo Diamond alivyomsifu Mungu kwa kumpa mwanamke mzuri lakini yeye hakutumia Kiswahili bali ametumia neno la Kiingereza lililotoholewa kutoka kwenye Kihebrania.
Wewe wacha kudanganya watu..elewa kuna tofauti kubwa ya KANZU YA SHEHE na KANZU YA PADR I ....praise the lord ni bwana asifiwe...na ni tofauti ALHAMDULI LAH....na sio bwana ashukuriwe.....na halelujah ni PIA NI TOFAUTI na ALAH akbar...nimekupa mfano sema ALAH AKBAR kanisani....kama utabaki salama....kwanza elewa MUNGU wa halelejah KAFIA MSALABANI...na MUNGU wa alah akbar HAKUZAA WALA HAKUZALIWA..ni MUNGU TOFAUTI..
 
No! Sijasema Uislamu na Ukristo ni utumwa bali Waislamu na Wakristo wasiosoma ni watumwa!!!

Ni watumwa kwa sababu, kwa mfano hapa watu wanatoka povu kwa sababu Diamond ambae Mwislamu ametumia neno "Hallelujah!" Ni kutokana na kutosoma ndio maana wanadhani hilo neno ndio Ukristo wenyewe kumbe ni neno tu lenye tafsiri ya kumsifu Mungu! Na ni kwavile tu Bible imetumia sana Kihebrania na Kigiriki ndo maana hilo neno lipo lakini kama original text ingekuwa ni Kiarabu kwa mfano, hapa leo hii tungekuwa tunazungumzia "Alhamdulillah" na sio Hallelujah!
Sasa nimekuelewa mdau mwenzangu
 
Mi sion tatizo hapo mana the girl make him say hallelujah kwamba mungu asifiwe kwa kumuumba au kwa sababu yoyote ile aloimaanisha bado anmsifu mungu kwa hilo
 
Back
Top Bottom