Maandamano ya 7/7: Nani anaenda kuandamana (?)

Maandamano ya 7/7: Nani anaenda kuandamana (?)

Sasa tofauti na hivyo ndio maana wana waterm kama wahuni.Hamko tayari kwa hili ambalo nimeuliza kwa maana kinachofanyika ni unafiki na uoga.

Ya hivyo siwezi.Kama umesoma historia ya dunia japo kidogo.Kosome situation kabla ya industrial revolution in Europe.Mnachotaka kufanya ndicho kile wale mabwana walikuwa wanafanya.Ukisasema maandamano lazima kuwe na organisation.Kwahiyo unataka tu mtu atoke kwake kwamba anaenda kuandamana hajui anaanzia wapi na kuishia wapi.(utakuwa kichaa kabisa au hujui unachofanya)

Mnaenda kuwapa polisi sababu ya kuwaua tena mara nyingine
Na kwa staili hiyo ndo matokeo yake ni vurugu na vitu visivyo takiwa
 
Yalikuwa nn
Hilo liko wazi.

Binafsi mwanzo nilifurahia sana kuona hatimae Watanzania tumeamka, ila badae nikagundua hamna tulichofanya zaidi ya kufeli.

R.I.P kwa walio poteza maisha. Nawapa sana pole walioondokewa na wapendwa wao na nawalaani na kuwaombea mabaya sana wote waliohusika kutekeleza kile kitu
 
Nilikuuliza yalipo pangwa mara ya kwanza ULIKWENDA?

We kaa kitako na utulie kama ulivyotulia mara ya kwanza

HAYAKUHUSU
Waache wenye shughuli yao…..,,, PERIOD
Hapo sasa ndo umeweka kwa usahih, "tuwaache wenye shughuli yao", hapo nimekuelewa mana hili haliwezi kua la wananchi.

Japo sasa inaleta wasiwasi nikijiuliza hili ni la akina nani na wana malengo gani. Naomba tu kwa mungu wawe na malengo mazuri na nchi pindi wakifanikiwa🙏🏽
 
Mm n familia yangu pamoja na ukoo wangu wooote.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Mkuu ukiona hivyo ujue haya maandamano HAYAKUHUSU………. Why bother?

Hujalizimishwa wala hulazimiki kuandamana…… tuache tunaojua kinachoendelea

Huwa napata sana ghadhabu🤬
kwamba huelewi kwanini watu wanaandamana?
Kwamba hujui kwanini maandamano yanakua organized kwa mtindo huu?
Unaishi nchi gani? Hii hii Bongo?

Usituchoshe mkuu, subiri maandamano ya umoja wa vijana ccm yana sifa zote unazotaka na posho juu……..Haya ya “kihuni” yako nje ya uwezo wako wa Kufikiri
MATAKÒ YAKO
Mkuu, mtu yeyote anayejifanya hajui kwa nini watu wanataka kuandama ni aidha ni mnufaika wa mfumo uliopo au hajitambui.
 
Hilo liko wazi.

Binafsi mwanzo nilifurahia sana kuona hatimae Watanzania tumeamka, ila badae nikagundua hamna tulichofanya zaidi ya kufeli.

R.I.P kwa walio poteza maisha. Nawapa sana pole walioondokewa na wapendwa wao na nawalaani na kuwaombea mabaya sana wote waliohusika kutekeleza kile kitu
Of course tulifeli ila haikuwa failure mana ujumbe ulifika, ila ujue hakunaga maandamano ya kumtoa mtu madarakani afu yawe maandamano ya amani.
 
Of course tulifeli ila haikuwa failure mana ujumbe ulifika, ila ujue hakunaga maandamano ya kumtoa mtu madarakani afu yawe maandamano ya amani.
At least tusinge focus na kuharibu na kupora mali tungekua na point
 
Hapo sasa ndo umeweka kwa usahih, "tuwaache wenye shughuli yao", hapo nimekuelewa mana hili haliwezi kua la wananchi.

Japo sasa inaleta wasiwasi nikijiuliza hili ni la akina nani na wana malengo gani. Naomba tu kwa mungu wawe na malengo mazuri na nchi pindi wakifanikiwa🙏🏽
Kwani “Mwananchi” ni nani?
Ni wale wanaomsimamisha Mwigulu awahutubie?
Ni wale wanaokwenda kwenye maandamano ya umoja wa vijana CCM?
Ni wale wanaojitokeza kwenye mikutano ya CHAUMMA?
Ni wale wanaolalamika TBC na kichwa habari “Wananchi walalamikia vyama vya upinzani kuleta vurugu”

Mwananchi ni nani?

Kwamba kwasababu jambo fulani HALIKUHUSU wewe na linahusu wengine wanakua sio WANANCHI?

Mkuu kama kweli hujui kwanini watu wanataka kuandanama basi there’s a very very thin line between you na MPUMBAVU……………..Am very sorry to say that
 
Nimeshaweka wazi kua natamani kuona wananchi tunaandamana ila kilicho tokea 29/10 hakikua tulichotakiwa kufanya na nina wasiwasi hata 7/7 bado sio wananchi wanaotaka kuandamana na hata kama itatokea basi haitoenda sawa kama inavyotakiwa kua. Hope nipo wrong
 
Wanaopanga maandamano wote wako nje ya nchi, wote hawatakuwepo nchini hio siku,
Na hakuna hata mmoja anaejua chocho za miji ya bongo ili kama mkizuwia hii njia mpite njia mbabala
wao wako huko mitandaoni na vikao vyao kuhamsisha watu waandamane ndio maana 29/10 watu walikuwa hawajui nini cha kufanya matokeo yake wakaanza kufanya uharibifu na wizi

Maandamano huko ulaya huwa hayakatazwi bali wanaweza kuwazuia wapi wasiende na wapi yaishie na waandamanaji wanakuwa wamejipanga kama wakizuiwa njia fulani wanajua njia mbadala ni zipi, lakini bongo ni makelelele tu mitandaoni bila mpangilio wala uongozi.
 
Hapo sasa ndo umeweka kwa usahih, "tuwaache wenye shughuli yao", hapo nimekuelewa mana hili haliwezi kua la wananchi.
Unless watoke nje ya nchi, ila kama ni raia ni wananchi pia.
Japo sasa inaleta wasiwasi nikijiuliza hili ni la akina nani na wana malengo gani.
Ni la wanamapinduzi, malengo ni mapinduzi ya kimfumo.

Wasemaji wa wanamapinduzi ni wanaharakati kina Mange, Maria n.k

Mbona mambo wanayasema wazi, kwanini usielewe?
 
Nikiwa kama mwananchi wa kawaida ninaetamani kuona nchi yangu inakua na uongozi bora unaoweka mbele maslai ya wananchi, nimeshindwa kuelewa hiki kinachopangwa kwenda kutokea siku ya 7/7.

Natamani kuona wananchi tunaamka na kupeleka ujumbe wetu kwa walio mamlakani, ila sidhani kama tuko tayari kufanya hivyo kwa sasa, hasa hii 7/7.

Naona kama wananchi mtaani hawana habari na hili jambo na hamasa yote inayofanywa ni kama inafanywa na kuishia mitandaoni tu, sijafanikiwa kukutana na mwananchi hata mmoja ambae ameongelea hili swala.

Kwaio naendelea kukosa jibu nikijiuliza ni nani anaenda kuandamana siku hiyo.

Sijui hata kitu gani kinachoendelea
 
Tumia akili ndogo tu. Huko mtaani nani ana uhuru wa kuongelea jambo hili? Lazima atajiingiza matatizoni. Ndiyo maana watu wanapashana habari mtandaoni, pia kumbuka hata walioko mtandaoni wanaishi mtaani na huko mtaani huwezi kuta anaongea haya anayopost humu kwa kuhofia usalama wake
 
29-10 lilifanywa kosa kubwa baada ya waandamanaji kuendekeza njaa na kuanza kuiba na kuharibu badala ya kupeleka ujumbe,, jamaa wananjia 1,000,000 za kuyazuia maandamano kwa sasa.
Kwa mtazamo wangu waliokua wanafanya uharibifu walipangwa ili kutoyapa uhalali maandamano
 
Back
Top Bottom