Maandamano ya Februari 20 Mbeya, kiongozi wetu atakuwepo nchini?

Mifumo Gani haifanyi kazi, hebu kuwa muwazi utaje baadhi ya mifumo isiyofanya kazi?
Mimi tena nikutajie?

Hapa Dar hakuna maji, umeme ,sukari,

Wewe ndio uitaje mifumo iliyoshindwa kuhakikisha Kuna umeme, maji na sukari Kwa uchache,

Karibu
 
Mimi tena nikutajie?

Hapa Dar hakuna maji, umeme ,sukari,

Wewe ndio ulitaje mifumo iliyoshindwa kuhakikisha Kuna umeme, maji na sukari Kwa uchache,

Karibu
Mimi sijazungumzia mifumo, wewe uliyetaja mifumo uwanja ni wako. Hayo matatizo uliyo orodhesha bila fedha yanatatuliwaje labda?
 
Kwahiyo Fedha za kutatua matatizo ndani ya nchi zinapatikana nje ya Nchi?

Kuna Nchi huko duniani yenye pesa za ziada zisizo na KAZI za kutugaia bure?
 
Wewe kama una amini Kiongozi wa nchi anakwenda kutembea na kutalii ni Sawa tu.
 
Salaam,Shalom!!

Baada ya kumaliza msiba, tuendelee na ujenzi wa Nchi yetu.

Yalifanyika maandamano katika majiji makubwa nchini ,Dar es Salaam na Mwanza,maandamano hayo yameendelea kupata mwitikio mkubwa wa wananchi, hayo yametokea kiongozi wetu ,Mkuu wa Nchi akiwa nje ya Nchi ziarani. Je ni coincidence au planned?

Kunako TAREHE 20 mwezi February 2024, yatafanyika tena maandamano ya Amani jijini Mbeya. HOJA kuu za wananchi zikiwa;

1. Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi, kabla ya Uchaguzi wowote.

2. Kukithiri Kwa Mgao wa Umeme,

3. Kuadimika sukari nchini.

4. Kupanda gharama za Maisha.

5. Madai ya Tume HURU ya UCHAGUZI Kwa kuondoa Miswada iliyo bungeni, Ili irejeshwe UPYA Kwa kubadili vifungu vya Katiba kumwondoa Rais kuteua Tume ya Uchaguzi na wasimamizi wake nknk, HOJA ambazo hazijapatiwa majibu Hadi sasa.

Ningependa kujua ikiwa kiongozi wetu, mkuu wa Nchi, Rais Samia Suluhu Hassan atakuwepo nchini siku hiyo au ataendelea na ziara nje ya Nchi.

Tunaomba live update tafadhali kuhusu maandamano.

Karibuni 🙏
Kila maandamano yeye hukimbia nchi.

Anaamini kuwa kukimbia changamoto ndiyo utatuzi wenyewe
 
Wewe kama una amini Kiongozi wa nchi anakwenda kutembea na kutalii ni Sawa tu.
Ikiwa wananchi wanashindwa kuzalisha Kwa kukosa umeme,

Ambapo umeme ungekuwepo, uzalishaji ungeongezeka, TRA wakapata Kodi ya kutosha,

Pasingekuwa na haja ya kwenda kutembeza bakuli.
 
Inavyoonyesha,

Maandamano yakiwa endelevu Kwa wiki hivi,

Atatokomea Huko once and for all!!
Kiongozi ambaye haamini kama nchi yake inaweza kujitutumua bila utegemezi wa misaada na kuuza nchi ni kiongozi anayeisaliti jamii yake.

Hatuwezi kuwa na fikra zilizoshindwa kuongoza nchi badala yake wanabadili badili sheria ili kupata fursa ya kuuza nchi halafu tuwaheshimu na kuwaenzi. Kimsingi Tanzania imecollapse kuanzia mfumo hadi misingi ya utawala wa nchi.

Tunahitaji a frest restart
 
Ikiwa wananchi wanashindwa kuzalisha Kwa kukosa umeme,

Ambapo umeme ungekuwepo, uzalishaji ungeongezeka, TRA wakapata Kodi ya kutosha,

Pasingekuwa na haja ya kwenda kutembeza bakuli.
Kumbe hakuna kinachoendelea kutatua tatizo hili la umeme?
 
Kiongozi ambaye haamini kama nchi yake inaweza kujitutumua bila utegemezi wa misaada na kuuza nchi ni kiongozi anayeisaliti jamii yake.

Hatuwezi kuwa na fikra zilizoshindwa kuongoza nchi badala yake wanabadili badili sheria ili kupata fursa ya kuuza nchi halafu tuwaheshimu na kuwaenzi. Kimsingi Tanzania imecollapse kuanzia mfumo hadi misingi ya utawala wa nchi.

Tunahitaji a frest restart
Mabadiliko ya haraka sana yanatakiwa.

Saizi Yale maigizo ya kumchangia achukue fomu yamekosa mvuto!!
 
Kumbe hakuna kinachoendelea kutatua tatizo hili la umeme?
Hizo juhudi zinanihusu nini mwananchi niliyelipia token ya luku na Umeme hamna?

Nisaidie, niwajibuje wateja waliokuja kunyoa kwenye saluni za wananchi Nchi nzima!!
 
Mabadiliko ya haraka sana yanatakiwa.

Saizi Yale maigizo ya kumchangia achukue fomu yamekosa mvuto!!
Kinachotakiwa kubadilika siyo kiongozi wa juu wa nchi bali chama kinachoongoza nchi kinapaswa kuwekwa pembeni ili kuruhusiu nchi isonge mbele kwa hatua za ukweli kabisaa.
 
Hizo juhudi zinanihusu nini mwananchi niliyelipia token ya luku na Umeme hamna?

Nisaidie, niwajibuje wateja waliokuja kunyoa kwenye saluni za wananchi Nchi nzima!!
Waambie mgao utaisha June mara baada ya megawatts 480 kuanza kuzalishwa bwawa la Mwalimu Nyerere. Hivyo wazingatie ratiba za mgao wa umeme kwenye maeneo yao.
 
Kinachotakiwa kubadilika siyo kiongozi wa juu wa nchi bali chama kinachoongoza nchi kinapaswa kuwekwa pembeni ili kuruhusiu nchi isonge mbele kwa hatua za ukweli kabisaa.
Ni Kweli kabisa,

Tubadili mifumo ya kiuongozi Kwa kupata Tume huru ya Uchaguzi na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wowote.

Kupatikana Kwa Tume huru ya Uchaguzi na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wowote,ni kupoiteza CCM Moja Kwa moja.
 
Waambie mgao utaisha June mara baada ya megawatts 480 kuanza kuzalishwa bwawa la Mwalimu Nyerere. Hivyo wazingatie ratiba za mgao wa umeme kwenye maeneo yao.
Kodi ya pango ,

Mishahara ya wafanyakazi itakuwaje?

Kodi ya mapato TRA itapatikana vipi?
 
Kodi ya pango ,

Kodi ya mapato TRA itapatikana vipi?
Unachoongea uko sahihi kabisa wala sikupingi. Waliopewa nafasi wamesema ivyo June 2024. Sasa ni aidha ubishe au uwe flexible kuokoa jahazi.
 
Riba za mikopo na mikopo italipika vipi ikiwa Nchi Iko gizani haizalishi?

Hiyo HASARA anabeba nani?

Tanesco wanadai tatizo Si uchache wa umeme, ni uchakavu wa miundombinu!!

Pesa alizopewa Makamba kufanya service zilifanya KAZI Gani?
 
Kwakweli hata mimi ni muhanga, ni vyema Makamba akatujibu pesa kapeleka wapi?
 
Hapo ilitakiwa akamatwe arudishe pesa hizo zitatue changamoto Tanesco wanazodai kukwamisha upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Kumwacha Makamba huru , kiongozi Akaenda kutafuta pesa zingine Kwa same issue hiyo haikubaliki.

Kiukweli CCM inachowafanyia Watanzania hakivumiliki,

Njia ya kuiwajibisha CCM itapatikana tu,

Ngoja maandamano yaendelee.
 
Hakuna marefu yasiyo na ncha, tusipo yashuhudia watashuhudia wajukuu zetu.
 
Back
Top Bottom