Maasai hawana habari za Yesu wala Mohamad ila wamenyooka kwenye misingi yao na maadili mazuri

Maasai hawana habari za Yesu wala Mohamad ila wamenyooka kwenye misingi yao na maadili mazuri

mkushite

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2021
Posts
666
Reaction score
1,619
Nikiwaambiaga watu ya kwamba Afrika tamaduni zetu na dini zetu za asili ni bora kuliko hizi dini zilizoletwa kwa ajili ya biashara ambazo ni ukristu na uislamu huwa wanabisha.

Hebu tazama maasai, hawa jamaa wanaweza ishi na mtu yeyote. Hawana tabia za ajabu ajabu na za kishenzi kama hawa jamaa walioshika tamaduni na dini za kigeni. Maasai anaridhika na kidogo alichonacho, hana tamaa za kijinga jinga.

Kabla ya uvamizi wa dini na tamaduni zao, sisi tulikuwa na maadili yetu na misingi iliyobora kwa ajili ya ustawi wa jamii zetu.

Kama tukikusanya tamaduni zilizo bora kwa kila jamii ya kiafrika na kisha tunatengeneza kitabu kama Bible ya kiafrika si tutaweza kuokoa kizazi hiki na kijacho?

Hawa jamaa walioleta tamaduni na dini ndiyo wanaleta na mambo ya ushoga na kama ushakubali tamaduni zao na dini zao na wamekubatiza majina yao ni lazima ukubaliane na ushoga wao.

Kwa sasa tuseme basi, tuwaachie tamaduni zao na dini zao. Wabaki na akina yesu na mohamadi wao sisi tutengeneze wa kwetu. Na inawezekana sana. Kama sisi tumepewa uzazi kwa nini unatulazimisha tusizae? Kama tuna nguvu za kufanya mapenzi kwa nini useme ni dhambi?

Ni sawa, tamaduni zetu nyingi zimekwisha haribiwa na hawa jamaa watenda laana. Tuige mfano wa jamii ya ki maasai ambao bado hawajachakachuliwa kwa kiasi kikubwa kulinganisha na jamii zingine. Tutengeneze mfumo mpya wa maadili kwa ajili ya kunusuru kizazi hiki na kijacho.
 
Hizi dini ni uhuni ni wachache sana kama mm huwa wanatambua hili uwe na upeo mkubwa sana
 
Cc Masai uwez sikia tumelawiti wtt..

Cc kwetu uwezi ckia vitimbwi vya migogoro ya ndoa Wala malii..

Cc Masai tunaishi kulingana na taratibu zetu katika Koo zetu ..

Cc Masai ktk maishà hatushindan Kwa kulogana na Wala hatuyumbishi na manabii uchwaraa..
 
Lakini mbona tunasikia umasaini hakuna albino wala vilema?
Je ni kweli huwa mnawauwa kwa kuwaona ni nuksi na hawahitajiki kwenye jamii zenu?

Naomba utufungue hapo kuhusu vilema kama ni siri nayo potezea tu
 
NAMI napotezeaa km ifatavyo mkuu.
 
Baadhi ya tamaduni za kiafrika ni za kishenzi mno.
Huo ushoga ni hiari yako kuuupokea au kupuuza lakini kuna mila za makabila ni ngumu mno kuishi nazo.

Kuna kabila mtoto akizaliwa nje ya ndoa anauwa, albino anauawa bila sababu za msingi.
Baadhi ya makabila ni wabaguzi hatari, walau hiki kiswahili kinatuunganisha la sivyo Tz isingekalika hii na huu muingiliano tulionao sasa.
 
Mumchukue na Mfalme Zumaridi awe kiongozi wenu.
[emoji38] [emoji23] [emoji38] [emoji23] huyo anatetea skm zaidi
Screenshot_20230317_125607_Instagram.jpg
 
Baadhi ya tamaduni za kiafrika ni za kishenzi mno.
Huo ushoga ni hiari yako kuuupokea au kupuuza lakini kuna mila za makabila ni ngumu mno kuishi nazo.

Kuna kabila mtoto akizaliwa nje ya ndoa anauwa, albino anauawa bila sababu za msingi.
Baadhi ya makabila ni wabaguzi hatari, walau hiki kiswahili kinatuunganisha la sivyo Tz isingekalika hii na huu muingiliano tulionao sasa.
Wasukuma wanatamaduni mbaya na za kikatili sana!! Ujio wa ukristo na uislamu umesaidia kuondoka au kupunguza kwa kiasi ukatili huo.
 
Wasukuma wanatamaduni mbaya na za kikatili sana!! Ujio wa ukristo na uislamu umesaidia kuondoka au kupunguza kwa kiasi ukatili huo.
Acha kabisa mkuu tawala za kichifu zilitesa mno raia,
Imagine unafanya biashara yako halafu watoto wa chifu wanakuja kula/kunywa bure na huwezi wafanya kitu coz ni watoto/wajukuu wa chifu.
 
Wasukuma wanatamaduni mbaya na za kikatili sana!! Ujio wa ukristo na uislamu umesaidia kuondoka au kupunguza kwa kiasi ukatili huo.
Mkuu sio hao tu, hata Wanyamwezi pia ilikuwa mtemi akifa wazee wa kimila wanachagua mwali ili ampakate marehemu na kufukiwa nae
Halafu familia ya msichana wanatamba kuwa mwanao kachagulia kwa heshima kubwa kuzikwa na Chief akiwa hai

Ila dini zimesaidia sana katika jamii na sio serikali
Ni Dini ndio zimebadilisha tamaduni za kikatili
Imagine msichana hai anafukiwa kwa upumbavu huo
 
Nikiwaambiaga watu ya kwamba Afrika tamaduni zetu na dini zetu za asili ni bora kuliko hizi dini zilizoletwa kwa ajili ya biashara ambazo ni ukristu na uislamu huwa wanabisha.

Hebu tazama maasai, hawa jamaa wanaweza ishi na mtu yeyote. Hawana tabia za ajabu ajabu na za kishenzi kama hawa jamaa walioshika tamaduni na dini za kigeni. Maasai anaridhika na kidogo alichonacho, hana tamaa za kijinga jinga.
kubwa kulinganisha na jamii zingine. Tutengeneze mfumo mpya wa maadili kwa ajili ya kunusuru kizazi hiki na kijacho.
Kwa hiyo unaona mila yao ya kuchomeka Mkuki nje halafu unazama kulala na mke wa mtu ni sawa?. Kwa kifupi Yesu ni wa kila mtu rafiki,ingawa mtu ana haki ya kumpokea au kumkataa kwa sababu zake binafsi. Tatizo ni kwamba hujamjua Yesu personally. Unaishi ukisikia habari zake Tu.
 
Wasiomkubali yesu watatupwa kwenye ziwa za moto wa milele, no discussion, no nini😞
 
Kwa habari ya dini lazima uelewe kuwa Mungu alitengeneza utaratibu kwamba zianzie sehemu Fulani Kisha zisambae duniani kote. Uchina wahindi wakorea bado wanadini zao za asili lakini nakuhakikishia Mungu wa Wakristo Na Kama wauslamu wanamudu huyo ndio sahihi na ametukataza kuchonga kinyago na kukiita Mungu kuabudu mizimu kufanya kafara za damu n.k miungu ipo Mingi Sana lakini huyu tunayemuabudu ndiye sahihi na bado tunakazi ya kuwaelekeza dunia nzima sio sisi tu tumeletewa hata marekani na dunia nzima wameletewa
 
Wamasai
Mtuambie Vilema na Albino wa Kimasai mnawapeleka wapi ?
 
Naskia huko umasaini kuna Ukeketaji
Hivi mnajua madhara ya kuwakeketa hawa dada zetu..
Na hilo limekaaje???
 
Back
Top Bottom