Maaskofu Katoliki acheni kuunga mkono bomba la mafuta. Nchi za zilizoendelea zinaondokana na matumizi ya mafuta sisi ndio tunataka kuanza kuyachimba!

Sijaona Maaskofu wa Kanisa Katoliki wanaingiaje hapa kwenye mada yako
Gazeti la Kiongozi linalomilikiwa na Baraza la Maaskofu Katoliki limeripoti kuwa maaskofu hao wanaunga mkononi uharakishwaji wa bomba la mafuta.
 
Swala la Ozone layer depletion siyo issue tena! Imetengenezwa. Imetengemaa kwa sasa.
Elezea kidogo imetengenezwa na nani na lini,maana ni juzi tu hapa kuna documentary moja niliiona inaelezea ku-repair ozone layer depletion is almost impossible...tena wakaonesha na baadhi ya nchi mfano India anga lake limejaa moshi mfano wa ukungu hadi watu hawaonani....vipi leo chap hivyo?
 
Hivi wewe unafuatilia EV and battery technology pamoja na maendeleo ya kuhamia kwenye renewable energy yanayofanywa na nchi zilizoendelea, au unafuatilia vilabu ya soka Ulaya siku nzima.
😂😂😂Unajikuta upo nje ya mda ni kwamba hujui kitu hata hyo technology unayofautilia unaparazia yaani huijui kiundani...Kaangalie mataifa makubwa wameweka mwaka gani ndo ukomo wa kutumia magari ya mafuta..
 
Nyie kila kitu mnapinga. Dunia lazima iwe na nishati mbadala. Kila kitu bado ni endelevu ndio maana hata ulaya pamoja na ugunduzi wa mashine bado kuna wafanyakazi wengi mno wameajiriwa viwandani.
 
Elezea kidogo imetengenezwa na nani na lini,maana ni juzi tu hapa kuna documentary moja niliiona inaelezea ku-repair ozone layer depletion is almost impossible...tena wakaonesha na baadhi ya nchi mfano India anga lake limejaa moshi mfano wa ukungu hadi watu hawaonani....vipi leo chap hivyo?
Ozone layer ipo juu angani kwenye Stratosphere, hapa tulipo sisi na ulipopasema kwamba India kuna ukungu watu hawaonani, ni sehemu inaitwa Troposphere. Uchafuzi wa troposphere, ni nadra kuingia kwenye stratosphere.
Sasa katika stratosphere kwenye OZONE LAYER - oxygen molecules zina react na UV RADIATION na kuendelea kujengeka na kutengeneza Ozone (O3/mara O2) na Oxygen. Yaani mwisho ile hole inazidi kupungua.
 
Hivi wewe unafuatilia EV and battery technology pamoja na maendeleo ya kuhamia kwenye renewable energy yanayofanywa na nchi zilizoendelea, au unafuatilia vilabu ya soka Ulaya siku nzima.
Umeielewa ripoti ya IEA niliyokuwekea? IEA report inatoa taarifa za kiulimwengu jinsi uwekezaji na matumizi ya nishati yalivyo.

Mimi ni mdau katika nishati jadidifu, kumbuka hilo.
 
Ozone layer ipo juu angani kwenye Stratosphere, hapa tulipo sisi na ulipopasema kwamba India kuna ukungu watu hawaonani, ni sehemu inaitwa Troposphere. Uchafuzi wa troposphere, ni nadra kuingia kwenye stratosphere.
Sasa katika stratosphere kwenye OZONE LAYER - oxygen molecules zina react na UV RADIATION na kuendelea kujengeka na kutengeneza Ozone (O3/mara O2) na Oxygen. Yaani mwisho ile hole inazidi kupungua.
Endelea kuelezea kwamba ozone layer inaadhiriwa na nini.? maana moshi wa viwandani umekataa zaidi unaelezea matabaka yaliopo kwenye uso wa dunia
 
Swala la Ozone layer depletion siyo issue tena! Imetengenezwa. Imetengemaa kwa sasa.
Mkuu, fafanua zaidi hapa kuhusu ozone layer kutengemaa.. kwamba hatupo kwenye hatari tena dhidi ya global warming? hii habari nzuri sana.
 
Ninaandika kwa mara nyingine kuhusu jambo hili ambalo wengi wenu hamtapenda kulisikia. Naandika kama mzalendo kwa nchi yangu Tanzania na sina interest nyingine yoyote kibiashara katika jambo hili. Naandika kwa kifupi tu hapa.

Ukweli ni kwamba dunia inakwenda kwa kasi sana. Mambo ya climate change sasa ni dhahiri na nchi zilizoendelea zimeonesha nia thabiti ya kuachana na mafuta ya miambani (fossil fuels) ambayo huchafua hewa na mazingira na kusababisha kuongezeka kwa joto na madhara ambatanishi.

Baadhi ya nchi za Ulaya kama Norway magari ya umeme yanazidi yale ya petrol/dizel na lengo ni kuondoa magari yatumiayo mafuta ifikapo 2030. Lengo hili limewekwa na nchi nyingi za Ulaya. China inaongoza kwa wingi wa magari ya umeme duniani ikiwa na magari milioni 7, ikifuatiwa na USA 2 milion na Germany 1.3 milioni.

Ukiangalia tunakokwenda utagundua kuwa future ya magari na mafuta ni fupi sana na sio zaidi ya miaka kumi kutoka sasa magari ya mafuta yatakuwa machache kuliko ya umeme duniani kote na hivyo soko la mafuta litaanguka.

Ndio kusema uwekezaji mkubwa ambao Tanzania na Uganda wanauweka kwenye bomba la mafuta ni upotevu wa fedha za maskini wa nchi hizi. Nani anawashauri viongozi wa nchi hizi?! Maaskofu katoliki acheni kuunga mkono msilolijua! Fuatilieni mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa technologia ya engine za umeme na hydrogen, la sivyo mnachangia kuwafukarisha watanzania!

Nina uhakika bomba la mafuta la Hoima-Tanga litakuja kutumia kusafirisha maji ya kumwagilia kutoka ziwa Victoria na sio mafuta.
Hivi wewe upo sawasawa kweli? Matumizi ya mafuta hayataisha hata siku moja, Wewe unajifanya mwana mazingira wakati hujui unachofanya
 
Ukweli ni kwamba dunia inakwenda kwa kasi sana. Mambo ya climate change sasa ni dhahiri na nchi zilizoendelea zimeonesha nia thabiti ya kuachana na mafuta ya miambani (fossil fuels) ambayo huchafua hewa na mazingira na kusababisha kuongezeka kwa joto na madhara ambatanishi.

Baadhi ya nchi za Ulaya kama Norway magari ya umeme yanazidi yale ya petrol/dizel na lengo ni kuondoa magari yatumiayo mafuta ifikapo 2030. Lengo hili limewekwa na nchi nyingi za Ulaya. China inaongoza kwa wingi wa magari ya umeme duniani ikiwa na magari milioni 7, ikifuatiwa na USA 2 milion na Germany 1.3 milioni.

Ukiangalia tunakokwenda utagundua kuwa future ya magari na mafuta ni fupi sana na sio zaidi ya miaka kumi kutoka sasa magari ya mafuta yatakuwa machache kuliko ya umeme duniani kote na hivyo soko la mafuta litaanguka.
Maaskofu wako sahihi

Magari ya umeme unayotolea mfano ndio yatasababisha climate change kubwa kuliko mafuta

Magari ya umeme yanatumia madini mbalimbali

Kupata madini ya kutengeneza battery moja tu ya gari la umeme unahitaji tani sio chini ya 90 za mawe uyapeleke kiwandani yachenjuliwe upate hayo madini ya kutosha kutengeneza betri moja

Tani hizo 90 ni kwa ajili ya kutengeneza betti moja

Hayo madini hupatikana kwenye mapori mengi yaliyoko Afrika. Hivyo.tujiandae misitu kuteketea wakichimbua hayo madini

Gari za umeme zitaangamiza zaidi Africa kwenye climate change
 
Ukiangalia tunakokwenda utagundua kuwa future ya magari na mafuta ni fupi sana na sio zaidi ya miaka kumi kutoka sasa magari ya mafuta yatakuwa machache kuliko ya umeme duniani kote na hivyo soko la mafuta litaanguka.
Battery yeyote inahitaji replacement iwe ya simu ,ya gari nk

Battery ya gari ya umeme ku replace inategemea aina ya gari bei.ya chini kabisa kwa vigari vidogo ni dollar 5000 sawa na milioni kumi na moja za Tanzania na juu ni dola elfu ishirini sawa na kama milioni 45 za Tanzania

Maana yake nini huko mbeleni tukiruhusu hayo magari ya umeme yawe ndio pekee pesa zetu za kigeni zote zaweza.ishia kununua betri tu za magari

Kwa taarifa hiyo ni moja ya factor watu Tanzania hata matajiri wakubwa hawaagizi hayo magari ya umeme

Sababu kitu kingine yanakula sana umeme na muda wa kuchaji ni mrefu sana iwe nyumbani au kituo cha kujazia tofauti na mafuta
Mfano Kuchaji charger ya kawaida nyumbani kwako waweza hitaji kuchaji hadi masaa nane hadi 12 kujaza full kutegemeana na aina ya charger uliyonayo bei za chini ni laki 8 za juu nzuri ni milioni tano za Tanzania sababu hilo.betri ni rechargeable kama la simu tu na likiwa full utatembelea kilomita 250 unatakiwa uchaji tena

Hata ukiwa na fast charger uwe mtulivu hadi ifikie full usubiri walau saa moja na umeme linaokula mwingi lazima uamkie shikamoo bill ya umeme

Umeme wa Tanzania na nchi nyingi Afrika bado mdogo hautoshelezi mahitaji sembuse wa kutosha magari ya umeme wakati viwandani tu bado hautoshi

Mafuta yataendelea kuwepo muda mrefu

Huwezi endesha kiwanda kwa kutumia umeme wa betri ya gari

Mafuta yanaendelea kuwepo tu
 
Ninaandika kwa mara nyingine kuhusu jambo hili ambalo wengi wenu hamtapenda kulisikia. Naandika kama mzalendo kwa nchi yangu Tanzania na sina interest nyingine yoyote kibiashara katika jambo hili. Naandika kwa kifupi tu hapa.

Ukweli ni kwamba dunia inakwenda kwa kasi sana. Mambo ya climate change sasa ni dhahiri na nchi zilizoendelea zimeonesha nia thabiti ya kuachana na mafuta ya miambani (fossil fuels) ambayo huchafua hewa na mazingira na kusababisha kuongezeka kwa joto na madhara ambatanishi.

Baadhi ya nchi za Ulaya kama Norway magari ya umeme yanazidi yale ya petrol/dizel na lengo ni kuondoa magari yatumiayo mafuta ifikapo 2030. Lengo hili limewekwa na nchi nyingi za Ulaya. China inaongoza kwa wingi wa magari ya umeme duniani ikiwa na magari milioni 7, ikifuatiwa na USA 2 milion na Germany 1.3 milioni.

Ukiangalia tunakokwenda utagundua kuwa future ya magari na mafuta ni fupi sana na sio zaidi ya miaka kumi kutoka sasa magari ya mafuta yatakuwa machache kuliko ya umeme duniani kote na hivyo soko la mafuta litaanguka.

Ndio kusema uwekezaji mkubwa ambao Tanzania na Uganda wanauweka kwenye bomba la mafuta ni upotevu wa fedha za maskini wa nchi hizi. Nani anawashauri viongozi wa nchi hizi?! Maaskofu katoliki acheni kuunga mkono msilolijua! Fuatilieni mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa technologia ya engine za umeme na hydrogen, la sivyo mnachangia kuwafukarisha watanzania!

Nina uhakika bomba la mafuta la Hoima-Tanga litakuja kutumia kusafirisha maji ya kumwagilia kutoka ziwa Victoria na sio mafuta.
Hakika uongo ukirudiwa mara nyingi huonekana ukweli. Hivi umewahi kujiuliza hizo nchi zinazopigia kelele hilo Bomba la mafuta mbona wao ndiyo wanaoongoza kwa kusafirisha mafuta na gas kwa njia hiyo hiyo?
Yaani ni kama wao kutuambia viwanda vinaongeza joto Duniani lakini wao kila siku wanaongoza kutengeneza viwanda na haitoshi wanashindana kutengeza WMD's kwaajili ya kumwangamiza huyo huyo Binadamu ambaye wanajifanya wanamlinda dhidi ya uharibifu wa Mazingira.
Amka Mkuu hakuna anayependa Africa iinuke na kujitegemea kwakuwa ndiyo soko kuu la bidhaa zao na huduma
 
Wazungu wamemlisha ujinga mleta mada hadi hajielewi

Hawezi hata kuwahoji swali kama hilo
Kalishwa uzungu hadi kuongea anapinda mdomo akiongea kizungu ili ufanane na wazungu

Wanaharakati ngozi nyeusi wasiojielewa wanatuangusha mno waafrika weusi wenzao yaani mada yake anajiona kashusha bonge la point

Very sad
 
Wazungu wamemlisha ujinga mleta mada hadi hajielewi

Hawezi hata kuwahoji swali kama hilo
Kalishwa uzungu hadi kuongea anapinda mdomo akiongea kizungu ili ufanane na wazungu

Wanaharakati ngozi nyeusi wasiojielewa wanatuangusha mno
Wanotegemewa kutupigania Africa wameshanunuliwa na wasaliti. Tuna safari ndefu kulikomboa Bara hili dhidi ya mirija ya unyonyaji kutoka Mataifa ya ughaibuni
 
Back
Top Bottom