Maaskofu matamko yenu yametosha sasa, ni muda umefika muende kwa Msajili wa Vyama vya Siasa mfungue chama chenu

Tukitafuta wahu 10 wanaoongoza kwa wehu hapa Tanzania, huchomoki kwenye nafasi ya 2 na ni kwa vile tu nafasi ya kwanza yupo THE BIG SHOW
 
Ebu punguza lugha chafu jadili mambo kwa hoja.
 
Hii laana umeitafuta kwa nguvu yako mwenyewe ,hivi walifaham kanisa hili? Mkuu fanya yako ,ila kaa pembeni na kanisa hili , tunza hii kwa siku zijazo
 
Kwa hiyo wakati wa Biashara ya utumwa Mashehe ndio walikuwa wapo kipaumbele kupigania Uhuru ?
 
Uovu Gani MAASKOFU wenyewe ni wezi tuh, MAASKOFU wameshiriki hadi kupokea mgao wa fedha haramu za Escrow kipindi kile wanajifanya wazalendo uzalendo wautoe wapi?
Wewe ndiyo maana tunasema huna akili.

Tuambie nani mpaka leo hii aliwahi kuhukumiwa kwa kuhusika kwenye pesa ya Escrow account? Rugemerila walimlazimisha akiri kosa, akakataa, na hawakuweza kumfanya chochote kwa sababu hakuwa na kosa.na mwisho akaachiwa.
 
Ni bahati mbaya sana kuwa nchi haina uhaba wa watu wenye fikra kama za huyu bwana (nahisi ni mwanaume). Sehemu kubwa ya jamii inapokuwa na akili za kiendawazimu kama hizi, tunakuwa na hali ijulikanayo kama ‘mass psychosis’ ambayo inasababishwa na watawala kufisha uwezo wa wananchi kufikiri kiusahihi. Kufishwa huku kwa uwezo wa wananchi kufikiri (menticide) kunatekelezwa kwa njia mbalimbali na watawala ikiwemo uminywaji wa haki za raia, utekaji, mauaji ya kiholela nk. Kwa hiyo hoja ya huyu mwenzetu ni kiashiria cha tatizo kubwa linalotukabili kama nchi
 
Sasa kwani ni uongo kuwa kanisa lilinufaika na pesa zile za wizi?

Kwahiyo kwa kuwa Ruge hakuchukuliwa hatua unadhani ilikua sahihi wao kuchukua zile fedha we nguchiro?
 
Wewe ni mjinga sana, unafurahia hali hii mbaya nchi inakopekekwa? Unadhani utabaki na hiyo nafasi milele?
 
Mara Leo wake na DP World,kesho waje na la wamasai shida YENU Nini?
Kukaa kimya kwa huu utawala siyo kwamba eti unawaogopa kama mnavyodhani,hamna mamlaka ya kuipangia serikali kitu chochote,hapa siyo Vatican tambueni.
Na hapo wewe ndie kwa hapo masjid kwenu.. ELIMU ELIMU ELIMU
 
Kiongozi wa dini kwa kiapo cha imani yake, anastahili kukemea uovu wa aina yoyote, uwe wa kijamii, kisiasa, kiuchumi, kimaadili au kiroho. Ukemeaji wa uovu hauna mipaka.

Labda useme kuwa kudhulumu haki za watu za kisiasa siyo uovu. Kuwaua watu kwa sababu za kisiasa siyo uovu. Nje ya hapo waache viongozi wa dini watimize wajibu wao.

Soma historia, utapata orodha ndefu ya manabii waliowakemea wafalme, na wengine hadi waliuawa na wafalme kwa sababu ya ukweli wao dhidi ya watawala ambao hawakutenda haki.
 
Mara Leo wake na DP World,kesho waje na la wamasai shida YENU Nini?
Kukaa kimya kwa huu utawala siyo kwamba eti unawaogopa kama mnavyodhani,hamna mamlaka ya kuipangia serikali kitu chochote,hapa siyo Vatican tambueni.
Hawatakaa kimya na utawala hautawafanya lolote. Wakati wanakomaa na magufuli alipokuwa anawakaanga kule kibiti mlikuwa wapi?
 
Bibilia inatutaka tusishuhudie uovu.Hivyo,Maaskofu wanakemea maovu Kwa watawala maana wakikaa kimya itaonekana wanaunga mkono maovu ya awamu hii ya sita inayoongoza Kwa ukatili
Wanapopokea hongo SI uovu huo
 
Hawatakaa kimya na utawala hautawafanya lolote. Wakati wanakomaa na magufuli alipokuwa anawakaanga kule kibiti mlikuwa wapi?
Hukuwaskia Hawa nguchiro enzi za magufuli wakiwa wanaleta Fujo kama hizi,pamoja na kuminya kwake Demokrasia kanisa lilikaa kimya kabisa,Leo midomo mireefu kama kakakuona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…