kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Dini sio mhimili miongoni mwa mihimili kwenye taifa. Kazi kubwa kupita zote za dini ni kukusanya sadaka na kazi nyingine zitafuatia tu. Hakuna tukio Wala kusanyiko la dini lisilokuwa na utoaji sadaka.
Ili dini ziwe imara lazima usalama, utulivu na hali ya uchumi wa waumini viwe imara pia, la sivyo kwenye machafuko hakuna mahubiri, kusanyiko na sadaka. Au nakosea?
Vitabu vyetu vya dini vinasema tiini mamlaka na mamlaka zinatoka kwa Mungu. Hivyo, kazi ya maaskofu na Masheikh ni kuziombea mamlaka zidumu na zitende haki na kutimiza matakwa ya wanadamu na sio kuzikosoa. Mlifanya hivyo wakati wa serikali za wakoloni fanyeni hivyo hata Sasa, miliziombea serikali za wakoloni zidumu, ziombeeni serikali za Africa zidumu. Maana kazi yenu ni sadaka na kuomba Mungu ili mazuri yatokee na mabaya yatoweke kwenye jamii. Kukosoa Mamlaka ni kazi ya wabunge na bunge na wanasiasa.
Kukosoa mamlaka ni chanzo kikuu cha aibu na mateso kwa watu wa Mungu tangu kale. Au nakosea?
Usheikh na uaskofu haukupi kinga yoyote pale unapoingilia mamlaka tangu enzi za akina Herode, Farao, Kaiser na Sultan. au nakosea?
Kama mnaona Kuna jambo haliendi vizuri kwa watawala kazi yenu ni kuomba Mungu na kufunga ili Mungu afanye jambo mamlaka itende haki na wakati huohuo wanasiasa nao wanafanya hivyo kwa kuikosoa mamlaka.
Kifupi kazi yenu ni kurekebisha kwa maombi na kazi ya wanasiasa ni kurekebisha kwa kukosoa serikali. Vinginevyo vueni tasbihi na rozali muwe wanasiasa.