Maaskofu na Masheikh ni raia pia, tiini mamlaka bila shuruti

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Dini sio mhimili miongoni mwa mihimili kwenye taifa. Kazi kubwa kupita zote za dini ni kukusanya sadaka na kazi nyingine zitafuatia tu. Hakuna tukio Wala kusanyiko la dini lisilokuwa na utoaji sadaka.

Ili dini ziwe imara lazima usalama, utulivu na hali ya uchumi wa waumini viwe imara pia, la sivyo kwenye machafuko hakuna mahubiri, kusanyiko na sadaka. Au nakosea?

Vitabu vyetu vya dini vinasema tiini mamlaka na mamlaka zinatoka kwa Mungu. Hivyo, kazi ya maaskofu na Masheikh ni kuziombea mamlaka zidumu na zitende haki na kutimiza matakwa ya wanadamu na sio kuzikosoa. Mlifanya hivyo wakati wa serikali za wakoloni fanyeni hivyo hata Sasa, miliziombea serikali za wakoloni zidumu, ziombeeni serikali za Africa zidumu. Maana kazi yenu ni sadaka na kuomba Mungu ili mazuri yatokee na mabaya yatoweke kwenye jamii. Kukosoa Mamlaka ni kazi ya wabunge na bunge na wanasiasa.

Kukosoa mamlaka ni chanzo kikuu cha aibu na mateso kwa watu wa Mungu tangu kale. Au nakosea?

Usheikh na uaskofu haukupi kinga yoyote pale unapoingilia mamlaka tangu enzi za akina Herode, Farao, Kaiser na Sultan. au nakosea?

Kama mnaona Kuna jambo haliendi vizuri kwa watawala kazi yenu ni kuomba Mungu na kufunga ili Mungu afanye jambo mamlaka itende haki na wakati huohuo wanasiasa nao wanafanya hivyo kwa kuikosoa mamlaka.

Kifupi kazi yenu ni kurekebisha kwa maombi na kazi ya wanasiasa ni kurekebisha kwa kukosoa serikali. Vinginevyo vueni tasbihi na rozali muwe wanasiasa.
 
Hongera kwa kupost. Ubora utaoneshwa na wachangiaji.
 
Moja ya wajibu mkubwa wa viongozi wa dini, ni kukemea maovu.
Waumini wakiwa waovu, watakemewa ili waache uovu.
Waliomo CCM na GoT ni waumini wa hao viongozi wa dini.
Kiongozi wa dini asiyehubiri haki na kukemea maovu, huyo sio kiongozi.
 
Moja ya wajibu mkubwa wa viongozi wa dini, ni kukemea maovu.
Waumini wakiwa waovu, watakemewa ili waache uovu.
Waliomo CCM na GoT ni waumini wa hao viongozi wa dini.
Kiongozi wa dini asiyehubiri haki na kukemea maovu, huyo sio kiongozi.
Governor Twining alikuwa msafi kwa kiasi gani? Sultan Said Balaghash alikuwa msafi kiasi Gani? . Waliwakemea waache wizi wa rasilimali zetu?. Maaskofu na Masheikh hawakuwepo? Nani walimtesa Mtume Issa bin Mariam/Masià? Dini haijawahi kushinda dhidi ya mamlaka tangu kale.

Dini kazi yake ni kuomba kwa Mungu tu kisha kukusanya sadaka. Wameruhusiwa kukusanya sadaka (Kodi) hata baada ya waumini wao kulipa Kodi ya serikali. Yaani muumini analipa Kodi mara mbili. Washukuru kuruhusiwa kutoza Kodi na kuiita sadaka.
 
Wafungieni makanisa yao na misikiti yao sasa
 
Governor Twining alikuwa msafi kwa kiasi? Sultan Said Balaghash alikuwa msafi kiasi Gani? . Waliwakemea waache wizi wa rasilimali zetu?. Maaskofu na Masheikh hawakuwepo?
Pole kwa uzwazwa.
Ya leo sio ya jana.
Kama wa jana hawakufanya, waliopo leo wameona wafanye, kuna tatizo kwenye hilo!!??
 
Ni kukusanya sadaka (maokoto) bhanawee!!! Wanakusanya sadaka hata kwenye mazishi na hata kwa wagonjwa.
Moja ya wajibu mkubwa wa viongozi wa dini, ni kukemea maovu.
Waumini wakiwa waovu, watakemewa ili waache uovu.
Waliomo CCM na GoT ni waumini wa hao viongozi wa dini.
Kiongozi wa dini asiyehubiri haki na kukemea maovu, huyo sio kiongozi.
 
Hao wenye mamlaka kwenye nchi ni waumini wa hizo dini. Viongozi wa kidini ni viongozi wao wa kiroho. Wanapokengeuka lazima waseme ili kuwaonesha njia sahihi.
 
Hao wenye mamlaka kwenye nchi ni waumini wa hizo dini. Viongozi wa kidini ni viongozi wao wa kiroho. Wanapokengeuka lazima waseme ili kuwaonesha njia sahihi.
Governor Twining hakuwa hakuwa muumini wao? Tiptip je, alikuwa haswali?
 
Kwahiyo kwa upande wa Mamlaka kazi ya viongozi wa dini ni KUSIFIA Tuu?

“Mama ni chaguo la Mungu”
“Wanao mkosoa mama Mungu awalaani” nk nk

Ila wanaosema
“Mauaji na utekaji yanapaswa kukomeshwa” hawa wanakua “Watumishi wa Shetani”?

BTW ni wabunge gani hao unaosema kazi yao ni kukosoa serikali?
Ni hawa wanaopinga kwa nguvu zote serikali kukosolewa?
 
No reform no election
 
Usemacho nikweli kwamba watumishu wa Mungu ni wanadamu.
Tena kama kwa ubindamu wao wanavyoweza kumkosea Mungu vivyo hivyo wanaweza kumkosea mtu na serikali pia na madhara yakatokea.

Je, huoni kama viongoz wa nchi wanatakiwa kujihubiri neno la Mungu(ikiwa wanaamini katika Mungu) kwakuwa hao watumishi wa Mungu wamekuwa duni sana machono pa hao wafalme?
 
Governor Twining hakuwa hakuwa muumini wao? Tiptip je, alikuwa haswali?
Lakin pia mkuu ujue kwamba kama katiba imewahukum hao watumishi wa Mungu kuwa wenye makosa, hilo linatosha kuwachukulia hatua ni muhimu sana kujua hilo.
Sio lazima tujifunze kwa akina hao sijui tifutifu.
Ila zingatia tuu kwamba viongozi wengi wanaamini ktk ushirikina na huko wengi wanatafta kibali mbele za watu na viongoz wenye mamlaka za teuzi.

Kwahyo usishangae kwanin hawana hofu kwa watumishi wa Mungu na Mungu wao.
Wangeamini sana katika Mungu mengine yasingekuwa stori kubwa.
 
Reactions: Cyb
Sio Kila mtu anaetekwa, Kazi ya maaskofu ingekuwa kuwaombea wale wote wenye tabia na matendo yanayosababisha watekwe waokoke na kuacha tabia hizo kwa msaada wa mwenyezimungu. Huwezi kuzuia mwenye mke asimteke mgoni wake, aliedhulumiwa fedha zake asimteke aliyemdhulumu.

Askofu kukosoa wanasiasa ni dalili ya kuacha kumuamini Mungu tena kama anayo nguvu za kuwaadhibu watekaji na kubadilisha tabia za watekaji. Kazi yao imebakia kukusanya bahasha za mapesa kwenye jumuiya, madhabahuni, misibani, kwenye sherehe, kwenye ndoa, kwenye miradi, nk. Wanadhani hatujui?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…