Maaskofu na Masheikh ni raia pia, tiini mamlaka bila shuruti

Hivi wewe umembaka mtoto wangu, umekata mkono wa mwanagu mwenye ulemavu wa ngozi, umefuga fisi wa kichawi ameua ndugu yangu, umeua mke wangu ukakata nyeti zake, tumechimba madini wote wewe akaenda kuuza na kuondoka na fedha zote, umeniuzia kiwanja ambacho umeshamuua mtu mwingine, unatumia cheo na pesa zako kutembea na mke wangu, ushashirikiana na wageni kuidhuru nchi kwa maslahi Yako, imethibitika pasipo shaka kuwa unataka kupindua mamlaka au kusababisha mauaji kwanini wewe mwenye matendo kama haya tusitekwe? Kwanini maaskofu na Masheikh wameshindwa kuomba watendo ya kuudhi kama haya yaondoke kwenye jamii?

Wameshindwa kuomba kwa Mungu mabaya yaondoke Sasa wanatumia njia ile ya wanasiasa huku wakijua kuwa njia ya siasa nayo Ina changamoto zake. Kwenye siasa Kuna matusi, kutekana, kuuana, vita, kupinduana, risasi na kunyongana.
 
Mimi nimeulizia tu vipi kuhusu upande wa pili wa Viongozi wa dini wakijihusisha na kuwasifia na kuwapongeza watawala.... hii mbona hamuwashambulii wanaingilia siasa?

Kwanini hao hao leo akisifia Mama ni chaguo la Mungu inakua sawa ila akikosoa anakua hamuamini Mungu?

What a double standard....
 
Nchi inaongozwa na UTAWALA WA SHERIA
Kama mtu kafanya uhalifu akamatwe afikishwe mahakamani na akikutwa na hatia apewe adhabu stahiki hata kama ni KUNYONGWA....... Sio kutekana kama VIBAKA

Kuhusu KUOMBA
Mkuu na umri wako huo bado unaamini kuna Mungu anasikia maombi?
Kwamba unaweza kuomba Mungu aondoe vibaka wote Tanzania na akawaondoa 😂😂😂😂😂

Ina maana huko Sudan, Gaza na mahospitalini walikojaa wagonjwa wenye terminal disease Mungu amefanya nini na watu wanaomba kila siku?

Hata vitabu vya hekaya za kusadikika kama bibilia na quran Fundi seremala na Mudi walikua wanafundisha na wanakemea maovu hawakuwa wakiomba maovu yaondoke
 
Dini ni ajira kama zingine,kama ilivyo siasa,ualimu,uinjinia,uaskari,udaktari na zingine.Binadamu walianzisha dini kwa lengo lakupumbaza wengine kwa minajili ya kuwajaza hofu,woga na kuwaambia kuhusu amani ili watawala wakisiasa watawale au kuongoza kwa utulivu.Hivyo ndivyo dini ilivyokua inatumika uko nyuma.Sasa hivi kwakua dunia imebadilika dini inaanza kupoteza umuhimu na watawala wanaanza kuwaona viongozi wa dini hawana tena umuhimu kwao kwasababu wanategemea vyombo vyakijeshi kuongoza.Kwahiyo viongozi wa kidini wanatakiwa wajue kua wao sio muhimu sana endapo mtawala atakua anaongoza vizuri bila kuwategemea wao kutuliza amani na utulivu.Sasa ni jukumu lao kuangalia namna gani yakuwafanya waendelee kuwepo kwakung'ata na kupuliza ili watawala waone umuhimu wao.Vinginevyo mtawala anaweza kuwafuta na akuna wanachoweza kufanya kwasababu dini ni ajira kama zingine.
 
Reactions: Cyb
Tanganyika siyo masikini kwa bahati mbaya isipokuwa ina wajinga wengi sn asee
Ni tajiri kama nchi gani ya Afrika? Acheni upuuzi wenu
Dini zao zimewaamuru kutii mamlaka na kuziombea maana zimetoka kwa Mungu. Kumbuka wakati vitabu vyao vinaandikwa mamlaka zote zilikuwa zikipatikana kwa ncha ya upanga.
 
Ni tajiri kama nchi gani ya Afrika? Acheni upuuzi wenu

Dini zao zimewaamuru kutii mamlaka na kuziombea maana zimetoka kwa Mungu. Kumbuka wakati vitabu vyao vinaandikwa mamlaka zote zilikuwa zikipatikana kwa ncha ya upanga.
Kwani ni kiongozi gani ambaye hatii mamlaka?

Au kwako wewe kutii mamlaka maana yeke ni viongozi wa dini kusifia mamlaka na sio kukosoa?

Kama hamtaki wakosoe basi wakemeeni pia wakisifia.... waambieni wasisifie wajikite na MAOMBI
 
Ni tajiri kama nchi gani ya Afrika? Acheni upuuzi wenu

Dini zao zimewaamuru kutii mamlaka na kuziombea maana zimetoka kwa Mungu. Kumbuka wakati vitabu vyao vinaandikwa mamlaka zote zilikuwa zikipatikana kwa ncha ya upanga.
Mwendawazimu mkubwa wewe
 
Kwani ni kiongozi gani ambaye hatii mamlaka?

Au kwako wewe kutii mamlaka maana yeke ni viongozi wa dini kusifia mamlaka na sio kukosoa?

Kama hamtaki wakosoe basi wakemeeni pia wakisifia.... waambieni wasisifie wajikite na MAOMBI
Kazi ya kuhoji matendo ya mamlaka kwenye majukwaa ya wazi ni kazi ya wanasiasa tu baaasi! Bunge ndio chombo maalumu cha kusemea malalamiko yetu kwenda kwa mamlaka. Mfikishie mabunge wako hoja zako kuhusu mamlaka akusemee. Wewe unaweza tu kwenda kulalamikia mahakamani baasi. Mchungaji hawezi kutumia madhabahu kuhoji mamlaka zilizotoka kwa Mungu. Kazi ya Mungu haihojiwi.
 
Mwendawazimu mkubwa wewe
Inamaana hiyo mistari haimo kwenye bibilia na msahafu? Wewe ni mwendawazimu usiyejua dini yako imekuamuru nini. Kama unataka kuhoji mamlaka vua kanzu na collar uwe mwanasisa, dini haina kichaka cha kujifichia na kutukana mamlaka, utachomelewa kwenye mimbari kama nguchilo kwenye shimo lake. Uliza wote waliowahi kufanya hivyo wakati wa akina sultan Balaghash, mfalme Kaiser, Herode, Nyerere, Magufuli, Mao, nk .
 
Tanganyika siyo masikini kwa bahati mbaya isipokuwa ina wajinga wengi sn asee
Ni miaka 64 Sasa tangu tupate Uhuru, huwezi kusema umaskini wetu umeletwa na Samia mwenye miaka 3 tu madarakani. Una jambo lingine kaka sio kuhusu umaskini. Nyerere alikuwa mwadilifu sana mbona hatukuendelea wakati wake wa kuiongoza Tanzania kwa miaka 27?
 
No reform no election
 
Kuna sehemu nimtaja Samia?
 
Reactions: Cyb
Wewe dini huijui Bali unachojua ni kuchagua vifungu vinavyokufurahisha wewe na unavyowalamba!
Dini na washika dini wote daima walikuwa ama wapo kwenye migogoro na dola zinazopuuza na kunyanyasa raia!
Go read your Bible or Quran!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…