Maaskofu na Masheikh ni raia pia, tiini mamlaka bila shuruti


NO REFORMS, NO ELECTION!
 
Wewe dini huijui Bali unachojua ni kuchagua vifungu vinavyokufurahisha wewe na unavyowalamba!
Dini na washika dini wote daima walikuwa ama wapo kwenye migogoro na dola zinazopuuza na kunyanyasa raia!
Go read your Bible or Quran!
Watu wa dini katika historia hawajawahi kushinda dhidi ya mamlaka kakamavu. Bwana Yesu alisulubiwa na mamlaka sembuse Hawa wetu
 
Sifa ya kwanza ya kutii Sheria ni kuwa wakweli,kumbe ukweli ndio Sheria ya kwanza kuliko zote na ninaamini viongozi wa dini wengi wanatekeleza ukweli huo ,ukiacha wale viongozi matapeli wanaoshiba kupitia siasa na kweli haipo ndani yao.
 
Sawa maaskofu hawana hiyo imani usemayo kuwalinda raia kwa maombi. Naama hawana imani,
Vipi serikali yenye jukumu hilo imeweza kuwalinda wanaanchi waliotekwa?.

Na kama hao maaskofu na mashehe wamekuwa si lolote yanini kuweka vitabu vya imani kuwaapisha hao viongoz waliowatakatifu kuliko hao watumishi wa Mungu?

Au kwanini mahakama (katiba) inawapisha mashahid mahakamani kwa hizo hizo imani zilipopungukiwa?
 
Watu wa dini katika historia hawajawahi kushinda dhidi ya mamlaka kakamavu. Bwana Yesu alisulubiwa na mamlaka sembuse Hawa wetu
Kama kwenye imani yako umejifunza hilo la Yesu kusulubiwa kwanini usishawishi serikali iwasurubishe haraka iwezekanavyo hao watumishi wa Mungu, ili tuendelee kuwa imara kiuchumi, kivita na kiintelenjensia?
 
Sasa mkuu kavuluta, hivi wew unadhani unaipenda serikali na rais SSH kuliko hao wanao hoji hayo?.

Na pia kwakuwa umekaa kuhukumu hao wakosoaji jiulize kwamba nikwamtazamo wako au katiba pia inasema hivo?

Kama katiba inasema hivo basi hiyo katiba kuu mara elfu kuliko wewe hivyo, acha wahukumiwe kulingana na sheria mama(katiba).
 
Mungu yupo na anazo nguvu nyingi sana, hivyo kuwaapisha kwa vitabu vya dini Kuna maana mbili; Mungu awape ulinzi, nguvu na hekima kwakuwa mamlaka imetoka kwako, pili ni kuwaita woga na hofu ya Mungu waapaji ili watende Yale yanayompendeza Mungu katika kuwahudumia raia.

Serikali Ina kazi kubwa na ngumu ya kulinda raia wake, kuwahudua kwa miundombinu, pembejeo, afya elimu , umeme, maji, nk. Sauti za huyooo huyooo mchinjeee mchinjeee kwa serikali ni sawa mtoto aliyebebwa mgongoni kung'ata meno mama yake mgongoni na shingoni; mama atafanya nn kwa jitoto lake hilo jehu?
 
Hapo nmekupata,
mtoto wa namna hiyo hakuna hukum zaid ya kumrudi,na sio kumwangamiza.

Hata mama wa huyo mtoto akiwaza kumuumiza sana huyo mtoto bado grandparents wa huyo mtoto wanaweza kumweleza mama wa huyo mtoto kwamba yeye alifanya utukutu zaidi ya huo lakin walivumilia.

Pili, mtoto anaweza kumng'ata mama yake mgongoni kutokana na kubebwa vibaya au mama yake kufanya vitu mtoto kujiona yuko hatarini.
Kwa ufupi kabla ya kumwangamiza huyo mtoto mama anatakiwa ajihskikishe dhamiriki yake iko kwenye utimamu na sio tuu kwasababu anao watoto wengi zaid ya huyo.
 
Watu wa dini katika historia hawajawahi kushinda dhidi ya mamlaka kakamavu. Bwana Yesu alisulubiwa na mamlaka sembuse Hawa wetu
Yesu anaendelea kuhubiriwa wakati huo akina Herode, Pilato na dola la warumi lishajifia!
Mtume Mohammed anaendelea kuheshimika wakati watesi wake washafutika kwenye historia!
Ushindi ni nini hasa??
Kifupi ni kwamba tawala dhalimu hazijawahi kushinda dhidi ya watu wa Mwenyezi MUNGU mwingi wa rehema mwenye kurehemu!
 
Aaaah, kaka wamekufa hao wote. Hata bob Marley, mangwea, Nyerere, Haile Ras, Sembuli, Maladona bado wanavuma ingawa wamekufa. Mamlaka hazichezewi na watu wa dini kwakuwa historia yao sio nzuri, wanaishia kuitwa wafia dini na mashahidi tu mbele ya hukumu za mamlaka.
 
Aiseeeee

Bado tuna safari ndefu sana kwenye ukombozi wa fikra
 
Aiseeeee

Bado tuna safari ndefu sana kwenye ukombozi wa fikra
Ni Serikali, bunge na mahakama, finito. Mengine yote kaa chonjo saa mbaya.

Dini hangaikeni na kumlilia Mungu awape busara na hekima viongozi wetu huku mkiendelea kukusanya bahasha za malimbuko, fungu la kumi, sadaka, zaka, mavuno, sadaka za kujimaliza na michango lukuki isiyokuwa audited Wala isiyohojiwa na waumini matumizi yake Wala idadi.
 
Fungeni na kuziombea taifa na viongozi wake wasambaze umeme na maji Kila kitongoji ili waumini wapate mwanga na maji ya kutawazia ya uhakika. Bila umeme magita na vipaza sauti kwenye nyumba za ibada ni Bure kabisa.
 
Maaskofu na masheikh (Ukiacha masheikh ubwabwa) kama ni raia kama raia wengine wanapaswa kuongea mawazo yao pia wakiwa madhabahuni. Wasikatazwe na huyo Samia na serikali yake ya mafisadi.
 
Vitabu vyetu vya dini vinasema tiini mamlaka na mamlaka zinatoka kwa Mungu. Hivyo, kazi ya maaskofu na Masheikh ni kuziombea mamlaka zidumu na zitende haki na kutimiza matakwa ya wanadamu na sio kuzikosoa.
Kwa hiyo wewe unafahamu ibada za hizo dini kuliko viongozi wa hizo dini?
Kukosoa mamlaka ni chanzo kikuu cha aibu na mateso kwa watu wa Mungu tangu kale. Au nakosea?
Kwamba watawala waachwe tu, waendelee kuteka na kupoteza na kuua?
Siku ulifikiwa wewe utasema hivyo?
 
Maaskofu na masheikh (Ukiacha masheikh ubwabwa) kama ni raia kama raia wengine wanapaswa kuongea mawazo yao pia wakiwa madhabahuni. Wasikatazwe na huyo Samia na serikali yake ya mafisadi.
Shida yao ni kwamba mawazo yao wanataka yawe mawazo ya waumini wao pia. Hapa ndipo mateso yao yanapoanzia
 
Kama tangu kale dini haijawahi kunyamaza dhidi ya uovu na Mungu hakuwahi kunyamaza basi hata sasa hakuna atakayemaza. Kazi ya viongozi wa dini ni kukemea uovu!
He who stands for nothing can fall for anything. Punguza cowardnes mjinga wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…