Maaskofu na Mashekhe: Tunataka tume huru ya Kijaji kuchunguza matukio yanayoendelea Tanzania kati ya Serikali na Chama cha Upinzani

Safi sana maaskofu ningewashangaa huyo Mungu mnayemtumikia ni Mungu wa aina gani kama hamwezi kukemea maovu haya.

Mungua awabariki pia muandae na vyeti vya kuzaliwa vya babu zenu na bibi zenu. Mungu awape nguvu kushinda huyu Babiloni
 
Ni wajibu wa viongozi wa Dini kukemea maovu maana "Haki huinua Taifa, Bali dhambi ni aibu ya watu wowote"

Wasipokemea uovu, nchi haitakuwa na amani maana kila mtu ataamua kufanya uovu wowote autakao, unadhani kutakuwa kuna Taifa tena? Vipi Serikali itakuwa tena?
Nawapongeza viongozi wa dini kutafuta suluhu ili kulinda AMANI ya nchi yetu, tusiingize Siasa kwenye mambo ya Msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbunge! Mwanamke! Akili mbovu tu! We unaamini nani anastahili kupigwa na askari. Mbunge unamuona ni kiumbe wa maana sana? Wapuuzi acha wapate zawadi yao.
 
Eti anajidai kuedit heading baada ya kuona tumewagundua, hatudanganyiki. Wadini wakubwa nyie. Ndugu zetu waislamu wanajitambua sana.kaeni na hao maaskofu wenu wa kasikazini.
 
Nani alikueleza amani inaletwa na dini au viongozi wa dini? Huo ndo udhaifu wa akili unaostahili kuuondoa. Inafikia hatua unaamini kuna wengine bora wanaoweza kukuletea amani! Ustaarabu wa dunia hii umeshatosha kuleta amani. Dini is nothing! Tena hiyo dini ndo tatizo! Wanajidai kutuletea tofauti zao ziwe za kwetu. Achana na akili ya aina hiyo.
 

Pamoja na kwamba umeamua kuchomeka dini ili kupoteza hoja ya msingi, ukweli ni kuwa hata hao viongozi wa dini wametumia muda mwingi kuanza kukemea ukatili wanaofanyiwa wapinzani kwa maagizo ya rais Magufuli. Hakuna asiyejua wala kuona wanachofanyiwa wapinzani kwa maagizo ya rais Magufuli na serikali yake kwa ujumla. Na kwakuwa watu wengi ikiwemo viongozi wa dini walikaa kimya kwa uoga, au kwa busara wakitegemea Magufuli na serikali yake wangebadilika, lakini hilo halijatokea na halionekani kutokea.

Viongozi wa kidini kwa kutambua nafasi yao, wameamua kusimama wazi hadharani bila kupepesa macho kuwa haya wanayofanyiwa wapinzani sio sawa wala sio haki. Hilo la kuundwa tume ya kijaji halikwepeki. Napenda nikusisitizie, nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi, hakuna mtu yoyote ataweza tena kuturudisha kwenye mfumo wa chama kimoja kwa shuruti. Magufuli kama Magufuli hilo haonekani kulijua, na kibaya zaidi kwakuwa watu wako kimya anadhani yuko sawa, na kwakuwa yuko live kila siku kwenye TV akitangaza miradi ya maendeleo, anadhani hiyo ni tiketi ya kuwanyanyasa wapinzani. Kwa taarifa yake haya anayoyafanya hayana nafasi kwa watanzania zaidi ya kikundi cha watu wachache wanaonufaika binafsi na utawala wa Magufuli.
 

Hoja yako ni nini hapa?
 
Hoja umeielewa ?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hapo mbona mashekhe sijaonabtamko lao
Unadhani ma sheikh ni wajinga kiasi hicho !! Bali wanajuwa kula na kipofu. Serikali kuu imechukuwa jukumu la kuwajengea makao makuu kwa gharama za 100% , unadhani watasema nini kwa sasa ?! Hiyo ni zaidi ya rushwa.

Ukweli unabaki kilichosemwa na maaskofu ni hoja. Na hoja hupingwa kwa hoja. Leta hoja ya kunyamazisha hoja yao. Usijifiche kwenye udini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukosefu wako wa elimu au unajitia uchizi?
Ndemeti!
 
Wanasiasa wafanye siasa na watu wa dini wafanye kazi za kiroho. Kuna vitu jamaa amesema vipo very clear ni kwanini viongozi wa KKKT wenye asili ya kichaga tu ndiyo wanalalamika na wanakuwa affiliated na Chadema? Pia ni kwanini viongozi wa RC na watu wengi wa kabila la wasukuma hawamsemi Magu? Hizi siasa za sasa ni za hatari sana na lazima zikemewe kwa pande zote mbili CCM na Chadema. Hatutaki machafuko kisa makabila,dhehebu au dini fulani inataka madaraka.
 
Hatuna taasisi nyeti zaidi ya urais. Ungekuwa unachukizwa na lugha chafu kwa dhati, unajua uanze na nani. Mtanzania yoyote aliyestaarabika anamjua.
 
Sasa hapo mbona mashekhe sijaonabtamko lao
Hujasoma kuwa ni kamati ya viongozi wa dini ndiyo iliyotoa tamko hilo? Hiyo kamati inajumuisha viongozi wawakilishi toka dini zote na madhehebu yote.
 
Hiyo ni fallacy...nilifikiri tutazame hoja yenyewe bila kujali anayeitoa hoja anatokea upande gani? Unataka kutuambia Askofu akitoka au mwenye asili ya kaskazini hoja yake inakosa umuhimu kwa sababu tu anatokea kaskazini? Hivi huu ujinga wa kutaka kuligawa taifa hili kwa misingi ya ukabila na udini nani anawajaza vichwani mwenu? Juzi tumemsikia mwenyekiti wenu pale Mbezi anamtaja Mushi kama mtu mwenye jina hilo kuwa "hapaswi kuaminiwa". Huu ni ujinga na komeni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…