Maaskofu wameitendea haki Katiba mpya - Warioba

Mbona mm nilikuwa kanisani anglikana leo padri hajaongelea katiba .mpya
 
Jinsi walivyosomewa waraka huo wasomewe pia Katiba Inayopendekezwa. Hivi hawa watumishi wakoje. Mbona Mitaguso yao ya Vatican I na II hadi ya African Synod sisi waumini hatukushirikishwa kuipigia kura. Kweli nimeamini na kwenye dini utawala wa kiimla unatawala. Sasa waumini kwa kuonyesha kukomaa kwenu kiroho na kimwili ipigie kura ya Ndiyo baada ya kuielewa Katiba Inayopendekezwa. Acha kukubali kila kitu kitokacho kwa hawa wazee. Wanaweza wakaamua kuwa kuanzia leo hakuna misa je mtafanyaje, mtawafuata. Ndo mana mnaambiwa akili za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Sasa ccm na hiyo katiba yao mpya wanataka kuwaongoza watu wa dini ipi? Labda ile dini inayoua maalbino, wachawi na waganga wa kienyeji.
 
Hata hapa Dar leo tumesomewa yaani ni hapana tu.namimi nimetoa waraka kwa ukoo wangu wote na wa mke wangu ni hapana tu.
 

Wewe nimnufaika wa mifumo mibovu ya nchi yetu rangi yako inaonekana.
 

Kama maneno ya Komba Marehemu (R.I.P.) vile! Ukweli wa Maaskofu na Mzee Warioba mnayemchukia na uongo wa ccm kamwe haviwezi kukaa pamoja. Asante wasema ukweli
 

Umeitwa kanisani? Umejipeleka mwenyewe. Kilichokupeleka?
 
Sasa ccm na hiyo katiba yao mpya wanataka kuwaongoza watu wa dini ipi? Labda ile dini inayoua maalbino, wachawi na waganga wa kienyeji.

Bakwata, nilimsikia shekh mattaka chanel ten akiisifia akiwataka wa bakwata waipigie kura ya ndio
 



HIVI kwanini iliitwa Rasimu...na kwanini ilipelekwa Bunge Maalum.....tuliamin Rasimu sio kitabu cha dini lazma kipitiwe ndio maana kilipelekwa bunge maalum...kingineee..kwa busara za wajumbe wa bunge maalum zaidI ya 400 waliobaki bungeni kwa ajili ya watanzania na kwa pamoja waliipitisha kwa nguvu moja katiba inayopendekezwa iliyobaki na zaidi ya asilimia 80 ya maudhui ya yaliyokuwa kwenye rasimu na asilimia zilizobaki ziliingizwa kwa maana ya kuboreshwa...sasa nashangaa wanaosema maudhui ya rasimu ya warioba yalipuuzwa...au mlitaka iende kama ilivyokuwa...sasa logic ya kuwa na bunge maalum ipo wapi.....me naona kuna tatizo kwa wanaopinga hii kitu...kuna exaxtly a Specific issue waliokuwa wanaitaka "Serikali 3" hahahahahahahaha kingineee kinachoshangaza ni kuwa asilimia 61 ya maoni ya wazanzibar yalitaka serikali ya mkataba...mbona Tume ya warioba iliyapuuzaa...au yale hayakuwa maoni ya wananchi....

Ifike mahali tutumie akili zetu kuchambua mambo, na wewe Babu uliekuwa katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba pumzikaa bhana tumekuchoka sana.
 
ni kwel huko nakanisa yote ya roman imesomwa? ngoja niulizie

Ndiyo imesomwa .
Mimi nilikua Msimbazi ikasomwa pale .
Iko vzr yaani hatuwezi kupigia Kura kitu tusichokijua....
 

Mkuu thread yako nimeisoma para ya kwanza tu nimegundua wewe sio mfatiliaji was mambo ya katiba. Ni hivi. Wale viongozi wa dini waliokuwamo bungeni hawakuteuliwa na taasisi za dini husika. Wale waliteuliwa na ccm. Majina yaliyopelekwa na taasisi hizo hayakupitishwa instead ccm wakaweka watu wao, hao kina kadiva,resembles etc.
 

anafata mkumbo tuu wala hajui anachokisema anacopy na kupaste tuu. Muelimishe huyo aelewe.
 

Mimi mwenyewe mseminari wa kaengesa achana na mbalizi hapa lakini kwa hili nawaumga mkono maaskofu wana point nyingi sana kwenye waraka wao
 
mimi binafisi tangu walipo nitolea nchi yangu TANGANYIKA nitajiandikisha kisha kura ya HAPANA kwa katiba pendekezwa,
wakirudisha kipengele cha serikali tatu na piga kura ya NDIYOOOOOOOOOOOOOO
 
Mbona mm nilikuwa kanisani anglikana leo padri hajaongelea katiba .mpya

Labda ulichelewa kufika hapo kanisani kwenu. Huku morogoro huo waraka umesomwa makanisa yote ya Anglikan. Na tumeambiwa tutapewa copy kwa wanaohitaji.
 

Kwa hiyo hoja yako unataka wawakilishi wa dini nao wangetoka nje ya bunge kususia kikao kama UKAWA? Ndiyo unataka kutushawishi tuamini kama ndiyo ungekuwa uamuzi sahihi? Kumbuka lile bunge lilitekqa na wanasiasa, ambao waliingia bungeni kujitengenezea ma shavu. kenya walikubaliana kuwa wale wote watakaoingia bunge la katiba hwatojishughulisha kwenye shughuli za kisiasa kwa muda wa kiaka saba tangu katiba ipatikane. Wawakilishi wa dini wangetoka pamoja na UKAWA unategemea matusi ambayo yengetukanwa na kina marehemu Komba yangekuwaje? Hii ndiyo hatua sahihi. Hawakutoka nje, ila kwa kuwa waliona kuna uhuni, ndiyo maana waliacha wamalize wanasiasa huku wakijua wao wana mahali pa kuongelea na ndiyo hapa sasa. katiba ni maridhiano wala siyo ubabe na utemi. Tangu lini Chenge akatunga katiba yenye maadili? Hata mwanangu wa darasa la tatu amekataa juzi kwa utashi wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…