Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jinsi walivyosomewa waraka huo wasomewe pia Katiba Inayopendekezwa. Hivi hawa watumishi wakoje. Mbona Mitaguso yao ya Vatican I na II hadi ya African Synod sisi waumini hatukushirikishwa kuipigia kura. Kweli nimeamini na kwenye dini utawala wa kiimla unatawala. Sasa waumini kwa kuonyesha kukomaa kwenu kiroho na kimwili ipigie kura ya Ndiyo baada ya kuielewa Katiba Inayopendekezwa. Acha kukubali kila kitu kitokacho kwa hawa wazee. Wanaweza wakaamua kuwa kuanzia leo hakuna misa je mtafanyaje, mtawafuata. Ndo mana mnaambiwa akili za kuambiwa changanya na za kwako.
mzee tunamshangaa anachong'ang'ani kitu gani yeye alishapewa heshima ya kuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba, sasa anadhani hiyo rasimu yake ndiyo ilitakiwa iwe basi isijadiliwe bungeni na iwe katiba mpya? Khaaaa aibu sana sana kwa huyo mzee
Jinsi walivyosomewa waraka huo wasomewe pia Katiba Inayopendekezwa. Hivi hawa watumishi wakoje. Mbona Mitaguso yao ya Vatican I na II hadi ya African Synod sisi waumini hatukushirikishwa kuipigia kura. Kweli nimeamini na kwenye dini utawala wa kiimla unatawala. Sasa waumini kwa kuonyesha kukomaa kwenu kiroho na kimwili ipigie kura ya Ndiyo baada ya kuielewa Katiba Inayopendekezwa. Acha kukubali kila kitu kitokacho kwa hawa wazee. Wanaweza wakaamua kuwa kuanzia leo hakuna misa je mtafanyaje, mtawafuata. Ndo mana mnaambiwa akili za kuambiwa changanya na za kwako.
Sasa ccm na hiyo katiba yao mpya wanataka kuwaongoza watu wa dini ipi? Labda ile dini inayoua maalbino, wachawi na waganga wa kienyeji.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema amefurahishwa na uamuzi wa Tamko la Maaskofu wa Makanisa yote nchini ya kuikataa Katiba Pendekezwa.
Jaji Warioba amesema ni ukweli ulio wazi kwamba maoni mengi watanzania waliyotoa yamepuuzwa kwenye Bunge la Katiba la Samwel Sitta na badala yake kuingizwa maoni ya watawala.
Jaji huyo mstaafu amesema Tamko la Maaskofu kuomba muda zaidi wa kusoma katiba pendekezwa kabla ya kura ya maoni ni muafaka kabisa hasa ikizingatiwa viongozi wa dini ndiyo wenye waumini.
Tayari leo Jumapili Makanisa yote ya Kikatoliki nchi nzima umesomwa waraka wa kinabii wa kuikataa katiba pendekezwa kwani imebeba maoni ya chama kimoja tu cha CCM.Na waraka umesisitiza katiba hiyo ilipatikana kwa njia ya HILA kubwa.
Mwaka jana Shura ya Maimamu wa dini ya Kiislamu ndiyo ilikuwa taasisi ya kwanza ya dini kuikataa katiba Pendekezwa na kuwataka Waislam wote kupiga kura ya HAPANA
ni kwel huko nakanisa yote ya roman imesomwa? ngoja niulizie
Hata hapa Dar leo tumesomewa yaani ni hapana tu.namimi nimetoa waraka kwa ukoo wangu wote na wa mke wangu ni hapana tu.
Naomba niseme mimi ni mkiristo tena Mseminari safi, niliyefunzwa nikafunzika. Ila naomba niseme MAASKOFU ni wanafiki.
Wakati wa bunge la Katiba, hatukuona kiongozi yeyeto wa dini ya Kikristo amabye alitoka nje kuungana na UKAWA, inakuwaje leo wanasema Katiba ni ya chama kimoja? Naomba niseme karibia viongozi wote wa dini ni wanafiki tu. Kitu kimoja amacho naamini kuwa wanaweza kuwadanganya wanadamu lakini sio MUNGU, Sizungumzii tu katika hili la kupinga katiba bali katika mambo mengi. Mimi huwa nawaona ni wa kawaida sana.
Kama kweli wanamaono toka kwa MUNGU kwanini wasingesimama kipindi kile na kukemea kisawasawa? na wangewaamuru wanaowakilisha watoke.
Naomba nisimulie kitu kimoja.
Wakati tukiwa seminarini pale Mbalizi Siminari, tulikuwa na Mkuu wa seminari (RECTOR) kwa sasa ni marehemu alikuwa anasema kwamba, ikitokea KIRANJA amekupa adhabu, halafu ukaigomea, maana yake ni kwamba umemgomea RECTOR ambaye amemteua huyo kiranja, na kama umemgomea Rector maana yake umemgomea Askofu wa Jimbo ambaye amemteua huyo Rector kuwa hapo, na kwa maana hiyo umemgomea Kadinali na kwa maana hiyo umemgomea Papa(Baba Mtakatifu), na kwa maana hiyo hiyo umemgomea YESU KRISTO ambaye kamteua huyo Papa, na kwa maana hiyo umemgomea MUNGU MWENYEZI aliyemleta mwanaye mpendwa duniani. Hivyo wewe uliyemgomea kiranja adhabu hufai kuendelea kuwepo hapo seminari, zawadi kubwa unayopaswa kuzawadiwa ni kufukuzwa seminarini. Na nikujuze tu kuwa seminarini viranja wana nguvu na wanaogopwa sana.
Sasa katika hili la Maaskofu, je ni nani alipendekeza majina ya hao viongozi wa dini walioyeuliwa kwenye bunge la KATIBA? na walikuwa wanamuwakilisha nani?
Hapo hapo niunganishe na hadithi nyingine.
Kulikuwa na kaka angu, yeye alikuwa kanisa moja la kilokole, sisi wengine tukiwa ni RC. Na yeye kaka yetu alikuwa anatuona sisi kama ni wahuni na tumepoteza mwelekeo, sasa kuna siku akasema ameoteshwa na MUNGU kuwa dada fulani atakuwa ndo mke wake na huyo dada walikuwa wanasali kanisa moja, lakini sisi wahuni tukamwambia kaka huyo dada unayetaka kumuoa hajatulia, na sisi tumekumbana naye sana katika matukio kadhaaa, yeye akawa anabisha, ikawa ni ugomvi mkubwa sana katika familia, yeye akasisitiza ameonyeshwa na ROHO MTAKATIFU, Lakini ukweli ni kwamba alikuwa anashinikizwa na mchungaji wa hili kanisa maana huyo dada alikuwa ni ndugu wa huyo mchungaji, kama mjuavyo siku hizi watu wanamfuata na kumuamini mtu zaidi kuliko neno la MUNGU. basi kama familia tukaridhia, na mahari ikatolewa. Sasa tukiwa tunasubiri kuanza mipango ya lini harusi ifungwe, siku moja kaka kwa macho yake mwenyewe akamfumania huyo mchumba wake anafumuliwa MARINDA. Akajifanya kutuficha lakini siku zilivyokuwa zinakwenda akasema yeye hatamuoa, tukamuuliza kwanini akasema ROHO MTAKATIFU amemtokea kuwa yule sio mke, kumbuka hapo Mahari tayari tumetoa.
Binafsi nikamuuliza hebu tueleze huyo MUNGU wako ambaye leo anakuonyesha kijani halafu kesho anakuonyesha nyekundu.
Sasa hizi habari zinafanana na haya wanayoyafanya maaskofu leo hii.
umeitwa kanisani? Umejipeleka mwenyewe. Kilichokupeleka?
mkuu thread yako nimeisoma para ya kwanza tu nimegundua wewe sio mfatiliaji was mambo ya katiba. Ni hivi. Wale viongozi wa dini waliokuwamo bungeni hawakuteuliwa na taasisi za dini husika. Wale waliteuliwa na ccm. Majina yaliyopelekwa na taasisi hizo hayakupitishwa instead ccm wakaweka watu wao, hao kina kadiva,resembles etc.
ndiyo imesomwa .
Mimi nilikua msimbazi ikasomwa pale .
Iko vzr yaani hatuwezi kupigia kura kitu tusichokijua....
Mseminari safi anakuwa padre maana lengo kuu la Seminari ni kuandaa mapadre,sasa we ulikuaje mseminari safi ukashindwa kuwa padre,ulikuwa hujui kuwa ukiwa seminari unaandaliwa kuwa padre.Wewe ni mseminari mnafiki,seminari kulikushinda.Anyway wenzako ni maaskofu safi ndo wameandika waraka.Wanasema muda wa kuisoma katiba uongezwe,sasa we unataka tupige kura bila kusoma? Usijifanye wewe pekee yako ndo umesoma seminari wengi wamesoma seminari ila wapo kimya.Unataka kutuaminisha kuwa kama maaskofu walibugi bungeni basi waendelee kutupoteza na siye,may be walibugi bungeni lakini sasa hivi wameona uhalisia na ukizingatia wawakilishi walikuwa wachache.
Naunga mkono muda usogezwe mbele tuisome kwanza kwa wale wenye kuielewa na wanaohitaji usaidizi basi wapate elimu ya kutosha
ni kwel huko nakanisa yote ya roman imesomwa? ngoja niulizie
Mbona mm nilikuwa kanisani anglikana leo padri hajaongelea katiba .mpya